Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, September 6, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-23‘Nilikuwa naomba kuongea na mume wa huyu dada..’ akasema Docta alitoka kwenye chumba cha maabara na kumkuta shangazi wa Maua akiwa kasimama pale mlangoni.

‘Unataka kuongea na Mume wake…! Kwanini Docta uongee na mume wake, wakati mimi ndiye nimemleta hapa hospitali?’ akauliza Shangazi wa Maua, na kabla docta hajajibu kitu shangazi akauliza `Kuna matatizo yoyote, maana huyu tulichomleta hapa ni hii habari ya kuchanganyikiwa, na….’ akawa anaongea shangazi akiwa anaonyesha uso wa wasiwasi, akiwaza mbali zaidi kuwa huenda binti yake ana matatizo mazito kinyume anavyomdhania.

‘Huyu mumemlta hapa, na sisi kama kawaida yetu, kwanza tunamchunguza kwa kuchukua vipimo vyote kama tulivyofanya, na….kwa vile bado yupo katika uchunguzi na uchunguzi wa matatizo kama haya sio wa siku moja, inahitaji muda, na baadhi ya vipimo ninavyo, …ndio maana nishauri kuwa ni vyema nikamuona mume wake, kwani kuna mambo mengine yanahitaji kuongea naye kwanza,…’ akasema huyo docta.

‘Mume wake ni marehemu, alifariki miaka miwili iliyopita, na tangu afariki, amekuwa katika hali hii mbaya, haamini, na hasahau, kiasi kwamba imezidi kupita kiasi, ilifikia hatua kama anataka kujiua, mara anatoka usiku na kupotea, na hii hali ndio inatutia mashaka mtu anatoka usiku na anakwenda asipokujua, na anaweza akafanya vitendo usiku, na ikifika asubuhi haui kuwa alifanya nini…’ akaelezea shangazi.
‘Hayo ndio nataka kuyasikia na tatizo kama hili, linahitaji maelezo yote mnayojua kuhusiana na yeye, chanzo chake , nini anakifanya….na pia lazimia tumchunguze afya yake, ikiwezekana kila kipimo, kwasababu mambo mengine yanaweza kutokea, ikazalisha matatizo mengine, …na ndio maana nikashauri hivyo, sasa kama mume wake hayupo, basi ngoja niongee na mgonjwa mwenyewe…’ akasema Docta.

‘Nakuomba tafadhali, kama kuna tatizo ambalo lilihitaji mume wake, ambalo unaona ni muhimu kuwepo mtu wa ziada, naomba uniambie mimi kwanza, kwasababu huyu ni binti yangu na mimi ndiye ninayemjua kuliko mtu yoyote, naomba uniambie mimi mwenyewe…’ akasema Shangazi na kukatisha maneo pale mlango ulipofunguliwa.
Wakati wanaongea na Docta , mlango ulifunguliwa kwa ghafla na akaingia Maua, aliona wamekaa muda mrefu na yeye kaachwa chumba kingine akisubiri, hakuipenda hali na mazingira ya hospitalini, akawa kama anaisikia kichefu chefu, …alitamani atoke akimbie….baadaye akaona awaondeee huko huko ndani awaambie kuwa yeye anaondoka.

