Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, July 15, 2011

Dawa ya moto ni moto-35



Maneno mimi siendi  huko nje ya geti , nataka kukutana na huyo anayejiona `kidume’ nataka kupambana naye…’ akasema Maua na kumshangaza Maneno. Maneno alimwangalia kwa makini na huku kamshikilia mkono, hakutaka kumwachia, kwani alikuwa anajua kuwa ni hasira, toka lini mtu akapambana na watu walio na silaha kwa mikono mitupu…akawa anajaribu kumvuta kiujanja ili watoke nje…, na wakati anatafuta mbinu za kumtoa mkewe nje, mara wakaona jamaa mmoja akija na nyuma yake yupo mwanamama bonge, ilibidi wote pale washikwe na mshangao kwani walijua kuwa hakuna hata mtu mmoja aliyebakia ndani, sasa wanashangaa hawa watu wametokea wapi, lakini haikuwa na shida sana kwani lile tishia la bomu lilikuwa limezimwa…
Wale jamaa wawili walipowakaribia, huku mwanamama akionyesha kuwa alikuwa akilia, na mwanaume akijaribu kumbembeleza, na kabla hawajafika pale waliposimama mara tena ghafla wakasikia sauti za watu wengine zikitokea upande wa pili yake, kutokea eneo la baharini, hawa sasa walikuwa ni askari polisi wakiwa wanakuja pale waliposimama akina Maneno na wenzake. Walikuwa na silaha zao, kuonekana bado wapo kazini wakiwa wamemshikilia jamaa mmoja ambaye alionekana kuvuja damu,  na mara kwa mara walikuwa wakimsema huyo jamaa na kumsukumasukuma, kuwa atembee kwa haraka kwani alionekana kama anakaidi hasa alipoona kuna kikundi cha watu kipo mbele yao…
‘Hahaha nyinyi mnapoteza muda wenu bure, …hii maana yake nini, kunidhalilisha au….mnanishika mimi kama nani mna ushahidi gani kuwa ni mimi ambaye mnayemtafuta, hebu waulizeni watu wote ambao mnawajua kuwa watakuwa mashahidi wenu, kuwa kweli walishawahi kuniona mimi, au kweli wananijua kuwa niliwahi kuwafanyia ubaya…hakuna hata mmoja, kama kweli watakuwa wanasema ukweli…’ akasema yule mtu.
‘Unajifanya mjanja saana, tutaona mbele ya sheria, unafikiri hatukujua hilo kabla, ujanja wako wa kujibadili sura ulishagundulika…ninakuthibitishia kuwa leo umefika mwisho wake, unafikiri sisi wajinga sana, kuwa hatujajiandaa kwa hilo…subiri hutaamini ukifika mahakamani, …angalia hawo wenzako walivyo wajinga, badala ya kujisalimisha wanataka kupambana na dola…sasa wamepata nini, wamejifanya wajanja sasa wanaenda kuliwa na mchwa makaburini, na huko nako adhabu inawasubiri, sasa bado zamu yako…bora utilize kichwa chako ufikiri jinsi ya kupunguziwa adhabu ya kifo….badala ya kunyongwa ufungwe kifungo cha maisha…lakini eti ujanja wa kukataa kuwa wewe sio wewe…unanishangaza sana’ akasema Inspekta akiwa kaongozana na yule jamaa huko nyuma yao wakiwemo askari wengine ambao walikuwa wanahakikisha hampi nafasi.
Alipowafikia akina Maua na Maneno, aliwaangalia kwa muda halafu akageuka upande wa pili yake walipokuwa wamsimama akina Bosi na mkewe, akasema `hebu waulize hawa kuwa waliwahi kuniona wapi…kama mimi ndiye mhusika…’ akasema kwa kujiamini.
‘Hilo halina maana hapa,…kwanza kwanini tuwaulize hawa, kama kweli huwajui kuwa uliwafanyia nini…ndio kwasababu wakati unawafanyia hukuwa na sura hiyo… tutaona huko mbele kwa mbele, hebu kataa kuwa hili jumba sio la kwako, kataa, tulipige mnada…’ akasema Inspekta.
‘Kuwa jumba ni langu sio sababu ya kunitia hatiani, unaweza ukawa na jumba lakini usiwe unalifanyia kazi wewe, umalipangisha…hapo umenoa Inspekta, nakuambia mtapoteza muda wenu na nitawashitaki kwa kunibambikia kesi za uongo….’ Akasema yule mtu huku akiangalia huku na kule.
