Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, September 2, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-22





‘Hivi nipo sawa kweli..!’ akajiuliza Maua, akavua miwani yake, huku akijisikia, kama kusinzia sinzia, na kichefuchefu, akainuka na kuangali kalenda ukutani, akahesabu siku, akatizama chini, halafu akasogea dirishani, na kuangalia nje, kwani alisikia mngurumo wa gari nje, na hii ilimuashiria kuwa dereva amekuja kumchukua ili akawahi darasa na mambo mengine hii imekuwa ni ada yake baada ya kupata kazi ya muda toka kwa watalii wale aliokutana nao huko mbuga za wanyama za Manyara, anaamuka asubuhi sana, anawahi ofisi yao ya muda, huko anakutana na ratiba ya siku na huenda asirudi nyumbani hadi usiku….

Mkataba huu kati ya Maua na hawo watalii, ulikubalika hasa pale aliporudi toka Zanzibar, kwani pia aliweza kusome ualimu kidogo, akajichanganya kwenye elimu ya mitandao kama komputa, kwahiyo kazi kama hiyo ilikuwa rahisi kwake, akawa mwalimu wao wa Kiswahili, na pia mwalimu wa ukalimani pale inapobidi, na kwa vile wale wazungu walikuwa na mkataba wa miezi sita, ya kuanzia na huenda wakakaa zaidi wakiwa kama wataalamu watafiti wa lugha na tamaduni za asili, Maua akaona ni ajira nzuri kwake, kuliko kukaa tu na kutegemea ufadhili kwani ajira nyingine za kuajiriwa, alikuwa keshazikataa lakini hii ya muda akawa na hamu sana nayo, licha ya kuwa kazi hii ilikuwa ikichukua muda karibu wote wa mchana na hata wakati mwingine usiku.

Maua kifika ofisi yake hiyo ya muda anakuwa na ratiba ya darasani, kwani wanafunzi wake walikuwa kumi na mbili, na pia alikuwa ratiba aliyopangiwa ya vitendo ambavyo ilikuwa ni kuzunguka na hao wazungu huku na kule, ili kujua jinsi wananchi wa Tanzania wanavyoishi, wanavyoongea, na wanavyowasiliana, tamaduni zao nyingine na hata vyakula vyao na hali hii ailimfanya Maua asiwe na muda wa kukaa kwake siku nzima, na wakati mwingine anaweza kukaa nje siku mbili au tatu akiwa na hawo watalii, na kwahiyo hakuwa na muda hata wa kukutana na ndugu au jamaa zake.

Siku, wiki, mwezi ukapita, na ikawa mwezi wa pili unaingia, na hapo Maua akajihisi kuna mabadiliko mwilini mwake, ilikuwa ni kawaida yake tangu walipoona na Mhuja, aliweza kukatiza miezi mitatu, akiwa na hali kama hiyo,…na mwanzoni walihis kuwa ana uja uzito, lakini walipokwenda kupima akaonekana hana uja uzito wowote, na wala hana tatizo lolote baya la kiafya. Na hata alipoiona hii hali akaona ni tatizo lile, lila huja na baadaye hali hujirudia kama kawaida. Na pia kwasababu ya mihangaiko na pilika pilika za kila siku za kibarua chake hakuwa na muda hata wa kufuatilia afya yake, ila ule muda mchache anaokuwa yupo peke yake nyumbani, ndipo anapojishuku,na kuazna kuwaza, lakini haimchukui muda kwasababu ya kuchoka hukimbili a kulala, ili aweze kuwahi kesho yake…,

Mwezi wa pili ulipokuwa ukiishia, akajipa moyo kuwa bado mwezi mmoja, mambo yakiwa hivi hivi inabidi niende nikamuone dakitari, kwani hata hivyo, kwa jinsi alivyokuwa kajiachia mwili , kwa kutokujijali, mwili ulianza kunenepa, kitu ambacho hakukipenda,…unene ukawa unamnyemelea hadi akafikia uamuzi wa kuiunga na kikundi cha hawo hawo watalii ambao ni wanafunzi wake, wao ikifika jioni wanakuwa na mazoezi maalumu ya viungo hasa muda wa jioni,na hii ikamfanya kujiongezea pilika pilika za siku nzima na usiku huwa na kazi ya kuandaa masomo ya kesho yake…

