Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, August 10, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-12




Docta Adamu alikuwa ofisini kwake, akiwa anapitia makabrasha mbalimbali ya kumbukumbu zake, hakuwa na hamasa ya mafaili ya wagonjwa, alikuwa akiwa na lengo la kumbukumbu za mahesabu, aligundua kuwa kuna hela zimeingia na hazionyeshi mlipaji ni nani, ila zimeanishwa kuwa zilikuwa zinalipia wagonjwa kadhaa waliotibia humo,…wagonjwa wenyewe, hata majina hayajaandikwa vyema, jina moja moja tu… hii sio kawaida, akasema labda wengine hawataki kujionyesha kuwa wao ni nani,…lakini wakija wakaguzi watamsumbua…akilini akasema hii haitampa shida sana, kwani angalau gharama za uendashaji zinakuwepo, ingawaje hazitoshi,…baadaye alipoona kuwa anatakiwa kulipia malipo mengi ambayo kuliko kiasi walicho nacho,…

Sasa Docta Adam akageukia kwenye watu wanaodaiwa, wakiwemo serikali, zikiwemo taasisi, …polisi na jeshi, na wote hawa walikuwa wadaiwa sugu,…akaandika kitu kwenye yenye mafaili, kumuhimiza mhasibu wake afuatilie, ….baadaye akageukiwa kwa wadaiwa wa kujitegemea akajikuta anakutana na bili ya mgonjwa asiyejulikana jina, akatizama maelezo yake, hayakumuingia akilini,…mgonjwa huyu..aaah,…

`Hawa watu bwana, wanaifanya hii hospitali kama ya serikali, kama ya kujitolea…lazima hili nilikemee…’ Akaliweka faili lile pembeni kwanza akiwa na nia ya kumuita mhasibu wake. Na wakati anainua faili jingine la mgonjwa mwenye kisa kama hicho, mara mlango ukagongwa…

‘Nani, ingia mlango upo wazi….’ Akasema kwa kuonyesha kuwa hakupenda usumbufu kwa muda huo kwani alitakiwa kuidhinisha malipo mbalimbali ikiwemo kodi za serikali na pesa waliyokuwa nayo haitoshi…na hapo alitamani angekuja mhasibu wake, na sio mgonjwa au mtu mwingine wa kumpotezea muda...Mara akaingia Rose!

Docta alibakia kumkodolea macho docta wake huyu , halafu akasema, ‘Rose kama sikosei wewe leo unaingia usiku, mbona umekuja saa hizi kuna kitu kimetokea au…kama ni mambo ya advance, hapana, hapana…hapana,…hapa nilipo kichwa kinauma, sijui haya madeni tutayalipaje’ akawa anaangalia pembeni, kuonyesha kuwa hataki kusilikila kitu, na lile faili alilokuwa akiliangalia akaliweka pembeni.

‘Bosi nimekuja kwa dharura,…lakini sio ya pesa, nina dharura mbili muhimu sana, moja ni ujumbe maalumu niliopewa jana, na pili nina kitu nataka kukufahamisha, sasa sijui nianze na lipi..’ akasema Rose huku akiwa bado kashikilia mlango, hakutaka kuuachia uwe wazi kabisa kwani bado alikuwa na wasi wasi na kitu fulani, na akaufungua ule mlango na kuacha nafasi ambayo anaweza kuangalia toka alipo na sehemu ya nje ya chumba hicho cha bosi wake na alipona kuwa ataweza kuona nje akasogea na kusimama ndani ya chumba, halafu akasogeza kiti kwa nyuma, ilimradi aweze kuona kwa nje…

Adamu akawa anamtizma kwa mashaka na kutamani kuangalia nini anachokiangalia kwa nje, na aliona ajabu jinsi gani docta huyo anavyoangalia nje mara kwa mara ,lakini akawa hana haraka naye kwani ukiwa na haraka katika kazi yake hiyo, unaweza ukatoa matibabu yasiyo sawa sawa, hiyo ndiyo hulka yake, na sio hulka yake tu bali ni hulka ya kazi hii ya udakitari,…kitu cha muhimu unapokuwa na mgonjwa mpe nafasi mteja wako ajieleze, mpe nafasi mgonjwa wako ajielzee kwa uhuru, kwani kila neno lake ni sehemu ya kutambua tatizo lake kwa undani. Akamwangalia Docta Rose akiwa na hamasa ya kujua nini kimemleta na ni lazima litakua jambo la dharura kweli…, kwani anamjua dakitari wake huyu hana mchezo katika kazi, …licha ya mapungufu yake ya hapa na pale, lakini anamkubali katika utendaji wake wa kazi.

