Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, August 12, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-14



Docta Rose alifika kwake akiwa anahema na hakujua itakuwaje kwani alichosikia kwa wale maaskari kilimtia kiwewe, hakuamini kuwa waliyosema ni kweli na kama ni kweli basi kakumbatia nyoka, nyoka mwenye sumu kali, ambaye akiamua kumuuma, hatapona, kumbe ni chui mwenye ngozi ya kondoo…basi sasa inabidi aachane naye mapema…lakini haiwezekani, mbona haiji akilini, …kila nikimwangalia ananipa jakaomoyo, kila akinisimulia kuwa hajijui, hajui nini kimemtokea anaonysha huruma…na kimazungumzo yanatia huruma sana, na kama ndivyo alivyo kabla hajapandisha basi, angepatiwa matibabu haraka, ili hali yake hiyo iendelee kuwa hivyo hivyo..’akajikua akiongea mwenyewe kama mtu aliyechanganyikiwa.

‘Huyo mtu hajijui na wala hajui nini kinaendelea, aliokotwa ufukweni, …..blabla…halafu eti akipandisha ma-she-ta-ni hata waje watu kumi anawasambaratisha…mshetani…mmh na balaa zaidi anawanyonga watu kama kuku….’ Alipofika hapo akasikia mwili ukizizima kwa uwoga,na akajaribu kuwaza, mkono wenyewe wa kunyonga mtu ndio ule, mbona ni laini sana, mbona haujakakamaa kama ule wa wapiganaji wengine, mbona hata sura, haijakaa kama walivyo maaskari wengine,…namuonea huruma huyu mtu, siui nifanyeje…’ hata kabla hajatulia akasikia hodi mlangoni…

‘Hawo ni polis au ni nani tena, ….nimechoka, sipati hata muda wa kupumua…nataka kupumzika sasa, na sitaki kusumbua kichwa changu tena na hawa watu na hata ….’ Kabla hajamaliza mlango ukagongwa mfululizo na ilionyesha kuwa asipofungua utaendelea kugongwa, akainuka kitandani na kulitafuta panga lake lilipo, halafu taratibu akatoka hadi varandani, na akausogelea mlango, akachungulia kwenye kitundu chake, na akamuona,…..oh, ndiyoo yeye tena…hakutaka hata kujificha, karudi tena, alijua keshatoweka, alijua sasa hana lawama na mtu, lakini huyu hapa tena, na ….

Mlango ukagongwa kwa fujo…na hili likaanza kumuogopesha Rose, akijua kuwa sasa huyu jamaa kaja na mabalaa, kaja na fujo, …akalishika panga lake na kujiandaa kwa lolote….simfungulii kabisa, atanitia hatiani, anaweza kuni…

‘Unataka nini kwangu, ….nakuomba uondoke, maana unatafutwa, wewe unajua kuwa polisi wanakutafuta, wewe….’ Akasema na kushindwa kumalizia, kwani moyo, akili na mwili vyote vilikataa kabisa kukubali hayo, kuwa huyu mtu kweli anatafutwa , huyu mtu kweli ndio yeye, ….hapana, ..na hata kabla hajawaza zaidi mkono ukajituma wenyewe na kujikuta kashika lamngo na kuufungua…
‘Kwanini unanifanyia hivi, nishakuambia mimi sijijui mimi ni nani, mimi najiona kama mtu aliyezaliwa karibuni tu ….nakutegemea wewe, wewe nakuona kama ndiye mke wangu sijui umeamua kunificha tu…basi wewe ndio Sweetie wangu na iwe hivyo, nakuona kama wewe ndio kila kitu..nakuomba uniamini hilo, kichwa changu hakijui kabisa yaliyopita, ni kama nimezaliwa siku ile nilipozindukana pale hospitalini, hapo ndipo kila kitu changu kilipoanzia, sijui kuwa nina wazazi, sijui kuwa nina ndugu, sijui kuwa nina mke…mmh,…sijui lakini…na baya zaidi sijijui hata mimi mwenyewe ni nani, sikumbuki hata jina langu…hivi mimi ni nani, hivii kweli…nimekumbwa na kitu gani….nisaidie doctor’ Akawa anasema yule jamaa huku kashika kichwa na Rose akawa kashikilia panga tayari kwa mapambanoo , akijua kuwa jamaa kaanza kupandisha, lakini yale maneno yake yalimfanya amuonee huruma, hata hivyo hakuliachia lile panga.