Siku moja alikuwa na mapumziko kidogo, na siku hiyo ilikuwa kama ya mapumziko kwake, lakini alikuwa na miadi ya kutembeleana na wanafunzi wake, kama kuongea tu, lakini haikuwa ni lazima, kwahiyo akajiandaa na kabla hajatoka kuelekea kwenye ratiba yake, mara shangazi yake akaja kumtembelea na wakawa na masaa machache ya kuongea na ndipo shangazi mtu akahisi tofauti fulani kwa binti yake huyu, na kama watu wazima, ikabidi amhoji , …..

‘Maua mwanangu tangu murudi toka huko kutalii kwenye mbugana shemei yako nakuona umebadilika sana, kitabia na hata maumbile, na sikuelewi elewi kwani pia nakuona kama unanikwepa kwepa, sidhani kuwa ni kazi inayokufanya unikwepe au tusionane, kwani hata kunitembelea angalau nusu saa, ukanijulia hali, ingelitosha tu, na hata nikija kwako sikukuti, hebu niambie kuna nini kinaendelea, au kulitokea nini kati yako na shemeji yako, maana hata mahusiano yenu nayaona kama yamepungua, nikimuulizi kuhsu wewe anasema hajui kabisa ratiba yako, na anadai kila akija kwako hakukuti, nay eye ndiye aliyekuwa msimamizi wako,…?’ akauliza shsngazi.

‘Shangazi kwa kuuliza hivyo wewe una maana ulikuwa unafurahia mimi kuwa katika ile hali,… mimi nilichojitahidi ni kutafuta njia ya kuondokana na yale mawazo, ambayo nahisi yalikuwa yakinipeleka pabaya na juhudi hizo naziona kama zimeanza kuleta matunda, kwasababu ninapokuwa sina muda wa kupumzika, nasahau matatizo yote, …’akasema Maua.

‘Sio kwamba sipendi hilo, ila pia lazima nijue afya yako, ni lazima nijue, …na nikuulize kitu kimoja, wewe nasikia ulipokuwa Arusha ulidai kuwa ulikutana na Mhuja, ni kweli au si kweli…? Akauliza shangazi.

‘Mhuja…?’ Maua akawa kama kashituliwa na kitu, kwani hata ile gilasi ya maji aliyokuwa kashika ilimdondoka, na akawa katulia huku kakodoa macho akiwa anaangalia mbele tu, kama vile anatizama kitu cha kutisha,… ghafla akaanza kutetemeka, na mara akashikwa na kitu kama kizunguzungu, hata kabla shangazi yake hajamfikia kumdaka,akawa keshafika chini , na kupoteza fahamu. Shangazi alichanganyikiwa akawa anajuta kwanini aliongelea hiyo habari,..kumbe haikuwa vyema kuongela maswala yake yaliyopita, aheri angejinyamazia kimiya, lakini hakuwa anajua hilo. Akajaribu kumpa huduma ya kwanza mtoto wae huyo mpaka akazindukana, hakuwa na haraka ya kumpeleka hospitalini, moyoni alisema sio kila tatizo kumkimbiza hospitalini…

Alipozindukana, Maua akainuka haraka na mara akaangalia saa yake , na kumwambia shangazi yake anataka kuondoka, ana miadi na watu wake, na hapo shangazi yake akawa mkali, na kumuuliza kuwa hivi anajali sana hizo pilika pilika, kuliko afya yake, haoni kuwa hiyo hali siyo ya kawaida..
‘Shangazi hali hii ni ya kawaida kwangu, tangu Mhuja aondoke, nimekuwa nikitokewa hivi mara kwa mara…nahisi kizungu zungu , na baadaye fahamu hunipotea, na wakati mwingine nikiamuka najiona kama nilikuwa kwenye ndoto, na …nakumbk hata nilipokuwa Arusha ilinitokea hivi huvi na hata nikajikuta …sijui ni kweli au la, ila Maneno aliniambi anilitoka kabisa na kwenda porini..’ akasema Maua.