 Maua akamwangalia sana yule mtu na kumbukumbu zikaanza kumjia,akaanza kuikumbuka ile sura…, ni kipindi kirefu sana mama yake akiwa hai, na ingawaje ….ndiyo  yeye,…huyo ndiye alikuwa akifanya kazi kwenye bustani ya wazazi wake, ndiye…huyu….ingawaje mama yake alisema siku moja alimkta nyumbani kwake akiwa karibu kufa, kumbe hakuuwawa, bado yupo hai, …kumbe ndiye huyu alikuwa akijifanya ….hapo hakusubiri kuulizia alichukua kibegi chake ambacho kina vyuma-vyuma vinavyoumiza akambamiza na hicho kibegi yule jamaa kichwani…ilitokea haraka sana, hata askari hawakutarajia hivyo,  kwani hata huyu jamaa alijikuta katika mshangao wakati kipigo hicho kikiingia kichwani…
‘Wewe vipi…mwehu nini…nita…ku…’ akasema wakati akizuiliwa na polisi na Maua akaondolewa pale mbele yake. Ikawa mshike mshike tena….
‘Wewe muuaji mkubwa …unajifanya mjanja sio, wewe ndiye uliyekuwa ukifanya kazi nyumbani kwa wazazi wangu kama mtunza bustani, …unajifanya sikukumbuki, wewe  ndiye uliyemzalilisha mama yangu hadi akawa mlevi…wewe ndiwe, …ulikuwa unatuma watu wachukue mapicha mchafu kwa ajili ya kupata pesa …`blackmailer’ mkubwa wewe…niacheni nimuonyeshe kazi huyu, anajifanya kidume…kumbe mwoga, kwanini ulikuwa unajificha huko chumbani kwako na kutufungia kwingine, kwanini hukujitokeze tukapambana na wewe uso kwa uso…muuaji mkubwa wewe..ngoja tu nipate nafasi nitahakikisha nakudhalilisha kama ulivyomfanyia mama yangu…hebi niachieni nimuonyeshe kuwa mimi sio mwanamke kama anavyonifikiria yeye….’ Maua akawa mbogo
 Mke wa Bosi naye alikuwa akimkagua sana yule jamaa ambaye alikuwa sasa kashikiliwa na polisi huku akiwa sehemu ya usoniimevimba…na aliposikia wasifa wa huyu jamaa akamchunguza vyema yule jamaa, na kwa  muda huo walikuwa karibu sana na yeye, akagundua jambo …macho ya yule jamaa, hayajifichi, …kumbukumbu zikaanza kumjia, hata sauti…ndiyo huyu mhasimu wake, … ndiyo yeye alikuwa akijbadilibadili, leo docta, kesho mtunza bustani, mara mkurugenzi na ….ndiyo yeye, aligeuka mara moja na kwa nguvu zote aliwarukia wote, si askari au yule jamaa aliyebakia amesimama, wote walikuwa chini…na mara yule mwanamama akamwinua juu kwa juu yule jamaa ambaye walishindwa hata wamuite nani…kwani hakutaka hata kutaa jina lake halisi ni nani…alimwinua kama kifurushi hewani na  kumbwaga chini kama gunia, ….ilitokea haraka, kiasi kwamba hata askari walipoweza kumdhibiti huyu mwanamama , jamaa alishakuwa katika hali mbaya sana…
‘Jamani twaomba msichukue sheria mikononi mwenu, kwani kesi hii inaweza kuwageukia  nyinyi wenyewe na kuitwa nyie ni wauaji,…kwanini mkimbilie kutumia nguvu wakati mnaona huyu keshashikwa, kafungwa pingu na sasa anakwenda mbele ya sheria, mnajua mkimuua huyu jamaa, hata kama ana makosa …nyie mtaitwa wauaji, …mtahukumiwa kama wauaji…achene sasa sheria ichukue mkondo wake, kwani mwisho wa yote ni hapa…kwenye mkono wa sheria….
 Watu waliokuwa mbali sijui walisikiaje, walianza kuingia kuona kuna nini, kwani walishasikia kuwa bomu limezimwa, na  mara gari la polisi likiongozwa na king’ora lilikuja na kumchukua mhusika mkuu, na maiti ya wenzake wawili ambao mmoja wao baadaye alitambulika kuwa ni msaidizi wa Inspekta, watu hawakuamini hilo, ….hivi kweli huyu jamaa naye alikuwa kundi moja na huyu mhalifu…naye alikuwa akijibadili sura mara kwa mara… na mwenzao mwingine alikuja kutambulika kuwa ni mheshimiwa katika ngazi za juu za serikali, wote walishirikiana katika kufanya uhalifu, kuagiza madawa ya kulevya na kuwadhalilisha raia kwa kuwachukua picha mbaya na kuwatishia kuwa kama wasipotoa pesa picha zao zitaonyeshwa kwa waume au wake zao au kuwekwa kwenye magazeti na mitandao….