Wakati anamwangali docta wake huyu, akakumbuka kuwa kuna barua yake ambayo alikuwa alitakiwa ampe, lakini alikuwa bado hajampa, na akaona huo ndio muda muafaka wa kumkabidhi, ilikuwa barua aliyoituma ngazi za juu kumuombea kwenda kusoma nje, na ilikuwa na majibu mazuri, wamepatikana wafadhili, na serikali imemkubalia ombi lake hilo….lakini kwake yeye alisita kumpa kwanza rose hiyo barua mpaka akamalishe masharti yakeambayo alitakiwa ayatimize ndipo aweze kuipata hiyo nafasi, na moja ya sharti ilikuwa kuhakikisha yule mgonjwa aliyepotea anatibiwa na kukabidhiwa polisi…lakini baada ya kutokea kutoweka kwa huyo mgonjwa, aliishiwa nguvu ya kumkabidhi barua yake hiyo na hakuwa na nafasi ya kulifuatilia hilo swala lake la kwenda kusoma, hata hivyo alijua kwa vyovyote lazima binti huyu akasome, huenda akawa nguzo muhimu ya hospitali yake…

Docta Adam akavuta droo za meza yake akaichukua ile barua na kuiweka mezani kwanza, kabla hata Rose hajaongea nini kilichomleta, akamwangalia Rose maachoni, huku akijiuliza nini hasa kimemlata.
‘Docta, Bosi, nashindwa nianze na lipi kwani yote ni mambo nyeti, lakini hayana budi yafikishwe kwako, najua upo katika wakati mgumu sana,…..na kama hivyo umesema upo katika bajeti ya malipo, lakini haya mambo mawili ni nyeti …na mtihani kwangu hata sijui nifanye nini…, lakini ndivyo ilivyo katika kazi zetu hizi, nimejifunza hilo, na nashukuru sana nimefanya kazi na wewe, kwani kutokama na wewe nimekuwa jasiri, kama isingekuwa hivyo, huenda jana hiyo hiyo ningelikwa nipo hapa ofisini na nisingetamani kurudi nyumbani kwangu…lakini nilipambana kiume,…’ akasema Rose na kuendelea kumtia hamasa docta Adamu kujua nini kilitokea.

‘Hebu anza na hilo la jana lililokufanya utake kukimbia kwako maana unaanza kuwa mwanasiasa maneno mengi….umebadilika sana Rose, sio kama siku za awali ambazo ulikuwa unadeka kama binti mwali…sasa naona umekomaa, haya ongea haraka maana unajua kazi zetu , muda ni kitu muhimu, lolote linaweza kutokea, na wewe unahitajika kurudi kujiweka sawa kwa kazi za usiku, sitaki mchezo sasa hivi hilo uelewe, na ujue bado kuna kazi kubwa ya kumtafuta yule mgonjwa…na…ok ongea kwanza’ akasema Docta Adamu na alipogusia hilo swal la mgonjwa aliyetoweka alikunja sura kuonyesha ni swala lililomgusa sana, na Rose naye aliposikia akitajwa huyo mgonjwa aliyepotea mara akatizama nje na alipohakikisha anachokitazama kipo akamgeukia bosi wake…na alionekana kiti alichokalia ni kiti-moto, hakikaliki na kumuacha bosi wake katika mshangao! ‘Huyu mtu ana nini…’ akawaza na bila kupoteza muda Rose akaanza kuhadithia tukio la jana, na alipofikia hatua ile pale alipogongewa malngo na kutoka nje, na aliporudi akakuta mlango upo wazi…akawa kama kashikwa na msisimuko fulani uliojaa na woga… kama mtu aliyetokewa na kitu ambacho hakimpi amani…

