Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeThursday, August 11, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-13Kamanda wa kikosi maalumu alionekana kutokutulia, akiwa anatoa maagizo huku anasikiliza simu, mbele yake walikuwa wamesimama wapiganaji, wakisubiri amri…alipotulia kidogo akaanza kuhutubu, kwanza kwa kuwaasa wapiganaji kuwa kazi iliyopo mbele yao ni kubwa sana ukizingatia kuwa watu wanaopigana nao ni maaskari walikuwa majemadari, wataalamu , na wanaojua mengi kuhusiana na vita. Hata hivyo aliwapa imani kuwa wao wanapigania haki, wanapigania nchi yao, wanawapigania raia wao, kwahiyo kushinda kwao ni dhahiri kuliko hawo watu walioasi ambao kwa asilimia kubwa walikuwa wakipigania ubinfsi wao, …’ mara akakatisha na kusikiliza simu…baadaye akaja mmoja wa kamanda msaidizi akawa anamnong’oneza sikioni.

Mara yule kamanda mkuu akaonekana kuvutia na yale mazungumzo aliyokuwa akinong’onezwa, na hata yule kamnda msaididzi wake alipomaliza, bado kamanda yule alionekana kuwa na hamasa, na akainua simu kusikiliza kutaka kujua zaidi na baadaye akatulia na akaanza kuongea kwa harakaharaka ili kumaliza ule mkutano kwa kusema

‘Kama nilivyosema sisi kama maaskari tunapigania haki ndani ya sheria ya nchi na kwahiyo tutashinda tu, na hivi sasa nimepokea taarifa kuwa mambo yameiva, kwani yule ambaye tulikuwa tukimtafuta siku nyingi, keshagundulika wapi alipo, kwahiyo kile kikosi maalumu kisogee mbele, ili tupeane majukumu,na wengine mrudi maeneo yenu mkisubiri taarifa yoyote…kwani vita sasa vinafika ukingoni, hawo majangiri, au magaidi sijui wameshaanza kutapatapa, wameishiwa, na sasa wanaanza kujitokeza kwa raia, na wengi wao wanaishia kufanya maasi kama vile kubaka raia, kuiba na hata kuua raia wasio na hatia…na hapo jukumu letu linazidi kupanuka ili kuisaidia polisi, kwa kuingia uraiani,…huko ilikuwa sio eneo letu, lakini kwa vile maadui wetu wameamua kujificha huko, tutawafuta huko huko…nawaomba tuwe macho wakati wote, .…’ akamaliza kiaskari na kuondoka pale kama ada yao.

Baadaye yule kamanda alikutana na kikosi chake maalumu na kuanza kukipa maagizo, na hayo maagizo yalitakiwa vitendo mara moja…, akaanza kuwaambia askari wake ` wapiganaji kuna watu waliasi jeshi, na watu hawo walikuwa maarufu sana, walikuwa wataalamu wa nyanja mbalimbali, viongozi wenye dhamana na wapiganaji wenye shabaha, hawa wote waliasi na kukumbia jeshi kwasababu mblaimbali, sasa hawa wamekuwa kikwazo cha kufikia malengo yetu, na mapambano yanakuwa magumu…hili naliweka wazi kwenu, kuwa huko tunakokwenda sasa hivi tunakwenda kukutana na watu wanaojua kazi….sio mchezo, lakini kwasababu sisi tupo kwenye haki, tutashinda tu….
‘Vikosi vyetu vitagawanyika kwenye sehemu tatu, kuna kikosi kitakwenda porini kupambana huko kitaongozwa na kamanda Mwitu, kamanda mwitu chukua watu wako waweke sawa na waelekeze kama nilivyokuelekeza ushindi upo mbele yetu, hawana kitu tena huko…’ kamanda Mwitu akasimama kiaskari na kundoka kama ada kufuta kikosi chake.

