Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeMonday, September 12, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-25‘Sweetie, sweetie….mke wangu mke wangu…kwanini…..’ Sauti ikasikika ikiita Sweetie, mara mke wangu…, na sauti ile ilikuwa kama ndoto masikioni mwa Rose, ilishafikia hatua ya kuzoea ile hali, kwani ilikuwa sauti ya mara kwa mara kutoka kwa mgonjwa wake! Alikuwa mara kwa mara akilala hata mchana hupiga ukulele…na hali hii mwanzoni ilikuwa ikimsumbua Rose, akawa anatoka chumbani kwake haraka kueleeka varandani kumangalia mgonjwa wake ananini…lakini kila mara akifika alimkuta kalala, ila anaopiga ukulele akiwa usingizini, na hivyo kujua ni ndoto zinazomkabili mtu kama huyu akiwa anajaribu kurejesha hali yake ya kukumbuka mambo yaliyopita, ambayoo hayakumbuki kabisa....

Leo sauti ile ilikuwa tofauti kidogo, ilionyesha kulalamika na kutoka kama mtu anatetemeka, hapo akaingiwa na wasiwasi na alivyokuwa akiita mke wake…akawa kavutika kujua huyo mke aanyemtaja ni nani….na mawazo hayo alikuwa akiyawaza akiwa kwenye usingizi wa kimang’amung’amu, ndipo ghafla akazindukana nab ado ile sauti ya kuita mke wangu , sweetie…ilikuwa ikiendelea, na haraka haraka akatoka pale kitandani bila kujali kuwa alikuwa kavaa nguo nyepesi tu za kulalia akakimbilia varandani na haraka akakaribia pale kwenye kochi alipolala mgonjwa wake ....

Akamuona kweli hali yake sio nzuri, kwani alimkuta akiwa anatetemeka baridi , akamshika na shavuni na kumkuta akiwa na homa kali…na kabla hajaamua afanye nini, mara yule mgonjwa akainuka na ghafla akamshika mkono wake na kumvuta pale alipolala, …kwa vile kitendo kile Rose hakukitegemea akajikuta akimdondkea yule mgonjwa pale kwenye kochi, na kabla hajainuka kujiweka vyme, yule mgonjwa aka m ng’ang’ania kama kumkumbatia, ….na Rose akajua ni kwasababu yule mgonjwa anasikia baridi naye akamshikilia vyema ili kumsaidia kumpa joto...

‘Oooh, Sweetie mke wangu, mbona unataka kuniacha, kwanini unataka kunisaliti…kwanini , kwanini…najua umeshafikia hatua hiyo, kama umetenda kwa matendo, …naomba nisikia kauli yako pia mdomoni kuwa kweli umenisaliti….oooooh.’ Yule mgonjwa akawa anasema huku kamng’ang’ania kweli kweli Rose, mpaka Rose akawa kama anakosa hewa, na alihitaji nafasi ya kukaa vyema ilia pate hewa, lakini yule mgonjwa, alikuwa kamshika kwa nguvu sana....

‘Sweetie, hebu niachie kwanza ….huoni unahoma kali unahitajika nikupe dawa ya kushuka hiyo homa….hebu niachieeee, kwa kwa wewe vipi…’ akawa anahitajii kujiondoa katika kule kushikwa kwake , lakini ilikuwa kama kashikwa na kibano cha chuma, huwezi kujibandua, alijitahidi kufanya hivyo, ili ajiondoe kataika hicho kibano, lakini ilikuwa kazi bure mwishowe akasalimu amri na kutulia kimiya, akiwa na matumaini kuwa baaaye ataachiwa. Na kila muda ulivyokwenda ndivyo alivyokuwa akihisi lile joto la yule mgonjwa la homalilivyokuwa linashuka, na baaaaye alihisi kuwa joto limekwisha na kilichokuwepo ni jasho, lakini hata pale alipojaribu kujibandua ilikuwa haiwezekani kwani huyo mgonjwa bado alikuwa kamng’ang’ania Rose, huku akisema hataka kumuachia kwasababu anataka kumuacha na kwenda kwa msaliti mwenza….sijui ndio nani huyo....

Walikaa vile hadi wote walipopitiwa na usingizi, na asubuhi na mapema, Rose aliinuka pale kwenye kochi na alipogundua kuwa alikuwa kalala kwenye kochi na yule mgonjwa, na kulala kwenyewe sio kwa mtu na mgonjwa wake bali ni kama mtu na mke wake, akainuka haraka na kujiweka vyema, na kutaka kuondoka kurudi chumbani kwake na kabla hajaondoka akageuka kumwangalia mgonjwa wake alikuta wanatizamana.

