Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, August 26, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-20



Ilikuwa jioni ya saa kumi na mbili wakati Maua na Maneno walipowasili Arusha, Manyara National park, na kwa vile walikuwa wamechoka kwasababu ya safari ya kutoka Dar, kila mmoja alikimbilia chumbani kwake ili kupata maji ya kuoga kwa kuondoa uchomvu wa safari, licha ya baridi iliyokuwepo muda huo, lakini maji ni muhimu ili kuuweka mwili sawa, na ikibidi kujipumzisha kidogo, waliahidiana kukutana baadaye ili kupata chakula cha usiku kabla hawajaanza kujua taratibu nyingine ambazo wenyeji wao waliwapangia.

Maua alipofika chumbani kwake taswira ya siku ile ya kwanza walipofika na Maneno ilimrudia tena, akaanza kuogopa, akaanza kuangali hukuna kule, alikuwa akitafuta kitu…hajui kitu gani, akaanza kukagua begi , lake,…lakini hajui nini anakitafuta…chupa, …mbona hakuna chupa kama hiyo, anatamani kufanya jambo, lakini akili haimtambuzi haraka ni jambo gani, moyo unamwenda kasi…natamani, natamani…..kujiondoa hapa duniani, …lakini hkuna kitu cha kunisaidia kujiondoa, …chupa ya sumu haipo, nitafute kamba nijinyonge…akawa anazunguka huku na kule, kichwa kinamwanga …kichwa kinamuuma…baadaye akagundua kuwa pale nje aliiona kamba, akacheka, akasema nimegundua kitu, kama siku ile nilishindwa kutumia sumu leo nitajaribu njia nyingine, akainuka kutoka nje, na alipofika pale kwenye meza kunapoweka runinga, mara taswira ya safari yao ya kwanza ikamjia kichwani, akasimama kukumbuka lile tukio, ilikuwaje siku ile ya safari ya kwanza..
*********
Siku ya safari yao ya kwanza walikuwa wamefika muda kama huu, muda wa jioni, na wakafikia hiyo hoteli Manyara Hoteli, ambayo walishawasiliana nao kabla, na walipata vyumba vinavyoangaliana, na Maneno alipohakikisha kuwa shemeji yake kaingia kwake yeye akaondoka kwenda kuongea na hawo wanaosimamia taratibu nzima za kwenda kuwaona wanyama. Kwani walipanga kuwa wakitoka hapo wanapitia na Ngororngoro National Park, …Maneno hakuwa na wasiwasi kabisa na shemeji yake, alijua kwa vile shemeji yake kachoka, basi akaifika kitandani ni usingizi kwa kwenda mbele, kwahiyo aliona ampe muda wa kupumzika wakati yeye anongea na hawo jamaa, na yeye akirudi atamtupia jicho mara moja kuangalia usalama , halafu na yeye atahitaji nusu saa tu ya kupumzzika kwake inamtosha kabisa, kwani alishazoea safari za mara kwa mara.

Huku nyuma Maua alijikuta moyo ukimwenda mbio, alikuwa kalifikiria sana jambo lake ambalo alilikusudia kulifanya, akaliendea begi lake na kulifungua, na akakipa kile alichokuwa akikitafuta, …alikitafuta kile alichokuwa akikitaka, kilikuwa chupa ndogo, chupa ambayo ilikuwa na dawa maalumu. Dawa ambayo kwake yeye aliivika jina la `mwisho wa matatizo’, Alipokipata kile kichupa akawaza hatua ya pili aliyoipanga kichwani, akatoka pale chumbani hadi meza varandani ambapo wanachangia na Maneno, kwani kulikuwa na vyumba viwili vinachangia sehemu ya kupumzika na kula, kujisomea nk, akafika hapo mezani, na kusema , hapa akipita shemeji ataiona hii karatasi ambayo alipanga kuandika ujumbe maalumu, akachukua kalamu iliyokuwepo hapo mezani na karatasi akaanza kuandika hivi;

‘Mimi ni Maua ninayeandika ujumbe huu’, akaweka saini yake, halafu aakendelea kwa chini yake
‘Ndugu zanguni, msije mkamshuku huyu shemeji yangu Maneno kwa kitendo hiki, nilichokichukua , kuwa labda ndiye kafanya hivi, hapana yeye hahusiki kabisa, huu ni uamuzi wangu mwenyewe, kwasababu nimechoka kuteseka , nimechoka kuvumilia na pia nimecjoka kuwasumbua, na ili kuondokana na haya ndio nimeamua kuchukua hatua hii….’

