Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, June 27, 2011

Dawa ya moto ni moto-26


      
Inspekta alimwangalia msaididzi wake usoni, kama vile anamsikiliza kile anachomwambia, alikuwa akimfahamisha maenendela ya kesi mbalimbali alizokuwa akizifanyia kazi, ikapita dikika tano ya ukimya, wakiangalia ushahidi mbalimbali walizokusanya kutokana na matukio ambayo yamekuwa yakizidi kila siku mpaka ikafikia kuitwa na kamishina kujieleza, walipofika huko waliulizwa wamfikia wapi na kesi mbalimbali ambzo zimekuwa zikizidi siku hadi siku na wananchi wanalalamika, na pia kwanini matukio yanazidi na wao wapo …walijitahidi kujitetea na wakapewa mwezi mmoja kuwa kama hawajamaliza hizo kesi na kupata ushahidi basi itabidi wanaondolewa kwenye huo wazifa…
‘Unaona jinsi bosi alivyokasirika,…mimi nilishakuambia kuwa huu ushahidi unatosha kuweka mambo sawa, mimi sioni kwanini tuhangaike sana wakati kila kitu kinajionyesha, huu ni mtandao mdogo wa watu wanaotaka kupata pesa kwa kutumia kashifa za watu, wachukue picha za watu mashuhuri waziweke kweny kanda au mtandaoni halafu wadai pesa, na …wahusika ndio kama hawa, tunawakamata tunawachulia hatua kazi imekwisha…’ akasema msaidizi wa Inspecta, ambaye alikuwa akifunua majalada ya kesi hiyo na vielelezo alivyokusanya, lakini Inspecta hakuwa akimsikilza sana msaidizi wake, alichokuwa akifanya ni kutikisa kichwa kuwa anakubaliana nacho lakini moyoni alikuwa hayupo kabisa..
‘Unanisikiliza lakini…nakuona haupo nami, tangu urudi huko ulipokuwa umejificha nakuona upo mbali kabisa na hii dunia, na …sikutaka kukuchafulia pale kwa bosi alipouliza ulikuwa wapi,…lakini hayo tuyaache…tulimalize hili tatizo.,vinginevyo cheo kitaota mbawa, na usipoangalia kama sio mimi kukichukua ujue ni yule kichaa atachukua nafasi hiyo…na akichukua yule kichaa, tumekwisha, …’ akasema msaidizi wake kwa utani.
‘Tatizo sio hiki cheo, na hakuna aliyezaliwa akajihakikishia kuwa atakuwa na cheo kama hiki…tatizo ni huu moto ulioanzisha na hawa watu tuwaitoa wa mtndao…moto huu sio rahisi kama unavyofikiria, unatakiwa uzimwe haraka kabla haujapamba moto…’ akasema Inspecta na kuinuka pale kwenye kiti
‘Sasa tufanyeaje, kwasababau juhudi za kila namantumefnaya, lakini kila tunapofika tunishia sehemu ambayo hatuwezi kwenda mbali zaidi…’ akasema Msaidizi.
‘Lakufanya lipo, lakini nasikitika kusema tatizo kama hali halihitaji kumwaga mtama kwenye kuku wengi, kwasababu hata wale waliopewa majukumu ya kiusalama huenda wapo kwenye huu mtandao…jambo jema ni kuhakikisha tunafanya kazi yetu, na muda utafika tutaliweka hili swala hadharani, …ila wasiwasi wangu ni kuhusu watendaji wetu , ni yupi wa kumwambimi na yupo wakutomwamini…upo na unendelea kuwaka chini kwa chini….ili siku ukilipuka juu, basi mambo yamekwisha…acha watu waone hayo majivu yametanda juu, wazanie hakuna moto…unajua tatizo kama hili kuna pande mbili, wao kama wao wamewasha moto wao,. Sisi kama sisi tuna moto wetu…lakini mwisho wa siku, ni kuona nani atauzima moto wa mwenzake…kwani dawa ya moto ni moto tu...hakuna kingine....!
‘Dawa ya moto ni moto..na nyie waswahili bwana…haya tufanye kazi maana hizo juhudi zako za chini kwa chini zatakiwa zionyeshe matunda, vinginevyo kama alivyosema Kamishina kazi tutaiskia kwenye bomba, watakuja wengine wanaojua kuwajibika…ok, sasa tuone huu ushahidi namba moja hapa alioleta huyu kijana wetu mimi namwamnia.