‘Docta wakati nimehakikisha kuwa hakuna mtu nje, baada ya kuzunguka nyuma ya nyumba na kuona kimiya, nikarudi kwenye mlango wa eneo langu, na mara mwili mzima uliniishia nguvu karibu nidondoke kwa woga, ndio maana na sema kufanya kazi na wewe kumenipa ujasiri wa hali ya juu nikakumbuka maneno yako kuwa unapokutana na matatizo jione kama upo na mgonjwa kwenye chumba mahututi, na mgonjwa huyo kaweka uhai mikononi mwake, licha ya kuwa uhai wa mtu ni swala la mungu, lakini ukiwa mbele ya huyo mgonjwa unatakiwa kujua kuwa mungu kakupa nafasi ya kumtetea uhai wake. Jipe moyo na jenga ujasiri kuwa sasa upo mbele ya hakimu mungu unatakiwa kutetea maisha ya mgonjwa wako, wewe ni wakili wake. …pambana na ujuzi wako, …na nilivyowaza hilo nikaanza kupambana kama vile napambana na amisha ya mtu, lakini hapa nilikuwa napambana kutetea maisha yangu…’ akasema Rose

‘Lakini ujuzi wako ni wa kidakitari sio wa kupambana na majambazi au sio hawo majangiri, waliokupa huo ujumbe ni kuwa wameishiwa huo ni uumbe wa mfa maji,…eti docta huoni kuwa huo ujumbe ni wa mfa maji…?’ akamuuliza,halafu kabla hajajibiwa akaendelea kusema, `Hawa watu wameanza kujitokeza wenyewe, mwisho wa siku watajikuta mbele ya sheria…hiyo njia wanayotumia ya mtutu wa bunduki sio njia ya halali ya madai …hata kama umeonewa vipi wewe kama askari unatakiwa kuwa mstari wa mbele kupambana kwa ajili ya nchi yako, kwa ajili ya raia, na sio wewe ugeuke kuwa mwiba, muuaji, mbakaji wa raia …’ akaongea Docta Adamu, na akainua mkono wake kuangalia saa, halafu akaendelea kusema;

`Kama ilivyo sisi madakitari..tunafanya kazi katika mzingira magumu, lakini tunapambana hivyohivyo na ukumbuke wakati mwingine unajikuta katika mtihani mgumu, mfano unamtibia adui yako, ambaye jana yake alitaka kukua, leo kaletwa mbele yako , yupo mahututi kwa ugonjwa wowote, na bado wewe kama dakitari unatakiwa kuyasahau yote ya jana unamtibia huyo adui yako kama mgonjwa mwingine yoyote na hapo hapo ukijua kuwa huenda akipona atakurudia tena kukuangamiza…hayo ndiyo majaribu ya kazi zetu, hatuwezi kufanya mapinduzi kwa kugeuza sindano za dawa kuwa silaha,…hiyo kwetu katu… kama dakitari aliyebobea katika kazi yake hawezi kufanya hilo…’ akasema Docta Adamu na Rose akaangalia nje akiwa na hamu ya kuelezea swala hilo lake kwa haraka, na wasiwasi ulikuwa umedhihiri wazawazi sasa.

‘Basi bosi, nikashika kitasa cha mlango ambao ulikuwa upo wazi, …inamaanisha kuwa aliyeingia hakuubamiza vyema mlango, kulikuwa na kauponyo kidogo, mimi nakumbuka niliubamiza vyema mlango wangu na sio mbovu, kuwa labda ulijifungua wenyewe….lakini upenyo huo usingekuwezesha kuona ndani, nilichofanya ni kuusukuma kidogo ili niweze kuona ndani na wakati huo ukumbuke panga lipo mkononi, nimegeuka kuwa askari wa silaha za jadi, na silaha yangu ni panga, kufa na kupona Bosi. Lakini kwa ndani kwenye varanda yangu kulikuwa hakuna dalili ya mtu, nikavuta hewa kwa kupitia puani ili nikisikie harufu, kwani nilikuwa nimejifunza kwa yule aliyeingia mwanzoni harufu yao, na kama ni yeye ningeliua kwa hiyo harufu, lakini sikusikia aina yoyote ya harufu.