‘Na kwenda porini, kufanya nini, na huko maporini sikulikuwa na wanyama wakali....mnona unanitisha Maua…., hebu nielezee hiyo ndoto yako ilikuwa kuwaje…

‘Shangazi mimi sipendi kuongelea tena mambo yaliyopita, ila nakumbuka, nilikuwa kwenye njozi, nikahisi sauti ikiniambia nitoke nje haraka, nikakutane na Mhuja, niliposikia hivyo, nikainuka haraka haraka, ilionekana kama ilikuwa nasubirii kupewa taarifa hiyo, na nikatoka nje,…’ akasema Maua.

‘Sauti hiyo ilikuwaje, …ni sauti ya kiume au ya kike, na …hebu nifafanulie vyema hapo…?’ akauliza shangazi

‘Siwezi kukumbuka vyema ni sauti ya kiume au ya kike, na haiwezi kuelezeka, inakuwa kama hisia , lakini hisia za kuamrishwa nifanye hivyo…’ akasema Maua.

‘Na kwanini ulipofika siku ile hukunihadithia hayo yote Halafu ikawaje…?’ akauliza shangazi

‘Shangazi mbona hinielewi , ninachojaribu ni kujisahaulisha, kwahiyo, mimi nilichukulia kuwa ilikuwa ni ndoto, ingawaje Maneno alisema kweli nilitoka, ..’ akasema Maua.

‘Sawa baada ya hapo ilikuwaje…nieleze kila kitu unachokumbuka, ili name nijue jinsi gani ya kukusaidia..’akasema Shangazi mtu.

‘Nilitoka nje, na nikawa nafuatilia hiyo amri ambayo naiita sauti, nikawa naamrishwa pita hapa kata kushoto…tukatembea wee, na wakati natembea, sijui nitambea wapi, wakati mwingine unajiona kama uanelea wakti mwingine unajikwa kabisa kwenye kitu kama majani,lakini hudondoki chini…mpaka tukafika mbali, na baadaye nilikuwa kama mtu aliyechoka, tukapumzika, katika ile hali ya kupumzika, nikawa kama nimezindukana toka usingizi wa kwanza…’ akasema Maua
‘Usingizi wa kwanza..?’

‘Ndio shangazi, wewe siunaweza ukaota ndoto ukaota kwa kujiona kuwa unaamuka kumbe bado upo kwenye ndoto, ukafanya shughuli nyingine, halafu ukasema ngoja nikalale, lakini yote hayo yanafanyika ukiwa kwenye ndoto…na ndivyo ilivyokuwa, niliota kuwa nimezindukana na kujiona nipo porini, katikati ya pori nene, kote mitimiti, halafu kumetulia, lakini sio kutulia kabisa , kulikuwa na sauti za kutisha tisha za usiku….nikawa nababaika nifanye nini. Nilitulia kidogo, halafu nikajipa moyo kuwa hapo hapanistahili kukaa, nikaanza kutembea kufutilia sehemu zenye uwazi, nikiwa nahisi kuwa nitafika nyumbani kwangu…’ akatulia Maua na kuangalai saa yake.

Shangazi yake akamwangalia kwa makini na kumwambia Maua ‘Wapigie simu hawo watu wako waambie kuwa hutakwenda huko leo…kwani tukimalizana hapa tunakwenda kumuona dakitari bingwa wa masuala haya…’ akasema Shangazi mtu.

‘Shangazi umeanza …mimi nimegundua dawa yangu ni nini, ni kujibidisha katika kazi zenye kunifanya niyasahau haya machungu yanayonikabili, wewe sasa unataka kunifanya niwe mgonjwa, na sitaki kuwa mgonjwa…nakuomba shangazi usinirudishe tena nyuma, huko kwa huyo dakitari siendi….’ Akasema Maua.

‘Maua mimi ni shsngazi yako, mimi mwenyewe nilikuwa nimefikia hatu ahiyo kuwa usiende huko kwa madakitari, haya maswala tunayatafutie ufumbuzi mwingine, lakini nahis kuna mabadiliko mwilini mwako ambayo , yanahitaji vipimo,na hili halitakiwi kusubiri….nakuomba sana, …jiandae twende tukamuona huyo dakitari, maswali mengine niachie mimi…’ akasema Shangazi mtu na Maua hakuona haja ya kubishana tena na shangazi akawapigia simu watu wake kuwa hatakuwepo leo, na baadaye akajiandaa wakaondoka kwenda kumuona dakitari bingwa.