                        ******
   Siku zikaenda, na watu wengine wakaanza hata kusahau, lakini sheria ilikuwa ikifanya kazi yake kwani, Ilikuwa siku nyingine ya kesi mbapo watu wengi waliokuwa wakiifuatilia hiyo kesi walijaa mahakamani ili waone nini hatima ya huyu mtu ambaye walishampandikiza jina la `kinyonga’! Kinyonga alifikishwa mahakamani kwa mara nyingine na leo ndio siku ya hukumu,…ilikuwa siku ya hukumu..kesi hii ilikuwa kubwa na yenye migongano ya kisheria, kwani mashahidii wengi walipoitwa , na kuulizwa je `huyu ndiye uliyemuona akija kukufanyia hivi au vile alisema ni yeye, walipoulizwa wana uhakika sura ndiyo hiyo, walisema sura siyo hiyo…sasa inakuwaje useme ndiyo yeye, wakati sio sura yake…ina  ila anahisi alijibadili sura..’ hii kuhisi ilileta utata sana, mpaka utaalamu wa alama za vidole ni zile ngozi ambazo alizokuwa akivaa vilipopatikana na kuvalishwa na hapo akaonekana jinsi gani alivyo kuwa akibadilika sura toka sura hii au ile, akawa kashindwa, …
‘Kabla ya hukumu, ndugu mshitakiwa bwana Freemason Kiburi a.k.a `kinyonga’..una la kujitetea…’ alipotamka hilo jina la `kinyonga’ watu wakacheka na kuzomea, hadi waliponyamazishwa na askari…
‘Yule jamaa alisimama, akawatizama watu, na baadaye akasema naomba jambo moja sana, hili ni muhimu kwangu, kuliko yote, na wahenga walisema asiyekubali kushindwa sio mshindani…ndugu hakimu, naomba nafasi ya mwisho ndogo sana, …kabla hujatoa hukumu yako, najua baada ya hukumu hiyo sitapata nafasi hiyo….’ Akainama na hakimu akamuuliza kuwa huo ndio utetezi wake
‘Utetezi wangu utakuja lakini naomba niongee na mmoja wa mashahidi, lakini sio hapa mbele, nipewe dakika tano tu niongee na yeye…’ akasema, lakini hakimu hakumpa muda huo akamwambia kama hiyo ni sehemu ya utetezi wake, anatakiwa aongee hadharani kila mtu asikie…, yeye akasema hilo hawezi kuliongea hadharani, …basi toa utetezi wako wa mwisho kabla ya hukumu!
‘Ndugu hakimu, haya ninayosema yanatoka ndani ya moyo wangu, kwanza yote niliyofanya, nawaombeni msamaha, najua sio rahisi kusamehewa kwa haya, lakini nyie mumesahau kuwa kuna watu waliwaua wazazi wangu…bila makosa, wapo nje…wamewanyang’anya wazazi wangu mali yao ambayo waliitafuta bila kwa jasho lao, …hawakuwahi kuchukuliwa hatua yoyote…
‘Leo mimi naonakan mbaya..ndio lazima nionekane mbaya kwani sio miongoni mwa watu mashuhuri…nakubali kupokea hiyo adhabu, lakini make mkijua kuwa mimi nilikuwa natetea mali ya wazazi wangu, ilibidi niichukue  kwa njia hiyo kwasababu kulikuwa hakuna njia nyingine…kwa kusema hayo naomba mahakama inifikirie ili niweze kuihudumia mali hiyo na kuhakikisha kila jasho la mzazi wangu limerudi mahala pake….’ Akatulia
‘Umemaliza..?’ akauliza hakimu
‘Ndio nimemalaiza kama hamtaki ombi , nimemaliza…’ akasema Freemason, a.k.a Kinyonga
Hakimu alisoma taarifa ya maksoa ya jamaa, na mwisho akatoa hukumu kuwa huyo jamaa kahukumiwa miaka 70 jela na adhabu kali….aliposema hivyo watu waksema `aaaah’ alistahili kufungwa kifungo cha maisha au kunyongwa…lakini watu wakasema akitumikia miaka yote hiyo akitoka ni mzee ambaye hataweza kufanya lolote….
                                                                      ********