‘Bosi nilianza kuwaza, kwanini nahatarisha maisha yangu, kwanini haya majanga yananiandama mimi, nikajiwa na wazo niurudishie mlango nije huku ofisini au niende polisi , lakini wazo la polisi nikalitoa kwani polisi kwenye hakuaminiki, unaweza kwenda ukageuziwa kibao, kwani mnaweza kuja nao wakakuta mtu hayupo, unafikiri itakuwaje. Nikaona nije ofisini,lakini ….nikasema ngoja nijipe moyo, nikausuka mlango taratibu , taratibu hadi wote ukabakia wazi huku nimejicha upembeni mwa ukuta, naagalia kwa kujificha, nikapitisha macho ndani , lakini sikuona mtu…ikawa mtihani, ina maana huyo mtu aliyeingia, atakuwa kajificha chumbani, au…

Nikajipa moyo nikaingia ndani, panga lipo mkononi, varandani hakukuwa na mtu na mlango wa chumbani sikumbuki kama niliufunga, kwani ulionekana dhahiri kuwa upo wazi, kama huyo jamaa aliamua kuingia ndani , basi hakutaka kuufunga ule mlango, nikawaza nifanyeje, nilichofanya niliparuza panga langu sakafuni, paaaah, …’ alipofika hapo akacheka halafu akaangalia nje.
‘Mbona unaangalia nje mara kwa mara , unanitia wasiwasi kuna nini huko…?’ akauliza Docta Adam
‘Bosi,nikajitutumua, nikajifanya sina uwoga nikaanza hatua za kunyata kwenda chumbani kwangu, moja ,mbili , tatu…nikawa nahesabu hatu hadi mlangoni mwa chumba changu, hapo nikaanza kumuomba mungu, nilimuomba anipe ujasiri, nikamuomba aniupeshia na balaa, kama ni adui alegee,kama ni nani sijui namtumainia yeye mungu ndiye atakayenisaidia na sio kwa ujasiri wangu, kwani sina ujasiri kwa lile alilolipanga…hutaamini mambi hayo yalinipa faraja nikaingia ndani ya chumba changu...

‘Nilitizama harakahraka kote sikuona mtu, nikasema moyoni ni yale yale ya mwanzoni, maana mwanzoni nilijiamini hivyo hivyo, nikavua nguo zangu, lakini nilipogeuka nyuma, mtu huyu, safari hii nikasema sifanyi makosa, nikaangali nyuma na mbele, nikasogea ndani, nikahisi mwili ukisisimuka, nikahisi kuna mtu ndani, nikainua panga juuu huku naangali huku na kule…sijiu kwanini mawazo yangu yote hayakunituma niangali dirishani, yaani mawazo yangu yote, kwenye kabati kubwa, ambalo mtu anaweza kuingia na kuificha, kilichonifanya niangalie dirishani na upepo, ambao ulilifunua pazia, na lile pazia lilikuwa kubwa sana, kwahiyo ukisiamama hapo unaweza ukafunikwa nalo, hata kama hukudhamiria kujifunika nalo…

‘Nikageuza kichwa, huku mwili umeanza kuogopa, kwani nilishajua kuwa kuna mtu, nilishajua kuwa kuna maadui wasionitakia mema, na ukumbuke jana tu kuna mwanamke kabakwa hadi akapoteza maisha, kuna watu wametekwa na inavyojulikana watu hasa vijana wanachukuliwa kwa nguvu ili wakajiunge na kundi hilo la wapiganaji wa msituni au akina mama wanachukuliwa kuwapikia na kuwahaudumia hawo wapiganaji…kwahiyo hapo nilipo , nilijua sasa ni zamu yangu, lakini nikasema sikubali, kama nikunichukua wanichukue nikiwa maiti na kama ni huo ubakaji wao, ama zao ama zangu , bosi nikageuka nikiwa na panga langu tayari kumwaga damu…nikiwa tayari kwa kesi ya mauaji