Kalamu ikagoma kuandika, alipoiangalia vyema akagundua kuwa wino umekwisha…akakumbuka kuwa katika begi lake kuna kalamu aliiweka na kitabu chake cha kumbukumbu …akaiendea huko chumbani kuichukua , aliitafuta kwenye bagi ikawa haionekani, mpaka akaamua kutoa vitu vyote kwenye begi na baadaye akaigunuda ikiwa imejificha kwenye kona ya begi.
Haraharaka akaichukua huku moyo ukimwenda mbio kwa jambo analotaka kulifanya, akatoka mle chumbani mbio kuelekea pale alipoiacha katarasi yake na ile chupa, alipofika pale akajikuta kashikwa na butwaa, akasimama akiwa kashangaa, kwani alimkuta shemeji yake kainama pale mezani anaisoma ile karatasi.

Maua akashikwa na butwaa, akabakia kasimama pale na kitu alichofanya ni kurudi kinyumenyume hadi karibu na mlangoni ili aweze kujiegemeza, kwanialishaanza kujisikia vibaya, alipojiegemeza kwenye mlango, akahema kwa nguvu, lakini hakuwa na cha kusema. Maneno aliinuka pale alipokuwa kakaka, na kumgeukia Maua, alipokutanisha macho ayke na ya Maua, uso wake ulikuwa sio ule uso wa Maneno anayemjuaa, alikuwa kabadilika, alikuwa siyo uso ulikuwa umekunjamana kwa hasira, na mdomo ulikuwa ukimcheza cheza, akitafuta neno gani alitoe kwanza. Alichofanya ni kuichukua ile chupa na kuyasoma yale maandishi yake, ambayo kuna maneno makubwa ya hatari, kuwa ile ni sumu kali, kwa ajili ya kuulia wadudu wabaya kama nyoka,na wengineo ni hatari kwa maisha ya binadamu, inatakiwa wakati unaitumia ambapo unachanganya na unga au maji, na alzimaa ukifanya hivyo uwe umevaa kinga mikononi….

Maneno alifungua kizibo cha ile chupa bila kujali yale masharti, akamsogelea Maua na kumwanmbia kwa hasira ‘ `Wewe si unataka kujiua, haya chukua kunywa yote, ..kunywa yote, haya kunywa, ufe, …amekufa rafiki yangu mkubwa Mhuja, sembuse wewe, …kwasababu wewe unachofikiria ni kuwa waliokufa wanafaidi saaana, haya kunywa…’ akamsogelea Maua na kumkabidhi mkononi. Maua aliishika ile chupa huku machozi yakimtoka, aliingalia ile chupa, na kuwaza, sasa anywe, au afanyaje….mikono ikaanza kumcheza, akawa kama anaisogeza ile chupa maeneo ya kichwa kama anataka kuinywa ile dawa, ….lakini mara chupa ikamtoka mikononi na kudondoka sakafuni, na mara Maua akayumba huyo akadondoka chini na kupoteza fahamu. Maneno alichofanya harakaharaka akaichukua ile chupa ya sumu na kuificha pembeni ya meza halafu….

‘Sijui ndio nimeua, lakini hakuwahi kunywa kama nilivyomwambia….ooh, kazi hii sasa…’ Akajikuta akihaha na kujiona kachanganyikiwa zaidi akazidi akijuwa kuwa Maua alishakunywa ile dawa kabla, na sumu inaonekana ni kali zaidi, na kwahiyo inabidi Maua awahishe hospitalini, au ni ile hrufu tu ya ile sumu alipoisogeza karibu na uso, hakumbuki vizuri kuwa aliifikisha puani au vipi, akajuta kwa nini alipaniki haraka na kumwambia maneno yale kuwa ainywe, na alifanya hivyo kama kumuonyesha tu kuwa alichofanya sio jambo jema…, akaona sasa kaua, … haraka haraka akakimbilia kule sehemu ya hotelini akanunua maziwa fresh, akarudi nayo kwa haraka, alipofika pale alimpomuacha Maua akamkuta hayupo, akaenda pale alipokuwa kaiweka ile chupa ya sumu, akaikuta haipo…mungu wangu, ina maana huyu mwanadada kaichukua kweli kaenda kujimaliza, …..