Ulikuwa ushahidi way a kuwa kuna watu wanaojihusisha na biashara haramu za kuchukua picha za watu mashuhuri, na kutumia vitisho kupata pesa, na kundi hilo limefikia hatua ya kuvunja ndoa za watu, kusababisha watu wajiue….na uchunguzi umebaini kuwa ni wafanyabishara wenye majumba ya starehe ndio wanaokodisha vijana kuifanya hiyo kazi,…
‘Unaona hii, wanafika watu kwenye starehe zao, hatuwezi kujua ni wapenzi au ni wanandoa waliovunja miiko ya ndoa zao wanaingie kwenye vyumba vya wageni, hawa wenye majumba haya wanakuwa na vyombo vya kuchukua picha, wanazichukua picha wanazitumia kutishia watu….la muhimu ni kujua ni nani na nani anafanya kazi hii…’ akasema msaidizi wa Inspecta.
‘Hilo ni sawa kabisa, na hii ni mbinu mbadala wa kundi mama…hilo silipingi kabisa, lakini kuna kundi mama, hilo ndio tunatakiwa tuliweke mkononi…’ akasema Inspecta.
‘Kundi mama gani bwana, wewe unataka kukuza jambo…hakuna cha kundi mama, hawa ni wafnyabaishara wachache , tuwakamate, weka ndani biashara zao zitaifishwe…basi tumemaliza kazi kama unataka kukuza jambo tutakesha hapa..’ akasema msaidizi.
‘Sawa wewe wasiliana na mwanasehria wetu ili liwekwe sawa, orodha ya hawa watu umeshaijua,. …fanya kazi, lakini kwanza mimi nina jambo nataka kulikamilisha, nisingependa kujiingiza kwenye hilo, wewe kamilisha wasiliana na mwanasheria wetu na nitatoa ushirikianaoo pale inapobidi, mimi bado kuna jambo nataka kulimaliza…’ akasema Inspekta.
‘Jambo gani mbona huwi wazi ..hii ni kazi yetu sote, wewe unaonekana unafanya kivyavyako…tutafika kweli ..? akalalamika Msaidizi.
‘Imbebidi nifanye hivi kwasababau ya usalama wa taifa…kila mara tukiliweka swala linalohusiana na kesi hii mezani watu wachache wanalichakachua, sasa …naona lazima kutumike mbinu za hali ya juu…, lakini usijali utapata mambo yote ya kesi hii mapema iwezekanavyo, kwasababu nguvu ya dola ni kubwa, haki wakati wote ina nguvu…hilo nakuhakikishia, hakuna hata siku moja mtu akawa mjanja wa sheria na kudumu na dhuluma yake, kwani dhuluma inapodumu…’ akasema Inspecta na haku,malizia usemi wake huo, na akiinuka kwenye kiti chake, baada ya kuangalia saa yake, alikumbuka kuwa ana miadi na jamaa mmoja ambaye aligundua kuwa ana fununu na jambo analolifuatilia…alitoka mle ofisini na kumwaacha mwenzake akiwa anaangalia  juu akiwa anatafakari maneno ya mkuu wake.
‘Huyu mtu ana kitu gani anafuatilia, …’ akawaza baadaye akachukua simu yake ambayo hutumia kwa kazi zake maalumu akatafuta namba , akaipiga na ilipopokelewa akasema maneno mawili tu. `mambo shwari..’
                                       ********
‘Jengo hilo unaloliona hapo mbele limejengwa kwa miaka 15, hutaamini …hilo , na nakuambia vifusi vilivyotolewa hamo vingeliweza kujaza eneo la kigamboni, ilifikia hatua watu wakawa wanajiuliza kuna nini kinachimbwa humo ndani…cha ajabu wajengaji wake walikuwa wageni watupu, na walipomaliza kazi ya ujenzi huo hawakuonekana tena, na sasa jengo limekamlika kilichobakia ni historia, hapo ndani ni starehe kwa kwenda mbele, …lakini hakuna anayejua kuwa chini kuna jengo jingine huenda kubwa kupita jengo tulionalo juu.’ Akasema Mzee mmoja.
‘Unasema na wewe uliwahi kuwa fundi wa hilo jengo?’ akauliza Inspecta
