Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeThursday, June 30, 2011

Dawa ya moto ni moto-27


Inspecta akiwa kavaa nguo za michezo, mfukoni kaweka chombo cha kuhifadhi sauti na zana zake za kazi, alimua kujihami kwa kila njia kwani hakutaka kumwamini yoyote, kwani kila aliyejaribu kumwamini mwisho wa siku anagundua kuwa na wale wale, …na anaweza pia akawa   mtego, kwani kundi analopambana nalo sio la mchezo. Amekuwa akikutana na jamaa yake huyu kwa mtindo huu huu, na aliogopa kuwa huenda wakawa wameshaugundua…
Wasiwasi ulimwingia hasa pale yule fundi aliyemtgemea kumpa taarifa muhimu kupotea , kwani hakumkuta kama walivyoahidiana na hakuwa na uhakika kuwa huyu fundi karudi kwao au ndio kapotea moja kwa moja,  kama walivyopotea mafundi wengine…kama alivyomuhadithia huyoo fundi mzee, hata alipofika sehemu ambayo mara nyingi wanakutana hakutokea na simu yake ikawa haipatikani . Aliamua kwenda sehemu ambapo alimwambia kuwa ndipo alipofikia , majirani zake  walisema hawajamuona toka jana, alipoaga kuwa anakwenda kutembea tembea.
‘Yule fundi bwana huenda kapata tenda kaamua kuishia zake, ..’ akasema jirani yake mmoja.
Na wakati anawaza afanye nini, au achukue hatua gani, akapata ujumbe kwenye simu  yake ikiwa na maneno machache, `tukutane ufukweni, mambo yameiva..’  Inspekta akatabasamu, kwani ni ujumbe muhimu sana aliokuwa akiusubiri, kama ni kweli basi mwisho wa kundi hilo haramu umefika…lakini bado alichukua tahadhari, kwani yoyote anaweza akatuma uumbe kama huo, kwani mtumaji hakutaka kujitambusliha au kuonyesha namba yake…akaamua kufuaa hisia zake tu, kuwa ni jamaa yake ambaye kaitolea kufa na kupona kuhakikisha kundi hilo linasambaratika.., ndipo akaamua kujiandaa na kuelekea huko ufukweni.
Alipofika ufukweni aliegesha pikipiki lake sehemu ya kulipia ili kuhakikisha usalama wake, halafu  akaingia chumba cha kubadili nguo na kuondoa uso wa bandia aliokuwa kauvaa.., akatoka mle ndani na kuanza kutembea kidogokidogo pembeni mwa bahari, akiwa anajaribu kutazama huku na kule kuona kuwa atamgundua mtu anayemfahamu…! Hakuona mtu ambaye alimtegemea,…akaanza kuingiwa na wasiwasi, je ule uumbe ulikuwa sio sawa, au jamaa yake kanaswa na hawo magaidi…alitembea kwa hali ile ya kuchunguza huku na kule…na alipoona muda umepita sana bila kuona dalili yoyote akakata tamaa. Akaona aendelee na mazoezi yake kama kawaida, kwa kuanza kukimbia kuelekea mbali na walipo watu wengi, alikimbia umbali kidogo na  mara alipogeuka nyuma kuangalia, akaona jamaa mmoja akija uelekeo wake, alionekana mzee na hata kimbia yake ilikuwa ya taratibu…
 Yule mzee alipoimkaribia akawa kama anampita Inspecta , halafu akaongeza mwendo kwenda mbele zaidi, na Inspecta akawa nyuma yake hadi wakawa mbali kabisa na upeo wa watu, yule mzee akaanguka na ilionyesha kuwa kaumia… na anahitaji msaada,…hapo  Inspecta akahisi kuwa kuna jambo, huyo anaweza akawa mmoja wa watu wake anaowatafuta.. ni mtego, akaangalia silaha yakle maalumu kuwa ipo sawa, na kumsogelea yule mzee
‘Vipi mzee unahitaji msaada, naona umechoka sana…’ akauliza inspecta.
‘Haswa, kwani mambo yameiva, nisaidie hadi kwenye kivuli kile pale…’ akasema yule mzee
Inspecta akamsaidia yule mzee hadi kwenye kile kivuli na walipofika pale ambapo pamejificha na hakuna mtu anayeweza kuwaona, yule mzee akavua kitu alichovaa usoni na kofia na akaonekana mtu mwigine tofauti…
Duh, mtani kweli wewe sasa nakuvulia kofia, maana kila siku unakuja na sura tofauti…’ akasema Inspecta
‘Kazi hii niliisomea kidogo, ingawaje niliamua kuwa docta, lakini mambo ya upelelezi bado yapo yapo, hasa kwa kipindi kama hiki…unakumbuka jeshini, tulivyokuwa…mimi bado kwenye mitandao nilikuwa najifunza mbinu za medali…ok, naomba uwe makini na kama umekuja na zile zana ziwashe kabisa, kwani haya niayakayokuambia ndio `hitimisho la hawa watu…amini hivyo, labda nyie mzembee..’ akasema Docta.