‘Rose, kwanini unanidanganya….?’ Akauliza yule mgonjwa swali la ajabu kwake.
‘Kwanini ninakuanganya Sweetie…mbona sikuelewi, maana usiku kucha ulikuwa anapiga ukulele, nimekuja kukuangalia unansihika kama vile mtu aliyeota ndoto ya kustisha na anaogopa kulala peke yake, na ulivyoning’ang’ania, inatisha mpaka nasikia maumivu viungoni…una maana gani kuwa nakudanganya...?’ akauliza Rose.

‘Nimekuota na inavyoonyesha kabisa, …hiyo ndoto ilikuwa inajaribu kuinikumbusha kitu, na ni dhahiri kuwa mimi nina make, …nikawa najiuliza huyo mke ni nani na yupo wapi, mbona haji kuniona…? Lakini cha ajabu wakati najiuliza hivyo huyo mke akaja mbele yangu, akiwa analia na kudai kuwa mimii ndiye niliyemkimbia, nimemuacha mwenyewe….na wakati anaongea, mimi nilionekana kuwa nimelala, yeye kasimama, kwahiyo sura yake usoni nilikuwa simuoni, na ndipo nikainua uso vyema kumwangalia….’ Alipofika hapo akamwangalia Rose, kwa macho ya hamasa….akasema ` Hutaamini mke niliyemuona kwenye ndoto hiyo….ana sura yake ilikuwa kama yako, sidhani kuwa ndoto hiyo imekuweka wewe kwasababu nakufahamu…;

Rose akatabasamu, na moyoni akawa anawaza ….kwanini huyu mtu akamuota mke wake na hata afikie kumfananisha na yeye….je hiyo ndoto inamaanisha nini,…inawezekana kweli kwasababu ya kukosa kumbukumbu atakuwa kamsahau mke wake, kama yeye mwenyewe hakumbuki jina lake, sembuse kumkumbuka mkewe… alipowaza hivyo akamtizama yule jamaa ambaye alikuwa naye bado anamtizama.

‘Kwahiyo ina maana kuwa una mke kweli, na wewe unamaanisha kuwa mimi ndio mke wako, nimeamua tu kukuanganya, ili iweje, ….?’ Akauliza Rose.

‘Hapo na mimi ndio nashindwa kuelewa, ili iweje, labda ni ndoto tu…lakini kwa jana, kila nilipoamuka najikuta naota ndoto hiyo hiyi, inajirudia kwa mtindo tofauti tofauti….. , na huyo mke niliyekuambia kuwa nimemuona alikuwa na sura kama yako wewe, sehemu nyingine sio sura ya moja kwa moja, lakini kila nilipohakikisha namtizama machoni namgundua kuwa ni wewe,…kwa maumbo kunaweza kuwa tofauti tifauti, yeye anaonekana kuwa ni mnene kidogo kuliko wewe, ila kisura mnafanana kabisa …lakini wakati mwingine mnakuwa sawa kwa sawa kila kitu, kama mapacha, labda uniambie kuwa mpo mapacha….au akweli labda mpo mapacha, hebu niambie umezaliwa peke yako kwenye familia yenu…?’ akasema yule mgonjwa.

‘Mapacha…..!’ hapo Rose akashituka, na kujaribu kukumbuka kitu, …alishawahi kuambiwa hivi siku moja, lakini ni muda kidogo, na aliyemwambia hakumuamini sana, aliua kuwa ni mbinu za wanaume za kutafuta uchochoro wa kuongea, mtu huyo alimwambia aliwahi kukutana na msichana wanayefanana naye sawa sawa…..! Alikumbuka kabisa mtu huyo alimuulizia kwa kusema kuwa `nyie mpo mapacha…’

Alijaribu kukumbuka historoa ya familia yao ambayo haijuizaidi ya kumjua baba na mama yake, lakini wahawajawahi kumwambia lolote kuwa ana ndugu mwingine, na wangeliongea saa ngapi, wakati wao wapo katika shughuli zao, na hata muda wa kukaa nao tangu alipokuwa mkubwa hajawahi kuupata. Wazazi wao ni wafanya biashara, na muda mwingi wanasafairi, na yeye shule soma yake ilikuwa shule za kulala tangu akiwa mdogo….hata hivyo kama kungelikuwa na ndugu yao mwingine angelimjua…lakini hata hivyo kwa kumbukumbu zake mtu aliyemuuliizia hivyo sio wa hapa nchini, akajaribu kumkumbuka huyu mtu alikuwa nani!

