Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, July 8, 2011

Dawa ya moto ni moto-32    Inspecta alikuwa kakata tamaa kabisa ya kuishi, kwani kile chumba kilijengwa kama tanuri na kusilibwa kwa vyombo imara, na sehemu iliyokuwa unaweza kupita ni mlangoni tu. Alichukua vifaa vyake vya siri kujaribu kufungua ule mlango lakini haikuwezekana, akajaribu mbinu zote za kijeshi lakini hazikuzaa matunda, na muda ulikuwa ukienda kwa kasi kweli…mara akasikia mlio wa hatari…akajua mambo yameshaiva…mara harufu ikaanza kubadilika, kwani gesi ilishaanza kuingia kidogo kidogo, hatua ya mwisho, alipoona gesi inaanza kuingia ndani akaweka kitambaa puani na mdomoni, ili ile gesi isimuathiri haraka, aliona ni heri afe kwa kukosa hewa, kuliko kufa na muunguza wa ile gesi, na kila muda ulipopita ndipo aliposhindwa kabisa kujizipa na kile kitambaa, kwani alikuwa akikosa hewa…
 Kila muda ulivyozidi, ndivyo hali ilivyozidi kuwa mbaya na  kuanza kuhisi ile gesi ikipenya kwenye kile kitambaa alichoziba puani na mdomoni…akaona sasa ni muda wa kuomba dua ya mwisho, kwani kila ujanja alioujua tangu aanze hiyo kazi ulimwishia, akajua kuwa basi ndio mwisho wake umepangwa uwe hivyo, kilichobakia ni kutubu dhambi na kusubiri umauti, akatulia na kuanza kumuomba mola wake, amsamehe madhambi yake aliyowahi kutenda…na mara hali ikamzidia na kuanza kuishiwa nguvu, na giza likaanza kutanda usoni, akadondoka chini, lakini alijitahidi kabisa kutokuondoa kile kitambaa mdomoni na puani, hata alipokosa fahamu , na wakati anafumba macho mara akaona anakokotwa , au anaburuzwa…!
                                                               ************
 Wakati haya yakiendelea harufu ya gesi ilishaanza kusikika kwenye lile jengo, na mkuu wa usalama akapata taarifa kuwa kuna gesi inatoa harufu, akaanza kufanya uchunguzi, na aligundua kuwa inatokea sehemu ya chini ya jengo, akaona awasiliane na bosi wake,  kutaka  kujua nini kinaendelea  huko chini, kwani hakuwahi kufahamsiha kitu…alipopiga simu kwa bosi, simu iliita kwa muda bila jibu, akaona huenda bosi hayupo ofisini kwake, kwahiyo alitoka haraka na kulekea eneo la chini, na alipofika kule aliona vyumba vyote vimefungwa , akaona ni heri arudi kwa bosi wake ofisi za kati…. kuhakikisha kuwa mitambo imeharibika na kuruhusu gei kutoka ovyo, au kuna jambo jingine, alipofika hakumkukuta bosi wake, ila kuna ujumbe kwenye mitambo ikisema bosi katoka, kaitwa nje , ana wageni anawapokea…yule mtu wa usalama kwa vile alikuwa akijua wapi pa kuzuia gei isitoke kwenye mitambo, na aliona akiacha hilo linaweza kuleta madhara, alichofanya ni kwenda kwenye ile mitambo na kuzima ile sehemu ya kuruhusu gei kutoka, na kuruhusu milango yote kufunguka …
Alienda kwenye mitambo ya kuangalia mizunguko ya watu kwenye jengo ili kujaribu kumtafuta bosi wake alipo, lakini hakuona dalili, hakutaka kukaguaa sana mle ndani kwani hakuruhusiwa mara kwa mra kuingia ofisi ile labda kwa dharura, akatoka mle ndani na kuurudishia mlango…
                                                                   ****