 Inspecta akakaa karibu na yule docta, akiwa bado na tahadhari, akasema `endelea docta,…najua una mengi yakuniambia tuanzie pale tulipoishia kwanza, kwani kile kisa kimenifanya nianze kuamini vinginevyo… na muda niliopewa na mkurugenzi unaisha...na unahakika wa usalama wako? Akauliza Inspekta.
‘Wasiwasi wangu ni kwako tu, mimi nimechukua tahadhari zote…kama ulivyoniona hata hivyo inabidi tuwe na tahadhari ya hali ya juu ,kwasababu hawa jamaa ni wakali…wanajua nini wanachokifanya.. je una uhakika hapa kutakuwa salama..? akauliza docta.
‘Kwa upeo huu tupo salama kabisa na sidhani kuwa kuna mtu atakuwa kanigundua…nilichukua tahadhari kwa hilo….wewe ongea tu’ Akasema Inspekta
‘Kwanza kabisa tuanzie nyuma kidogo pale tulipoishia, kwani kwa muda mfupi nimegundua mengi na sikuamini nilipokutana na jamaa huyo, ambaye ndiye anasadikiwa kuwa ni kiongozi…na kama asingenisimulia mwenyewe nisingeamini hivyo ..ni kichekesho kidogo na mapaka sasa sijajua yupi ni yupi, labda leo usiku ndipo tutamgundua …kwanini nasema hivyo, utajua jinsi nitakavyokusimulia..wewe kama askari utagundua mwenyewe...ngoja nikupe kisa kwanini ilitokea hivyo…na mabdiliko yake toka makusudio ya awali na kuingia katika sura mpya..ambayo kama itafumbiwa macho jamii itaharibika…juhudi za makusudi zinatakiwa kuondoa hiyo hali…nisikiiza kwa makini sana…’ akasema Docta akijaribu kukaa vyema.
‘Kuna jengo lililopo ufukweni, kule kigamboni jengo kubwa ambalo limekuwa simulizi, ukubwa wake unaouona juu, haulingani na huko ndani…, hilo ndilo linalomilikiwa na mkuu huyo wa kundi,…akiwa na ubia na watu toka nje…limejengwa kwa muda mrefu kidogo. Ndani ya jengo hilo ni chuo cha kundi ambalo mwanzoni lilianzishwa kwa lengo moja, la kusaidia dhamira ya huyu jamaa kiongozi wa kundi ambaye hata sura yake kamili haijagundulikana kuwa yupoje, kundi hilo linajulikana kwa siri kama `kundi la malipizo’ ndilo jina la siri, na hiyo ndiyo `password’ yao, …`malipizo’…utajiuliza malipizo yana maana gani, lakini chanzo cha kuundwa hili kundi limetokana na hisia hizo , na hayo mengine unayoyaona ni kama viini macho ili dunia ipumbazike na jamaa akamilishe azima yake bile kuhisiwa vibaya..hiyo ndiyo ilikuwa nia ya mwanzoni…’ akasema docta huku akikaa vyema ili kuleta hicho kisa ndani ya kisa,
`Swali linakuja ilikuwaje mpaka kukatokea `malipizo’, hapo nisikilize kwa makini kwani ni kisa kirefu kidogo lakini nitakifupisha ili twende na muda. Kisa hiki kinaanzia tangu mtu akiwa na miaka 7 hivi, na hadi sasa  muhusika huyo anaweza akawa na miaka 38 au zaidi…na mikakati ilikuwa taratibu na chini kwa chini na kwa uangalifu sana..kisa hiki kanisimulia mhusika mwenyewe..ingawaje bado sijamjua vyema sura yake…na alifikia kunisimulia haya wakati nilipokubaliana naye kuwa nipo tayari kujiunga na kundi hilo…jamaa akanihadithia kwa vile alitokea kuniamini tangu mwanzo, kama alivyonielezea…sasa alinijuaje, na sura yake sijaijue vyema, inakuwaje…ndio maana nataka unisikilize kwa makini, na nakusimulia haya kama nukuu;
                                                                             *******
‘Nilikuwa mtoto wa miaka saba niliposhuhudia mama yangu akiuwawa kinamna…sio kwa kuchomwa kisu au kwa bastola, ila kwa kuogopa kashifa, ambayo ilipikwa vyema, na marafiki wa baba yangu kisa kikiwa ni mali, na watu hawo hawo waliomuaa mama , ndio waliohusika kumuua baba na hutaamani kuwa mauaji ya baba yalipangwa kinamna, huku mama akiwa kahusishwa bila ya yeye kujua hilo, …. Ilipangwa mbinu kwa familia hiyo na maadui wa familia kuwa mume wake ana mahusiano na mke mwingine na huyo mke mwingine anataka kuhodhi mali yote kiujanja…mama akanasa kwa uvumi huo…