‘Docta umeshanichukua vipimo, naomba majibu yake maana kesho nina darasa, siwezi kushinda hapa, nihitaji muda wa maandalizi , naweza kwenda,…au kama majibu ni leo au kuna lolote..?’ akauliza Maua, na Shangazi akamkonyeza docta kumuashiria kuwa asimwambie lolote kwanza.
‘Matatizo yako sio ya kuharakisha, yanahitaji tukae tuongee, kwanza niliona ni vyema tukaanza kwa kuchukua vipimo vyote ili kuhakikisha kuwa hakuna tatizo jingine, na hili ndilo tumelifanya, tunasubiri matokeo yake, na wakati tunasubiri hili nilitaka kujua historia yako , maelezo yako kwa ujumla, …’ akaongea Docta.
‘Kwanini docta yote hayo…? Akauliza Maua na kumwangalia shangazi yake,
‘Maua hapa umeletwa kwa tatizo gani…? Akauliza Docta
‘Hawa ndio wameniambia natakiwa kuja kukuona, lakini mimi Docta sina tatizo lolote, nimeshajijua nini kilikuwa kinanisumbua, ilikuwa ni mawazo mengi, na…’ akawa anaongea Maua huku anatizama saa yake.
‘Sawa kabisa, nakuunga mkono sana, na hivyo ndivyo inatakiwa, lakini kwanini ikafikia hivyo, ukawa na mawazo mengi, kwanini uwe unapoteza fahamu mara kwa mara, hayo na mengine mengi yanatakiwa yachambuliwe na mwisho wake tunakuwa tunapata suluhisho kama mataibabu…ndio tumeshajua kuwa kuna kiini ambacho kimeanzia baada ya kuobdokewa na mume wako…lakini hilo linaweza likawa na sababu ya matatizo uliyokuwa nayo kabla bila kujijua, na sisi kama wataalamu tunatakiwa tunatakiwa tuyagundue hayo…sasa kwanza kabla sijaongea na wewe nilikuwa naomba niongee na mzazi wako, halafu wewe tutaongea na kupangiana siku ya kuonana tena, nakuhakikisha kuwa nitakuwa sichukui muda wako mwingi…’ akasema Docta.
‘Lakini shangazi wewe ndioumenilea, uliwahi kukutana na matatizo kama hayo kutoka kwangu..?’ akamuuliza shangazi yake.
‘Wewe nisubiri kwanza nikaongee na docta, haya tunayotaka kuyafanya ni kwa afya yako, usiwe kama mtoto mdogo wa kulazimishwa kunywa dawa…’ akasema shangazi yake kwa ukali na Maua akanywea na kutoka mle ndani kwenda kusubiri kile chumba alichokuwa mwanzoni, alipofika hapo akawa anawaza mengi, kwanini huyu docta atake kuongea na shangazi yake wakati yeye ndiye mgonjwa, yeye sio mtoto mdogo…au nina ugonjwa mbaya nini..lakini kweli najisikia siku hizi kuchoka, na…hapana…hapana….siumwi mimi….
Baadaye shangazi akatoka na kumwambia Maua docta anataka kuongea na yeye, wakaingia kwa docta wakiwa wote wawili, ilionekana shangazi hakutaka kabisa binti yake kuongea na docta wakiwa wawili, akawa yupo pembeni akimsikiliza Docta anavyomuhoji Maua.
‘Maua mengi ya historia yako nimeyasikia toka kwa mzazi wako, lakini hata hivyo wewe siomtoto mdogo, na kwa vile uliwahi kuolewa, tunasema wewe ni mtu mzima, naomba nikuulize swali moja ambalo majibu yake yanaweza kunisaidia katika kazi yangu,…..
**************
Maneno alibakia kaduwaa hata kuwakaribisha wageni wake alishindwa, akabakia akiwaangalia kwa mshangao, na wale wageni wakawa wameduwaa pia, hawakuweza kusema kitu wakawa wamesimama pale mlangoni. Na aliyeanza kuongea ni Maua akasema kwa sauti ya kitoto, mtoto anayedeka kwa mzazi wake;