‘Kamanda Mgumu, wewe na kikosi chako elekeeni ufukweni, kule kuna silaha zinategemewa kuingizwa leo usiku na hawa waasi, na waasi wengine watakuwepo huko, mnatakiwa kupambana nao, na ikibidi muwakamate wote na silaha zeo, maagizo nimeshakupa, ..kazi njema, ushindi daima…’ Kamanda mgumu akaondoka kiaskari kwenda kuchukua watu wake.

Pale wkabakia watu wanne, wakiwa wanasubiri majukumu, lakini kulipita kitambo kabla haijatolewa amri kuwa hawo watu wannne watafanya nini..baadaye kamanda mkuu akasema ‘sisi tuliobaki tuna kazi maalumu, kazi ngumu kidogo, na mimi nitaiongoza mwenyewe, sitaki makosa, akawasogelea na kuongea kama ananong’ona , ikiwa na maana kuwa anachowaambia ni siri kubwa;
‘Kuna habari kuwa mtu tunyemtafuta yupo eneo maalumu ambalo nitawambia tukiwa njiani, na mtu huyo ni yule mtaalamu wa silaha. Mtu huyu wengi hawamjui, kwani aliasi muda kidogo, …sio kwamba aliasi, hapana, aliondolewa kutokana na matatizo, hapa wanayemjua ni Kapteni Gango na Luteni Ijiru, wao waliwahi kufanya kazi na huyu mtaalamu. Mtaalamu huyu alipewa mafunzo nchi za nje, ikiwemo Israeli na hata Marekani, na kwahiyo sio mchezo, pamoja na utaalamu wa kivita kama kamando, ni mtaalmu wa kutengeneza silaha aina yoyote, na ilifikia hatua akawa anabuni silaha za hatari mwenyewe, ikiwemo mabomu…

‘Huyu mtu alikuja kuchanganyikiwa baadaye akawa kama zezeta fulani, na uzezeta wake ukawa unabadilika na kuwa mtu mkatili ajabu, anaweza akamshika mtu shingo akamvunja, anaweza akamshika mtu akamuuma kwa meno mpaka akakata nyama…ikafikia hatua mpaka jeshi likaona haiwezekani kuwa naye kwenye uwanja wa kivita, ni hatari…akapelekwa kutibiwa nje…aliporudi akawa kama katulia, lakini ghafla akaibuka, kuibuka kwake ni kukaa kimiya tu, ni ukimuuliza kitu hajui, na wala hajijui,…sasa ikawa ni kwa vipindi, mara anakuwa mzima mara anabadilika,…watu wengine wanasema ana mashetani, wengine wanadai ni laana za wazazi wake,….utaalamu wetu kihospitalini ukagonga ukuta, ikabidi arudishwe kwao, kwa matibabu ya asili…na tangu afike kwao akawa kama mtu aliyechanganyikiwa, hajui kuwa yeya ni nani anatoka wapi anafanya nini…kwahiyo hata ule utaalamu wake wa silaha, na uaskari ukawa kaputi, ..zero kabisa….

‘Hawa wenzetu walioasi wakamtafuta,…wengi wao wanamjua kwasababu wamefanya akzi naye wakaanza kumweka sawa, na kumtibia wanavyojua wao, nasikia akawa mzima, na akawa anawatengenezea silaha, silaha zenyewe za hatari,…lakini kwa taarifa za ndani hakupona kabisa, yeye hupewa kazi maalumu kuwa tengeneza silaha, akimaliza ile kazi hakumbuki tena alichotengeneza,kwahiyo kuna watu waliwekwa karibu naye, kumuiga na kujifunza utaalamu wake…wapo vijana wana akili za hali ya juu, lakini ndio hivyo, wamejiunga na waasi kwa tamaa, wakawa wanafunzi wa huyo jamaaa, na kwahiyo kukazuka wataalamu wapya, ambao ndio hawo wanaotengeneza hizo silaha zisizo na kichwa wala mbele, wao wanaagiza sehemu ya vifaa, mwisho wa siku wanaviunganishana kutengeneza silaha za hatari zaidi, zisizo na vipimo, kwasababu hawajafikia ule utaalamu wa huyo jamaa, wanajua juu juu tu, ila silaha ni silaha,zinaua, zinaangamiza na zingine ni sumu, na mabomu yanalipuka bila kujua lini au muda gani, hayakuweza kuweka kitaalamu …sasa vitu kama hivyo vikizagaa uraiani, kutatokea majanga ….