Siku moja Maua akiwa katulia na mume wakiwa nje ya bustani , alikuja Inspekta…wakashituka kidogo, kwani kujiwa na askari bila taarifa inaleta wasiwasi hata kama huna kosa, wakabakia mdomo wazi. Inspekta aliwasilimia na kuwatoa wasiwasi, kwa kuwaambia kuwa amepita tu mara moja kusalimia, hakuna jambo baya. Na baaada ya kutulia kidogo akipata maji ya baridi, akajifanya kama kakumbuka jambo na kumwambia Maua, kuwa alipata ujumbe toka kwa Freemason, kuwa anakuomba umtembelee gerezani, yupo gereza la Ukonga. Uumbe huo ulipitia kwa Inspekta mwenyewe, ilia je amshawishi Maua afike huko gerezani, kwani huyo jamaa alikuwa na ujumbe muhimu…anaomba sana amuone Maua… Maneno na Maua wakabakia kushangaa huyu mtu anataka kumuona Maua kwa lipi, anatka kumuomba masamaha …Maua akamwambia Inspekta kuwa hataki kumuona huyo mtu kabisa, kwani akimuona atamkumbusha mengi, na huenda akshindwa kuvumilia, yeye anatamani kulipiza kisasi kwani adhabu aliyopewa haistahili, ni ndogo sana…
‘Najua una uchungu sana, lakini usikatae wito, kwanza kasikiliza anachokuitia halafu utajua nini la kufanya baada kusikia ulichoitiwa, ama kukataa au kukubali,…’ akasema Inspekta.Halafu kabla hajaondoka akauliza hali ya baba wa Maua inaendeleaje.
‘Baba anaendelea vyema, ile gesi haikumuathirii sana, tunamshukuru sana yule mlinzi aliyekuja kuwaokoa mapema, kabla ile gesi haijasambaa mle ndani…watu wengi waliokuwepo hapo walijua kabisa kuwa wameshakufa….hata baba yule mhasimu wake naye hajambo, hutaamini kuwa sasa ni marafiki wakubwa, marafiki wa uzeeni…
Kesho yake Maua akaondoka kwenda Keko gerezani hakutaka kuongozana na mume wake, kwani ndivyo alivyoagizwa na huyo jamaa kuwa aje peke yake. Alipofika akasubiri chumba cha wageni, na huyo jamaa akafika, akiwa kasindikizwa na askari, alikuwa kakonda kwa muda mfupi, alipomkaribia Maua akasimama kwa muda, na mara machozi yakaanza kumtoka…
‘Unajua kwanini nalia, unafanana sana na mama yangu…lakini hayoo tuyaache, …kwanza kabisa naomba unisamehe…ujaribu sana kunisamahe, kwasababu unavyohisi wewe kuwa nimefanya ubaya, ndivyo ninavyohisi mimi jinsi gani wazee hawo wawili na mama yako walivyowafanyia wazazi wangu…sijui nikuelezeje ili uelewe…’ akasogea kwenye meza na askari alikuwa kasimama hatua chache kama alivyoagizwa kuwa huyo mwanamama anaweza akaleta vurugu kwahiyo asicheze mbali.
‘Ndilo hilo uliloniitia, kama ndio hilo, nasema hivi…kafie mbali, ..mimi naondoka zangu’ akainuka kuondoka.
‘Sio hilo Maua, nikuulize swali kuna mtoto anaweza kumkana mzazi wake…hata kama kamkosea kiasi gani, mtoto anaweza akamkana na kumkataa kabisa mzazi wake..? akauliza na kutulia.
‘Una maana gani kusema hivyo…kwasababu sikuelewi, usinipotezee muda hapa, wewe ni mhalifu na dawa ya uhalifu ndiyo hiyo, usitafute mbinu za kukwepakwepa majukumu ya wafungwa kwa kutafuta mtu wa kuongea naye…nenda kasote huko ndani…’ akasema Maua, na mara kabla hajainua mguu, wakaja jamaa wawili wakaongea na yule askari, mmoja wapo akatoa kidude kidogo cha kuweka kwenye simu(memory card), akampa yule askari..yule askari akakiangalia, ina maana alishaambiwa kuhusiana na hilo, lakini bado alitaka uhakika zaidi akapiga simu na kuulizia kuhusiana na hicho kitu, akaambiwa hakina maneno amfikishie huyu jamaa, lakini asibakie nacho…
Yule askari akasogea pale walipokaa Maua na yule jamaa Yule jamaa alikichukua kile kudude, na akawatizama wale vijana wawili, walikuwa wakifanana sana na huyu jamaa, ilionakana kuwa ni mzazi wao…
‘Maua naomba usifanye hivyo, kwani licha ya kuwa nina makosa, licha ya kuwa unaniona nimefanya mabaya, lakini hata kama ungekuwa wewe upo katika nafasi yangu ungefanya hivyo.Na nikuambie ukweli yote hayo nimefanya kwa ajili yenu, wewe na ndugu zako hawo wawili. Hao ni ndugu zako, watakuwa nawe bega kwa bega katika maisha yako, …’ Alipotamka hivyo Maua akageuza uso kwa hasira akiwaangalia wale vijana wawili ambao walitabasamu ….yeye alimgeukia huyo jamaa na kwamwangali kwa macho ya hasira ni kusngaa..
