Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeMonday, August 1, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-8Rose alifika mapema hospitalini na baada ya kuweka vitu vyake haraharaka alimwendea docta mwenzake aliyekuwa na zamu na kupewa maelezo ya wagonjwa wake , na hatimaye akafika kwa mgonjwa wake maalumu, alimtizama kwa makini huku akisikiliza maendeleo yake ambayo hayakuonyesha mabadiliko yoyote zaidi ya yale yale aliyoyaacha jana. Na ailipoisha mzunguko wa kukabidhiwa majukumu ya siku, na kabla hawajaingia kwenye kikao cha asubuhi kama kawaida yao, akaona arudi kwa yule mgonjwa wake maalumu amuona tana, ili ajue nini cha kuongea kwenye kikao chao cha kila siku asubuhi,
Docta Adamu alifika kwenye ile wodi, na kwenda moja kwa moja kwa yule mgonjwa akaona hakuna mabdiliko ni kama alivyomuacha jana, lakini vipimo vinaonyesha kuwa huyo mtu yupo hai,… lakini uhai uliopo ni kwa vile damu inafanya kazi na mapigo ya moyo yapo katika mwendo wa kuridhisha,cha ajabu mtu huyo hafungui macho, na iliyobakia labda juhudi nyingine zifanyike, kitu ambacho docta Adanu alikataza kuwa wasubiri kwanza siku ya leo kama hali itakuwa hivyo , inabidi njia nyingine zitumike …
Alipofika kwenye kile kitanda Rose alimshika yule mgonjwa mkono, akauminya akachukua mkono mwingine akafanya hivyohivyo halafu akamuuliza nesi kuwa kamfanyia usafi na kumpa dawa zake akaambiwa kila kitu tayari, akasimama pale kwa muda huku akimwangalia yule mgonjwa kwa muda halafu sijui kitu gani kikasema ajaribu kuweka masikio kifunai kwake, ili sikie mapigo ya moyo, ingawaje vyombo vyote vilikuwa vikionyesha kuwa sasa mapigo yapo sawa, sawa, akaweka masikio kifuani mwa yule mgonjwa akaona yanapiga kama kawaida, na wakati anainua kichwa ili amwangalie yule mgonjwa usoni, na hapo uso wake ulikuwa haupo mbali na uso wa mgonjwa akakuta wanaangalia ana kwa ana na yule mgonjwa…
Rose alipata mshituko wa mwaka kwani hakujua kuwa mgonjwa keshafungua macho, na aliambiwa na docta aliyeondoka kuwa muda wote mgonjwa huyo alikuwa kafumba macho akiwa bado yupo kwenye usisngizi mzito kama mtu aliyekufa, hata nesi aliyemfanyia usafi alisema hivyo hivyo…lakini macho aliyoyaona pale yalionyesha kabisa kuwa mgonjwa huyo alikuwa kayafumbua muda mrefu.. ulikuwa mashituko mkubwa kwa Docta Rose
Ule mshituko ulimfanya adondoshe kalamu na kadi la yule mgonjwa na kubakia kamwangalia yule mgonjwa na yule mgonjwa alikuwa naye kamkodolea macho Docta….
‘Sweetie, …Sweetie, I love you …don’t leave me, …..your only in my heart…’ akasikia maneno hayo yakitoka mdomoni mwa yule mgonjwa, akimaanisha kuwa ‘mpenzi……nakupenda , usiniache…’…Rose akawa anajiuliza anamaanisha nini `Sweetie’ ni jina la mkewe, mchumba wake au kwani ni neno wanalopenda kuitana wapenzi…na linamkumbusha mbali sana, na kumfanya akose raha, na macho yakaanza kujaa machozi…je huyu mgonjwa anamaanisha nini kwani haiwezekani kabisa kuwa anamwambia yeye…akamsogelea karibu kumwangalia machoni, na macho yao yakakutana…kwa mbali sana Rose aligundua kuwa ingawaje mgonjwa huyo aliyatamka hayo maneno lakini inaonyesha bado akili yake haipo hapo,…akachukua kidole na kufanya kama anataka kugunsa mboni ya macho ya yule mgonjwa, lakini hakuona kupepeseka kwa macho, … kwahiyo inawezekana anamuwaza mtu fulani, …au anakuwa kama anamuota huyo `Sweetie wake’ … ingawaje macho yapo wazi, lakini bado yupo usingizini…