‘Sweetie, nakuomba nipumzike, maana naona akili imechoka, kwanini wale polisi wananitafuta, kwani umesema na nimewasikia pale nilipokuwa nimejificha kuwa wananitafuta mimi , …wewe mwenyewe ulinishauri nijifiche, kwanini, hukuacha wakanikamata nikajua moja…mbona sasa wataka kunikamatisha kwa hawo watu wanaoonekana kuwa hawana huruma na wagonjwa… eti wananitafuta mimi, kuwa ni mtaalamu wa silaha, silaha gani hizo, mbona sikumbuki kabisa kushika, silaha….ooh, nakumbuka kitu kama hicho….lakini sikumbuki ilikuwa ni nini…sio kutengeneza, hapana ni kulenga shabaha…ilikuwa ndoto au…sikumbuki, lakini sijui silaha, silaha gani na kwanini silaha, mimi sio askari…sikumbuki kama niliwahi kuwa askari, sijui uaskari…hilo nalikana kabisa….Sweetie, …mmh, napenda kukuita hilo jina, ulisema unaitwa nanii vile…mmmh, mbona kumbukumbu hazikai vyema, mmmmh, yes, unaitwa Rose,…Rose hivi kweli sura na mwili huu ni wa uaskari…haiwezekani, wale wanabahatisha, …’ akasema na kukaa kwenye kochi huku akiangalia nje, na mara akinuka na kusimama kwenye dirisha bado akiwa anaangalia nje

Rose bado akiwa kashikilia panga juu, akimtizama yule mtu jinsi alivyosimama pale dirishani, na kusimama kule kulimkumbusha jinsi alivyomukuta siku ile alipoingia chumbani kwake, na alimuona baada ya lile pazia la dirisha kufunguka. Yeye alikuwa kashikilia panga juu, akiwa anamkaribia kumkata nalo kichwani, alikuwa kadhamiria kweli, kwani alijua ni mmoja wa maharamia ambao wanakuja kubaka watu, na baya zaidi alivuka mpaka, wa kuamua kuchukua khanga yake na kujifunga nayo kama mtu yupo kwake....

Alikumbuka siku ile alipotaka kufanya mauaji, sijui kama angeua ingekuwaje…kwani alimsogelea panga likuwa juu, alipomfikia, na kwa nguvu moja, alilishusha lile panga ili litue kichwani, na kabla halijamfikia, yule jamaa aligeuka kwa haraka, na alipoona panga linamjia, akashikwa na fadhaa na kwa haraka akainua mikono juu na kuliwahi lile panga…Rose alimpomuona ni nani lile panga llikamtoka mkononi, akabakia kushikwa na mshangao, akiwa haamini macho yake, akiwa kalegea na kingine zaidi alijikuta akihisi asivyotaka, moyo ukawa unamwenda mbio …na alichoweza kusema ni kutamka maneno haya `mamamama, mungu wangu ningeliua kiumbe kisicho na hatia…mamamama’

