Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, June 14, 2011

Dawa ya moto ni moto-21



Maneno alitafuta kila kona kama alivyoagizwa na Bosi, lakini hakuona dalili ya hicho kitu alichoagizwa, mpaka akaona sasa wenye ofisi ambao wa;ipewa taarifa kuwa Maneno anakuja kuchukua vitu vya mkewe vilivyopo humo ndani , kakawia sana, anafanya nini, lakini kila alipotoa kichwa kuwatizama aliwaona wakiwa katika shughuli zao tu. Maneno alipoona kashindwa kabisa akampigia simu Bosi kule hospitalini na Bosi hakuamini kuwa kile kitu ambacho yeye mwenyewe  alihakikisha alikiweka sehemu salama na isingekuwa rahisi mtu kukiona kweli hakipo, …akajaribu kumwambia Maneno atoe kila kitu kwenye ile droo ya meza na kukung’uta, lakini hakikupatikana kitu.
Akiwa anatafuta akakumbuka jinsi mambo yalivyotokea kwa haraka na kujikuta kwenye matatizo ya ajabu, kupigwa na hata kusingiziwa kichaa, na baadaye akakutana na huyo jamaa ambaye alimuita. Alishangaa kwani alitegemea kuwa aliyemuita ni mkewe, lakini akamkuta ni yule jamaa  ambaye alishuhudia siku ile akipigwa chuma cha kichwa na mwanamke bonge.
‘Pole sana, yule mwanamke bonge alitaka kukua kabisa kama nisingeingilia kati alitaka kumua hata mke wangu, na kwa muda ule nilikuwa sijui kabisa ni mke wangu…’ akasema Maneno.
‘Umeshaonana na mke wako,..?’ akauliza Bosi.
‘Nimeonana naye juu kwa juu, kwani wakati naingia ndipo nikakutana na kisanga kingine, yaani sijui mke wangu ana balaa gani, kwani nimeshuhudia dakitari akitaka kumpiga sindano ya kumuua, aiakponea chupuchupu…’ akasema Maneno.
‘Je uliwahi kuongea na mke wako lolote…?’ akaulizwa tena.
‘Hapana, hawakunipa nafasi, na hata hivyo alizirai kabla sijapata muda huo na polisi wakaja nikasingiziwa ukichaa…hutaamini’ akasema Maneno.
‘Sasa kuna kazi moja, mkeo anaumwa na kuna vitu vyake aliviacha pale ofisini kwake, niliwaambia wafanyakazi wasiguse chochote na mlango ufungwe, hilo ni swala la kawaida kwani kuna mtu kazi yake kufunga mlango na haruhusiwi kugusa kitu chochote, kwahiyo nina uhakika kila kitu kipo kama kilivyokuwa. Ukachukue mkoba wa mke wako, halafu kwenye droo za meza, droo ya juu kabisa ya meza ambayo kuna kiti chake anapokaa, kuna file la bluu, lifungue, ndani yake utakuta bahasha ya khaki imeandikwa jina la mke wako, ina mkanda wa DVD, ambayo imewekwa picha za mvuto. Hayo ni maswala ya kibiashara, kuvutia kile kilichopo ndani, na mara nyingi ile picha sio sawa na kilichopo, ni kuvutia bisahara zetu, usijali sana hiyo picha ilivyo juu..’ akatulia Bosi na kumwangalia Maneno ambaye alitulia kimiya akisikiliza.
‘Tahadhari kubwa, hiyo DVD, ipo nusu haijakamilika, na ukiicheza tu umehaibu kila, inatakiwa mapaka ikamilike ndipo ichezwe, kwahiyo usije ukajaribu kuicheza, unanielewa lakini…wewe chukua hakikisha umeificha mahala ambapo haitaonekana kamwe mpaka mimi nitapokutana na wewe…..ni kazi za kiofisi lakini hazijakamilika, na mimi na Maua ndio tulipewa hiyo kazi na kwasababu haijakamilika hatuwezi kuiwakilisha ofisini…sawa, natumai umenielewa, usijaribu kuicheza utakuwa umeiharibu kabisa na kazi yote impotea…’ akasisitiza Bosi.