‘Unajisikiaje mgonjwa, ….unajua upo wapi hapa…’ akauliza Rose kupima kweli je mgonjwa akili yake inafanya kazi
‘Don’t leave please, please my sweetie, I need you my Sweetie, don’t ever leave me, …remember our promise…that we will be togather….to…to..gather…rrrr…’ mara yule mgonjwa akaanza kukoroma kama mtu aliyekuwa kwenye usingizi mzito. Rose akamsogelea na kumkuta keshafumba macho akaangalia vipimo akaona mapigo ya moyo sio mabaya, ina maana karudi tena kwenye usingizi. Akawaza ina maana huyu mtu hajui Kiswahili, ina maana huyu mtu inawezekana ni huyo wanayemtafuta, ...kwani wanasema huyo jamaa anayetafutwa hajui vyema Kiswahili….hapana haiwezekani, hawezi kuwa gaidi huyu…akawaza halafu akamwangalia tena na kumkuta kalala kama mwanzo akafunua mboni zake za jicho akakuta kweli kalala tena.
Akaamuita nesi ambaye alikuwa katoka kidogo, na alipofika nesi akapewa maagizo kuwa kama itatokea huyo mgonjwa akaamuka amuite. …`hakikisha akiamuka tu unaniita haraka iwezekanavyo…naona ana dalili za kuamuka..?’a akasema Rose
‘Mbona dalili hizo nimezisikia toka jana kuwa ataamuka, ataaamuka lakini hakuna lolote, mimi nahisi huyu mtu anahesabu siku tu…’ akasema nesi.
‘Hiyo sio kauli ya kazi zetu nesi, kazi zetu ni kuokoa maisha ya watu, wagonjwa wetu. ..na kauli yetu daima ni kuwa mgonjwa atapona, sio kinyume chake asipopona tunatakiwa tujilaumu…, ingawaje ni kadara ya mungu, lakini moyoni tunatakiwa tujute….sasa wewe nakuona huelekei huko unakata tamaa mapema, usitoe kauli kama hiyo tena,…hakikisha akiamuka unaniita…’ akasema Rose
‘Sawa bosi nilikuwa nasema tu, …sina nia mbaya…’ akasema yule nesi huku akitandika mashuka kwenye vitanda vingine vyema na huku akijiiba kumwangalia yule mgonjwa kwa macho ya mashakamashaka. Aliona mgonjwa yule anampotezea wakati wake, alikuwa anataka ajiibe atoke akabangaize huku na kule, lakini kutokana na yule mgonjwa inabidi asitoke humo ndani kabisa…
Rose alikimbilia kwenye ukumbi wa mkutano na kukuta wenzake wameshaanza kikao na yeye alisubiriwa kutoa taarifa yake na mpangilio wakazi yake ya siku hiyo. Alielezea kazi zake na jukumu kubwa alilo nalo mbele yake kuwa ana mgonjwa maalumu ambaye anahitajika kuwa karibu naye sana…na alipoulizwa kuhusu hali ya huyo mgonjwa inaendeleaje akasema bado hajazindukana…
‘Kama hajazindukana nina mpango wa kumuondoa hapa tumpeleke hospitali za serikali, kwasababu gharama zake zinazidi kuwa juu na hatuna uhakika wa kulipwa hela yetu ni vyema tumpelek hospitli za serikali ili wao wajue jinsi gani ya kumhudumia,…na kama akizindukana, haraka tumkabidhi kwa polisi…’akasema Docta mkuu.
‘Lakini itakuwa sio vyema kumuondoa mgonjwa huyo katika hali kama hiyo kwa sasa, ni vyema tuhakikishe amezindukana kwanza …’ akasema Docta Rose.