‘Untie, mimi napoteza muda wangu ,hapa sasa hivi nina miadi na watu wangu, naomba niondoke, mimi sina mazungumzo na…huyo mtu wako, akanyosha kidole kimuonyeshea Maneno, na kitendo kile kilimfanya Maneno ashangae na hapo akazindukana kutoka kwenye ule mshangao na kuanza kuwakaribisha, na wakati anafnya hili macho yake yalikuwa kwa Maua, alishangaa kumuona alivyobadilika, kwa kipindi cha miezi kadhaa ambacho hakuwa wanaonana kumetokea mabadiliko makubwa, Maua kanenepa kawa mweupe zaidi ya weupe wake…
‘Sawa Maua kama hiyo kazi yako ni muhimu sana, wewe nenda , lakini tafuta muda muafaka tuongee kwa marefu na mapana, na kama una tatizo hakikisha unaniambia, sasa hivi nataka tuwe karibu kuliko muda wowote ule, kwani nimeongea na docta wako kwa kirefu,…usiione kuwa u mzima,…’ akasema shangazi, huki akimkagua Maua maumbile yake.
‘Shangazi , mimi sina matatizo kwa sasa, nimeshapona, na nakuhakikishia kuwa kazi yangu hii ndiyo tiba yangu, sitakimatibabu mengine…’ akasema halafu kama vile kakumbuka , akamgeukia Maneno na kumsalimia na kumuomba samahani kuwa hakumsalimia kabla. Maneno akamjibu kuwa hakuna mataizo ila hata yeye anaomba msamaha kwa kutowakribisha na kubakia kuwashangaa, aliwashangaa kwa kuwa wameongozana..halafu akamalizia kwa kuulizia hali yake Maua kwa sababu amesikia kuwa wametoka kwa docta,
‘Mimi sijambo, ila shngazi kama ulivyo wewe alitaka nikamuone huyo docta bingwa wenu, amaenihoji maswali mengi utafikiri mimi ni mfungwa, mwisho wa siku akaniambia natakiwa mara kwa mara niwe namtembelea, lakini….’ Akabenua mdomo na kutaka kuondoka, akaanga kwa kusema kuwa sasa hivi hana nafasi ya kukutana kutana na watu kutokana na ratiba yake,..
‘Lakini hata hivyo mbona simu yako nakupigia haipatikani, umebadili namba …?’ akauliza Maneno.
‘Mara nyingi natumia namba zao walizonipa, kwasababau ya kuogopa usumbufu, wakati upo darasanai watu wanakupigia, haileti picha mbaya, namba ile bado ipo, ila kwa muda nikiwa sina kazi..’ akasema Maua na kuondoka zake….
Walibakia shangazi na Maneno wakiongea, na ilionekana walichokuwa wakiongea ni jambo zito sana, jambo ambaloo lilimafanya Maneno achanagnyikiwe, , lakini mwisho wa siku walifikia muafaka kuwa Maneno ahakikishe ameonana na Maua …
***********
‘Halloh, mimi ni Maneno , Maua, nakuomba tuonane , nina jambo kubwa, na muhimu nataka kuongea na wewe, na naomba ikiwezekana kama ratiba yako haina nafasi uombe zarura, hili jambo ni muhimu sana…’ akasema Maneno.
‘Sawa, fika nyumbani nip oleo nyumbeni , tuna mapumziko ya siku nzima leo, ..’ akasema Maua.
Maneno liondoka kwake hadi nyumbani kwa Maua, alipofika alimkuta kakaa kwenye kochi, na alipomuangalia alimuona kama ana mawazo mwengi sana, hakutaka kudadisi zaidi akaanza kuongea mambo mengine kama kuvuta muda kabla hajafikia lengo lake, na hapo Maua akaona anapotezewa muda akauliza.
‘Nakumbuka kwenye simu umeniambia kuwa una jambo muhimu unataka kuniambia, naomba uniambie, sipendi kuwekwa rehani,,!’ akasema Maua