Akaingia chumbani hakuna mtu, …ooh, sasa ukisikia kuumbuka ndio huko, akaona heri akaiwafahamishe watu wa ile hoteli ilia pate msaada wa haraka, lakini kabla hajaenda mbali akaona arudi kuhakikisha kuwa kweli hayupo, maana akiwaambia walinzi ina maana kila kitu kitakuwa kimejulikana, na hakutaka kashifa kama ile iwepo na kusambaa, huwezi jua, hata waandishi wa habari wanaweza kuipata na kuiandika na matokea watazidi kumchanganya huyo binti, na alipoingia kwenye eneo la chumba chao akamkuta Maua Maua kakaa kwenye ile meza aliyokuwa kaiweka ile karatasi, na alikuwa kashika kijitabu chake cha kumbukumbu.

‘Sheemeji vipi , upo sawa kweli…?’ akauliza Maneno.
‘Nipo sawa, nilikwenda kuitua ile chupa ya sumu…niliogopa huenda umeenda kuwaita maaskari…nikaona heri niondoe huo ushahidi…’ akasema Maua.
‘Lakini shemeji tulishayaanngea haya maswala na kujua yamekwisha nini tena,….’ Akauliza Maneno kwa huzuni.
‘Hata mimi sijui shemeji kun kitu kinanivuta nifanye kile nisichokusudia, sijielewei kwakweli, na hii inanispa mashaka kuwa kumbe mtu unaweza kujiua bila kupenda…’ akasema Maua akiwa bado kachanganyikiwa.
‘Sasa sikiliza ni bora twende kwenye hospitali ya karibu tuone kama watatusadia kwa hilo..’ akasema Maneno.
‘Hapana sasa nipo kamili, ile hali imeondoka kichwani…nahisi kuna kitu kisicho cha kawaida, sio akili yangu…lakini nitajitahidi kuishinda hiyo hali..’ akasema Maua, lakini Maneno hakuwa nan a raha tena, hata ile hamu yote ya kuja kuona wanyama ilimuishia, lakini akajikaza na kuanza maneno yake ya kuchekesha hadi shemeji yake akatabasamu…

Hawakuongea sana, na baadaye waliitwa kuwa kuwa kuna safari ya usiku kwenda kuwaona baadhi ya wanyama, ikawa ni nafuu kwa Maneno, kwani hakujua jinsi gani atamlinda yule mwanadada, walitoka nje na kuanza kuupata ubaridi wa Arusha, ambao ulichanganyika na upepo mwanana unaotoka kwenye ziwa Manyara! Walitoka pale na kutembea kidogo kama utangulizi ili waone baaadhi ta wanyama, kama, pundamilia, na wengineo hawakutakiwa kwenda mbali zaidi kwani safari yao ilikuwa ni kesho ambapo wangeliweza kuwaona wanyama wengi na mengineyo, na hapo uso wa Maua ukaanza kung’aa.kwa furaha na moyoni akasema safari kama hii tulikuwa tumeipanga na marehemu mume wangu.

‘Kwa makadrio ziwa hili linakadiriwa kuwa kilometa 230 za miraba , ana mbuga yenyewe ina kadiriwa kuwa na kilometa za miraba 330, ikiwa na vivutio vizuri kwa macho ya wanadamu, watalii hufika kwa wingi kuangalia vivutio hivyo, licha ya wanyama kuna ndege wazuri, wadudu watambao, kama nyoka na jamii yake, kuna bustani za kuvutia, wanyama wa kila aina mutawaona, na pia kuna mabonde mazuri yaliyojipanga kwa mvuto wa aina yake!




‘Jina la mbuga hiyo lilitokana na neno la kimasai la `manyara'! Ambalo neno hili lina maana ya aina ya mmea, amboa hutumika kwa kuwalishia wanyama, ni chakula kizuri kwa wanyama , kwa kitaalamu nafikiri mmea huo unaitwa Euphorbia tirucalli! Pia ndani ya mbuga hiyo kuna miti mikubwa, maji yabubujikao na misitu minene, ambayo yote ni kivutio kikubwa sana kwa watalii….’ Akawa anaongea jamaa anayehusika na hifadhi hiyo, ambaye alisema yeye sio mhusika kamili, muhusika kamili watakuwa naye hapo kesho. Maua alifuatlia sana maeelezo hayo kama vile mwanafunzi asiyetaka apitwe na jambo, na kumfanya Maneno aanze kujisikia furaka kuwa angalau sasa shemaji yake kaanza kujirudi, maana alishaanza kutishika kuwa itakuwaje, huyu mtu, huenda ana sumu nyingine kaificha na usiku anaweza akajiuia,...