‘Inspekta ni masahibu gani yamekukuta, naona ulikuwa unapikwa na gesi…’ alisikia sauti ikimuuliza, baada ya kupata huduma ya kwanza toka kwa docta…. haraka haraka akaanza kuzivuta kumbukumbu zake na akainuka na kuangalia huku na huku,akasema `ahsante docta, lakini naona hakuna muda wa kupoteza, …hayo tutaongea baadaye…Naona tutoke kwanza humu, kwani kwa huku chini huwezi kuongea na simu. Wakatoka kwa kutumia ile lifti kwa kufuata namba ile ya tisatisa, na walipofika juu, akaweza kupiga simu… Alijikagua na alipoipata simu yake, akapiga namba fulani na kuanza kuongea na mkurugenzi wake, alimweleza kwa kifupi na jinsi gani anahitaji msaada wa haraka….’ Alipomaliza, akainama kwenye kiatu chake akatoa silaha yake maalumu ambayo alijua haitamsaidia sana, lakini ni bora kuwa nayo kuliko kweda mikono mitupu kamwambia Docta `unakumbukumbuka ujasiri wa jeshini, naomba leo ujikumbushe kimatendo, ..’
‘Wewe sasa naona unanitia matatani, lakini sawa twende.’ Akasema Docta na kumfuata Inpekta nyuma
Wakarudi kwenye ile lifti na kushuka chini, wakawa wanaangalia zile namba, waligundua kuwa kwa kwenda chini kuna sehemu mbili, kwahiyo walisimamisha sehemu ya kwanza, hawakutaka kufika chini kabisa , na waigundua kuwa enep hilo lina ofisi nyingi, wakajaribu kufungua kila ofisi na kukuta milango inafunguka, lakini kulikuwa hakuna watu, zaidi ya vifaa vya ofisi na kumputa….na mwisho kabisa wakaona ofisi ambayo ilionekana kabisa ndipo kwenye mitambo ya umeme au na mtambo mkubwa wa mawasiliano ya jengo zima, alikumbuka ramani aliyowahi kuipata toka kwa mmoja wa watu waliobahatika kuingia humo ndani,  akaufungua mlango akakuta unafunguka, wakaingia ndani na wakajikuta kwenye chumba ambacho kilijaa mashine kubwa, ambayo ilikuwa ikiona jengo zima….
Harakaharaka waliangalia kila eneo na wakaona eneo moja kuna wazee wawili wamelala, na ilionekna gesi ilishaanza kutoka kwenye kile chumba, walichofanya walitafuta chumba kilichoonyeshwa kuwa ni chumba cha wauguzi, na kuita kuwa waende chumba cha wageni maalumu chumba namba kumi wakatoe msaada, na waliposema hivyo, kweli walitoka watu wawili na kukimbilia huko, na walipotizama chumba kingine cha chini waliona mwanadada akiwa naye kalala sakafuni, wakatoa taarifa kwa wauguzi waende huko haraka…
‘Huyu jamaa atakuwa kaenda wapi? ..’ akauliza docta
‘Labda aliona mambo yanamshinda akaamua kukimbia…’ akasema Inspekta
‘Inawezekana kweli..hivi hebu angalia huku…’ akasema docta, na walipoangalia sehemu ya chini, waliona kunaonyesha mlango ule ulioandikwa usiguse huku, na ulikuwa wazi, na kulionekana kama kuna kitu kinainia kama boti…kumbe ule mlango ulikuwa unatokea baharini….walipoangalia waliona watu watano , wawili wazungu na watatu waafrika…waliona wakiingiza maboksi kwa maboksi kwa kutumia kigari kidogo na ilionekana ni mizigo mingi, ikaingizwa kwenye chumba maalumu, na wale wazungu wawili wakatoa karatasi wakampa yule mwafrika mmoja akaandika andika halafu akamrudishia yule mzungu mmoja zile karatasi, wakapeana mikono.
Inspekta alipoona hivyo akatafuta sehemu mle ndani mpaka akaona simu  ya mezani ambayo aliitumia kupiga namba za nje, na kwa bahati nzuri ikawa inapatikana aliongea na mkurugenzi wake wakmueleza nini ameona na anahisi nini, kwahiyo aliomba askari wa majini wafike eneo hilo haraka iwezekanavyo wawahi hiyo meli iliyopa karibu na eneo hilo…waliambiwa kuwa hiyo meli ilifika jana usiku, lakini hkukuwa na taarifa zozote kuwa ni ya nani, na askari wameshatumwa….
‘Sasa kazi nikuwafuatilia hawa waafrika watatu ni yupi ndiye mhusika mkuu, maana kama unavyowaona wote wanafanana…’akasema Inspecta.