‘Nilipogeuka, nikamuona huyo jamaa, kasimama dirishani…’ akasita kidogo akiangalia nje, na bosi wake uvumilivu ukamshinda akainuka akitaka kusogea aone nini anachoangalia Rose , mara kwa mara, hakusogea sana, akachungulia lakini pale aliposimama mlango ukawa unamzuia, ila sehemu kubwa alikuwa anaona nje ya ile ofisi, hakuona kitu, akawa anahisi kuwa huenda docta kaua, na hapo anawasi wasi wa kukamatwa na polisi, ….akaanza kuogopa, kesi nyingine ya mauaji ambayo itaingiza kashifa kwenye kazi yao….hapa sasa ni kumtoa huyu docta mkukumkuu, kabla polisi hawajaingia hapo…

‘Docta, naona unapoteza muda na maelezo yako, na…polisi …sema umeua…aaaah, kama umeua, mimi siawahi kukushauri hivyo kamwe….,hebu sema ukweli, kama umeua hapa sio mahala pa kujificha, sikiliza docta…’ akawa anamsogeza kiti kilichokuwa kinamzuia ili apite akutane na Docta amtoe nje, kama nikuongela hilo swala, linatakiwa wakaliongelee nje ya ofisi, kwake, sio hapo…, na wakati anaongea hivyo mara kwa nje askari na gari la polisi likaingia,… Na Docta Rose naye aliposikia mngurumo huo akatambua hawo ni askari polisi, akasimama pale alipokuwa kakaa, na macho yakaanza kumtoka kwa woga, …..

‘Sasa umeniltea balaa Docta Rose, …kanini hivi, …kila mara ni wewe unakuwa wa kwanza wa kuniingiza matatani, unawaona hawo jamaa…..umeniletea balaa…sijui tufanye nini…hebu niambie haraka kumetokea nini, umemua nani…alikuwa nani….’ Akasema Docta Adamu, akawa anatoka pale kwenye meza yake aakijitahidi kuyaondoa yale mafaili kwenye meza, na kuyatumbukiza kwenye droo ya meza haraharaka, huku kwa jicho moja akimwangalia Docta Rose,…na wakati huo Docta Rose alikuwa kashika mdomo huku kaangalia nje kwa kupitia dirishani,…na mara ghafla, akageuka haraka, na akawa kama anaonyesha ishara kwa nje, kule alipokuwa akingalia mara kwa mara…kama anaongea na mtu kwa ishara, lakini alikuwa hatoi sauti, na kumfanya docta Adam afikirie kuwa huenda Docta Rose kaja na rafiki yake anajaribu kumuomba msaada fulani, akaamua kutoka pale alipokuwa kasimama, na kutoka kabisa eneo la meza, kwahiyo akawa yupo pale alipokuwa kakaa Rose, akitizama kwa nje, na hapo waliposimama walikuwa wakiona sehemu ile wanapokaa watu wanaosubiria wagonjwa wanaotaka kumuona Docta Adam..

Cha ajabu alichokiona kule ni hawo maaskari waliokuwa wamevalia nguo zao na silaha mikononi, wakiwa wanaingia mmoja baada ya mwingine, walikuwa watano…oh, ina maana ni kweli, ina maana Rose kaua,…mbona ….hapana haiwezekani, ….mungu wangu hawa maaskari wamekuja kumkamata muuaji, na mimi sasa nitashitakiwa kama msaidizi….na wakati sijui lolote…mungu kazi hii sasa imeharibika, ….bonge la soooo!

NB. Nashukuru kwa leo nimeweza kuandika sehemu hii, nimeiandika asubuhu subuhi, kwa kujiiba, ….TUPO PAMOJA

Ni mimi: emu-three

6 comments :

Pam said...

bp juu, nasubiri kifuatacho.

emuthree said...

Pole sana Pam! Wanasema heri Bp ya kupanda kuliko ya kushuka! Tupo pamoja !Pole sana Pam! Wanasema heri Bp ya kupanda kuliko ya kushuka! Tupo pamoja !

EDNA said...

Duuh endelea kutupa ohondo mwawane.

Iryn said...

Heee hatari cjui hata hapo itakuwaje tena... Mpaka naogopa

Simon Kitururu said...

Nimepita chapuchapu ila sijasoma bado episodi hii!

Ntarudi baada ya masaa fulani kwa kuwa kijiwe hiki huwa natulia kwanza kabla ya kudadavua!:-(

Precious said...

Mambo juu ya mambo jamani maana presha juu naogopa hata kuendelea na next episode.