‘Upande wa kasikazini mwa ziwa hili la Mbuga hizi za Manyara kuna athari za volikano, na kuna maji yanayotiririka kutoka kwenye bonde la ufa! Na kutokana na kuwepo kwa maji maji ya mara kwa mara hali ya hewa ya maenao hayo ni kama mnavyoiona, upepo mwanana wenye ubaridi, na kama mnavyoona majani yanaoenakana ni ya kijani…!’

Baadaye walirejea kwenye hoteli ya Manyara na Maneno alimsindikiza shemeji yake hadi mlangoni mwa chumba chake, alitamani kuingi akukagua humo ndani kuhakikisha kuwa kuna usalama, lakini akasita kufanya hivyo, na Maua alipomuona shemeji yake akiwa na mashaka akaona umuondoe hofu akamwambia…

‘Shemeji usiwe na wasiwasi na mimi tena, unajua nilipowaona hawo wanyama na kuiona hali ya hewa ya hapa ilivyo kwakweli nilifarijika sana, nimegundua kitu kimoja kuwa kweli kufa kupo, lakini pia uhai unahitajika sana, na mtu wa kumtumania ni mungu, aliyeumba kila kitu, mtu utakufa lakini ni kwa siku zako, lakini sio ujiue, na sio umchezee mungu, angalia wanyama hawa wanavyoishi, wamechanganyikana, na wengine hukimbizana kuuana…nawaza sana na kujuta kuwa kwanini nilitaka kuchukua hatua kama ile ina maana nimeguka kuwa mnyama kujiua mwenyewe…najuta sana shemeji naomba unisamhehe na nawaomba msamha wote kwa jinsi gani nilivyowasumbua, na shemeji hili lililotokea hapa naomba liishie hapa hapa…’ akasema Maua huku akionyesha uso wa huruma, mpaka Maneno naye akamuonea huruma, hasa alipomuona machozi yakimtoka usoni, akatoa leso mfukoni, na kumbe leso aliyokuwa nayo niile iliyokuwa na tone la damu la siku ileee..! Amekuwa akitembea nayo kama kitu gani muhimu sana mfukoni mwake, alipogundua kuwa ndiyo ile leso akairudisha haraka mfukoni na kugeuka kutaka kuondoka akasema;

‘Sawa nimekuelewa shemeji, na nashukuru sana mungu kuwa hatimaye umeshaanza kurejea duniani, maana ulikuwa dunia gani sijui, jitahidi sana kuyasahau yote, ..ujue kuwa kuondoka kwa Mhuja sio mwisho wa dunia, wapo wengi wameondoka kabla yao, lakini dunia bado ipo, kwasababu hayo mambo mungu kayaweka ili yawe mitihani kwetu, hapa dunia ni kama mapito tu, kila mmoja yupo safarini, na kuondoka kwa mwingine inatakiwa iwe maandalizi kwa yule anayebakia ….’ Akaongea Maneno, akijarinu kutafuta maeno ya kidini yanaingia akilini.

Na kweli siku hiyo ikaisha salama, na asubuhi sana Maua aliamuka asubuhii na mapema na kujiweka tayari kwa safari na hata alipokutana na shemeji yake alishangaa kumuona anamkudolea macho, maana tangu mumewe Maua aondoke , Maua alikuwa kabadilika kupita kiasi, alikuwa hajipambi tena, alikuwa kaanza kuvaa ovyo ovyo, ..lakini leo akaonekana tofauti, Maua yule anayejulikana alianza kuchanua tena.

‘Leo shemeji umetoka bomba, mwanamke mrembo, na …..mmh, kila mmoja atapinda shingo kwa kukuangalia…’ akasema Maneno.
‘Acha utani wako shemeji, na jinsi nilivyokonda naonekana kama mwanamke wa miaka isiyo yangu…’akasema Maua akishika kwenye mifupa ya shingo
Maua kweli alikuwa mrembo, na leo aliamua kuvaa sweta jekundu na gauni jeupe refu, lenye mikono mirefu, na kichwani akaava kofia pana, utafikiri alikuwa akijifunika jua, sijui mwenyewe alikuwa na maana gani…

‘Unajua shemeji hizi nguo alininunuliwa shemji yako siku moja kabla hajaondoka, alitaka nizivae siku tukisafiri kuja mbuga za wanyama, aliwaona wazungu wakiwa wamevaa hivi ambao walituambia kuwa walikuwa wanakuja huku kwenye hifadhi za mbuga za wanyama, Mhuja alipowaona walivyokuwa wamevaa akapendezewa sana akasema siku hiyo nitakununulia nguo kama hizo, uonekane kama yule dada Muingereza alivyo vaa, akaninunulia kwa msharti kuwa nitazivaa siku ya safari yetu ya kuja huku kwenye mbuga za wanyama…sasa leo nazivaa kwa heshima yake…’ akasema Maua huku machozi ya kimlenga lenga.