Maneno akiwa nyumbani kwake, alijiona hayupo katika hali ya kutulia, alikuwa akijiulza mengi kichwani, alikuwa kaacha njia panda na alikuwa mara kwa mara mtu akigonga hodi anajua ni maaskari wamekuja kumkamata. Alikumbuka vyema siku ile alipoachana na shngazi wa Maua alivyomuacha kwa hasira akimwambia kuwa anakwenda kwenye vyombo vya usalama kuhakikisha kuwa anachukuliwa hatua kwa tendo alilolifanya.

‘Shangazi kwa kweli mimi najutia sana kwa kitendo kile, na kama hiyo itasaidia naomba ufanya hivyo, ili mioyo yenu iridhike, kwani nakiri nimetenda kosa ,ingawaje pia nakiri kuwa kosa hilo nililitenda nikiwa sipo sawa, sijijui kabisa…lakini nani utamwelezea akuelewe, hakuna…kwahiyo iliyobakia nikujitolea hata kufungwa ili mnisamehe, ili mioyo yenu iridhike…’ alasema Maneno, lakini sngazi alikuwa keshaondoka.

Kesho yake alifika kwa Maua akakuta hayupo, akajaribu kumpigia simu ikawa haipatikani, na anavyojua simu ile ilikuwa mpya, kabisa, simu ile alipewa na hawo watalii, ni zile simu imara kabisa ambazo chaji yake inaweza kukaa hata siku nne bila kuchajiwa …kwahiyo inaweza kuwa kaizima …kwasababu inasema kabisa simuu unayopiga haipatikanii kwa sasa…au kabadili namba, na kwaninii abadili namaba bila kumwambia, haiwezekani, …alikuja karibu kila siku lakini hakumkukuta na taarifa aliyoipata abadaye ni kuwa anafanya kazi na wale watalii.

Na siku moja akakutana na shangazi wa Maua wakasalamiana na baadaye wakajikuta wakiongea, na kinyume na alivyotarajia maneno, kuwa akikutana na huyu shangazi atakuwa kamkunjia uso kamnunia kama adui yake, lakini alishangaa kumuona shangazi anaongea naye ki kawaida bila jaziba, na baadaye akajikuta akiulizwa swali la kumshangaza, swali ambalo hata yeye alitaka kumuuliza shangazi huyo, aliulizwa kuwa Maua yupo wapi, naye akajibu hajui, hana mawasiliano naye…takribani tangu warudi toka Manyara, akaongeza kusema kuwa anashangaa kuwa hata simu inakuwa imezimwa au kabadili namba ya simu, na hata akamuuliza Shangazi kuwa anajua lolote kuwa Maua kabadili namba ya siku yake, shangazi akajibu kuwa hajui, ingawaje kweli alikuwa kapewa namba mpya na Maua ambayo alipewa kwa masharti kuwa asimpe mtu yoyote ile namba hata Maneno kwani ni namba yake ya kazini.

Kila wanapokutana na shanagazi yake huyu mazungumzo yao lazima yaende hadi kugusia yale yaliyoyotokea kule Arusha, na hata leo walipobahatia kukutana, na hata pale walipojitahidi wasililiongele hilo swala tena yeye Maneno mwenyewe alijikuta akijitumbukiza kwa kuliongelea kinyume na alivyokuwa kaahidi moyoni mwake, na kujikuta akianza kujitetea kuwa hakumbuki kuwa alimshika shika kumlazimisha kabisa, ilitokea akiwa usingizini na kujikuta walikiwa wamekumbatiana na moja likazaa jingine….

‘Hebu nikuulize, Maua alikuita uje ulale kitandani mwake, au ilikuwaje ukaja mpaka ukalala pembeni yake…halafu ukatimiza matamanio yako.,,? Akauliza shangazi mtu
Maneno akasononeka moyoni, kusikia maneno yale toka kwa shangazi, akajitahidi kuwa na subira na kusema, ‘Wakati nilipohakikisha kuwa kalala,…naweza kusema hivyo, kuwa alikuwa kalala, nikawa naondoka pale kitandani, ukumbuke nilimbeba mimi hadi kitandani kwake, nikamlaza, na kuhakikisha kuwa katulia na yupo salama,… na wakati nataka kuondoka, mara mkono wangu ukashikwa,…..’ akasema Maneno.