Baaaye sana akakumbuka kuwa mtu huyo alikuwa sio wa hapa nchini, ilikuwa ni semina moja ndani ya nchi ya jirani, na wakati wapo hospitalini wakifanya matembezi mbalimbali, alikutana na Docta mmoja ambaye alimganda sana, akawa anataka urafiki nay eye, na katika kuongea naye huyo octa alimwambia kuwa anafanana na mtu anayemjua, na wanafanana sura sawa kabisa, kama mapacha, akataka kujua kuwa ana ndugu yoyote anayeishi hata nchini, lakini hakuwa naye , kwahiyo aliona kama ujanja ujanja wa yule mtu wa kutaka kuongea naye….

‘Kwakweli mimi sina pacha mwenzangu, nimezaliwa peke yangu, kwahiyo hilo lisiwepo akilini mwako Sweetie…’ Rozi akamwambia mgonjwa wake, huku akizidi kutafakari kuhusu hilo kuambiwa kuwa anafanana na mke wa huyo jamaa. Ina maana kumbe huyu jamaa ana mke wake, na mbona imetokea kuwa karibu sana naye na kuhisi kuwa anavutiwa naye, na hata kutamani kuwa angelikwua yeye ndiye huyo mke anayemuwaza….akawaza sana Rose.

‘Sasa kama huna pacha, kwanini nimuote mtu mnayefanana naye sawa kwa sawa…basi kwa mpangilio huo ndio maana akilini mwangu imefikia hatua ya kuwaza kuwa wewe ndiwe mke wangu, ……lakini swali linakuja baadaye kuwa kama wewe ndiwe mke wangu kwanini unifiche!’Akasema yule mgonjwa na kusogelea dirishanii akawa anaangalia nje na kumpa Rose nafasi ya kutafakari yale aliyoyasikia na akawa anahisi kuwa huyu mgonjwa sasa akili inaanza kumrejea kidogo kidogo…na akawa na shauku kubwa ya kutaka kumuuliza maswali mengi, lakini kila swali lililomjia akilini, aliliona halifai kwa muda huo, na baadaye akamuuliza;

‘Hebu nikuulize, kwa akili yako, wewe unahisi kuwa wewe ni mzaliwa wa nchi hii….?’ Akauliza Rose.

‘Hilo swali nimekuwa nikijiuliza hata mama akilini, ..lakini kama sio mzaliwa wan chi hii, basi nafanya nini hapa, imetokeaje nikaja hapa…nilikuwa natalii…nilikuwa na…na….hapana lazima kuna sababu na kama ni mzaliwa wan chi hiii mbona sina ndugu….ina maana kwelii nipo peke yangu, yanwezekana kuwa hivyo, lakini watu wote wasiniue …haiwezekani?’ akawa anaongea kwa kujiuliza maswali mengi na huku akiwa anaangalia nje. Akawa anatizama mandhari ya nje, kama vile ndio mara ya kwanza kuyaona, akajaribu kuyaunganisha na yale aliyoyaona kwenye ndoto, lakini kila alipounganisha aliyaona kuwa yanatofautiona….!

‘Hata kwenye ile ndoto mandhari niliyoyaona kule yana utofauti na mandhari ya hapa…hasa kwenye ndoto ya jana, ilikuwa sio kama zile ndoto zenye utata zilizotangulia na zakunitia kiwewe…hii ilikuwa imetulia na kuelezea jambo linaloonekana lina ukweli, yenyewe ilikuwa kama inaonyesha hali halisi….maeneo tuliyokuwepo na huyo anayeonekana kuwa ni mke wangu yanaonyesha kabisa ni nyumbani kwangu…na hata huyo mke wangu alipokuja kunilalamikia kuwa nimemuacha peke yake ilionyesha kuwa yeye katokea chumbani na kunikuta mimi nimelala kwenye kochi, na kochi hilo sio kama hili…yeye alitokea chumbani na kuanza kunilalamikia kuwa nimemuacha, kwanini nimuache…ndio labda ni kwasababu ya ndoto, lakini kwanini mimi nililala kwenye kochi na yeye akalala chumbani…inaleta picha kama hii hapa, wewe umelala chumbani na mimi nimelala kwenye kochi , lakini mandhari yapo tofauti kabisa…’ akasema yule jamaa.