‘Hilo tutaongea baadaye mimi na wewe…ila hilo la kumuondoa hapa halipingiki , kazindukana au hajazindukana, …hata hivyo huyo mgonjwa sasa ni swala la polisi wao watajua jinsi gani ya kumshughulikia tusije tukafuga mtu ambaye atakuja kutupa shida baaadaye….umesema hajazindukana kabisa…?’ akaulizwa Rose
‘Mhh, bado kabisa….’ Akajikuta Rose akitamka maneno hayo huku moyo ukimsuta kuwa kadanganya na huku kichwani akijiuliza kwanini kafanya hivyo, inaonekana anachotamka kinatoka bila kusudio, na hakujua kwanini, kwani alijua kuwa huyo mgonjwa alizinduka mara moja na ile ni dalili kuwa hayupo kwenye hatari tena na kilichokuwa kinasubiriwa ndio hicho, ili wakakabidhiwe polisi na huenda hatamuona tena…
‘Sawa huyo ni mtu wako na ukumbuke huo ni mtihani wako, ukifeli kazi hapa utaisikika kwenye bomba…, kwa sasa mimi nitaonana na wanausalama tuone jinsi ganii tutakavyomuhamisha kutoka hapa, mengine tutaongea baadaye, na kila mmoja akawajibike , mjue hii sio zahanati ya serikali ingawaje imekuwa karibu na serikali kwa utendaji wake mzuri, pale inapobidi tunatoa msaada lakini wa dharura, na dharura hiyo haitakiwi izidi wiki, hatuna uwezo huo, vinginevyo mtakaosa mshahara, …tutaifunga zahanati hii na mimi sitakubali kwa uzembe huo…tawanyikeni mkawajibe…
Baada ya kikao hicho Rose aliamua kurudi kule wodini ili kuona hali ya mgonjwa wake, alipofika alimkuta kama alivyomuacha, akamchukua vipimo vya kawaida na kabla hajaondoka, akamwangalia sana yule mgonjwa usoni, na wakati anamwangali mawazo yake yalikuwa mbali sana, na hili limekuwa likimjia kila mara hasa baada ya kukabidhiwa huyo mgonjwa,…amekuwa kama katoneshwa kidonda kilichopona, na kujikuta akiwaza sana yaliyopita , kumuwaza msalaiti wake…`kwanini huyu mtu anafanana sana na msaliti wangu…’, akajiuliza kichwani, haiwezekani, isije ikawa ndiyo yeye…hapana yule alikuwa mrefu na mweupe kidogo, …na hata hivyo msaliti wake alikuwa anajua Kiswahili ingawaje anakiongea kwa kuchanganya na kiingereza, kwasababu ya kusomea huko na kuishi sana huko… sio kama huyu, huyu anaonekana hajui Kiswahili…,
Wakati anamuwaza msaliti wake, ambaye alimfanya apoteze fahamu siku alipopokea barua yake kuwa harusi haipo tena …`sitoweza kuisahau siku ile…ilikuwa kama kisi kinapitishwa moyoni mwangu…sitamsahau jamaa huyo na sidhani kama nitaweza kumsamehe…ni muuaji …’ alisema kichwani mwake, huku kumbukumbu za tukio lile zikimrejea kichwani tena hasa kuanzia pale alipofika chumbani kwake….
, kwani alipofika chumbani kwake kama walivyokuwa wamepanga yeye na rafiki yake ubaada ya kupata usingizi kidogo na kumaliza kuoga, yeye atachukua baadhi ya nguo zake anazoona zinafaa kuvaliwa siku hiyo elekee kwa shoga yake, wajaribu kuangalia ni ipi inayofaa kwa siku hiyo. Basi alipofika akajitupa kitandani huku aiwa na mawazo ya maandalizi ya harusi yake, ambayo ilikuwa mbele yake. Alikuwa hana mawazo kabisa na sherehe ile ya kumaliza masomo yake, sherehe ile aliiona kama inampoteze amuda wake, kwani kehsamaliza hatua kubwa , mitihani kafanya vizuri, kilichobakia ni kupangiwa kazi na baada ya hapo watajuana yeye na mume wake, ingawaje walishakubaliana kuwa baada ya ndoa wanaondoka pamoja kwenda huko Marekani ambapo ataendeleza amsomo yake.