Ama kweli Maua ni mrembo, kila kitu chake ni kizuri, hata vile alivyokuwa hajipendi alikuwa mzuri kwa jinsi hiyo, sasa ndio kajiweka kiurembo zaidi, basi hapo Maneno alijikuta mwili mzima ukimsisimuka, alibakia kumwangalia bila kummaliza, mwishowe akasema kimoyomoyo;
‘Ama kweli munguu anajua kuumba viumbe vyake, halafu ndio alitaka ajiue, si hata mimi ningejitundika….mmmh, nijitundike kwangu mimi haiwezekani, maisha yalivyo matamu haya…’ akaikuna kichwa.

‘Shemeji vipi naona macho hayabanduki kwangu, mpaka watu wanakushangaa unavyoniangalia…’ akasema Maua, na kumfanya Maneno ageuka kuwaangalia watu, lakini aligundua kuwa watu walikuwa wakimwangalia Maua kwa uzuri wake, wala sio yeye jinsi anavyo muangalia Maua, akatabasamu na kumsogelea Maua , ilimradi akae karibu naye ili watu wamuone kama yeye ndiye …mmh, mume wake…

‘Ahsane sana shemeji yangu kwa kunijali, isingekuwa wewe sijui ingekuwaje, ilishafikia hatua najiona kama bua, kama mfu , yaani anatembea kama roboti…lakini kwa juhudi zako sasa najiona mzima, nshukuru sana, na wla sijui nikulipe nini, mungu atakuzidishia heri na wema wako huo, najua siku ukimpata mwenzangu atashukuru sana kuwa kapata mume, wewe nakuona una upendo sawa na alivyokuwa mume wangu..’ akasema Maua wakiondoka kuelekea huko mbugani.

Moyoni Maneno alisema, `Sidhani kama nitaweza kumpata mwingine anaye fanana na wewe, namuomba mungu kuwa wewe unikubalie niwe tu uwe wangu…sijui kama utakubali ombi langu hilo…ooh, mungu nisaidie siku ikifika nikimtamkia tu , aseme nimekubali, sijui siku hiyo nitafurahi kiasi gani….`
‘Unikubalie mama weee, tatatatata, .
‘Mawazo yangu uyajue, tatatat…
‘Nisipate taabu kwa ajili yako weweee…’


Akajikuta anaimba wimbo huo kwa sauti, na kwa Maua hakushangaa, maana Maneno anapenda kuimba, halafu akianza kucheza, halafu kuchekesha…yaaani ukikaa naye ni raha kwa kwenda mbele..alkini hata kwa vimbwanga vyake vyote hivyo, Maua alikuwa kapooza,hadi siku za karibuni tu…na wakati wanatembea Maua akawa anamuwaza huyu Maneno kwa wema wake huu, akafikiria zaidi ya kufikiria, akikumbuka siku ile alipomsimulia kuwa yeye ndiye aliyekuwa wa kwanza kumuona kabla ya Mhuja na ndiye aliekuwa wa kwanza kumpenda kabla ya mume wake, ila bahati haikuwa yake…na hapo ile taswira ya siku ile alipomuona alipokuja kumtembelea kuja kumuona shemaji yake, akijua kuwa ni sio Maua anyemjua, lakini…!

***********
Siku ile Maua alikuwa kakaa chumbani, alikuwa anasubiri mume wake amuite waondoke kwenye safari hiyo waliyopanga, na akawa kajiandaa vyema kwa kuvalia nguo maalumu. Mara alisikia Mhuja akiongea na simu na alipomaliza akamuita kwa sauti kuwa kuna mgeni anakuja, kwahiyo watachelewa kidogo kuondoka, basi ikabidi ajilaze kidogo kitandani na wakati anasubiri mara akasikia sauti ya mtu akipiga hodi, na akaskia huyo mgeni akiongea na mume wake.
‘Kwanza nataka nimuone shemeji ..’

‘Kwanza nataka kuiona hiyo zawadi..’ ilikuwa kama mzozo, na akona amuone nani huyo anayezozana na mume wake kiasi kwamba inakuwa kama vurugu, akainuka pale kitandani na kujiweka vyema halafu akachukua hatua ndogo ndogo kutoka chumbani kwenda varandani, alikuwa kama anayemelea kuwaangalia bila wao kujua kuwa anawaangalia.