‘Sawa, kwanini niicheze na kitu kisichonihusu…ila nataka kumuona mke wangu kwanza, nijue ana hali gani..? akasema, Maneno.
‘Hapana mkeo kwa taarifa nilizozipata hutaruhusiwa kumuona,…wewe kafuatiliea hilo swala nililokuagiza, kwani hilo ni la muhimu sana, kwani najua kitu cha kwanza ambacho kitamuumiza mke wako nikuona hiyo kazi imepotea au kaichukua mtu na kuicheza na kuharibu kila kitu…wewe nenda haraka kahakikishe kuwa ipo , halafu nipigie, simu na kama utakosa sehemu ya usalama ya kuihifadhi bora uniletee hapa, nitajua mwenyewe jinsi ya kuihifadhi…’ akasema Bosi na kutulia akijua kuwa kampata aliyemtaka. Na kweli bosi akaondoka harakaharaka bila hata ya kuaga madakitari na kuelelekea ofisi ya akina Maua, na alipofika hapo akawaelezea walinzi nini katumwa, na walinzi wakawasilinana na Bosi kuhakikiasha kuwa ni kweli, akaruhusiwa kuingia ndani.
 ‘Sasa hiyo DVD ipo wapi, mbona nimetafuta kila kona ya chumba, huko kwenye droo za meza alizoniagiza, hakuna kitu,…ngoja nimwambie sijaiona maana kukaa muda mrefu kwenye ofisi za watu ni noma..’ akasema huku anaendelea kutafuta, na baadaye akampigia simu huyo Bosi kuwa katafuta kote hakuna kitu kama hicho.
‘Sasa hilo balaa, ina maana kuna mtu aliingia humo ndani akakiona hicho kitu na kuondoka nacho , sasa atakuwa nani…’ Bosi, alijaribu kufikiri nani anaweza kuingia mle ndani, kwani chumba kile mwenye ufungua ni yeye na Maua tu. Na kama alivyosikia Maua anaumwa na alikuwa hawezi hata kutoka nje, je alimtima mtu au ilikuwaje, …ina maana Maua kaamua kufanya hivyokuhakikisha kuwa kazi yake inakamilika , …haiwezekani, lazima nifanye mpango nitoke humu nikaonane naye. Lakini walisema hawezi kuongea, yupo kama zezeta , nitawezake kuongea naye?.
                                              ***************
Inspecta alijinyosha mara mbili, akainuka pale kitandani alipokuwa kajilaza na kusimama, halafu akafunua pazia la pale chumbani kwa uwazi mdogo wakuweza kutizama nje, alipoona nje hakuna mtu anayetizama upande ule, akalifunua lile pazia kwa mapana ya kuweza kupata hewa halisi ya nje. Alikuwa kachoka kukaa mle ndani ya chumba kile kama mafichoni, ingawaje mara kwa mara alikuwa anapata nafasi ya kutoka nje akiwa kajibadili kwa namna ambayo asingekuwa raisi kugundulika, na kupita huku na kule katika kazi yake ya kuchunguza nyendo za hawo maadui wake, lakini hali ile ya kuwa mafichoni haikumpa raha…!
Akalifunga lile pazia na kuamua kunyosha miguu kwa kutembea mle kwenye kidispensari baada ya kuona kuwa hakuwa wagonjwa ambao wamefika siku hiyo. Alitoka mle kwenye kile chumba na kuelekea kule ambapo ni ofisi ya yule dakitari anayemiliki hiyo hospital. Kwanza akapitia chumba cha maabara, akakuta dakitari wa maabara akiwa katika shughuli zake, hakumsemesha akafulululiza hadi kwenye ofisi ya huyo dakitari, na kwa vile alihisi yupo peke yake humo ndani akafungua mlango taratibu, bila kubisha hodi, kwani walikuwa watani, na walikuwa wakitaniana sana…!