Kabla ya huyo msaliti wake alishawahi kuchumbiwa na jamaa mmoja toka huko kijijini kwao, jamaa huyo alimpenda sana Rose, ingawaje Rose hakuwa na mapenzi naye sana, ilibidi ampende kwasababu ya ile lugha kuwa asikatae riziki, kwani huyo labda ndiye chaguzi lake toka kwa Mungu, hata hivyo wazazi wa pande zote mbili wana urafiki wa muda mrefu, …kilichomkwaza zaidi na jamaa huyo ambaye ni mfanya biashara ni kuwa yeye alimwambia kuwa hataki asome, anataka amuoe awe mke wa nyumbani, au amfungulie zahanati huko kijijini, lakini yeye awe kama msimamizi tu. Jamaa huyu alikuwa anapenda sana kujinata, kuwa yeye ni tajiri na kweli alikuwa tajiri, familia yao ilijaliwa kuwa na utajiri toka enzi za mababu zao…yeye anasema kuwa hapendi mke wake awe anahangaika, kama ni pesa anazo, sasa kwanini mke wake afanye kazi ili iweje…siku moja wakati Rose karudi likizo, akaamua kumtembelea jamaa yake huyo alifika nyumbani kwake na kukuta walinzi wanamzui kuingia akashangaa kulikoni.
Akalazimisha na kuingia ndani,…na kuwaacha walinzi wakiwa wameshika vichwa vyao…na Rose akawa na shauku ya kujua kwanini kwasababu walikuwa wakimjua kuwa ni mchumba wake mtarajiwa sasa kwanini wamkatalie kuingia…Akaingia ndani moja kwa moja…akiwa na shauku ya kujua kwanini wanamzuia kuingia… aliingia hadi varandani,…alishawahi kuingia hapo mara nyingi , kwahiyo alijua wapi ni wapi, ingawaje lilikuwa jumba kubwa la kifahari…lakini safari zote alizowahi kua hapo hakuwa na mazoea sana ya kuingia chumbani kwa yule jamaa, licha ya kuwa alishawahi kumshawihi kufanya hivyo , na siku moja karibu akubali akarudia mlangoni na kukimbilia kwako…leo akajitosha chumbanikwa hasira…hasa baada ya kukorofishana na wale walinzi kwanini wanamzuia kuingia, kwahiyo aliona kun ajambo…akaamua kuingia hadi chumbani ili kuona kulikoni, ndipo akamkuta jamaa akiwa kitandani uchi na wanawake wawili….alipiga ukunga wa nguvu na kuwafanya wale wazinzi waliopo pale kitandani kushituka…na kutoka kwenye lile jumba kama mwehu…
Alipoondoka hapo hakurudi tena, na wakati yupo njia kachanganyikiwa akagongwa na gari…na kupoteza fahamu. Alipozindukana alijikuta yupo hospitalini, hakuumi asana, ni michibuko midogomidogo, na akajikuta mbele yake yupo jamaa mtanashati, mrembo kavaa vizuri, akimwangalia kwa macho ya huruma, akamsogelea pale kitandani aliporuhusiwa na docta, na kujitambulisha kuwa yeye ndiye aliyemgongwa kwa bahati mbaya, kwani alikuwa katika mwendo wa kasi na yeye ina maana Rose aliingia barabarani kwa ghafla, na ikshindikana kufungwa `breki’, ila alijaribu kumkwepa ndipo akasukumwa na kudondoka nje ya barabara..
‘Samahani sana, lakini ulionekana kuwa na mawazo mengi sana, mpaka unaingia barabarani huku hujielewi …tunashukuru mungu hukuumia, pole sana…’ akasema yule jamaa. Na jamaa yule alikwua mwema sana kwake na alihakikisha kuwa anapata huduma zote, na kwa vile hakuumia aliruhusiwa kurudi nyumbani. Na hakuishia hapo alifika hadi nyumbani kwao kujitambusha na kuanza mazoea ya kuja mara kwa mara nyumbani kwao Rose. Alikuwa mpendevu, mcheshi na kumjali sana Rose, mapaka Rose akaanza kusahau machungu yaliyompata kwa uda mfupi, lakini walisema wahenga kuwa mtu akiumwa na nyoka akiguswa na ukoka bado atashituka tu….