‘Ndio nilikuwa fundi mkuu wa sehemu ya juu, huko chini sikuhusishwa kabisa…licha ya kuwa nina utaalamu huo, …lakini  hata hivyo sikuwa mjinga, siku moja moja huwa nadadisi nini kinachoendelea huko chini, maana kifusi kilkuwa kingi kinatolewa toka huko chini, …lakini udadisi wangu uliishia kuchungulia tu, …maana kulikuwepo na walinzi ambao walikuwa hawaongei, wanakuonyeshea kwa ishara tu… kuwa ondoka hapo, usisogelee huku au …au kama kuna kifusi kinatoka chini, tunatolewa nje kabisa…Basi sisi tukamaliza eneo la juu tukapewa mshiko wetu, tukaishia…
‘Sasa hicho kifusi kilikuwa kinapelekwa wapi..?’ akauliza inspecta.
‘Kilikuwa kinasafirishwa, kilitoka humo kikajazwa kwenye vyombo maalumu na unajua hapa ni ufukweni, meli inaegeshwa kwa mbali, na kifusi hicho hupelekwa hadi kwenye hiyo meli, na kinapelekwa kusikojulikana….Na nikumbie jambo moja wenzangu waliojifanya midomo mirefu, walipotea kimiuiza, mmoja baada  baada ya mwingine.  Mimi n ilipoona hivyo, kuwa wote waliopotea ni wale ambao waliokuwa wakijua hiyo sehemu ya chini…na nimebakia peke yangu…, nikahama jiji, na kwenda kijijini, nilikaa miaka mitano huko kijijini, baadaye nikaamua kurudi tu nikijua hakuna baya linaloendelea tena...’ Akasema fundi
‘Uliporudi ikawaje..?’ akauliza inspecta
‘Nikafunga mdomo wangu kama kawaida, na wewe ni mtu wa kwanza kumsimulia hiyo taarifa, naogopa sana,…hata hivyo nimekuwa nikihakikisha kuwa sionekani kabisa, na kuacha kabisa kuja maeneo ya huku…nilikuja lkaribuni kuchunguza nini kinaendelea huku na ndipo nikakutana na wewe na kwa vile wewe nakuamini sana nikaona nikusimulie hili jambo, labda linaulikana kwa serikali au labda jhalijulikani, lakini kwa vile naipenda nchi yangu nikaona lazima nilifikishe kwa watu ninaowamini, ili moyo wangu utulie, na sasa najue limefika hata wakinikamata sijui wanaua au wanafanyaje,nitakuwa sina wasiwasi tena …, ila mungu akipenda naona kesho narudi kijijini  kwetu,,,maana nimesikia tetesi kuna watu wananiulizia, nina wasiwasi ndio hao jamaa…’ akasema yule fundi kwa wasiwasi
‘Unaweza kuwajua hawo watu kwa sura ukiwaona…’akauliza Inspekta
‘Nawajua…kama unataka kuwajua kesho nitakupeleka mahala wanapopenda kukaa, huwa wana taxi zao wanaziegesha maeneo yao kwa ajili ya wageni wao…’ akasema fundi
‘Wageni wao, wageni gani hao..? akauliza inspekta
‘Wageni toka nje…kuna wageni ambao wakifika hapa nchini wanachukuliwa juu kwa juu, na wakiondoka ni hivyohivyo…’ akasema fundi kuonyesha anajua mengi sana, lakini alikuwa akiongea kwa wasiwasi, na Inspekta akawa na hamu ya kumuhoi tena baadaye kwani kwa muda ule alikuwa kapokea simu kuwa anahitajika ofisini, ikabidi amuulize yule mlinzi maswali ya harakaharaka.
‘Hebu niambie huo ujenzi wa chini kwa chini ulikuwaje…, maana nijuavyo jengo refu kama hili linahitaji utaalamu wa hali juu, cjoni kuwe kunajengwa, na juu …hapo kuna tia utata kidogo? Akauliza Inspekta.
‘Kama nilivyokuambia sisi hatukuruhusiwa kabisa kujihusisha na lolote la ujenzi huo wa chini, lakini utaalmu ulitumika kuwa eneo la juu lina upana wa kutosha na kulikuwa na mihimili yake, na huku chini kutakuwa kama panajitegemea…ni utaalmu tu umetumika kwa mafundi wanajua hilo…nikuambialo walikuwa wamaingizwa vibarua vya ujenzi wa juu lakini hakuna hata mmoja angelijua kuwa kuna ujenzi kama huo, kama sio hivyo vifusu na nondo na …ujenzi huo ulichukua muda sana…sijui wamejenga nini huko chini… ila nahisi kuna kitu chini kwa chini…na nahisi kuna eneo kubwa sana, kuna kipindi watu walilalamika kuwa ardhi eneo hilo inatikisika kama tetemeko..hawakujau ni kwasababau gani, mimi nilijuahilo kuwa ni mitambo inayongurumiswa humo ndani,…nan i kwasababau ya ujenzi ulikuwa ukiendelea huku chini…