‘Kwa taarifa kamili silaha hizo zimeanza kuingia auraiani, …zinafanyiwa ujambazi…ili wapore wapate pesa, wapate chakula, wapate wapiganaji wapya….,watu wanuliwa kiajabu mkichunguza hamuwezi kugundua silaha ya aina gani iliyotumika, …kumbe ndio hizo silaha zakubunibuni…na chanzo ni huyo jamaa yetu na wanafunzi wake….

‘Karibuni huyu jamaa kaanza kupandisha , alipandisha akasambaratisha wanafunzi wake karibu wote waliokuwa karibu naye, aliwawaua kama kuku, ananyonga kwa mkono wake mwenyewe, mmoja baada ya mwingine,…hutaamini hilo, na alipohakikisha kawamaliza akatoweka….inasadikiwa alikimbia hadi ziwani akazama, wengine wakadai keshakufa ,… lakini hakufa, kaokotwa ufukweni akiwa kazimia hajijui, na tujuavyo matatizo yake yakitulia anakuwa hajijui , hajui kabisa afanyalo…na inasadikiwa aliokotwa akiwa kazimia na akapelkwa hospitali ya Adamu, lakini huyo Adamu anakataa kuwa hana mtu kama huyo…

‘Sisi ni tunajua nini tunachofanya, na kama nilivyowaambia huyo mtu, sio mtu wa mchezo, yeye akikushika anakunyonaga kama kuku,…anakuwa na nguvu ya ajabu sana, kiasi kwamba watu watano wenye nguvu hamuwezi,kumkamata, akiwa katika hali yake hiyo,…utapigasindano za usingizi zitaisha, na badala ya kummaliza nguvu, ndio unamuongezea nguvu…hiyo ndio ajabu yake…utafunga kamba za chuma, zitakatwakatwa…huwezi amini mpaka ukutane naye akiwa katika hali hiyo…akianza kupandisha ananguruma kama simba, na usiombe akaipata silaha hata mje kikosi kizima anakimaliza,…macho yake yanakuwa makali kuona risasi ikija, anaikwepa kiajabu kabisa… huyo hata huwezi kumuita komandoo, bali umemendo…

‘Mimi nazungumza hili kwasababu nimeshuhudia yote hayo hadi hatua yake ya mwisho tunamrudisha nyumbani, na nilikuwepo kwenye kikosi cha kumrudisha nyumbani….sio habari za kuvumisha, bali nimeziona kwa macho yangu mwenyewe,…. lakini hali kama hii inakuwepo tu pale anapokuwa kapandisha sijui ndio mshetani au ni kitu gani kinamvaa mwilii…ndio maana nimewaomba nyinyi toka kikosi maalumu cha serikali twende tukamkamate pamoja nawajua nyie sio watu wa mchezo,,…na zoezi hili litafanyika leo hii bila kuchelewa, na kibali cha awe mzima au hai, lazima akamatwe kimetolewa… mpo tayari…’ kamanda akawauliza wapiganaji wake.

‘Afande, mkuu, sis tupo tayari,…mimi namjua na uhatari wake, lakini siri kubwa ni kumkuta akiwa hajapandisha, na hapo tunaweza kumdunga sindano za usingizi, na kumfungia kwenye chumba maalumu….ila onyo, tusimuonyeshe kuwa tuna nia mbaya, tusijifanye kuwa tuwababe mbele yake…pili kama imetolewa amri, ya hai au kufa, basi mimi sioni kwanini tumlegezee…tuondoe uzia mkuu, maana akibakia hai itakuwa shida kwetu, lakini twendeni kwanza tukutane naye…kama ni yeye kweli …tuna akzi ngumu, maana sijasikia ile kashikashi yake ….’ Akasema yule Kapten.