Na hata Rose aliporudi chuoni, huyo jamaa alikuja na gari lake akampeleka hadi chuoni kwake. Kipindi hicho ulikuwa mwaka wake wa pili wa kozi ya udakitari ambayo inachukua miaka mitano. Katika miaka mingine mitatu wakaanza kujenga urafiki, kutumiana barua, kuwasiliana kwa simu na akija likizo wanakutana wanongea na kuzoeana sana na ilipofikia mwaka wa mwisho wa masomo yake, yule jamaa akamwomba uchumba.
‘Hapana siwezi kabisa kuwa mchumba wa mwanaume yoyote, nimeshasalitiwa na mwanaume niliyemwamini kabisa, ambaye wazazi wake wanajuana na wazazi wangu, anafahamika vyema, lakini alichonifanyia sitakisahau kabisa maishani…sasa sitaki kujiingiza kwenye matatizo mpaka nipate kazi yangu na kuhakikisha kuwa kosa hilo halitatokea tena…baada ya hapo nitaamua kuwa nataka kuolewa au la….’ Akasema Rose.
‘Hilo sio tatizo mimi nakupenda sana, na nipo huko Marekani , nisingependa kuoa wazungu, nataka nioe binti wa kikwetu,..mrembo kama wewe, msomo kama wewe… na ni matarajio yangu kuwa huko utasoma masomo yako yote, hadi uwe dakitari bingwa, hilo kwangu ni muhimu sana napenda mke msomi, baadaye tunaweza kufungua zahanati yetu, lakini kipa umbele ni kusoma kwanza au sio…?’ akasema mpenzi wake huyo. Na kauli yake hiyo ilimvutia sana Rose, ingawaje ilimchukua muda kukubalina ana ombi hilo, lakini baadaye akakubali, na kwa vile jamaa yake huyo alikuwa anakuja mara moja moja kutoka Marekani kuwatembelea wazazi wake…harusi ikapangwa haraka haraka, na kuwa safari hii akija kwa ajili ya ikizo fupi kwa kusuio moja tu la kuona na kuondoka, watafunga ndoa ya haraka na fungate inaenda kufanyika huko Marekani…, kwahiyo ajiandae!
Kumbukumbu zake zilipomfikisha hapo alijikuta machozi yakianza kumjaa machoni na kutamani kama angelikuwa na uwezo angelimtafuta huyo jamaa amkate kate na mapanga, na moyoni aliwachukia wanaume wote akisema kumbe wote ndivyo walivyo …na maandishi ya ile barua ambayo yalikuwa madogo madogo, yakiwa yameandikwa kwenye karatasi liyokunjwa mara mbili, na maandishi hayo yalitosha nusu ya upande mmoja wa ile karatasi. Ndivyo anavyoandika barua zake, maandishi madogo madogo na mara nyingi hayajai ukurasa mmoja.
Na alipoanza kuisoma ile barua pale kitandani macho yake yalikuwa kama yameshikwa na ukungu, akawa haoni vyema, ndipo alipoamua kwenda dirishani ili ahakikishe kuwa kweli alivyosoma ni sawa au anaota…hakuwa na guvu hata za kusimama, lakini alijitahidi hadi akafika dirishani kwenye mwanga mzuri, ili kwanza apate hewa kwani aliiona hewa ya mlendani ni nzito…pumzi ilikuwa ya shida…kama roho inataka kutoka na pili mwanga mle ndani ulionakana mdogo akaona autafute mwanga wa ne kwa kupitia dirishani…akafika dirishani na kuirudia ile barua…yale maneo yakawa kama yanajirudia rudia machoni mwake…lakini alihakikisha kuwa ni kweli kilichoandika …hapo hapo akajikuta anashikwa na kizunguzungu na hapohapo akadondoka chini na kupoteza fahamu.
Alipoingia rafiki yake na kumkuta katika ile hali, ndipo akaikuta hiyo barua ikiwa mkononi mwake, ikiwa imeandikwa kwa lugha ya kiingereza ikisema hivi ;