‘Huo ndio ukweli, kama hutaki, unataka huo ukweli ulivyo, …na hilo ndilo nililokuitia…., na hiki hapa ni kikadi ambacho nimehifadhi maeelzo yote ya sehemu ya mali yako, kila mmoja nimempa haki yake, hakuna mwenye haki ya kugusa mali ya mwenzake, na kila mmoja nimempa kitu kama hicho, kichukue kaweke kwenye simu yako, au mtandao unaokubali, utapata maelezo yote…na ndio maana nilikuita kwa siri na kuna jambo ambalo natakiwa nikuambie wewe peke yako…nawaomba nyie wengine muondoke…’ akasema na wale vijana wawili wakaondoka.
 Akamuinamia Maua na kunong’ona, ili hata yule askari asisikie anacho mwambia ‘Namba ya siri ya kukifungua hiki ni `jina lako, tarehe yako ya kuzaliwa, mwezi na tarakimu mbili za mwisho za mwaka wako wa kuzaliwa…,’ halafu akainua kichwa na kuongea kwa sauti ‘ Najua utakuwa uanjiuliza nimejuaje wewe umezaliwa lini…najua hadi saa uliyozaliwa, kwasababu wewe ni damu yangu..usishangae sana, …mengi nilishakuelezea siku ile kwa juu—juuu, lakini ndivyo ilivyokuwa, kuwa katika mahusiano ya kukaa karibu na mama yako, ndipo mama yako akashika ujazito wako, na haikuwa kazi rahisi mama yako kuniambia, na mimi ndio nilimshindikiza kuwa wewe ni binti yangu, ….akakataa katakata…lakini ulipozaliwa ili kuondoa huo utata, mama yako alikwenda kupima, …ilibidi apime, kwani hata yeye mwenyewe alishangaa kupata hiyo mimba!
 Nakuambia haya ili ujue ukweli, kwani…mama yako na baba yako walikuwa hawaivani kwa muda mrefu, licha ya mama yako kuitolea kudhalilika kwa ajili ya mali yake…ilifika wakawa hawalali chumba kimoja na mumewe…sasa mama kajiona ana mimba afanyaje, siunaua tena wanawake, ikawa siku za mwanzoni za kujihisi , alichofanya nikujiilazimisha mapenzi na baba yako…lakini, utamdanganya nani…mimba ikakua, ukazaliwa! Kama ujuavyo mimi sikuwa namshinikiza moja kwa moja, watu wangu ndio waliokuwa wakimfuata, kuwa asipotoa hela, wanamwambia baba yako kuwa wewe sio binti yake….mama anachanganyikiwa…kwakweli ulipozaliwa, ukakua, ikawa kila nikikuona namuona mama yangu….siku moja nikamwambia mama yako, kuwa wewe ni mtoto wangu, akabisha, nikamwambia kama anabisha tukapime, …’
‘Sasa Maua huo ndio ukweli, ukubali usikubali…na kama unahitaji ukitoka hapa waambie hawo kaka zako wakuonyeshe picha ya bibi yako yaani mama yangu mzazi…kama utaona hiyo picha ya mama yangu hutaamini , wewe na yeye kama mlizaliwa mapacha… hili analijua baba yako, lakini kwa afya yake naomba usimsumbue…unaweza ukamuua, kwani katika kitu ambacho baba yako hakutaka kukisikia baadaye, ingawaje mwanzoni alipohisi alitamani akumalizia mbali, kama isingekuwa mimi ungelikuwa maiti…lakini baadaye alibadilika na kukupenda kupita kiasi, hakutaka tena kusikia kuwa eti wewe sio binti yake…ukitaka kamuulize, lakini huenda ukamshitua kupita kiasi…..’ Yule jamaa akainuka pale alipokuwa amekaa kwani muda ulishakwisha….akamtizama Maua halafu machozi yakambubujika.
  Maua alikiangalia kile kudude alichopewa akatamani kukitupa, akamwangalia yule jamaa akisindikizwa na wale askari, bado akiwa na hasira naye, akitamanii awakimbilie na kumrarua-rarua vipande, lakini kuna hisia nyingine ikaanza kujijenga, …oh, kumbe eti ni baba yake…oh…akawa kama anachanganyikiwa `Hapana haiwezekani, mtu kama yule awe baba yangu…hapana…hili bado sijalikubali…hapana akatoka mle gerezani kama sio yeye…na aliondoka moja kwa moja hadi kwa baba yake, alipofika akakuta watu wamejaa, na alipouliza vipo, akaambiwa baba yako keshatangulia mbele ya haki…msiba!