‘Alikushika na kukuvutia kwake, au alikushika tu…na alikuita njoo Maneno, au shemeji usiniache, naogopa au kitu kama hicho, njoo tulale na je aliwahi kutaja jina Mhuja?’ akauliza Shangazi
‘Nakiri kuwa alinishika tu, sio kwa kuning’ang’ania, hapana alinishika tu…na ndio nakumbuka alitaja jina, lakini sina uhakika kuwa alitaja Maneno, au shemeji au…sina uhakika kama alitaja neno… Mhuja’ akasema Maneno

‘Kwahiyo wewe kwa kukushika mkono ukaona kakuribisha ulale naye au sio…? Ukaona nafasi ndiyo hiyo, ile nafasi uliyokuwa ukiingojea ili utimize malengo yako, hivi wewe huoni kuwa alikuwa kwenye ndoto, na kwa kukushika huo hakukushika kama wewe…?’ akauliza shangazi mtu kwa hasira
‘Sio hivyo shangazi, nilihisi kuwa bado ana wasiwasi ndio maana nikarudi tena pale kitandani kumpa imani kuwa nipo naye…’ akajitetea Maneno, lakini shangazi hakuwa na nia ya kusikiliza zaidi

‘Ina maana hata nyumbani kwake hujawahi kwenda…?’ akauliza shangazi
‘Nimewahi kwenda lakini simkuti, na unajua tena kazi yangu, muda kwangu ni finyu, lakini karibu kila siku ninayokuwa nipo hapa Dar napitia hapo kwake lakini simkuti, na najiuliza kwaninii hata asinipigie simu, kwasababu namba yangu anayo, sijui kabisa nimemkosea nini, naumia sana shangazi, na kama ulivyosema siku ile utanipeleka kwenye vyombo vya usalama, nasubiri ili nijikoshe, nidhibiwe ili hiyo dhambi initoke….’ Akasema Maneno hukuu moyoni akijuta na ingawaje kwa sehemu nyingine ya nafsi alikuwa akiona hana hatia,…

‘Wewe Maneno, hilo linafanyiwa kazi uchunguzi bado unafanyika, na kama itagundulika vinginevyo, kuna madhara yoyote umemsababishia binti yangu kwa tamaa zako za kimwili,…nakuahidi kuwa kama mimi sio shangazi yake,…nitakaa kimiya, lakini kama mimi ni shangazi yake niliyemlea huyo binti, nitahakikisha unajuata, wewe subiri tu, siku ukiona maaskari wanakugongea mlango ujue unaenda kuozea jela, wewe si kidume, kidume mjana sio, wenzako owanatongoza, wewe una…aaah, naona hata kinyaa kuongea na wewe…’ akasema na kuondoka zake.

Maneno yale yalizidi kumuumiza sana Maneno nakujiona amezalilika sana…, akajipa moyo na kusema kimoyomoyo, na baadaye kwa sauti alipohakikisha kuwa shangazi keshaondoka, huku akiwa kapaangalia pale shangazi alipokuwa amekaa, kama vile bado yupo nakusema kwa sauti ya kingonge ‘Nimeshajuta shangazi, ingawaje …mmh, nitampigania Maua mpaka hatua ya mwisho, hata kama nikuwekwa jela nipo tayari, nitatumikia kifungo, lakini nikitoka nitahakikisha kuwa Maua, anakuwa wangu, huyo mimi nimekabidhiwa na Mhuja, huyo ni wangu….huyo ni wangueeee, na mimi ni wakeeee…hata kama watu watasema sana, mimi sintojali…yeye ni wangueee, na mimi ni wakeee’ akawa anaongea mwenyewe huku anaimba, wakati huo shangazi alikuwa keshaondoka.