Ina maan wewe kuwahi kabisa kupenya na kuangalia huko chini..? ‘ akauliza Inspecta
‘Hapakuruhusiwi kabisa, na hata huo ujenzi wenyewe mara nyingi ulikuwa ukifanyika usiku, na huwezi jua kuwa kuna sehemu ya chini  watu wanafanya kazi, huwezi gundua…kwasabaabu kumzibwa kama kawaida,…ikifika muda kifusi kinatolewa ndipo utaweza kugundua hilo, na kifusi hicho hutolewa na `lifti’…’ akasema fundi
‘ Unasema  na `lifti’... hiyo lifti ilikuwa ikitolewa sehemu gani ya jengo…na huo mlango wa kwenda chini upo sehemu gani ya jengo…?’ akauliza Inspekta
‘`Kwenye hiyo hiyo `lifti’ ya kupanda na kushuka ndipo hapo hapo walipokuwa wakitumia, kuna jinsi wanabonyeza wenyewe, na lifi inapitiliza, lakini sio rahisi kwa mtu baki kuingia humo,….sio rahisi kabisa…nasikia ukiingia tu, unaonekana kwenye mitambo yao…kuna ulizi wa hli ya juu’ akasema fundi.
‘Naomba kesho tuonane ili ukanionyeshe hapo ambapo watu huegesha magari yao…na kama unafuatiliwa ni bora uwe na tahadhari na nionavyo mimi unahitaji msaada wa ulinzo kwani tutakuhitaji wakati ukifika…’ akasema Inspekta na kuachana na huyo mzee  ambaye alionekan kuchoka sana, na sio sababu ya umri bali inaonekana kutokana na maisha..alifikiri anamgeukia na kumpa pesa kidogo ya kumsaidia siku mbili tatu. Jamaa akashukuru sana.
                                                                              *************
   Maneno akisimama akaanza kuzozana na mkewe baadaye akaichukua laptop yake ikiwa bado na ile CD, na kuikumbatia kuhakikisha kuwa Maua haichukui, akamwangalia mke wake ambaye alikuwa kakasirika karibu ya kuzima, alikuwa kauinua mikono juu kuonyesha kuwa hataki kuongea kabisa na mumewe, lakini Maneneo akamwambia mke wake.
‘Huu ni ushahidi wa mambi unayonifanyia, nimekuwa gizani wakati wote, kumbe mwenzangu una lako jambo, una mpenzi wako wa pembeni, Bosi, bosi, kumbe ni bosi wa kila kitu….hii lazima niifikishe kwa baba yako, ili kama kuna lolote litakalotokea niwe nimesafisha mikono yangu…’ akasema Maneno.
‘Unasema nini…unataka umepekee baba yangu huo uchafu…hebu fikiria vyema…ukimpelekea baba ndio atafanya nini…ndio ataninyima, na kunyang’anya kila kitu…sio ndio unavyotaka, na wewe ?...halafu huo mkanda una nini kibaya, wewe unajua kazi yangu ni nini…unaishi unakula, …unajua pesa mimi nazipataje…’ akasema Maua kwa hasira
‘Ina maana tunaishi kwa pesa haramu, maana unavyodai ni kuwa unajiiuza …’ akasema Maneno na kunyamziswa kwa kofi ambalo hakulitegemea na hata Maua hakutaraji kufanya hivyo kwani alionekana kubakia mdomo wazi, na kusema `samahani sikutaraji kufanya hivyo…ila umeniuzi …kama wewe ndio unafanya hii kazi ambayo imenisababishia hadi niumwe , niwe zezeta…na mwisho wake ndio huu unataka kuniaua kabisa…’