                                                                      M w i s h o

Jamani na huu ndio mwisho wa kisa chetu, kama mumekipenda nashukuru sana, na kama kuna makosa hapa na pale ningeshukuru kama mngenisaidia kunisahihisha,  kwa maoni kwa wingi ili kikija kisa kingine tusirudie haya makosa, na ili munipe moyo wa kuandika kisa kingine.
Nawashukuruni sana kwa kuwa pamoja nami, tukutane kwenye kisa kijacho, sijui tuanze na kipi…nitawaambia baadaye!

Ni mimi: emu-three

4 comments :

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Dah...Imekwisha kiaina! Mbona hatujajua alichokiona Maua kwenye kile kikadi?

Bando nna haaaam ya kujuaa....lol!

samira said...

m3 upo juu leo mwisho wa kisa hiki na imetulia na imeeleweka mimi nimefatilia tangu sehemu ya kwanza sikuona tatizo lolote hongera
sifa zote za uandishi wa kitabu unazo m3 kwa nini hutowi vitabu
hata ivo tupo pamoja usijali cant wait kisa kipya

ERNEST B. MAKULILO said...

Asante sana M-3 kwa kazi njema ya mikono yako na ubongo wako. Kwa kweli nimejifunza mengi mno, na nimeburudika sana.

Tunasubiria kisa kipya.

Mungu akupe nguvu zaidi. Tunakuombea afya njema M-3

MAKULILO

Faith S Hilary said...

Kwenye story wengine tumeshazoea "happy ending" lakini hii imeishia soooo sad! Sad na story yenyewe pia sad kwamba kisa hiki kimeisha lakini pia ndio mwanzo wa kisa kingine so I can't wait!!! Pia M3, jinsi ulivyoikata story huku na kule ili wasomaji tujue vipi tunaunganisha, sio kila anayejiita "writer" ana kipaji hicho so well done! Niliipenda story, kitu tofauti na ordinary, absolutely great! Always nipo hapa for the next big thing :-)