Baba alikuwa mfanyabisahara wa madini, na alifanikiwa kupata eneo lenye madini na kutajirika kwa muda mfupi, na baadaye akaingia ubia na marafiki zake wawili, ambao walikuja kumsaliti baadaye , eti kwanini baba yeye awe anapata hisa kubwa zaidi ya wenzake wakati wote walihangaika hadi kufanikiwa kupata eneo hilo lenye madini. Mgogoro huo ulifikia hatua ya kugawana maeneo na hata walipogawana, bahati ilimwangukia baba kwani eneo lake ndio lilikuwa na madini mengi, kuliko maeneo ya wenzake ..hapo wivu, uadui na… ukaanza, na uhasama ulijenga chuki kubwa sana...
‘Unajua mume wako ana kimada, kila anapokwenda safari anafikia kwa huyo kimada, na imefikia hatua kuwa anataka kumgawia eneo lake la madini, ukizubaa utakosa kila kitu…’ akaambiwa mama na shemeji yake ambaye ni rafiki wa baba katika biashara, na mwanzoni mama hakuamini lakini alipochunguza akamfuma baba akiwa na huyo mwanamke.. . Mwanamke  ambaye alitumiwa na huyu rafiki yake wa karibu …baba bila kujua akahadaika kimapenzi na huyo mwanamke…na hata kabla mapenzi hayo hayajapamba moto, mama akatonywa na huyo jamaa kuwa aende mahali fulani atawakuta mumewe na huyo mwanamke…na kweli aliwakuta, ..mama alikuwa ni mtu wa hasira sana.
‘Sema tumfanyeje mumeo baada ya kumfumania, kwani huenda huyo mke kama anavyodai ana uja uzito wa mumeo, na mali ndiyo hiyo itakwenda kwake…’ akaulizwa mama, naye kwa hasira akasema `muueni, na hawara yake..’kauli yake ikachukuliwa na kufanyiwa kazi na kweli baba alivamiwa na kundu la vijana waliotayarishwa na katika vurumai hiyo baba akachomwa kisu, na alikufa baadaye…, kipindi hichoo nilikuwa bado mdogo sana , sikujua nini kinaendelea …mama hakuamini kuwa maneno yake yalichukuliwa kirahisi na watu wakafanya mauaji hayo mabaya, eti yeye ndio katoa amri…mambo yaliisha kienyeji,kwani hakukuwa na ushahidi wa kuwakamata wauaji, kwa insi ilivyopikwa mwisho wa siku  mama akakabidhiwa miradi ya baba , lakini akawa anafuatwa na wale watu aliowaambia kuwa wamuue baba, wakimdai pesa, kila mara…wakitishia kuwa kama wasipopewa pesa watatoa taarifa polisi.
 Kumbuka wale marafiki wawili wa baba bado walikuwa wakimezea lile eneo la baba mate, na walipoona kuwa baba hayupo wakamhadaa mama kuwa waingie ubia, ili waweze kuunganisha nguvu kama walivyokuwa na mumewe, na mama akakubali kwani hakuwa na utaalamu mkubwa sana wa amambo hayo, na hapo wakatumia kila mbinu mpaka mali yote ikawa mikononi mwao, na mama akawa kama mshirika tu asiye na usemi wowote, ndipo akaamua kudai haki yake…
Hawa marafiki wawili ingawaje walikuwa na ubia na baba , na sasa na mama, lakini wao wawili walikuwa hawapatani, na hili lilimsadia mama, vinginevyo wangekuwa wameshamuondoa mama siku nyingi.., na eneo hilo baadaye likataifishwa kuwa ni eneo la serikali na wao wakaachiwa sehemu ya hisa,ambayo hakuwa na faida sana,..lakini kulikuwa na mali nyingi aliyokuwa kailimbikiza baba, na hawa marafiki waili walikuwa wakijua hilo na walikuwa wakihisi kuwa mama anazo au anajuwa wapi mali hizo zilipo , lakini hutaamini mama hakujua kabisa wapi hiyo mali ilipo…wakahisi mama anawazunguka,…!
 Hawa watu wakaanza mikakati ya kummaliza mama kila mmoja kivyake, wakamtegea ulevi, ambao ulimwingiza mama katika kashifa kubwa sana, …mama alipoonyeshwa hiyo kashifa akajikuta katika hali ngumu, na aliogopa ikisambaa, atadhalilika sana…akaamua kujiua kwa sumu kama ilivyoonekana, hivyo…huenda sumu hiyo iliwekwa na hawo watu au mama mwenyewe ndiye aliyeamua kunywa sumu ili kuepukana na kashifa hiyo…haipo wazi sana…lakini mama alikufa kinyama peke yake chumbani mwake…akihangaika kupata msaada, wakati sumu hiyo ikifanya kazi yake tumboni..nilikuwa sipo, siku hiyo yalipotokea hayo, nilirudi kesho yake na kukuta watu wamejaa…ndipo nikasikia kuwa mama kanywa sumu eti kujiua kuogopa kashifa…sikukubaliana na hilo..namjua sana mama yangu ni jasiri kupambana na matatizo..lakini ningefanyaje…