‘Wewe ..Sweetie, unataka kuniua, nimekukosea nini jamani, …mimi sio jambazi, mimi sio…oooh, na sijui kwanini niliingia hapa na kuzania kuwa nimeingia nyumbani kwangu, na nilipoiona hii khanaga nikakumbuka kama niliwahi kujifunga khanga kama hii, …sijui kwa vipi, nikavua nguo na kuivaa, nikakumbuka kuwa natakiwa kuoga, lakini nivae khanga kwanza, …nikaivaa, nilipotafuta maji nikaona hakuna, nikawa najiuliza nitayapata wapi,…yanapatikana wapi maji… ndio nikasogea dirishani kuangali nje nikiwaza, hapa ni wapi, nimefikaji, mbona mazingira yanakuwa kama magenimageni,…mara wewe unakuja kwa nyuma kutaka kuniua, kwanini, kwa vile nimetoroka hospitalini…Sweetie, nimekukosea nini…tafadhali niambie ukweli…’ akasema yule jamaa
‘Sahamani sana sikujua kuwa ni wewe, wapo watu wabaya wanakuja kuja humo kwangu, wapo watu wauaji na wabakaji…sasa, nilipokuoana upo humu nikajua kuwa wewe ni wao….samhani, lakini mbona umetoroka hospitalini..unajua hujapona?’ akauliza huku akimwangalia bila kujua nini afanye, ila moyoni alijikuta akifarajika kuwa nagalau amepatikana na alijua sasa atamchukua na kumpeleka kwa bosi wake mambo yatakuwa shwari,...

‘Nilisikia watu wakiongea kuwa natakiwa kukabidhiwa polisi, natakiwa kupelekwa kwenye jela ya wafungwa wa kivita…niliogopa sana, kwani mimi sijui vita, najua amani akili yangu inahisi hivyo..sasa iweje nipelekwe kwenye jela ya kivita?...nikaota ndoto mbaya sana, kuwa nipo chini ya maji, natapatapa, na mbele kuna mamba anakuja, nikaanza kuogelea kumkimbia…niliogelea sana, lakini kila nikiangalia nyuma namuona huyo mamba ananikaribia, ooh, nikaanza kutapatapa na kuogelea kwa kasi, lakini wapi huyo mamba alikuwa karibu sana ya miguu yangu, nikajitupa kwa juu…kumbe kujitupa kule , kulikuwa kwa kweli, nilijikuta nipo chini ya kitanda, kwa woga wa ile ndoto na kwa woga wa yale niliyoyasikia, nikakurupuka huku mwili ukiwa hauna nguvu, nikaziona nguo zangu mlizokuwa mumeziweka karibu na kitanda, nikazibeba, nikatoka mle hositalini kwa kujikongoja na bahati nzuri, wakati natoka nikaona gari likiwa linajiandaa kuondoka, nikajitahidi hadi nikapanda kwa nyuma, bila dereva kunijua tukaondoka na hilo gari, ….na ndicho kilichonisadia kuondoka haraka hapo hospitalii, na nilipofika ufukweni nikaoga nikabadili nguo nakuvaa nguo zangu halafu nikajilaza kwenye kivuli, nilipozindukana nikaanza kutangatanga…..

‘Basi nakumbuka hayo, lakini sio ya nyuma,sikumbuki kabisa maisha yangu ya nyuma …sijui kwanini sikumbuki…pale ufukweni, nikaanza kutembea,…lakini mwili ulikuwa hauna nguvu, na nilijiona nina njaa,…nina kiu, lakini sikutamani maji ya ziwa…sikupenda harufu yake, nikaanza kuchunguzachunguza huku na kule, mapaka nikafika huku kwenye nyumba za watu, na bahati nzuri, nikaiona hii nyumba, nikasema ngoja nijaribu hapa, nikaujaribu mlangu kama unafunguka nikakuta unafunguka, nikaingia ndani, lakini kitu kimoja kilikuwa kikinituma kuwa hapa ni kwangu kuwa kuna mtu…kama vile mke wangu,…nilihisi kuwa nimeoa, nina mke, na hapa ni kwangu…basi hiyo hali ikanifanya niingie ndani nikagundua chumba hiki, na nilipofika humo chumbani, nikaona kama niliwahi kuwa na chumba kama hicho …nikaiona hii khanga, nikahisi kuwa natakiwa kuivaa, ili nikaoge…yote hayo yanakuja kuja akilini kuwa labda nilikuwa nafanya hivyo…lakini kwa ujumla sikumbuki …’ akasema huku anaangali nje