Alipotokeza kichwa tu, macho yake yakakutana na huyo mgeni, na mara akaona kitu cha ajabu, kwanza aliona aibu kujitokeza kabla hajaitwa, na hakutaraji kuwa ataonekana , lakini zaidi ya yote ni jinsi huyo mgeni alivyomkodolea macho, na alibakia hivyo kwa muda hadi Mhuja alipogeuka kuangalia kule mlangoni, akakuta mkewe akiwa kasimama huku akionyeshwa kukerekwa na jinsi anavyoangaliwa na Maneno, naa kwa vile Mhuja anamfahamu sana rafiki yake kwa vimbwanga vyake, akainuka na kumsogelea mkewe na kuanza utambulisho.

`Maneno huyu ndio shemeji yako , sina lakukuambia zaidi kwasababu macho yako mwenyewe na jinsi ulivyoshangaa imedhihirisha kuwa umemkubali…au sio’ akasema Mhuja akiwa kamshika mkewe kiuona na kutembea naye bega kwa bega..tete-a-tete, kumleta varandani, na Maua akiwa na aibu akawa anafuatana na mumewe had1 karibu na pale aliposimama Maneno akiwa bado kaduwaa, na macho yake yalikuwa hayabanduki kumwangalia.

Baadaye Maneno akajishitukia na kuanza kujibaragua kwa kusema; `Unajua Mhuja, umeniacha hoi, kweli wewe unajua kuchagua ,kweli wewe umenipiga bao, tena la kisigino, ….mmmh, shemeji usione ajabu, mimi na Mhuja ni hivi..’ akaviunganisha vidole huku bado alimwangalia kwa macho yasiyoaamini kuwa hicho anachokiona ni kweli au anaota…

‘Kweli asemavyo Maneno, mimi nay eye tumetoka mbali, toka chekechea hadi shuleni, chuoni hadi kazini..kwahiyo tunajuana na nakuomba ujaribu kumzoea kwani anaongea, unajua kuongea, basi huyu anaongea, hapa tu anaona aibu kwa sababu ni mara ya kwanza kukuonaa, lakini akianza mbwembwe zake utacheka, mpaka mbavu zitauma..’ akasema Mhuja, na Maua akajiuliza kama hapo huyo rafiki yake kaona aibu, je akiwa hana aibu itaakuwaje…maana yeye ahjazoea kukaa na mwanamue akawa akamchangamkia kiasi hicho, hawezzi kumpa nafasi hiyo, kwahiyo hapo alijionea taabu tu…

‘Rafiki yangu huyu anaongea kama kaseti iliyofunguliwa, na ukiwa naye huwezi kuchoka, maana anajua kila kitu…’ akasema Mhuja na kumuelekeza mkewe akae kidogo, na wakawa wanaongea mazungumzo ya kawaida, mpaka wakajisahau kuwa walikuwa na safari….

‘Maua mbona umeduwaa hapo kama….unanitisha au unataka kufanya kama siku ile….Maua akawa kaduwaa tu anaanglia ile kamba…huku anaomba Maneno aondoke, ili aweze kufanya lile linalimvuta kufanya hivyo…

Je ni kitu gani hiki kinamuandama Maua , kachanganyikiwa,...hata mimi sijui kwakweli ngoja tuone toleo lijalo, tuwepo pamoja. Samahanini sana kwa sehemu hii, inawezekana haijakaa vyema kidogo, kwani nimekuwa nikiiandika katika mazingira magumu, nilichelewa kufika ofisini, lakini nimekuwa nikiiandika kidogo kidogo kila ninapopata upenyo hadi hapo nilipofikia…natumai mtaielewa vyema,
******


Ni mimi: emu-three

3 comments :

Anonymous said...

Sio TU visa , bali pia unatangaza utalii wetu, sio visa tu, bali pia unatukumbusha hitoria, tukio zima la mv bukoba, nakupa tano

Precious said...

what i can say to you M3 is your so GIFTED.....

emu-three said...

Ahsante sana Any wa 10:53 am, na pia Ahsante Precious kwa kunipa moyo, nilikuwa nimekata tamaa kabisa na sehemu hii, maana nimeona watu kimiya, hawasemi lolote, lakini najua watu wapo busy na sikuuu, nami itabidi nisubiri kwanza ....Ki-doogo, au mwasemaje?