Siku mbili baadaye nikasiki kuwa kuna watu wanataka kuniua na mimi…nikashangaa mimi mtoto mdogo nina kosa gani…na kweli usiku mmoja nikiwa nimelala, nikasikia watu wakiongea nje, nikatoka taratibu kwa kujificha, ndipo nikawasikia wakisema waiwai kuwa huenda mimi najua wapi madini yalipowekwa…kisa hicho cha madini nilikisia kwa mama, kuwa kuna madini mengi baba yangu alikuwa kayakusanya na hawo marafiki zake wawili wamekuwa wakimsumbua mama kuwa anajua wapi yalipo…lakini mama akasema hajui kabisa…sasa mama kaondoka wanamsaka yeye..afanyeje…akakimbia na kujicha chooni!
`Nikiwa chooni, huku nalia kimiya kimiya kwa huzuni na woga, nikajikuta nachimbachimba ukutani kwa kijiti, na mara sehemu ya ukuta ikamomonyoka, na kwa mshangao nikaona sehemu iliyotengenezwa kama kiboksi na ndani yake kulikuwa namfuko wa nailoni, nilipoutoa nikaona vito vizuri,kwa wakati huo niliona kama gilasi za rangi, ingawaje nilishawahi kuonyeshwa na mama kuwa madini yapo vile, lakini kwa muda ule sikuwekea manani kabisa kuwa ni vito vya thamani… ila nilijiwa na mawazo ya kuvificha mahali pazuri…nilipoona hakuna watu tena, nikatoka, nikakimbia sana hadi eneo ambalo mama alikuwa kajenga nyumba…ni sehemu za ufukweni…lakini nyumba hiyo ilikuwa haijakamilika, nia yake ni kujenga hoteli… nikachimba shimo, halafu nikachukua cement nikakoroga, nikasiriba kwa juu na kuweka mchanga juu. Halafu nikahama kabisa meneo hayo
 Nilitorokea sehemu nyingine ya mjii,..na nilipofika huko nikaishi kama mtoto wa mitaani, bahati nikapata mtu wa kunisomesha, nikasoma hadi sekondani, sikuendelea zaidi nikaingia kwenye biashara za mitaani, hata kuuuza unga,…maisha yangu yakawa yakubahatisha, baadaye nikapata rafiki akanichukua hadi nchi za nje, huko nikasoma, na kujua lugha mbalimbali nikajisomesha mambo ya upelelezi binafsi, nikasomea hata udakitari..nilikuwa na akili ya ziada…kiasi kwamba wazungu wenyewe walinishangaa…lakini akili yangu haikutaka kutulia katika huo udakitari, akili yangu ilikuwa katika chuki ya kulipiza kisasi,…kwahiyo nikawa nasomea na mambo mengine ya kugundua dawa ambayo inaweza kumbadili mtu kimawazo na vitu kama hivyo…
 Nikiwa nasoma huko nikakutana na rafiki mmoja akanishauri kujiunga kwenye kundi lao ambalo lilikuwa na mambo ninayoyataka, …kujifunza kutumia silaha,ujanjaujanja wa mazingaumbwe…kutengeneza madawa ya kulevya , utapeli basi nikawa katika fani hiyo…niliweza kujibadili badili nipendavyo kwa kutumia aina fulani ya ngozi laini…nikiwa huko nikaajiriwa na kundi moja la ujambazi, karibu nishikwe, nikatoroka na kurejea nchini, na niliporudi nilijifanya hohe hahe wa kutupwa, hii ikiwa moja ya mbinu yangu  ya kuanzia, ili niweze kupata kazi kati ya hawa waliokuwa marafiki wa baba zangu, …hakuna aliyenigundua kabisa kwa jinsi nilivyokuwa nimebadilika.…
Jambo moja ambalo lilinisaidia ni kuwa niliporudi lile eneo la mama nililikuta vile vile,..  na gofu la jengo ambalo lilikuwa halijamaliziwa …lilikuwa limezungukwa na magugu mengi, nikatafuta lile eneo nilipokuwa nimeficha yale madini yangu, ..ilikuwa kazi kubwa sana kuvunja hadi kufikia pale nilipoweka ule mfuko, ambao ulikuwa umenatana na cement, lakini nikayapata madini yangu, na wakati huo nilishajua madini yakoje, na kweli yalikuwa madini ya thamani kubwa sana, nikauza baadhi nikaliendeleza lile eneo la mama kwa kujenga nyumba ambayo niliipangisha, mimi mwenyewe nikawa naishi kihohehahe. Upande mmoja, na upoande wa pili docta bingwa… nilifanikiwa hili kwa kuwa najibadili katika sura mbili, nikitembelea nyumba yangu nakuwa na sura ya mtu mwingine mwenye hadhi tena dakitari….na nikienda hapo ninapofanya kibarua nakuwa hohehahe, hili kwangu ilikuwa kazi ndogo..
Siku moja nikapita kwa mmoja wa maadui wangu, nikamuona mama mmoja akinyweshea Maua, nikamuomba nimsaidie na akakubali, nikafanya kazi hiyo vizuri, na yule mama akanipenda kwa kujituma kwangu akaniambia ataniajiri kwa kazi  za nyumbani, nikakubali na mtego wangu wa kwanza ukakubali…nikaanza mikakati ya ndani ya nyumba ya adui wangu namba moja….
Je ni mikakati gani hiyo na tuendelee kwenye hitimisho la kisa hiki!-Ni mimi: emu-three