‘Sio mimi nimekufanyia hivyo, ni matendo yako machafu na sioni kwanini unaniomba samahani wewe ndio mume wa nyumba hii, nifanye utakavyo, piga vibao, ongeza kingine...nashukuru sana mke wangu, kwani habe jiulize na ujiweke katika nafasi yangu…ungejisikiaje ..uone vitu kama hivi…ufanyiwe kama hivi na mkeo..nini maana ya ndoa..?’ akasema Maneno na kutoka pale chumba caha mongezi na kukimbilia chumani mwake, akamuacha Maua akwia kainama chini, katahayari, na kashindwa afanyeje..akilini mwake alishaweka kuwa mume wake ndiye mzandiki wake, anafanya hivyo ilia pate fedha…ana tama za kijinga…akaanza kujenga chuki!.
                                                          *************
 Maneno alipofika chumbani mwake akachukua kila kitu ambacho anaona ni chake, akaweka kwenye begi kubwa la safari akatoka chumbani harakaharaka, akitaraji atamkuta Maua hapo barazani ili amuage, lakini alipofika hapo  alikuta Maua keshaondoka, hakutaka kumpigia simu, akachukua pikipiki yake na kuingia nayo barabarani   moja kwa moja hadi kwenye kibanda chake, ilikuwa nyumba ya vyumba vitatu, na karibu kila kitu alishanunua!
‘Sasa kazi imeanza, nifanyaje, niende nikamuone baba mkwe…, lakinii nahisi Maua keshakwenda huko, kuniwahi, sasa…hapana ngoja niende kwa rafiki yangu…mpiga picha’ akatoa ile CD kwenye laptop, na kuificha sehemu ambayo alijua hakuna anayeweza kuipata, akatoka nje akachukua pikipiki lake hadi kwa rafiki yake, alipofika akakuta mlango upo wazi, akashangaa sio kawaida ya rafiki yake, …haachi mlango wazi hata siku moja, akaingia ndani kwa haraka, akakuta kupo shangala baghala, vyombo vimevunjwa, meza zimevunjwa…kila kitu kipo juu-chini!
‘Mpiga picha…mpiga picha..’ akaita jina ambalo ndilo linalojulikana sana, lakini hakusikia kitu, akatafuta kila kona ya nyumba, hakuona mtu, na mbaya zaidi nyumba hiyo alikuwa wakishi wapangaji wawili na mpangai mwingine alikuwa kasafiri kwenda kwao, kwahiyo kulikuwa hakuna wa kumuulizia…akakumbuka jambo ambalo aliambiwa na rafiki yake jana yake.
‘Kama utafika unikute sipo au kuna jambo limetokea, angalia kwenye kona hii inua kitanda, hapa kuna shimo, unachotakiwa kufanya, hika kamba hii ivute kwa juu kutafunuka halafu utaona zana zangu nyeti…au nenda chooni angalia  juu ya ukuta utakuta maelekezo…!’ alipokumbuka hivyo akakimbilia chooni kwanza na kweli juu ya ule ukuta aliona karatasi yenye maelezo.
‘Kwenye ile sehemu kuna kamera yangu ndogo, ndani kuna mkanda maalumu, uchukue na upeleke kwa Inspekta, lakini kabla ya kufanya hivyo, hakikisha umeweka akiba yako, toa kopi nyingi, na ingia kwenye mtandao tuma kwenye e-mail yako, hiyo picha nzima, kwa ajili ya kujihami, hata ikipotea utakuwa na ushahidi mzima! Usimwamini yoyote  zaidi ya Inspecta…hakikisha hizo zana haziingi mikononi mwa hawa watu, zaidi ya inspecta..’
 Alipomaliza kusoma yale maelekezo akakimbilia chumbani na kufanya kama alivyoagizwa, akakuta kila kitu , kamera ndogo kama simu, na baaadhi ya CD, na akavichukua vyote na kutoka navyo nje akihakikisha amefunga mlango vyema akalirukia pikipikii lake hadi kwake, na alipofika hakupoteza muda akaanza kufanya kama alivyoagizwa
  Alichukua simu yake ndogo, akapachika waya halafu akaunganisha na computa yake ndogo, akabonyeza sehemu na picha zikaanza kuonekana, alitizama kwa muda halafu akachukua santuri ndogo za kunakili na kuanza kunakili kile kinachoonekana kwenye computa ndogo, alipomaliza santuri , akachukua nyingine, na nyingine, halafu akachukua santuri, na mbili akaziweka kwenye kabati ambalo alilifunga na funguo, nyingine akaweka kwenye koti lake alilokuwa kavaa!