‘ Maua, kuna usemi usemao kuwa kila jambo hutokea ili iwe sababu, na huenda inatokea hivyo ili iwe heri kwa wanadamu. Naomba unielewe Maua kuwa sina maana mbaya, na sikutakii mabaya katika masiha yako. Nakurejesha kidogo nyuma, siku ile tulipokuwa Arusha, nakumbuka uliniuliza maswali mengi na mojawapo ya mswali yako nilishindwa kukujibu, leo nimekuja nikiwa tayari na majibu yake, kwani nilihitaji muda wa kutafakari sana kabla sijakujibu.

‘Maswaligani shemeji, mimi nakuomba tusikumbushane yaliyopita na hata docta alinishauri hivyo, kama ni hayo yamepita na nimeshasahau, …kwani yana msingi gani kwako hayo maswali?’ akauliza Maua.
‘Yana msingi mkubwa sana, yana maana kubwa sana kwangu na kwako, unakumbuka uliniuliza ni nani aliyekuokoa siku ile, ambaye ndiye alikubeba hadi chumbani kwako,,? Akauliza Maneno bila kujali maneno ya Maua kuwa hataki kukumbushwa yaliyopita.

‘Ilikuwa ni ndoto, najua wewe ulitaka kunichezea akaili yangu, ningeliwezeje kutoka usiku hadi kwenye pori la hatari, na sizani kuwa kuna joka kubwa kama lile..ilikuwa ni ndoto na wala sitaki kujikumbusha kichwni.
‘Mua ilikuwa sio ndoto, ni kweli tupo yaliyotokea siku ile….’ Akasema Maneno na kumwangalia machoni Maua, na Maua alikuwa kama anatafakari kitu, halafu akauliza kaam ilikuwa ni ndoto, ni nani basi aliniokoa ni nani aliyenibebea hadi chumbani kwangu , na ni nani aliyelela name siku ile….’ Akauliza Maua akiwa bado anatafakari kwa undani, alionekana kuwa na mawazo mazito, na kumfanya Maneno awe na mashaka kwa hayo anayotaka kumwambia, aliombea ingeliwezekana shangazi yake angelikuwepo, lakini kutoka a makubaliaono yao, huo ni mzigo wake, vinginevyo aatkwenda kuozea jela….

‘Maua, ile haikuwa doto, mimi ndiye niliyekuokeoa kutoka kwenye lile joka,nikakubeba hadi chumbani kwako…’ akasema Maneno. Na hapo hapo Maua akainuka palealipokuwa kakaa na kumwangalai Maneno kwa hasira, …na machozi yakaanza kumtoka kama mvua, …na baadaye akaanza kulia kwa kwikwi…
Baadaye akanyamaza na kumwangalia Maneno na kusema `wewe nishetani, wewe ni muangamizi mkubwa, ina maana wewe ndiye tuliyelala naye usiku na sio Mhuja sio, wewe ndio ulichukua matatizo yangu ili uinufaishe nafasi na tamaa yako sio…unajifanya mpole, unajifanya una huruma, kumbe nia na lango lako lote lilikuwa hivyo, una maana gani, unajifanya ulikuwa rafiki mwema wa Mhuja, kumbe lengo lako ni ingine kabisa….ulinifanya nini usiku ule, nakuombe uniweke wazi, ….? Akauliza Maua.

‘Maua nakuapia kwa mungu kuwa mimi sikumbuki kukulazimisha…mimi nilishitukia tu tupo kwenye tendo hilo, na …ooh, shemeji nisamahe sana, sikuwa na nia hiyo mbaya, ….nakuomba sana nipo chini ya miguu yako..’ akasema Maneno hadi kupiga magoti, lakini alikuwa bado yupo mbali na aliposimama Maua akainua kichwa kuangali juu, alikuwa kama anamuomba Mungu wake, alikuwa anaomba kitu kikubwa kuwa kimpishie mmbali na Maneno alikuwa na hamu ya kujua nini anachokiomba…

Maneno akamwangalia Maua machoni, lakini hata pale Maua alipotizama chini hakuweza kumtizama Maneno machoni. Maua alikuwa sasa kaangali chini, alikuwa hana nguvu ya kumtizama shemji yake machoni, alikuwa haamini maneno aliyoyasikia sasa hivi kutoka kwa shemeji yake kuwa ndivyo ilivyotokea usiku ule, alishafikia tamati kuwa ile ilikuwa ni ndoto, na hata kuanza kusahau, sasa habari hii inamtonesha, na inamti amaozi makubwa sana…na hapo akaumbuka siku ile ilivyokuwa;

Siku ile alipoamuka asubuhi alijipa moyo kuwa ile ilikuwa ni ndoto, lakini kadri muda ulivyokwenda na kutafakari vyema aliiona kuwa ni kweli na kuwa lile tendo lilifanyika kiukweli, alikumbuka jinsi alivyokuwa akimtizama shemeji yake siku ile, lakini sheemji yake alikuwa hamtizami machoni,…na kuna muda aliwaza hivyo kuwa huneda, labda ndiye alifanya ujanja wote huo, ili amfanyie hayo ambayo leo anadhihirishiwa kuwa ndivyo, hapo chuki ikaanza kumjaa Maua moyoni mwake, alitamani kama kungelikuwa na silaha ….