6 comments :

Anonymous said...

Jamani, Boss wangu mbona unakatisha utamu? usichelewe sana, manake utamu utapotea mdomoni.

Nimeipenda hiyo kisa ndani ya kisa.

2po pamoja mkuu.

BN

emu-three said...

Usijali Bosi BN, tupo pamoja, mambo ndio hayo...! Unajua kitu kinaitwa `kuibia' ukiwa shuleni, basi huwa wakati mwingine naandika kwa kuibia...lakini hivyohivyo kidogo kidogo , sasa kisa kipo mteremkoni...TUPO PAMOJA

samira said...

m3 mambo yamenoga na mimi leo umenipa nuru ya kuona au kujuwa kwa ujumla hawa maaduwi ni akina nani
zaidi nasubiri sina haraka
unajitahidi dada or kaka unisamehe

emu-three said...

Samira Mpendwa nashukuru sana kuwa kweli tupo pamoja kivitendo ubarikiwe sana! Ama kwa hoja ya samahani kuwa umesema kaka au dada naomba usijali kabisa vyovyote uitavyo kwangu ni sawa ilimradi urizike. Naomba nikuulize je wewe ungependelea niwe kaka au dada?barikiwe sana! Ama kwa hoja ya samahani kuwa umesema kaka au dada naomba usijali kabisa vyovyote uitavyo kwangu ni sawa ilimradi urizike. Naomba nikuulize je wewe ungependelea niwe kaka au dada?

samira said...

m3 usijali tupo pamoja kama dada au kaka kwangu ni sawa tu naheshimu sana kazi zako ndani yake mafunzo tunayapata na kujuwa dunia ikoje
big up m3

Anonymous said...

Good day! Do you use Twitter? I'd like to follow you if that would be ok. I'm undoubtedly enjoying your blog and look forward
to new posts.

Also visit my web-site; samsung galaxy s4