‘Kwa mtizamo wako, kwanini huyo mke wako akawa anakulalamikia hivyo…, mlikuwa na msuguano, mlikuwa hamuelewani…kwanini ifikie umuhame chumbani?’ akauliza Rose.

‘Nimeliwaza hilo, kwanini nilale sebuleni yeye alale chumbani, ….sidhani kuwa nilikuwa na msuguano na yeye, labda ni kwasababu ni ndoto ambayo mara nyingi huletea taswira ile iliyopo mbele yako, taswira uliyokuwa ukiiwaza au inayokuzunguka, halafu hukupeleka huko inapotaka kukuonyesha jambo,…na kwa mahesabu mliyonipa tangu nifike hapa ni karibu mwaka na kitu, au sio…au hata miaka miwili inakaribia au sio, ….kwa hali kama hiyo inaashiria kuwa hata kama wangelikuwa ndugu zangu watakuwa wamekata tamaaa na mimi…na hawo nugu zangu ni akina nani, wapo wapi?’ akauliza yule jamaa.

‘Hilo nalo swali, maana mimi nimejitahidi kupeleleza kila kona, kila mahali ninapopajua kwenye nchi hii, lakini hakuna hata mtu mmoja aliyewahi kuiona sura yako, imefikia hadi nikapeleka tangazo na picha yako kwenye vyombo vya habari kutangaza, lakini hapajawahi kutokea mtu kudai kuwa anakufahamu au kumuona mtu kama wewe…kwahiyo wewe huna nddugu, huna mke kama unavyodai, umetokea kusikojulikana…ndio maana hata kipindi kile maaskari walikuwa wakikuhisi vibaya, na ulikuwa ukiongea mananeo ya Kiingereza’ akasema Rose.

‘Hahaha…labda nimedondoka toka mbinguni, labda….., lakini mimi nina imani kuwa nina ndugu, na huenda nina mke na mke hyo huenda anafanana na wewe kama sio wewe …..’ na mara wakasikia mlango ukigongwa, na Rose akaenda kuufungua huo mlango ambao ulikuwa umefungwa kwa ndani, na akawa anaongea na huyo mtu , yeye akiwa ndani na huyo mtu akiwa nje, na badaye akarudi akiwa na barua mkononi, hakuufunga ule mlango kwa ndani tena, aliurudishia tu….

‘Barua ya madai, inanitaka niwepo kwenye kikao cha wadhamini nikiwa na hela au …’ akashinwa kuongea zaidi huku kaishikilia ile barua. Akilini alikuwa akiwaza jukumu kubwa aliloamua kulibeba, wema wake ambao hajui ni kwanini kaamua kuutenda, halafu aakmwangalia yule mgonjwa wake , na machozi yakawa yamemjaa machoni. Hapo yule jamaa akamsogelea na kua kusimama mbele yake, akainua mkono wake na kuyafuta machozi machoni kwa Rose. Rose akatamani ule mkono uendelee kuwepo usoni mwake, akawa anahisia nyingi amabzo hakuzitaka zimtawale akilini…

‘Inaniuma sana kuwa dunia hii kuna watu wema, lakini watu hawawathamini, watu wema mara nyingi, wanaishia kufahaika, kwani kutenda wema ni mtihani mgumu sana, na matokeo yake ni kuonekana si lolote, hasa pale wema huo unapolinganishwa na baya dogo, au na mambo mengine yaanayofamnywa na wengine, ambao sio kuwa wanatena, wema, ila wanafnya hivyo kutokana na nafasi zao…lakini kwa vyovyote iwavyo, wema hauozi…tena wema uene zako, ipo siku utalipwa tu…!’ Akasema yule jamaa, na mara akashuka mikono yake na kumshika Roze mabegani, akamsogelea na kuwa naye karibu kama vile watu wanaotaka kukumbatiana, lakini sio ile ya kushikana kabisa.

‘Nahisi wewe ni mke wangu, kila hisia zinanituma hivyo, natamani iwe hivyo, natamani ingelikwua ni kweli…lakini kama yupo mke wangu mwingine zaii yako, …atakuwa katika hali gani, kama kweli ananipena kwa moyo wake, anaweza akavumilia kukaa peke yake mwaka mzima…? Akauliza huku akimwangalia machoni Rose. Rose naye akawa anamwangalia machoni, na hisia zao zikawa mbali zaidi ya walivyotarajia, kwani ghafla walijikuta wameshikana, na kilichowashitua ni mtu aliyegonga mlango kwa fujo, na hata kabla hawajaachiana mlango uakfunguliwa.