‘Lakini kwanini nimekuwa mjinga wa kujidanganya, ni lazima nikubali ukweli kuwa mume wangu keshakufa na lolote linalotokea leo kuhusu yeye, kumuota na…hayo yote ni mawazo tu..’ akawaza na kutafakari hivyo, akamwangalia Maneno, ambaye likuwa anamtizama kwa uwoga na halafu akageuka na kutizama pembeni na bila kujijua akasema kwa sauti ‘Lakini mume wangu ni marehemu …’

‘Huo ndio ukweli ulivyo Maua ukubali kwenye nafsi yako kuwa Mhuja hayupo hapa duniani tena ni marehemu’ akasema Maneno aliposikia kauli hiyo, na kupata nguvu kuwa sasa anaweza kuongea kile alichotaka kusema. Na Maua aliposikia kauli hiyo ya Maneno akili yake ikawa kama imezibuliwa na kuwa kwenye dunia nyingine tena, ikatoka kule kwenye mawazo ya kwanza na kwenda mbali zaidi ya kuwaza akawa sasa anamuona mtu, ingawaje anayemtizama kwa wakati ule ni Maneno, lakini alikuwa hamuoni Maneno, kwa mbele yake alikuwa akimtizama mtu mwingine tofauti, alikuwa akimtizama Mhuja…na sura yake ilipojaa mbele yake, machozi yakaanza kumtoka kwa fujo….

Maneno alipoona kuwa Maua anamtizama yeye huku analia, akajua sasa anasikilizwa na kulia kule huenda kukasaidia kuondoa yale yote yanayomzonga moyoni, akaendelea kuongea kwa kusema ‘Maua hebu jiulize wewe mwenyewe, familia ya akina Mhuja mwaka huu wamesoma dua ya kuwaombea waliotangulia kama unavyokumbuka na katika orodha ya marehemu jina lake lilikuwa la kwanza kutajwa kwa kurehemewa, …hebu jiulize kama wangekuwa na mawazo kama yako wangelifanya hivyo, ina maana wao kweli hawana uchungu na mtoto wao…?’ akauliza Maneno na kumwangalia Maua ambaye alikuwa bado anabubujikwa machozi kama mvua.

Maneno akamtizama Maua kusubiri kuwa atasema lolote, alichoona ni mtu kamkodolea macho huku akiwa anatokwa na machozi, akasita kidgo kuongea lakini baadaye akasema `Maua leo niomekuja kwako maalumu kukuambia jambo muhimu sana, ….naomba unielewe, kuwa silisemi himi kwasababu ya shinikizo la matatizo yako, nalifanya kwa kuwa nina nia nalo….’ Akasita kuongea na kumtizama Maua, cha ajabu alimuona akiwa bado kamkodolea macho, nay eye akatizama pembeni na kusema.
Maua hata kama unajiona kuwa umepona, lakini kwangu mimi, hata kwa shangazi yako na hata docta tumeliona hili kuwa bado hujapona, na docta kashauri kuwa bado una matatizo , matatizo ambayo yanahitaji mtu wa kuwa karibu naye wakati wote…lazimia uwe na mtu anayekufahamu fika, kwa mfano anaweza akaja rafiki yako akakuulizia mambo yaliyopita, na matokeo yake akakurudishia uchungu, yeye akaondoka, huku nyuma wewe ukaanza kubadilika na labda ni usiku, ukatoka na kwenda kusikojulikana…nakutolea huu mfano kwasababu huishi peke yako katika hii dunia, watu kama hawo wasiokujua watatokea na kukuumiza moyo wako, licha ya kuwa nia yako ni kusahau kabisa, lakini ukikumbushwa hayo utakuwa unarejeshwa kwenye majonzi, na inawezekana kabisa yakatokea kama yale ya Arusha, na je kwa muda huo utakuwa na nani anayekujua vyema….. ‘ Maneno akawa anaongea na kurudia rudia maneno kwa msisitizo, na akawa sasa kama anamsogelea, akijaribu kuona Maua atafanya nini akimsogelea karibu, lakini alichoona ni mtu kumtizama tu huku analia

Baadaye Maua akatulia na kupikicha macho yake, akawa kama vile kazindukana toka katika dimbwi lile la mawazo, akahema kwa nguvu, halafu akatizam tena kwa mbele, sasa akawa hamuoni yule aliyekuwa akimtizama mwanzoni, yupo Maneno , yupi sheei yake, ambaye analeta habari asizozitaka…..Maua alimtizama Maneno kwa mcho ya chuki, akawa kama anataka kumwambia usinisogelee, shetani mkubwa wee, lakini hayo yalikuwa akilini mwake, akawa anamwangalia tu kwa macho hayo ya chuki, yakiwa yamegubikwa na wingu la machozi…

