Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, August 4, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-9




‘Anaendeleaje huyo mgonjwa, wako …’Rose akasikia hilp swali likiulizwa tena nakumfanya apate nguvu ya kuinuka vyema kwani alikuwa kainama wakati anambusu yule mgonjwa shavuni, lakini macho yake yalikuwa hayajabanduka kumwangalia yule mgonjwa ambaye naye alikuwa kamwangalia bila kupepesa macho…mmmh, sasa nimumbuka, akajikuta akisema kimoyomoyo…na halafu akageuka kumwangalia yule aliyekuwa akimuuliza hilo swali kuhusu mgonjwa.

‘Naona…a.a..kuna matarajio kwani nilikuwa nataka kuhakikisha kuwa mapigo yanaenda vyema,…a..a, unajua docta…bosi… imefika hatua siamini haya mashine tena, inakuwaje huyu mgonjwa, maana, kama unavyoona kila kitu kinaonyesha kuwa kipo sawa, lakini…..’ kabla hajamalizia yale maneno akageuka kumwangalia yule mgonjwa na kumkuta kafumba macho yake kuonyesha kuwa bado kalala,..oh, akashukuru mungu.

‘Kama vipimo vinaonyesha kuwa kila kitu kipo sawa, haina haja ya kuvitilia mashaka,walioviunda walitumia akili nyingi sana, wewe unachofanya ni udhaifu wa kibanadamu tu kuwa `huamini’ unataka iwe unavyotaka wewe…atainuka tu, kinachotakiwa ni kufuatilia taratibu zote, dawa na kuhakikisha mnamchua mwilini ili damu itembee..,sipendi kukufundisheni hilo kwani najua unajua vyema kazi yako ila nilikuwa nataka kuongea na wewe ofisini kama umemalizana na huyo mgonjwa….’
‘Kama umemalizana na huyo mgonjwa….’ Kauli hiyo ilimfanya Rose ageuke kumwangalia bosi wake, ana maana gani, macho yao yalipokutana, bosi wake alitabasamu kidogo huku kamkazia macho halafu akatikisa kichwa kuonyesha kuwa alichosema ndio hivyo hivyo..

‘Sawa bosi ngoja nimuweke sawa halafu nakuja huko tuonane…’ akasema Rose

‘Sawa,…hakikisha unafanya hivyo….’ Akasema huku anaondoka taratibu akikagua vitanda vingine kwa macho,

Rose aligeuka kumwangalia yule mgonjwa pale alipolala na sasa alimkuta kafumbua macho, na yale macho yalikuwa yakipepesa-pepesa kuonyesha kuonyesha kuwa kuna uhai, akamsogelea pale kitandani akitabasamu, halafu akamwinamia yule mgonjwa kumtizama machoni. Na kabla hajamuuliza kitu yule mgonjwa akawa ndiye wa kwanza kutoa kauli, lakini alianza kwa kukohoa ili kusafisha koo, na hali hii ilimfanya Rose ageuke huku na kule kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayewaangalia…akasema`Sweetie…’

‘Kumbe umezindukana …?’Rose akamuuliza

‘Sweetie,…..Kwani nipo wapi hapa…’ akasema yule mgonjwa

‘Kwanini unaniita Sweetie…?’ akamuuliza Rose

‘Kwani wewe sio Sweetie, sijui kwanini nakuita hivyo…kwani wewe ni nani…na mimi….mbona sie-sielewi kitu..aaah,.. nahisi kichwa kitupu kabisa, kama bua, hakijui kitu chochote…nahisi kama kichwa hakina kitu kama kopo tupu…sielewi, …mmh, …nisamehe sana, ila huo ndio ukweli, …umesema wewe unaitwa Sweetie…’ akasema Yule mgonjwa akihangaika kukumbuka kitu.

‘Wewe tulia tu, na ningeomba utulie haswa, kwani nimemwambia bosi wangu kuwa hujazindukana , ili upate muda wa kufikiri vyema….naomba uchukulie hali hii kuwa niya kawaida, tuliza kichwa chako,…unanielewa ninayosema…’ akasema Rose akiwa anamwangalai mgonjwa ambaye alikuwa kamkazia macho..kama anajaribu kumkumbuka, au bado yupo mbali kimawazo!

‘Sweetie….mmh, …..naona kama naota….nipo wapi vile, umesema wewe waitwa Sweetie ….?’ Akasema yule mgonjwa akijaribu kuinua kichwa, lakini hakuweza kabisa kufanya hivyo akajikuta anashngaa, na kumwangalia Rose.