‘Kwani tatizo kama hili lilishakutokea mara nyingine?’ akauliza Rose
‘Tatizo gani,…mmmh, hili la kusahau…sijui kama nina tatizo hilo, sijui kama nilishawahi kuwa hivi, sikumbuki kabisa, naona ni kitu cha ajabu kwangu, kusahau, hapana, sijawahi, sijui kabisa, kama nina tatizo kama hili…kwa ujumla hiki ni kituko kimeingia mwilini mwangu…’ akasema huku akishika kichwa.

‘Wewe siulikuwa askari unayetengeneza silaha, …wewe ..’ Rose akajikuta akipayuka
‘Askari?...anayetengeneza silaha….hahaha, wewe Rose Ina maana umeshawamini hawo maaskari, kuwa mimi ni askari….hapana, sijui, na sidhani kuwa mimi ni askari, kwanini niwe askari…’ akainua mikono yake na kujiangalia, kama anajikagua…’hapana huu mwili sio wa uaskari…eti mimi nilikuwa askari..hapana, hilo nalikataa kabisa, kama nikufanya kazi , labda ya ofisini, labda…, hilo naweza kulikubali..lakini uaskari hapana…’ akageuka na kumwangalia Rose.Rose alipoona kuwa bado kalishikilia lile panga, na mkono umechoka, akalibwaga chini na kugeuka, akitaka kukimbilia chumbani.

‘Jipe amani Rose, kuwa huru na mimi, na ili kukuhakikishia kuwa mimi sio huyo mtu wanayemtafuta twende kwa yule bosi wako tena, nina uhakika sasa hivi wale polisi wameshaondoka,kamweleze ukweli kuwa mimi niliamua kutoroka kule hospitalini sio kwasababu mbaya ni kwasababu ya kuogopa ile ndoto na yale mazungumzo…twende nipo tayari kujipeleka hata huko kwa hawo maaskari…’akasema huyo mtu akitaka kuondoka.

‘Subiri kwanza…wewe, unasema ujipeleke kwa hawo maaskari, mmmmh, hapana, …unawajua hawo maaskari au unawasikia tu, wakikuweka mikononi mwao umekwisha, kwanza hadi kufika huko gerezani kwao, utakuwa unatambaa kwa tumbo watahakikisha wamekugongagonga hivyo vifundo vya miguu, mpaka vilegee, na ukifika huko wanakukamatisha kwa watu waliofyatuka akili, utazalilishwa, utapigwa…ukitoka hapo sio wewe tena, ni nusu mfu…’ akasema Rose, kwa kumuonea huruma huyu mtu ambaye alishaanza kumuogopa lakini kila hatua ilivyopita humo ndani akajiona anamzoea tena…, .

‘Sikiliza kama haki ipo, na kama hawo maaskari wanafuata haki,basi sizani kuwa nitafanywa hivyo, kwasababu mimi najiona kabisa sina kosa, najihis hivyo…mimi sio huyo mtu wanayemtafuta, labda wamefananisha nahisi hivyo, labda kwa vile mlisema niliokotwa ufukweni, na huyo mtu alipotelea huko…kwani …eeeh, hebu nikumbushe kidogo, mnasema niliokotwa ufukweni, nikiwa nimezimia, kwanini niokotwe ufukweni,…sikumbuki vyema, kuwa nilikuwa ufukweni, nikaumwa…sikumbuki hata kidogo…kuna jambo hapo nataka kuligundua, na naona heri nifike huko ufukweni waliponiona ili nijaribu kuvuta kumbukumbu…naomba unipeleke nikapaone, maana sijui ni wapi hasa!’ akasema na kuanza kuondoka, na Rose naye akafikiri kwa makini, akipima hayo maneno …halafu akaanza kumfuta nyuma baada ya kufunga mlango wake.