Alichukua simu yake akatafuta mtandao wa yahoo, akatuma zile picha kwenye anuani ya barua pepe yake. …wakati anaendelea hivi, akahisi nywele zikimcheza, hii ni moja ya dalili kuwa kuna kitu kisicho cha kawaida, akahisi kuna mtu anamchungulia …akatizama huku na kule huku akitega masikio, lakini hakusikia kitu… , ila hisia zilimuelezea kuwa kuna mtu au kitu kisicho cha kawaida. Akazima komputa yake, akazima taa kwanza akachukua ile simu, aliyoikuta kwa rafiki yake na kuiweka kwenye koti lake na kufunga vyema…akaanza kuangaza huku na kule kama ataona kitu kikitembea….
Alipoona kimya akaamua kuwasha taa akahisi hayupo peke yake ndani ya chumba, aliwaza huyo aliyeingia ni nanii na aliingiaje, wakati chumba chake alikifunga, akaogopa kugeuka haraka, akijua kama ni adui atajua kuwa kagundulika na anaweza akachukua hatua haraka ya kumwangamiza kabla hajajiandaa, kwahiyo akajifanya kama vile hajui kuwa kuna mtu. Mwili ulianza kumzizima kwa woga, akahisi kuwa huyo mtu aliyepo nyuma yake ana nia mbaya, …
Akahesabu moja mbili tatu..akainama chini kidogo halafu akageuka…alipata mshituko ambao hajawahi kuuona katika maisha yake, alibakia mdomo wazi, akataka kupiga yowe lakini sauti haikutoka kabisa, na kabla hajafanya kitu, kisu kilichotupwa kwa ustadi kilimchanya pembeni mwa shingo na kwenda kuzama ukutani mwa chumba.
‘Hilo ni onyo, mshikaji, kuwa hatutaki mzaha, unamuona mwenzako alivyo, hapa anahesabau masaa kabla hajakutana na mtoa roho, na wewe ukileta ubishi na kutoshirikiana na sisi ni swala la sekunde chache utaiona dunia nyingine, kwetu hakuna shida, …siunajua tena tunachojali ni pesa…’ ilikuwa sauti nyuma ya mwili unaovuja damu, sura ya mtu ilikuwa imebadilika kabisa, sura ya mtu aliyekuwa naye jana, leo siye yule mtu tena, macho yalishanza kuonyesha weupe, labda ni kwasababau ya kuvuja damu nyingi.
‘Usiwaambie lolo…te, acha nifa, nimeshakufa…na wewe hata ukiwaambia, wata-ku-ua tu…’ kabla hajamaliza maneno kisu kilipita shingoni, na kusambaza damu chumba kizima, kilichofuta ni mkoromo….
 Jicho lilimtoka jamaa, akajua kweli hawa watu hawana mchezo, kweli mwenzake ndio huyo kaaga dunia, inayofuata ni zamu yake, kwa macho ya kujificha akachungulia dirisha, akaona kuwa ule upenyo na utaalamu wake wa sarakasi atapenya tu, na hiyo ndio njia pekee.
‘Ukileta ujanja utatangulia mapema, mkakutane na huyu kikaragosi wako, sasa amepata faida gani, hebu jiulize na wewe amefanya nini na kapata faida gani,…zamu yako, wapi ile kamera mliyochukulia zile picha za video, na wapi picha za video, ….hatutaki kupoteza muda, wewe kifo chako bado, sema ukitupa jibu muafaka , basi huenda bosi akaridhika uka…’ kabla hajamaliza nilikwisha hesabu moja mbili tatu, nikajikumbusha mbinu zangu za sarakasi wakati nikiwa shule, niliruka juu, na kichwa kilitangulia mbele nikapenya kwenye dirisha na kutua nje, na kabla sijatua vizuri, nilijizungusha hewani, kuhakikisha kama kuna kisu kimetupwa kisinipate, …nikatua kwenye majani , na kabla sijatulia nikaruka juu tena na kutua juu ya ukuta unaozunguka nyumba na kupaa hewani, nikijua sasa ama kufa kwa  kisu au bastola au kufa kwa kugongwa na gari au kudondokea kichwa kwenye lami…..yote nikamkabidhi mungu….!