‘Wo..wo…wo….kumbe ndio ujanja wako Rose…unajifanya umemleta huyu mgonjwa hapa, kumwangalia kwa karibu lakini nia yako ni …..utaniambia nini wakati nimewafuma moja kwa moja, ni kwa vipi docta akwa anakumbatiana na mgonjwa wake kama hivyo….mmmh, hata aibu hamna, hata kuachiana ahamtaki kama vile mumenataishwa an gundi….’ Ilikuwa sauti ya Docta Adamu, ambaye alikwua kasimama mlangoni huku kajawa na hasira, na hisia za wivu zilikuwa hazielezeki.

Rose na mgonjwa wake, walishituka toka katika hali ile waliyokuwa nayo, lakini cha ajabu hakuna aliyekuwa na wazo la kumuachia mwenzake, walikuwa wamekumbatiana na hawakuwa na lepe la aibu kuwa wanachokifanya ni kiteno cha aibu, na mara Rose akaonoa mikono yake toka kwa mgonjwa wake na kusogea nyuma, akapangusha macho yake huku akionyesha kutahayari kidogo, alimwangalia bosi wake na kujua sasa tatizo limekuwa kubwa, kama sio kutafutiwa njia za kufukuzwa kazi , basi watakuwa akianamwa na hata usalama wa huyo mgonjwa wake utakuwa hatarini.

‘Nilichoshuhuia hapa leo kimenipia picha halisi ya kwanini Rose umekuwa ukimtetea huyu mgonjwa, na siono kwanini tumuite mgonjwa….huyu…huyu….’ akasema Adamu huku anamnyoshea yule jamaa kidole na hasira alizokuwa nazo zilikuwa hazifichiki, ilionyesha hahiri kuwa kama atapata nafasi ya kufanya ubaya , hatasita kufanya hivyo, ila alikuwa anatunza heshima yake, asije akaleta sifa mbaya na majirani wa hapo.

‘Bosi nilishakuambia , maisha yangu hayakuhusu, huyu sasa hivi yupo mikononi mwangu, na nina uhuru wa kufanya lolote liwalo kwake, nikijua nini ninachokifanya, ….nakuomba useme lililokuleta uonoke kwani huu ni muda maalumu wa kumchunguza mgonjwa wangu….’ Akasema Rose huku akimshika mkono mgonjwa wake, na hapo kuzidisha chuki kwa Docta Adam. Adamu akaingia ndani akiwa na nina ya kufnya jambo baya…lakini simu ikakasikika kuwa kuna mesji imeingia, na alipoisoma ile meseji ikamfanya ashituke na hata kuanza kurudi kinyume nyume akisema;

‘Sawa kama umeamua kuwa hivyo, sawa, ….naona umeota mapembe, sijui unataraji nini kwa huyo mgonjwa wako….Sweetie wako….sawa, ila natumai batia toka kwa wadhamini umeipata, lengo langu kubwa ni kuja kjadili jinsi gani ya kulishughulikia hilo jukumu, kwani yaliyoanikwa hapo ni maneno mazito, ambayo yanahatarisha ajira yako…lakini nilichokiona hapa inaonyesha wazi kuwa umedhamiria, na sina jinsi ya kukusaiidia kwani mtoto akililia wembe mwache, ukimkata atajua hatari yake…..na nakuhakikishia kuwa …mimi kama sio docta mkuu wa hiyo hospitali, …utanikumbuka….utanikumbuka…’ akawa anaongea huku akionyesha uso wa chuki …na akatoka nje na kuufunga ule mlango kwa kishindo

***
Docta Adamu alitoka kwenye chumba cha mkutano na kuwaacha wadhamini wapate nafasi ya kumjadili, hali hii ilimuweka katika mawazo makubwa, akiwa anafikiria juhudi zote alizozifanya mwanzoni na kuwa anasifiuwa sana, zimefikia ukingoni, ina maana tenda wema mara 99, lakini ukitenda kosa moja kila kitu hakikumbukwi tena, hata hivyo kosa gani alilolifanya kama yeye…na kwanini tangu amuajiri docta Rozi amejikuta akiwa kwenye mitihani mikubwa, ni kwasabaabu yake, au ni kwasababau ya uzaifu wake wa kumpenda yeye…au ani kwasababu ya mgangano uliopo ndani ya familia yake, ambayo ilifikia hadi amuache mke wake….?