‘Nimekuambia utulie kwanza, usiwe na haraka….mmmh, Mr nani vile…?’ akasema Rose na kujaribu kuulizia jina la huyo mgonjwa.

‘Mr Nani vile, ndilo jina langu hilo….?! Hapana sikumbuki kabisa kuitwa hivyo,…umesema naitwa nani…Mr Nani…sikumbuki jina hilo..labda…maana kichwa hakina kitu…nikuambie kitu…ili nijue nipo wapi naomba nitoke nje…, na nakutegemea wewe Sweetie, maisha yangu yapo mikononi mwako…nakuomba sana, unilinde, sijui kwanini nakuambia hivyo, ila nakuamini hivyo…..ila cha muhimu na cha kwanza nakuomba unisaidie nitoke humu, unipeleke sehemu salama…..naomba usiniache nikachukuliwa na …maji…na maji….mmmh, ‘ Alipotamka maji, akawa kama anashituka, na kugeuza macho huku na huku, halafu kasema `…humu ndani ya maji… sitakumbuka kitu kabisa, nipo kama naelea…najiona kama nipo ndani ya maji….hivi kweli tupo majini au …sielewi…samahani sana…Sweetie…nakupenda sana, usiniache…mke…aah, sielewi…’ Aliposema hivyo yule mgonjwa, akakunja uso….na hasa alipotamka hilo neno `maji’ akawa analirudia rudia, na baadaye akaanza kulalamika ….akisema;

‘Kichwa…..kichwa….nahisi kama maji yanaingia kichwani….kichwa…..aaaaah, maji, ….maji….nazama..nipo ndani ya maji,,,,kichwa…….Sweetie….mke…mmmh,… Mr Nani…..hapana. ….Sweetie……nazama..niokoe…niokoe, nazama….kwaheri mpenzi…’akaweweseka mara akazama kwenye usingizi…
Rose alipohakikisha kuwa yuke mgonjwa kalala tena kama kwanza, akachukua karatasi yake na kuandika kuwa mgonjwa alizindukana mara moja… halafu akaendelea kulala, lakini inaonyesha kuwa fahamu zimeanza kumrejea, anahitaji uangalizi wa karibu sana…akaweka ile karatasi kwenye kumbukumbu za yule mgonjwa halafu akamwangalia yule mgonjwa kwa makini na alipohakikisha kuwa sasa kalala kama mwanzoni, akamsogelea na kumshika mkono wake, akauinua juu, halafu akauchilia taratibu, ulikuwa umelegea kabisa, akaangalia mashine inayoonyesha mapigo ya moyo, …akaona kila kitu kipo shwari…halafu akainama kumkaribia usoni…akakaa hivyohivyo akimwangalia machoni, halafu kasema;.

‘Sweetie, nitakulinda usiwe na waswasi…’ halafu akahisi hayupo peke yake, kuna mtu nyuma yake, akainuka kwa haraka vile alivyokuwa kamwiinamia yule mgonjwa na kuguka nyuma na ghafla akajikuta wanaangaliana na Docta Adamu, na akawa anajiuliza moyoni huyu mtu amekuja saa ngapi. Docta Adamu hakusema kitu alichukua zile kumbukumbu za mgonjwa akamgeukia Rose na kwambia amfuate ofisini. Na Rose kwa vile alikuwa kamalizana na yule mgonjwa, akawa anamfuata nyuma bosi wake, na nesi ambaye alikuwa akifanya usafi akachukua nfasi yao kuhakikisha yule mgonjwa habaki peke yake…na walipofika ofisini kwa bosi wake, bosi akaanza kusema;

‘Unajua nimekusubiri sana, mpaka nikawa na wasiwasi huenda huyo mgonjwa kazidiwa, naona kama …ok,…’ Akafunua kumbukumbu za yule mgonjwa kabla hajasema neno alilokuwa kaksudia kulisema..` hapa kwenye kumbukumbu umesema alizindukana mara moja,…mmmh, alipozindukana hakusema lolote,… hakuongea kitu chochote…?’ akauliza Docta Adam

‘Alitamka neno moja tu `Sweetie...’ akasema Rose kwa kifupi hakutaka kuongea mengi ili ajaribu kumsubiri bosi wake kuwa anajua nini zaidi!