Ule mlango ulipokuwa na upenyo mdogo akasita kidogo, kwani alisikia sauti za watu wawili wakiongea, akataka kuufunga ule mlango haraka na kurudi alipotoka, kwani itakuwa sio vyema kuingilia mazungumzo ya watu na asije akakutana na mtu anayemfahamu ikalatea matatizo, lakini kabla hajausindika vyema ule mlango, akajikuta akivutika na yale mazunguzo ambayo aliweza kuyasikia vyema, toke kwenye ule upenyo wa mlango, alisikia maneno ambayo yalimgutua kidogo, ikabidi ausimamishe ule malango kwa mguu na kuanza kusikiliza yale mazungumzo.
‘Rafiki yangu, nimekushawishi sana, lakini huelekei,  wewe nishakuambia utakufa masikini, miaka mingapi umeutumikia ujuzi wako huu, na isingekuwa wazo la kufungua hiki kidispensari ungelikuwa  bado unagombea daladala…,na labda ungelikuwa mlevi wa kutupwa. Ujuzi wako ni adimu sana hapa nchini, na kama ungelijiunga na kundi letu ungekuwa mbali sana, watakulipa vyema na marupurupu ya kila namna. Lakini hebu jione ulivyo…,unapata nini, nakushauri kubali ombi langu,…hutajijutia kamwe, na utajipa mwaka mmoja tu,   halafu utakuja kuniambia….’ Akanyamaza kidogo
`Kiukweli rafiki yangu utakuwa huna haja ya kazi,…utafanya tu kwa vile ni kitu unachokipenda, lakini sio kwa shida hilo nakuahidi, ila inataka ujasiri na moyo sugu…hasa mwanzoni, hasa unapopewa kazi maalumu, mimi mwanzoni nilisita kabisa, nilipoambiwa hili, lakini hawa jamaaa ni wajanja, walichofanya ni kuigusa hisia yangu ya ndani, na wana mbinu nyingi zaidi ya hizo hasa wakikuhitaji sana. Kwa mfano mimi walikuwa wakinihitaji sana, wakatumia mbinu nyingi sana, hawakunipata kirahisi, mwishowe wakaamua kutumia njia ambayo wanaitumia sana kwa watu walioshindikana.
 ‘Sio kwamba mimi ni mdhaifi kiasi hicho, lakini hutaamini walininasa kwa kile kitu ambacho mwenyewe nilikuwa nakipiga vita sana, kwasababu walinihitaji sana kwa ujuzi wangu….’ Akasema huyo mtu mwingine, ambaye kwa hayo maongezi alionekana labda na yeye ni dakitari. Na Inspecta akasikia Dakitari wa pale akauliza njia gani waliyotumia. Yule mtu mwingine hakusema ni moja kwa moja ni njia gani kitu gani akaendelea na mazungumzo yake kwa kusema.
‘Hawo watu wasikie tu hivyo hivyo kinadharia, wanaitawala dunia sasa hivi kivitendo, wanaweza kufanya watakavyo, kuwapata wawatakao, kwa njia mbalimbalinia, na sio kwamba wanalazimisha, ila ikibidi wanafanya hivyo kwa utaalamu zaidi. Mimi walipoona nimeshindikana wakatumia mbinu ndogo tu. Nikanasa kilaini sana…’ akacheka yule mtu na akawa kama kainuka kwenye kiti au kukaa kwenye kiti, kwani kulisikika kama sauti ya kiti kikisogezwa.
‘Hivi leo huna wagonjwa, naona kimya kabisa..’ akauliza huyo mtu mwingine.
‘Leo sina, nimeweka tangazo kuwa tunafanya ukarabati na mahesabu yetu kwahiyo kuna siku mbili hatutakuwa na wagonjwa wakija hapa…’ akasema yule dakitari.