Akiwa hana nguvu kabisa, alitoka mle kikaoni na kushukuru kuwa angalau amepata nafasi ya kupumua, lakini hata hivyo aliona kuwa ni heri angelikuwepo mle na kujua nini kinachoendelea, maana sasa ndio hajuii kabisa watakuwa hawa wadhamini wameamua nini….akawa anayawaza yale mashambulizi yalivyokuwa yakitolewa, licha ya kuwa wengine walithamini juhudi zake lakini wapo wengine inaonyesha dhahiri wanampiga vita, ….akakumbuka jinsi gani hawo wanaompiga vita walivyokuwa wakitoa hoja zao za kumdidimiza…walikuwa wakimshambulia wazi wazi na hata kuonekana hawezi kazi kabisa, kila dondoo iliyosomwa ilimshutumu yeye, na hata kuzarauliwa kuwa utendaji wake haufanani na cheo chake. Na hata kila alipojaribu kujijitetea alijikuta kama ndio anajitia matatani.

‘Hebu angalieni mafaili ya hawa watu waliotibiwa bure, na gharama nyingi zimetumika kwa matibabu yao, je hii hospitali ni ya serikali, hii hispotali ni kutoa cha kutoa misaada, …tunakuuliza wewe Docta Mkuu, kama ulianzisha kuwa iwe hivyo, kwanini usingeenda huko serikalini ukaomba kuwa hospitali hii ni ya kutoa misaada…hebu tuambie nini lengo lako la kufanya hivyo, je gharama za matibabu hayo ni nani aliyejidhamini, na kama wapo mbona hawalipi…?’ wakaja juu wadhamini na wadau wa hospitlini hiyo.

‘Nimechunguza sana majalada ya wote waliotibiwa bure na nimegundua kuwa wote walipitia kwa huyo msaidizi wake…Docta Rozi, na hata mafaili mengine ameweka saini ya kudhamini, kuwa talipia, inaonyesha kuna kitu kinaendelea hapa kati yako na msaidizi wako, je ni nani wako huyo kuachilia maswala ya kikazi, ni ndugu yako,au mna mahusiano ya kimapenzi ndani ya kazi, maana hatuoni msingi wa yeye kufanya aliyofanya kwa kujiamini kiasi hicho….tunaomba maelezo yanye kujitosheleza, vinginevyo, sisi tunatoa dhamana zetu, na ikiwa ni hivyo gharama zote itabidi uzibebe wewe, na ujue kama tutaenda kisheria, …..’ akasema mmoja wa wadau na hakumalizia hatua hiyo.

‘Kwanini tusimuite huyu Rozi kwenye kikao maalumu, tukamhoji na….kama hafai aondolewe, maana kikao kilichopita tulishapitisha azimio hilo, kuwa madakitari wote watakaoajiriwa hapa lazima wafuate taratibu za hospitali binafsi, kuwa hospitali hii sio kituo cha kutoa huduma za bure, na kama ikitokea hivyo, lazima taarifa zifikioshwe kwa wadhamini, wakipatikana watu wa kutosha kujitolea kulipia gharama hizo nipo mataibabu hayo yafanyike, na kama ni mgonjwa wa dharura, lazima dharura za mawasiliano zipatikane, je hawa wote walifuata taratibu hizo, n nani aliwadhamini hawa watu….hebu taumbie Docta Adam….? Akasema mdhamini mwingine.

Baada ya majdala wa muda, wajumbe waliomba Docta Adam atoke nje ya kikao ili wapate kumjadili vyema, na uchunguzi wa kina ufanyike, na hilo likakubaliwa na kumwamuru Docta Adam atoke nje kikao! Na kama ataitwa kujitetea, au kama hataitwa leo ataitwa siku nyingine, ila waliamua kumpa nafasi ndogo ya kujitetea...hata nafasi hiyo aliyopewa kujitetea alishindwa aongee nini cha zaidi kwani yote aliyokuwa kajiandaa kusema alishayasema awali

Docta Adamu alisimama na kujaribu tena kujitetea, lakini hakuambulia huruma, na yote aliyoongea yalionekana ni udhaifu wake na kutokuwajibika kwa jukumu alilopewa na hapo kikao kikamwamuru atoke nje, ili wao wapate nafasi ya kuteta bila kuwepo, na uchunguzi mkubwa ufanyike, ili kuangalia ni kwanini hayo yote yamefanyika, na hata hivyo kikao hicho kilitoa miezi mitatu ya kuhakikisha kuwa gharama zote zimelipwa na kama hazijalipwa awe amewapata wadhamini, na kama hakuna wadhamini, aandike barua ya kuwa kashindwa kazi, ili atafutwe mtu mwingine….