‘Sweetie??’ akauliza Docta Adam, na kujaribu kusoma maelezo ya kumbukumbu za yule mgonjwa, halafu akainuka kwenye kiti akafikiri kwa makini… , halafu akaisogelea simu,…akaanza kupiga namba, halafu akasitisha kuzipiga zile namba akageuka kumwangalai Rose, huku akiwa kamwangalia Rose, huku anairudisha ule mkono wa simu mahala pake.

‘Unajua Rose, kila nikitaka kuchukua uamuzi huu, naingiwa na simanzi…najawa na huruma, maana ilivyo, watu wa usalama wanamtaka huyu mtu, ni muda mchache tu, jamaa wao anayemfuatilia huyu mgonjwa alitoka hapa…na vitisho vingiii…wanavyodai ni kuwa huyo jamaa ni mmoja wa wapiganaji wa msituni, katoroka au kapotea, na ilivyo,…’ Akasonya Docta Adamu na kuonyesha uso wa mashaka…na akaendelea kuongea `…Na ilivyo… wengi wanaokamatwa hupelekwa kwenye jela ya wafungwa wa kivita, umeshaisikia hiyo jela, …?’ akamgeukia Rose na kumkazia macho halafu akasema; `…Hiyo jela ni balaa...jela hiyo …mmh, niliwahi kuitembelea siku moja, katika harakati za kuwatetea watu kama hawa wanaofika hapa, hapa imekuwa sehemu ya wagonjwa kama hawa, wanakuwa wameumizwa vitani, ….na kiukweli nilipofika hapo siku hiyo sikuamini kuwa binadamu anaweza kuishi hapo…ni mithili ya jela ya vichaa, …watu hapo wanatamani kufa tu…na kila mara unasiki mayowe, watau wanapata vipigo, wanateswa…maana muda wote ni mateso.

‘Nikuambie Rose kila aliyefika hapo kama atabahatika kutoka ni `tahira’ ni mgonjwa ama wa TB, au `ukimwi’ au ni kiwete…au ni maiti anakwenda kuzikwa…ni jela ya mateso, …kwasababu wanawachukulia hawa watu kama magaidi…hawastahili kuishi na hapo huwatesa ili wataje wenzao walipo….’ Akasema Docta Adam na kumfanya Rose atetemeke kwa woga utafikiri ndiyo yeye anatarajiwa kupelekwa huko, akimuwazia mgonjwa wake…aliogopa huku kayatoa macho kumkodolea bosi wake, ambaye alipoona kuwa anaongea lugha ya kumtisha …akatabasamu na kusema `mbona unaogopa hivyo, kwani wewe ndio unakwenda huko…mmh, usiseme unamuonea huyo mgonjwa huruma, mimi ni zaidi yako, lakini…’
‘Sasa kwanini watu wafanyiwe hivyo, na je wanauhakika gani kuwa wanaowapeleka huko ni magaidi…? Huo ni unyama bosi, tusihusike kuwatesa watu wasio na hatia, nina imani huyu mgonjwa sio gaidi..!’ akasema Rose

‘Nikuambie Rose, huyo sio wa kwanza kuletwa hapa na hali kama hiyo hiyo na niliwahi kuwapokea wengine wawili niliwaonea huruma sana, na hawo maaskari wakaja hapa na kuwachukua kwa nguvu, walipoteswa saana walisema ukweli..kumbe kweli walikuwa magaidi , wapiganaji wa msituni….karibu ninyang’anywe kibali cha kuendesha hii hospitali, kwa kuonekana kuwa eti ninashirikiana na hawo watu kwanini niliwatetea, mpaka nikasaidiwa na mkubwa mmoja huko serikalini, ndipo mpaka leo naendelea na hii kazi…kwahiyo siwezi kuwaamini tena hawa watu, unawahurumia wanakutelekeza mwishoni, kwao hiyo ni mbinu ya medani , kwangu ni hasara….kwahiyo usiniambie kitu…! ‘ akasema Docta Adamu.