‘Hawa watu inaonekana kuna vitu wanavyaa, ili kuficha sura zao, cha muhimu ni kuwaweka mikononi mwa polisi , halafu tutawajua yupi ni yupi…’ wakati wanaonge hivyo, mara wakaona kwa nje maaskari wakifika kwa wingi…na huku ndani kwa chini, wale jamaa watutu walikuwa wakiongea,na mara mmojawapo akaondoka kwa haraka na kuingia kwenye lifti…wale wengine waliondoka na kuingia kwenye chumba kilichokuwa chini, ilikuwa ni ofisi kubwa ambayo nayo ilionekana na vifaa vingi kama vilivyopo huku walipo Inspekta, na Inspecta akahisi wataonekana…
 Mara mlango ukafunguliwa, inspecta na docta wakati huo wamejificha, wakamuona yule jamaa akivua kitu usoni, na alipomaliza, loooh, alitokea jamaa ambaye hawakumbuki kabisa kumuona awali, jamaa yule akachukua kitu kama mafuta akajipaka usoni halafu akaenda kwenye jokofu akatoa chupa akajimiminia vinywaji, na mara akasema…ooh, nimeshahau, hawa watu watakuwa wameshakufa…duuh, mbona balaa, sikutaka wafe mapema hivyo…akasogea kwenye ile mitambo, na mara akashituka, na kuanza kuhaha…`polisi.., haiwwezekani…akavaa kitu masikioni na kuanza kuwasiliana na watu wake..
‘Mumeona hiyo…polisi wameingia, hakikisheni hamuonekani, ni mpango wetu ni ule ule, …hujulikani wewe ni nani, na kama kuna lolote hakikisheni njia ya kutoke chini ipo wazi…mimi naweka mambo sawa, kama hakukaliki nitayeyuka kidogo…’ akabonyezabonyeza, na kukatokea sauti ya  ti-ti-ti…ikiashiria onyo, akasema kwa sauti,` kama watanishinda, hawatapata kitu…’ akasema na alipogeuka akajikuta anashikwa na mshituko kwani alijikuta hayupo peke yake…
‘Oh, hahaha Inspekta, afadhali hukudhurika, maana ilikuwa sio nia yangu, kweli mshika mawili moja humponyoka, ila nilijua kuwa wewe ni askari unaweza ukatoka, kwani gesi yenyewe , ilikuwa kidogo, kisogo…na ilikuwa ya kutishia tu, ila masikini wale wazee, nashangaa, wametolewa mle ndani, nilitaka wasote kidogo, hata…lakini sikuwa na nia mbaya…..’ akasema  na kuangalia saa na akasema kwa haraka, ‘Sina muda wa kupoteza, semeni shida yenu, kama ndio mumekuja kunikamata, sipo tayari, kwanza nionane na wakili wangu,…’ Inspekta akamsogela yule mtu, akitaka kuhakikisha hafanyo lolote baya akiwa na silaha yake ile maalumu, akamkagua kuhakikisha kuwa hana silaha na kweli hakuwa na silaha,
‘Upo chini ya ulinzi, na tunaomba usilete ubishi, kwani mwisho wako umefika…’ akasema Inspekta.
‘Hahaha, Inspekta, mwisho wangu ulishafika siku nyingi,unaona hapo juu, hilo ni bomu, ambalo nilipofika na kuwaona hawo askari nje nilijua mambo yameharibika, ila nataka ujue ukweli kuwa sikuwa na nia ya kukuua wewe, nimechelewa kukutoa mle kwasababu niliitwa na wageni muhimu sana…katika kujadiliana nao, nilipoona muda unakwwisha nikawasha `remote’ ya kuzima,ili gesi isitoke, ile hata ningekuwa mbali vipi ingezima kila kitu, lakini nilishangaa haikubali, ina maana kulikuwa na mtu alibonyeza kidude cha kuzua,…na kweli nilipowauliza wenzangu, mmoja aliniambia alifanya hivyo kwa vile alikuwa na kisasai na wewe…nilichanganyikiwa, ndio maana nilirudi haraka kuhakikisha mambo yapo sawa, nikakuta …haya mabadiliko…samahani sana…kwa hilo…’ akasema huku anaangalia saa