`I am very sorry to inform you that, our weeding will not wake out! I know how you will feel about it! But they said, what arranged by God may never cancel! I have met another fiancée, and we expecting to marry each other tomorrow, I hope you will meet someone else, more handsome than me..with everything , I am very sorry!
JACK.


Tafsiri yake…

‘Samhani sana kukufahamisha kuwa harusi yetu haitawezekana tena! Najua utakavyojisikia, lakini walisema kuwa kile kilichopangwa na Mungu hakiwezi kuzuilika! Nime kutana na mchumba mwingine, na tunatarajia kufunga naye ndoa kesho. Ni matumaini yangu kuwa utakutana na mvulana mwingine mrembo kuliko mimi. Mwenye kila kitu. Samhani sana.
JACK


Rose akajiona anaingiwa na uchungu na hasira kwa pamoja, akageuka kuondoka, hakutka hata kumwangalia yule mgonjwa wake tena, lakini kabla hajainua mguu wazo likamjia kuwa amchunguze vyema maungoni yule mgonjwa huenda kagundua kitu kinachoweza kumsaidia, kwahiyo akamsogelea na kumuondoa shuka huku anamkagua kwa macho kifuani, akainama na kumgeuza kumwangalia mgongoni, halafu akawa kamwinamia akimtizama usoni, ….sijui kitu gani kilimshika, akasema moyoni, `samahani sana sina jinsii inabidi tuagane leo maana najua bosi wangu alivyo, lazima utaondolewa hapa…nimekuzoea kwa muda mfupi , japo ni kwa hali kama hii…’ akasema kwa sauti ndogo, halafu akainama kumbusu shavuni akiwa na maana ya busu la kwaheri…akasogeza uso wake na mdomo wake ukagusa shavu la yule mgonjwa…

‘Rose mgonjwa anaendeleaje…’ sauti iliyomshitua na karibu amdondokee yule mgonjwa kwa kukosa nguvu, alishindwa hata kugeuka kumwangalia ni nani, na alijua kabisa ni nani na kama kaona alivyokuwa akimbusu huyo mgonjwa itakuwa ni moja ya kisingizio cha kuonekana kuwa hana nidhamu ya kazi….mungu wangu hili sasa ni balaa...ni skendo...!
Akaomba mungu amsaidie …kwani hakuwa na nia mbaya…na kabla hajageuka au kumjibu huyo aliyemsemesha macho yake yakatua machoni kwa yule mgonjwa,…akajikuta wanatizamana macho kwa macho na yule mgonjwa…
mshituko mwingine…

NB: Hata mimi nilipoyasoma hayo maneno ya ile barua macho yangu ymeingia ukungu, …na bado nikajikuta nikipata mshituko mwingine …mshituko gani huo…nimeshindwa kuendelea hapa, naona tuweke kiporwa tena, natumai tupo pamoja na blog yenu hii INAPENDA KUWATAKIA RAMADHANI NJEMA KWA WAISLAMU WOTE DUNIANI NA KUSEMA RAMDHANI NJEMA,...Ni mimi: emu-three

6 comments :

chib said...

Nami nasema, bado tupo pamoja

Mimi said...

Jamani em-three unajua kututega. yaani hadithi inazidi kunoga. keep it up dear, usichoke kupost kila siku please...mana imekuwa kama maji lazima ninywe

emu-three said...

Ninafurahi sana mkinitumia meseji, na nashukuru sana kwa wale wanaofanya hivyo, mungu awabariki sana, ... ni kwanini nasema hivyo, ni kwasababu ninapoandika nipo peke yangu, na wakati mwingine katika mazingira magumu ya kujiiba, huenda katika kuandika harakaharaka kuna makosa au huenda haijakaaa vyema, ..wewe ukisoma ni rahisi kugundua hilo, basi nitumie maoni yako ili nijue.
Nawashukuru sana Mkuu Chib na Mimi kwa kuwa wa kwanza kuonyesha kuwa tupo pamoja na wengine wote, tuendelee kutuma maoni, kwani nayahitaji sana,
Kisa kinaendelea...

Iryn said...

Mmmnh mambo yanazd kunoga sa cjui itakuwaje hapo daah.. Pamoja sana

emu-three said...

Iryn nashukuru kuwa mpenzi mwema wa blog hii

Rik Kilasi said...

Duh umetisha mkuu mie nasubiri kwa hamu ilivyoendelea lol