‘Maua kwa ujumla kwa usalama wako unahitaji mtu wa kukaa nawe karibu, si usiku wala mchana, hebu nikuulize kweli ilikuwaje hadi ukatoka usiku kama ule hadi maporini sehemu ambayo usingeweza kwenda mwenyewe ukiwa na akili zako kamili, huoni kuwa umekumbwa na ule ugonjwa…ugonjwa unaomfanya mtu afanye matendo akiwa usingizini…, wewe ninavyokujua unaogopa sana nyoka hata kuitizama kwenye runinga hutaki, lakini siku ile ulikuwa nalo mwilini mwako, limekuzingira…hebu fikiria…kwa ujumla unahitaji mtu wa kuwa naye karibu, la sivyo tutasikia mengine, na mimi sitakubali hilo…’ akasema Maneno na moyoni Maua akasema ndio maana ukafanya ushetani wako huo, lakini hakutoa kauli hiyo kwa nguvu, hakutamani kuongea kwani kama angeliongea angesema maneno machafu na mwisho angekumbwa na balaa jingine, akabakia kimiya na hata kufunga macho yake.

‘Maua samahani najaribu kukurudisha nyuma, ili uone hatari iliyopo mbele yako…hebu jiulize wewe mwenyewe siku ile ulitokaje ndani na kutokomea maporini, na huku ushindwe kutoka na kutokomea mjini au hata baharini, na kwa ujumla hali kama hiyo unaweza ukawa uantembea bila kujali mgari au nini, kwasababu wazo lako linakuwa kufanya jambo moja, na mengine huyaoni…’ akasema Maneno…na hapo Maua akayafungua macho yake na kitu kama uwoga ukamwingia, kuonyesha naye anaikumbuka ile siku, ….analiona lile joka aliloliona kwenye njozi…ooh, sio njozi eti ilikuwa ni kweli…akazidi kufunua macho kwa woga, kama vile analihisi lile joka lipo karibu yake…

‘Sasa Maua nakuomba sana, sio kwamba nachukulia nafasi hii kama kisingizio, lakini …nafanya hili nikiwa nahitaji, nikiwa natamani, nikuwa na upendo wa dhati kwako. Mimi na Mhuja tulikuwa marafiki, tulikuwa tukipendana zaidi ya ndugu na wakati mwingine tulikuwa tukitaniana kuwa `mke wake ni wangu na mke wangu ni wake’ ulikuwa ni utani, lakini sasa naona imefikia mahali kukiri kuwa natamani iwe hivyo…naomba iwe hivyo…Maua nakuomba kwa mikono miwili nakuomba unipe nafasi ya Mhuja…’ akatulia na kumwangalia Maua

Maneno alimshngaa Maua kuwa haonyeshi dalili yoyote ya kukubali au kukataa, na inaoenakan kama vile hayupo hapo kabisa, alikuwa katulia kimiya kama vile hajamsikia na Maneno akaendelea kuongea kwa kusema, `Mhuja kaondoka,na kiukweli kunahitajika mtu kuziba nafasi yake…na mtu huyo ni mtu anayekujali, anayekufahamu na anayekupenda kwa moyo wake wote, kama alivyokuwepo Mhua nap engine akakupenda zaidi yake, huwezi jua, …na Maua mtu huyo, hayupo mbali nawe, mimi ninakuahidi kuwa hutajijutia…nakuomba tafadhali unikubalie ombi langu la mimi kuichukua nafasi ya rafiki yangu mpendwa, …’ akasema Maneno a kushika kifuani kwake kwa mikono miwili.

‘Maua kiukweli mtu huyo anahitajika kwako haraka iwezekanavyo, na mimi ndiye ninayefaa, kwa sifa zote nilizozitaja, …hata hivyo baada ya tukio lile la Arusha, nimekuwa nikiteseka sana, kwasababu tendo lile lilitokea bila dhamira yangu…sikujielewa ilikuwaje …na siwezi kuvumilia zaidi, hasa nikikuona unavyoteseka, na kuweka maisha yako kwenye hatari. Mimi nilikabidhiwa kwako na Mhuja, nihakikishe usalama wako, sasa iweje nishindwe hilo…hata hivyo Maua nitashindwa kabisa kukuangalia machoni, kama tutakuwa tofauti, najisikia uchungu sana, nasononeka sana….Nakuomba unisamehe kwasababu lile limetokea na huenda limetokea ili iwe hivyo, ili upate mwenza wako anayekustahili..…’ akasema Maneno huku akimsogelea Maua na kuja kumpigia magoti mbele yake...’