‘Wachunguzi wetu wanasema ndiyo yeye, ila kipindi walichomuoana alikuwa hajapandisha na inaonyesha bado yupo katika hali ya kuzimia…ila wanasema kuzimia kwake ni kwa machale, wasio mjua wataona kalala, kumbwa yupo macho anawasoma kiaina…na anaweza akaamuka na kutoweka, …hilo ndio hatari zaidi, akitoroka hapo akaingia uraiani, atanyonga raia..’ akasema mkuu
‘Mkuu, tupo watano tu hapa, na ukumbuke kumpeleka nyumbani tulikuwa watu ishirini, na tuliweza kusambaratishwa, mapaka alipokuja yule mzee wa kule kwao akampa dawa gani sijui ndio akanyamaza, ….nina wasiwasi, …lakini twendeni tu..’ akasema Luteni

‘Hapa tupo watano, lakini kwa utaalamu wetu tunazidi mia…ndio maana nimewachukua nyie wataalamu, wa kila Nyanja, mumeiva, kikomandoo na kiutalaamu..twendeni kwenye gari….’ Akasema Mkuu
Kikosi hiki maalumu kikaelekea hospitalini kwa Docta Adamu, walipofika kama walivyotegemea, waliambiwa mtu huyo hayupo, kama ndio huyo wanayemzungumzia, alitoweka kiajabu, na mapaka muda ule walikuwa bado wanahisi kuwa yupo karibuni watampata tu. Hapo mkuu akaja juu, kuwa maagizo yalitolewa kuwa akiwa katika hali yoyote njema taarifa zitolewe imekuwaje akatoweka, na yule mtu aliyepewa hiyo kazi akasema kama alivyoambiwa ni kuwa bado walikuwa hawana uhakika kuwa ndiye yeye au ni mtu mwingine.

Amri ikatolewa atafutwe huyo mtu haraka, ndipo msako mkali ukaanza kwenye wodi na kila kona ya hospitali, lakini hawakumkuta mtu kama huyo, na hili likamfanya Docta Adamu akamatwe kwa ajili ya kuisaidia polisi. Na kwa kufanya hivyo, ikasababisha raia waipate hiyo taarifa kuwa dakitari wao kakamatwa, na haijulikani nani aliwapa taarifa, raia wakaungana na kuanzisha maandamano, kuwa wanamtaka dakitari aachiwe haraka…

NB, Ngoja niishie hapa ili nipate muda wa kuichunguza hii sehemu, ikizingatia tumeingilia sehemu nyeti na mkumbuke Rose, alikuja kwa docta, na alikuwa hana amani,na bosi wake alishamuhisi kuwa huenda kaua, na kama kaua, alimua nani? au alikuwa na kitu gani cha kumfanya asiwe na amani, na ukumbuke alikuwa hajamaliza kumsimulia Bosi wake…mnakumbuka hilo?
Nimeiandika sehemu hii harakaharaka na tunaweza tukakosa mtiririko mwema, tukutane sehemu ijayo, nitaangalia yote hayo kwenye sehemu ijayo…TUPO PAMOJA

Ni mimi: emu-three

1 comment :

Precious said...

Me nazidi kuchanganyikiwa tu maana natamani kujua nani aliingia nyumbani kwa Dr. Rose wakati mlango alifunga na nini alichokuwa anamsimulia Dr. Adam na maandamano ya wananchi vp yatasaidia dr wao kuachiwa? nasubiri kwa usongo m3 lete mambo na pole kwa majukumu yako mengi ya utunzi na ya kijamii.