Walifika kule ufukweni na kwa mbali waliona kikosi cha maaskari wakipita na silaha, ilionekana kuna shughuli maalumu kwani hata watu walionekana wakiondoka, na Rose akajaribu kuulizia watu kuwa kuna nini, wakasema kuwa hata wao hawajui vyema, lakini ikwa ufupi wamsikia kuwa kuna `operesheni maalumu’ na huenda kukawa na mapigano, kwa uzoefu wao, wanaposikia `operesheni maalumu’ baadaye huandamana na mapigano, kati ya askari wa serikali na waasi wa msituni, kwahiyo watu wanaondoka kwa kujihami…

‘Hapa sasa hapakaliki, ila sehemu uliyookotewa ukiwa umezimia kama mfu ni pale, karibu kabisa na maji, ulikuwa juu ya matakataka yale pale yaliyotupwa nje ya maji, ni siku nyingi zimepita kwahiyo hata yale matakataka ambayo yalikuwepo mara ya kwanza, yakiwa mengi kuliko leo yamepungua…walipokuona walijua umekufa, wakawaita maaskari, na ukachukuliwa kama maiti hadi hapo hospitalini kwetu…aliyekupokea hakufanya makosa alikuingiza kwenye vipimo kwanza, na hili ndilo linalofanya hospitali yetu ionekane bora, kuwa tunajali vipimo kwanza….vinginevyo ukapelekwa muchwari, kwani ulikuwa maiti-maiti, kwa kuangalia haraka walijua kuwa wewe umeshakufa…’akasema Rose, na alishangaa kumuona yule jamaa akiwa kasimama huku akiyangalia maji kwa makini na kama vile anawaza jambo fulani…

‘Twende zetu umesikia wanavyosema hawa watu kuwa kuna `operesheni maalumu’ na haijulikani ni nini, na mara nyingi ukisikia `operesheni’ ujue kuna mapigano yatakayofuta, ndio maana watu wanajihami wanalijua hilo… kuna mapigani hapo, na …twende twende, mimi naona nikakukabidhishe kwa bosi, ili tuwe katika usalama zaidi, tutamwelezea kwa undani na natumai atatuelewa , ila kwa sasa tupitie nyumbani kwanza ukapate chochote maana hujui huko mbeleni itakuwaje…’ akasema Rose, na kweli wakaondoka hadi nyumbani wakapata chakula, na kila mara Rose alijaribu kumdadisi huyo mgonjwa aliyekuwa katoroka, lakini hakuona lolote linalofanana na hayo waliyosema hawo maaskari zaidi ya kuwa huyo mtu hajijui na hajui anapotoka, ….na anakuwa hivyo kabla hajaanza kupandisha!

‘Mimi naona upumzike tu, huko tutakwenda kesho, maana sasa hivi hakuna usalama, na….’kabla Rose hajamaliza mlango ukagongwa, na kabla hajasema lolote mlango ukafunguliwa, na wote wakageuza macho yao mlangoni…hawakuamini, walijikuta wakihema juu kwa juu, kwani aliyekuwa kasimama mlangoni si mwingine bali nii docta Adam. Docta Adamu aliingia ndani akiwa kasawajika usoni, alionyesha uchomvu, baada ya hekaheka na kupambana na askari, kubebwa juu kwa juu hadi kituo cha polisi,….ili akafunguliwe mashitaka ya uzembe kwa kusababisha mtu anayetafutwa na jeshi kupotea …..Alipoingia alishikwa na butwaa, kwanza alifikiri labda ni mpenzi wa Rose, ambaye hamjui, lakini amjuavyo Rose, alikuwa kaapa mbele yake kuwa hataki tena mwanaume, sasa huyu ni nani…!
Kabla hajasema samhani kuwa kawaingilia bila hodi, macho yake yakatua kwa yule mtu, na akabakia kumwangalia kwa makini, na alipohakikisha macho yake akaanza kusema, huku akimsogelea yule mtu kwa karibu, na ghafla akasimama, alipokumbuka jambo, akasogea kinyumenyuma, na kusema;
‘Rose, huyu mtu ….si ndio yule mgonjwa aliyetoroka, si diye huyu anayetafutwa kama …oooh, Rose unafanya nini jamani, kwanini unapenda kuniweka rehani….huyu hatakiwi kukaa humu, …ngoja niwapigia polisi..ooh, hawa maaskari waje wamchukue haraka…mimi nimeponea tundu la sindano, na nawashukuru sana raia wema, kwa kuamua kuandamana kwa ajili yangu na sijui nani kawafahamisha na kuwaunganisha kwa muda mfupi, ….wamejitokeza watu wengi ajabu, kupinga kitendo cha mimi kukamatwa….nawashukuru sana…sasa wewe unataka kutibua juhudi za wananchi, unafikiri wao watatuelewaje wakikuta tunawakumbatia maadui wao…!’ akatoa simu yake , lakini Rose akamwahi kabla hajaanza kupiga namba.