Maua alibakia akiwa kama kashikwa na mshangao, akawa anamwangalia Maneno anavohangaika, lakini kwa uumla alikuwa hamuoni yeye, …kulikuwa na taswira nyingine ilikuwa inaonekana mbele yake, taswira ya aliyekuwa mume wake. Sasa hivi ile taswira ilikuwa kama anamwangalia kwa macho ya kutaka kujua atatoa kauli gani kutokana na ombi alilopewa na Maneno, na uso wa hiyo taswira ulionyesha chuki, ukiwa kama unasema `wewe ni msaliti, wewe umefanya nini, …’ Maua kuhisi hivyo akageuza kichwa kutizama pembeni lakini akakutana na taswira ile ile, sasa ikimwambia `unaona ulivyo mnafiki, hata kuniangalia unaishindwa, kwasababu umenisaliti…wewe ni msaliti..’ akageuka upande mwingine na huko tena akakutana na uso kama ule ukimwambia; `haya toa jibu..toa jibu, …na jibu gani utaweza kulitoa wakati umeshafanya kwa vitendo, ..iliyobaki ni kauli kwa watu lakini kwa matendo umeshatoa jibu…mkubalie msaliti mwenzako…kwaheri, nakutakia mafanikio mema…’ Maua alipoyasikia maneno hayo kihisia akaanza kulia na kusema kwa sauti.

‘Hapana mimi sio msaliti Mhuja, katu sikutarajia kufanya hivyo… na wala sikujua kuwa imekuwa hivyo…nilijua ni ndoto…hapana siwezi kukusaliti Mhuja, ….nakupenda mume wangu, nakuomba usiniache…nakuomba tafadhali,…sijui kilitokea kitu gani mpaka ikatokea hivyo…..sijui, na sijui na kitu gani kinanilazimisha kufanya hivyo….nakuomba Mhuja unisamehe, nipo tayari kuja huko ulipo, nipo tayari..hata sasa, nipo tayari…oooh, mungu wangu nimefanya nini…nisamehe mungu wangu….mungu wangu nakuomba unichukue roho yangu ikaonane na mume wangu…ooooh’ Akashikwa na kitu kama kizungu zungu akadondoka chini na kupoteza fahamu...


Ni mimi: emu-three

6 comments :

Yasinta Ngonyani said...

Afadhali umerudi maana duh!..Nilikuwa nyuma kidogo katika kusoma lakini sasa nadhani nipo sawa na wengine..na naona mambo yanaendelea hapa sijui itakuwaje ....

emu-three said...

Da Yasinta na wapenzi wa blog hii! Sijasafiri au kwenda wapi bali ni vikwazo vilivyo juu ya uwezo wangu! Hapa natamani ningelikuwa na komputa yangu na internet! Da Yasinta na wapenzi wa blog hii! Sijasafiri au kwenda wapi bali ni vikwazo vilivyo juu ya uwezo wangu! Hapa natamani ningelikuwa na komputa yangu na internet!

Swahili na Waswahili said...

Pole sana ndugu yangu hayo yatakwisha tuu, uwe na wakati mwema, Pamoja sana.

Anonymous said...

Du kila nikifikiria wewe mtu yaani kama ungekuwa unawatungia hawa watu wa tansia ya filamu hapa kwetu umgeleta mabadiliko makubwa ktk script.
Hivi we na shingongo nani mkali..

ROGER-UK

Precious said...

M3 ni mkali Shigongo hamfikii hata nusu yake....jamani nilibanwa wk nzima nakosa hata time ya kuingia huku yaani mpk nikajihisi napata homa kila nikijaribu nichungulie kdg siwezi kabisa.. M3 una changamoto kubwa sana kipaji ulichonacho ilikuwa uwe na kila kitu ikibidi ndio iwe ndio kazi yako, sometimes nawaza hicho kipaji ungekuwa nchi za mbali ungekuwa milionea all in all Mungu mkubwa ipo siku mambo yatakaa sawa tu.

Anonymous said...

Em3 wala usijali mungu ni mwema siku zote, atafungua njia utapata computer na internet yako unatowekea vitu hadi usiku wa manane, jamani maneno hadi nakuhurumia.