Ni mimi: emu-three

7 comments :

Anonymous said...

Hii imekaa vyema mkuu, maana nimesoma na kurudia na kurudia...safi sana, lete vitu mkuu usicheleweshe!

Anonymous said...

Ni kweli Anony.1. Tupo pamoja mkuu.

BN

samira said...

ni nzuri na inaeleweka m3 tupo pamoja

Faith S Hilary said...

mmmh Maneno kajiingiza kwenye balaa gani tena hili...mara hiki mara kile...uhondo wala hauishi mi nipo kama kawa kama dawa hehe...

Anonymous said...

Vipi mkuu, mbona kimya tena!!!!!!!
Tupe huo uhondo, usichelewe Boss.


BN

emuthree said...

Wapendwa, Samahanini sana nimeshindwa kuweka sehemu inayofuata leo, hata mimi inanipa shida sana kwani nalishaajiandaa niandike nini, lakini duuh, majukumu...umeme, foleni na nini vile ...?.
Msijali wapendwa nitajitahidi kuweka sehemu inayoyofuatia, na huenda ikawa ni mwanzo wa hitimisho wa kisa hiki! KWANINI YOTE HAYO YAMETOKEA, MPAKA BLACKMAIL, MPAKA ....KUMBE NI...tutaona sehemu inayofuta!

Anonymous said...

Walk casually in a sexy shop with him and buy some toys together
so then it will feel completely natural to try the new toy.
my webpage > http://www.sextoysdiva.com