Docta Adamu aliondoka pale na kurudi ofisini kwake, na alipofika alishindwa kuvumilia, akaamua kuwa alzima akamuone Rozi, kwani kajitolea kwa ajili yake, na makosa yote yaliyofanyika yametokana nay eye, kwa kujifanya ana huruma, wengi wanaodaiwa ni yeye alipitisha kuwa huduma itolewe, na hata huduma ilipotolewa, hakuaweza kuwapata wadhamini, na baya zaidi wakikutana na bosi wake huyo humdanganay kuwa keshawaona wadhamini, lakini hakuwa na nyaraka zozote ambazo wanaizinisha hawo wadhamini, ….alijitahidisana kufuatilia baadhi yao na hata kupunguza punguza hizo gharama, lakini wakati yeye anafanya hizo juhudi bado mwenzake alikuwa akiongeza malimbizko ya watu wanaotibiwa bila malipo na bila wadhamini….

‘Huyu mtu nimembeba vya kutosha najua ni docta mzuri, na tukimkosa huyu mtu, itakuwa shida sana kumpata mtu kama yeye, lakini lazima aheshimu taratibu za kazi, inavyojionyesha ni kuwa mtu huyu bado anazile hulka za hospitali za serikali, lakini mbona ameondoka huko muda mrefu, na kama mtu anayejali sheria za kazi huwa anabadilika mara moja kutokana na sheria mpya, sasa kwanini inakuwa kinyume kwa Rozi….akawaza hadi kufikia kuamini kuwa huenda anafanya hivyo kwa vile kaweka swala la mapenzi mbele….….

‘Kwanini Rozi hataki kubadilika, nimejaribi kumbadilisha lakini haelekei, inafikia hata kunidharau…hapana lazima sasa nimbadilikie……lakini nikifnaya hivyo huenda ikawa sababu ya kukataa ombi langu, name nampenda sana, nataak anikubali niwe mume wake,…sasa nifanye nini, maana nimekaliwa kooni na hawa wadhamini,….ngoja huko kwake ,niende nikaongee naye, kama atakuwa yupo na mimi basi sio mbaya kwa inzi kufia kidondani, lakini ni kama…kama kweli atanithamini na kukubali maombi yangu, vinginevyo nitanawa mikono yangu, maana huwezi kuumia kwa ajili ya mtu asiyekuthamini…basi sina jinsi….akubali awe mke wangu, au ashike hatamu zake ….ooh, .ngoja nikamuone kwanza,…’ akafunga ofisi na kundoka kuelekea kwa Rozi, bila kujali kuwa huenda kikao kikamuita, alikuwa keshaamini kuwa kutokna na majailiano yale , hawataweza kmuhitai tena…

Alipofika maeneo anapoishi Rozi , alikuta ukimiya na hali hii ilimpandisha zile hisa za wivu, akasogelea mlango na kujaribu kuskiliza kwa ndani, alishangaa sana mabadiliko hayo, kwani mara nyingi akifika hapo anakutana na redio ikiongea kwa sauti au mziki ukiwa nalia kwa sauti kubwa…lakini leo alikuta tofauti hata kwa rafiki yake ambaye walikuwa kama wanashindana kuliza redio zao…leo kote kulikuwa kupo kimiya. Mwanzo alianza kwa kugonga mlango kwa taratibu, lakini hakupata jibu, na hapo zile hasira za chuki alizozipata kikaoni zikaanza kujirudia tena, alikuwa keshahisi kuna kitu kinaendelea humo, kwanza alijiuliza moyoni huyo mgonjwa anayekaa humo analala wapi na Rozi analala wapi….akasema leo lazima ajue na ikibidi lazima afanye juhudi za kipekee kuhakikisha kuwa mtu huyo hakai humo ndani, lazima amtafutie huyo mgonjwa sehemu nyingine….