Siku hiyo akiwa peke yake ndani, alihisi hali sio njema, alikuwa anahisi hatari, nywele zinamsisimuka, na hata akili yake binafsi ilikuwa haitulii,…akawaza kwa muda na baadaye akawaza kuwa ni vyema aende kwa Maua, na akimkosa atakwenda kwa shangazi yake,…na kama pia atamkosa huyo shangazi wa Maua, inabdia amtafute shangazi yake mwenyewe, amtumie yeye kama msuluhishi, na anahisi kuwa wakikutana mashangazi kama wazazi, huenda mambo yakawekwa sawa.., Akaona hilo ni wazo zuri, akaingia ndani na kuvalia vyema, halafu akatoka chumbani kwake na kukaa varandani, akiwa bado anatafakari hilo wazo. Na akiwa kwenye lindi la mawazo mara mlango ukagongwa, akainuka haraka akijua hao ndio maaskari wamekuja, wameshamuwahi kabla hajaweza kufanya alilolikusudia, akajijutia kuwa kwanini wazo kama hilo halikumjia mapema...! Oooh, sasa Maneno nimeumbuka, ingawaje nilishajua hawa maaskari watakuja muda wowote, lakini hapana, maisha ya jela, hapana, ….hapana, kwa jinsi nilivyohadithiwa…oooh, mungu nisaidie mambo haya yaishe kwa amani,…..

Akiwa anaanza kuogopa, akikumbuka jamaa yao mmoja aliyefungwa kwa kutuhumiwa tu , na hata awalipogundua kuwa hana kosa, akaachiwa, lakini afya yake ni tete, anakohoa mfulululizo, anajikuna kama oho nzuri, kakonda ile mbaya, …na akikuhadithia habari za huko hutoaamani kwenda jlea hata siku moja, sasa yeye ni zamu yake, alipowaza hilo zaidi akatizama mlango wa nyuma, akaona hapana kwanini niteseke kwa kitu ambacho nahisi sijafanya makusudi, akaaunagali ule mlango ambao ulikuwa uangongwa, halafu aakitazama mlango wa nyuma, akaanza kurudi kinyume nyume kuufuata ule mlango wa nyuma,…

Aliukaribia akasimama, akiwaza kitu anachotaka kukifanya, anatoroka kama vile ana kosa…hata kama hana kosa kwa hali ilivyo hakuna atakayemkubali,…lakini Maua na shangazi yake watamuonaje,… kwahiyo….nikafe jela kwasababu ya mpenzi, na je kweli Maua ananipenda, hilo sina uhakika nalo, na hata kama ataamua kunipenda, sijui kwa njia gani,…nikaenda jela kama nilivyomuahidi shangazi, .. je nikitoka jela, nikiwa hoi kwa magonjwa ya ajabu ajabu, Maua atanikubali kweli, sidhani,…akamuwaza huyo jamaa yao anayemjua aliyekuwa kafungwa kimakosa, akajiweka katika nafasi yake kuwa ni kama yeye, halafu ndio anakwenda kwa Maua kuwa nakutaka kukuoa…itahitaji moyo kunikubali…sasa nifanyeje,… na je nikitoroka ina maana kazi basi tena….
Je Maneno atachuku hatua gani, tuwepo

Ni mimi: emu-three

6 comments :

Precious said...

Mmmhhh kasheshe juu ya kasheshe...nawatakia w/end njema M3 na wadau wote wa blog ya Diary Yangu.

emu-three said...

Nashukuru sana Precious kwa kuwa mpenzi wa kwanza wa blog hii kutoa maoni katika sehemu hii ya 22, nakutakia na wewe wikiendi njema, pamoja na wapenzi wengine wa blog hii;TUPO PAMOJA

Pam said...

duh story yazidi kuwa na changamoto maskini Maneno ukarimu wake unampa tabuuu shangazi nae mikwala haya tuwemo.. Asante P kwa nice wish ya weekend iwe kwako pia...

Simon Kitururu said...

Mmmh kweli kasheshe! Ijumaa njema Mkuu!

Anonymous said...

Hiyo ni fortune mistake (kosa lenye bahati). Nampongeza Maneno sioni kwanini shangazi anaweka ngumu! Haya na tuone atamfunga kwa sheria gani. Maneno, Maua ni wako mwenyewe kama ulivyoimba. Mhuja alimwoa kwa makosa tu na ndio maana hakuishi!

Anonymous said...

Maneno wala usiogope kasi hicho simama kama mwanaume, sijaona kosa lako kabisa.Maua ni mjamzito kasheshe kwa shangazi sasa. Big up em three.