‘Bosi sikiliza kwanza, usikimbilie kwanza kufanya hivyo, wewe ni dakitari, umeshanifundisha kuwa tusichukua maamuzi juu juu bila vipimo…naluomba ujaribu kumpima, kwa kumhoji, ili uone ukweli kutoka kwake, hebu muhoji uone kama kweli ndiyo yeye wanayemtafuta au ni kufananisha tu…huyu haendani kabisa na huyo mtu wao, huyo hana kabisa dalili za uaskari, nafikiri kuna makosa yametokea, tutamwingiza mtu mwingine hatiani bure, ukumbuke ile jela ilivyo, na huyu mtu ni mgonwa bado,…nakuomba kwanza jaribu kufanya utafiti wako kabla hujafikia uamuzi huo…tafadhali bosi…’ akasema Rose karibu kumpigia magoti bosi wake na kumfanya Adamu abakie ameduwaa na huku anamgeukia yule jamaa.

‘Wewe ni nani…umetoka wapi na kilikukuta kitu gani hadi ukapoteza fahamu..?’ akauliza Docta Adamu kwa sauti ya kiaskari.

‘Docta, …ooh, Bosi, mimi sijui , sijijui, na ..sielewi nini kinaendelea, siwezi kukujibu hayo maswali yako kwani hata mimi ninajiuliza hivyohivyo…sijijui kuwa mimi ni nani, natoka wapi,nimekutana na masahibu gani…na kwanini nilipoteza fahamu…sijui kabisa….naombeni munielewe hivyo…’ Akasema yule mtu.

‘Unaona Rose, yale yale tuliyoambiwa, tabia nizilezile alizosema yule mkuu wa kikosi, mimi nashauri hivi, na sio nashauri, ila ndivyo ilivyo, kuwa ili kufanya maisha yetu yawe salama, ngoja nimuite yule mkuu wa kikosi yeye atagundua ukweli, na atajua nini la kufanya kuhusu huyu mtu, lakini kukaa na huyu mtu hapa ni kutaka kunimaliza, na hata wewe utakuwaje na uhakika wa usalama wako, humjui huyu mtu hana ndugu, eeeh, hujui kuwa ndio yeye au la, na hata kama sio yeye, utakuwaje na imani naye…ukae naye humu ndani, hujitakii mema hapana hilo haliniingii akilini ngoja nimpigie mkuu wa kikosi, yule ni muelewaji sana…atapima mbivu na mbichi, na alisema anamjua huyo mtu kwa sura…kwahiyo…acha nimpigie simu….’ akaanza kubonyeza kwenye simu yale na kabla hajaanza kuzitafuta namba, mlango ukagongwa kwa fujo…wote wakageuka kuangalia mlangoni..moyo ukiwa lipulipulipu….na kugongwa kukawa kwa fujo, kuonyesha huyo mgongaji hana subira….

Nb, je tuendelee au tuishia hapa kwa muda?


Ni mimi: emu-three

1 comment :

Pam said...

OMG!!!!!!!!!!!!!!!!