Alipoona kupo akimiya akagonga kwa hasira kwa nguvu, na alipoona hakujibiwi kitu akaufungua ule mlango, ambao ulikuwa haujafungwa kwa ndani na ulipifunguka, alijikuta akikosa nguvu, alijikuta akitahayari, alijikua akiviimba kifuani kwa hasira, na altamani kufanya jambo ambalo lisingesahaulika, lakini alijizuia ….na hata alipiojizuia, bado majibu aliyoyapata mle ndani yalimzidisha ile hasira aliyokuwa kaificha…na kabla hajafnya baya zaidi akasikia maeseji ikiingia kwenye simu, na alipoisoma akaona anahitajika kikaoni haraka……

NB KISA HIKI KIMETOKEA KIPINDI CHA AJALI YA MV BUKOBA, NA KWA SIMANZI KUBWA SANA, TUKIO HILI LIMETOKEA TENA HUKO ZANZIBAR, BLOG HII INATOA POLE SANA KWA WENZETU , NA TUPO PAMOJA KATIKA MSIBA HUU MKUBWA WA TAIFA HILI, MUNGU AWAPE SUBIRA WALE WOTE WALIOPOTEZA NDUGU ZAO NA TWAMUOMBA MWENYEZI MUNGU AWALAZE WALIOTANGULIA MAHALA PEMA PEPONI, `INALILLAH WAINA ILAH-RAJ'UN'


Ni mimi: emu-three

10 comments :

samira said...

kisa kimenoga ila rose namuhurumia mapenzi yake ni ya mda jamaa akirudisha kumbukumbu atamkimbia tu
m3 thanks na pia msiba ni wetu wote ilobaki tuwaombee walotangulia mbele ya haki kwa ajali hii ya meli
m3 leo vipi kazi zipo kama kawaida nilisikia rais katangaza siku 3 nijulishe pls

emu-three said...

Kweli Samira huu msiba ni wetu sote, kilichobakia ni kuwaombea waliotangulia wapate makazi mema peponi. Siku tatu za maombelezo ni za kupepea bendera nusu mlingoti sio za mapumziko,tupo kazini kama kawaida

Pam said...

pole kwa waliopoteza wapendwa na mungu awatie nguvu majeruhi wooote wapone haraka..

samira said...

thanks emu 3 kwa kunijulisha god bless you

emu-three said...

Nawashukuru sana Pam na Samira kwa kuwa pamoja nami. Meseji hii nimeiandika kwa kutumia simu ya kiganjani nikiwa kitandani afya kidogo imetetere. Hata hivyo tangu asubuhi hadi hii jioni hakuna umeme ndio twaenda kununua mishumaa hivyo.

Yasinta Ngonyani said...

Nilikuwa na mikikimikiki mingi mno na leo naona angalao pole sana kwa kutetereka. Na pia nami nasema ni kweli ni msiba wa wote/TAIFA nzima.
Mwenzangu Rose hapa namuhurumia mmmhh ngoja nisendelee na niona nini kilitokea....

Precious said...

Kwa kweli ni msiba mkubwa tena ukiangalia unaendena na riwaya yetu ya Akufaaye kwa dhiki ndio rafiki wa kweli..Mungu awape nguvu wafiwa na majeruhi na wapumzishwe kwa amani waliotangulia mbele ya haki mbele wao nyuma sisi. M3 pole sana Allah akuponye haraka uendelee na libeneke.

Anonymous said...

Poleni wa Tanzania wote kwa ujumla wa bara na visiwani, mungu wape faraja ya kweli wote waliopatwa na msiba huu moja kwa moja. Tuko pamoja, nahisi huyo mgonjwa ni mhuja alisombwa na maji kipindi cha ajari na kapelekwa nchini Uganda, pole kwa Rose maana yanayomwandama sasa nashindwa hata kupata jibu atatatuaje, maana deni kubwa na kisha penda sweety ambae ana mke tayari japo hakumbuki vizuri. Du! no comment.

samira said...

pole sana m3 i hope u get well soon
na tatizo la umeme ndo linonifanya nisau sahau

emu-three said...

Nawashukuruni sana wapendwa nashindwa hata la kusema. Nimejituma hadi ofisini maana nisipofika ina maana sitaonana na nyie , angalau ofisi wana jenerata, licha ya mikwala yao ! Tupo pamojaNawashukuruni sana wapendwa nashindwa hata la kusema. Nimejituma hadi ofisini maana nisipofika ina maana sitaonana na nyie , angalau ofisi wana jenerata, licha ya mikwala yao ! Tupo pamoja