`Lakini sasa kuna dakika kumi na tano zikiisha hizo, sote hapa tutakuwa majivu, ili nifanye mtakavyo, itabidi mniruhusu nitoke, …la sivyo…hakuna ujanja tutakufa sote humu ndani, hilo ni bomu likilipuka hapa, sijui itakuwaje…sijui..mna hiari kama mnataka kunichukua haya, …twendeni…lakini ‘ akasema na kumuacha Inspekta kinywa wazi.., na yule jamaa akaendelea kusema , ‘Mimi siogopi kupelekwa mahakamani, lakini kwanza nataka kuhakikisha kuwa kila kitu change kipo sawa, …kwani nina uhakika kuwa nilichofanya ilikuwa ni kudai haki yangu, na kulikuwa hakana njia nyingine, hili bomu hakuna wa kulitegua mpaka mwenyewe niwepo, kwani namba zangu za siri hakuna mjanja wa kuzigundua….kwahiyo mnasemaje. …’ akasema huku anaangalia saa yake
‘Wewe huna akili kabisa, …upo chini ya ulinzi, hilo bomu utalitegua  tu…naomba usisogee….’ Inspekta huku akiangalia ile mitambo, alitaka kutumia nguvu, lakini kabala hajafanya hivyo, wakasikia mlango ukifunguliwa…
Mlango ikafunguka na watu wawili wakiwa na silaha waliingia, walikuwa wale jamaa waliokuwa huko chini, walipofika tu wakawawahi akina Inspecta na mwenzake kwa kuwaambia kimono juu, wakapiga risasi pembeni kuonyesha kuwa hawana utani, lakini ilionekana dhahiri kuwa hawakutaka kuwazuru inspekta na mwenzake, wakasema, `bosi twende tupo tayari….’ Yule Jamaa akasema kama nilivyosema, nataka kuweka mambo yangu sawa, mkizuz baada ya dakika kumi tano, msinilaumu…’ akatoka na hao jamaa huku akicheka kwa dharau. Inspecta naye, hakutaka kutumia ile silaha yake, au kupambana nao akawaacha waondoke…akasogelea ile mitambo, na kweli akaona sehemu inaonyesha bomu ikimulika rangi nyekundu kuonyesha hatarii, alijaribu kukumbuka wapi yule jamaa alipokuja alibonyeza, akabonyeza…kukatokea maneno ya kuuliza namba ya siri…
`Zimebakia dakika kumi..’ akasema Docta, na inspecta akachukua simu na kumpigia mkurugenzi wake na kumuelezea hali halisi ilivyo..akaambiwa kuwa kwa nje wameshaweka ulinzi wa kutosha asiwe na wasiwasi na mtaalamu wa  mabomu keshaingia ndani…akamwelekeza wapi wafikie, na haikuchukua muda jamaa akaja na mtaalamu wa mitambo ya kumputa…na taarifa ilikuwa imeshasambazwa mle ndani  kuwa wote watoke , na ilionekana dhahiri watu wote walishatoka kwenye hilo jengo, na wataalamu walikuwa wakihangaika kulitegua lile bomu kwa kila hali,….
‘Hili bomu linahitaji namba ya siri, …baya zaidi linatumia halionekani wapi lilipo, ….tukigundua tunaweza kulitegua, lakini je kwa muda huu mchache tutaweza hili….naomba mumkamate huyo mtu…kwani hapa tunacheza na muda, na maisha ya watu, na hayo yakiendelea hakikisheni watu wote wametoka na eneo lote la huku baharini hakuna watu…. hatuwezi kukadria hasara itakayopatikana, au usalama wake..’ akasema mtaalamu.


         Ukawa mshike mshike
NB, Jamani samahanini, hii nimeilazimisha huenda ina makosa hapa na pale, lakini niliona niiweke tu juu kwa juu wakati komputa ikiwa bado kwenye matengenezo...kwani leo ni ijumaa, na sipendi niwaweke hadi jumatatu...Jumatatu huenda tukamalizana na hiki kisa, kama huyu `mrusi' ataondoka..TUPO PAMOJA


Ni mimi: emu-three

2 comments :

ERNEST B. MAKULILO said...

Asante EMU-THREE. Tunasubiria muendelezo.

Weekend njema

MAKULILO

samira said...

m3 pole na mrusi yaani mimi ninavyopenda kuwa online siku ikinitokezea kama hivi naweza pata homa
tuendelee na kisa chetu mambo yamenoga jamani mauwa sijuwi vipi na maneno wake unajitahidi sana m3
cant wait