‘Bosi nikuambie kitu, usiwaambie kwanza hawo maaskari kuwa huyu mgonjwa kaamuka, mimi nitahakikisha napata ukweli, kutoka kwake, ninauhakika sio gaidi, nakuomba sana bosi…tafadhali nipo chini ya miguu yako’ Akasema Docta Rose huku akitaka kumpigia bosi wake magati, lakini baadaye akaona aibu na kugeuka upende mwingine, akitafakari jinsi gani ya kumuokoa yule mgonjwa akikimbuka yale maneno ya yule mgonjwa asiyejulikana jina akimwambia…,
’’… na nakutegemea wewe Sweetie, maisha yangu yapo mikononi mwako…nakuomba sana, unilinde, sijui kwanini nakuambia hivyo, ila nakuamini hivyo;…’’

‘Unanishangaza sana Rose, nakumbuka mwanzoni hukupenda kabisa kumhudumia huyo mgonjwa hasa ulipoona kuwa ni mwanaume, …tabia yako ya kuchukia wanaume imeishia wapi…nakumbuka kabisa ulisisitiza kuwa tuwaachie polisi wamchukue huyo mgonjwa, nikagundua kwasababu ya hiyo tabia yako, na nikakushinikiza ili kuondoa hiyo tabia isiyofaa…ulisema kuwa maaskari watajua wenyewe jinsi ya kumhudumia huyo mgonjwa, sasa naona umebadiliak kabisa, ..halafu naona unakuwa karibu sana na huyo mgonjwa, hata nilipokukuta pale nilikuona kama unaongea peke yako…utafikiri unaongea na huyo mgonjwa wakati yeye kalala, …..unanishangaza sana Rose

Rose akatabasamu huku akiwaza hayo manenoo ya bosi wake, ambayo yalikuwa na ukweli, hata yeye mwenyewe alijihisi mabadiliko, na mabadiliko haya yalianza tu baada ya kumuona huyu mgonjwa, …akawaza ni kwa ajili ya huruma au kuna la zaidi, au kuna hisia za kimapenzi…hapana sio mapenzi, sina mapenzi tena na wanaume, nimegundua hawapendiki…akageuka na kumwangalia bosi wake ambaye naye likuwa kazama kwenye mawazo akiwaza nini afanye kuhusu huyoo mgonjwa, alikuwa akimuone huruma, lakini yeye kama yeye angefanyeje…au atumie mbinu ya Rose kusingizia kuwa hajazindukana…

‘Ok, Rose, hebu twende huko wodini , nataka kumwangalia huyo mgonjwa na kama kazindukana, nikimhoji nitagundua ukweli wake kuwa ni gaidi au ni mgonjwa tu wa kupita njia, na pia ili nijue jinsi gani ya kupambana na hawa watu, kuna serikali kwa jili ya kurejeshewa gharama zetu, kuna polisi kwa ajili ya kumkabidhi huyu mgonjwa kwao, kwa vipi, itabidi nimsikie huyo mgonjwa kama kazindukana atotoa kauli gani…ok, twende….’ Akamshika Rose mkono na kutoka naye kuelekea wodini!
Walipofika wodini kuangalia kitanda kipo cheupe, hakuna cha mgonjwa au nesi…wakabakia mdomo wazi, na kabla hawajaamua kwenda kumtafuta nesi aeleze nini kimetokea ghafla nesi naye akaingia akiwa kabeba mashuka na kuwakutwa mabosi wake wanachungulia kitanda cheupe, hakuna mgonjwa…

Ni mimi: emu-three

7 comments :

samira said...

rose kazi huna mama jamani mgonjwa wetu itakuwaje bora nisubiri
m3 kazi nzuri nimeipenda
nawatakia ramadhani kareem

Pam said...

uhondo unaendelea duh m3 kazi nzuri natamani nijue kitakachofuata!!!

emuthree said...

Nashukuru sana Samira kuwa tupo pamoja, na wewe pia twakutakia Ramadhan Kareem!

Pam, tupo pamoja, nashukuru kuwa umaitahidi mpaka umefikia hapa , sasa tunaenda sambamba. Hata mimi natamani kujua nini kitakachofuta. Tupo pamoja, na wengine wote, karibuni kwa maoni!

Precious said...

Jamani M3 natamani kujua nini kimetokea mgonjwa kaenda wapi? Dr. Rose nini kitatokea kazi atafukuzwa au itakuwaje. Tuko Pamoja sana tu. Precious

Rachel Siwa said...

Ndugu kazi nzuri mpaka raha,Mungu akubariki sana!

Iryn said...

Mmmnh sasa huyo mngonjwa jamani nae kaenda wapi jaman?? Mbona analeta balaa tena... Sasa cjui itakuwaje tena... Thnxxx much m3 n'always i wil try 2 be the mpenz mwema of thc blog of urs keep it up

Simon Kitururu said...

DUuh Mkuu!Nasubiri iendelee!Kazi bomba sana!