‘Safi sana, sasa kumbe tunaweza kufanya jambo moja muhimu sana, ambalo itabidi nikuambie wewe kama rafiki yangu, lilitakiwa kufanyika bila ya wewe kuambiwa lakini sikuona vyema nikakuficha, kwasababu na wewe wahitajika kujiunga kundini, kama hutojali.
‘Hapana ndugu yangu mimi sihitajiki kujiunga na makundi ambayo hayatambuliki kiserikali, na pili kwa jinsi ulivyonielezea, inaonekana hakuna wema kwenye kundi hilo, hebu niambie nini kusudio la kundi hilo, …mpaka nishawishike kujiunga, sababu ni mali au sababau ni nini, kwanza umesema walikushawishii hukupenda, na wakatumia njia fulani, njia gani hiyo…’ akauliza dakitari.
‘Naona unavutika sasa, naogopa kukuambia mengi, kwasababu huenda wakaamua kutumia hiyo njia kwako, lakini kwako nikujuavyo inaweza isiwe rahisi, ila wataongezea nguvu nyingine, ambayo wakitaka iwe hivyo, au la wanaweza kutumia njia nyingine, ilimradi wakunase,…kuna nguvu za ziada wanatumia, hiyo nguvu sikuambii kwa sasa ni nguvu gani, ila kwangu mimi walinipata kirahisi sana hata kabla ya nguvu hiyo. Unajua sisi wanaume ni rahisi sana kushawishika hasa anapokuwepo mwanamke kama mshawishi…’ akasema na kucheka, na dakitari naye akacheka na kusema kwake sio rahisi kihivyo.
‘Najua sana rafiki yangu, lakini wenzako wanajua hilo kabla, hili nakuhakikishia,...’ akanyamaza kidogo. Halafu akaendelea kusema `Sasa mimi walijua kuwa wakifanya hivyo wataninasa kirahisi, …unajua walichofanya, walinifanyia kisa kibaya sana, cha kuninasa ,walijua sisi kazi zetu wakati mwingine ni za usiku, na zamu za usiku zina mitihani, hasa unapopangwa na vibinti ambavyo havijatulia. Walifanya hivyo, na sijui ilikuwaje hadi binti kama huyo tukawa zamu naye, maana huwa hapangwi na mimi…’ akatulia tena.
‘Bai siku hiyo nikapangwa naye kama msaidiizi wangu wa karibu, na huyo binti alionekana na adabu ,mzuri, katulia kwa saa za kawaida, ila ilipofika usiku…nina uhakika walimtumia wao, sijui kwa vipi, kwani mpaka sasa sijagundua. Wakati ilipofika usiku tupo mapumzikoni, alileta kinywaji, tukawa tunakunywa pamoja, nilianza kulewa, sio kawaida yangu, nikaanza kujihisi tamaa, inautawala mwili wangu na kumuona yule binti tofauti, …sijui kilichofuta zaidi , kwani nilimtaka kimapenzi. Yule binti kama nihisivyo ni kweli alikuwa anajua nini anachokifanya akakubali….’ Akacheka na mwenzake akacheka pia, na kumwambia huo ni udhaifu wake asisingizie kuwa kuna lolote la ziada lilifanyika.
‘Inawezekana hakuna kwa upande wangu…lakini kwa mazingira yangu, hata ungekuwa wewe ungesalimu amri…., inawezekana labda kwangu ilikuwa ni udhaifu wangu, lakini siunaijua familia yangu ilivyo, unamjua mke wangu alivyo mrembo, nisingeweza kushawishika kiasi hicho, na kinywaji nakitumia sana, sijawahi kulewa, kukosa kujitambua kama ilivyokuwa siku hiyo! Kiukweli siku hiyo, nilikosa adabu kabisa,  nilichanganyikiwa nikafanya vitu vya ajabu kabisa…’ akasema yule mtu mwingine.
‘Halafu ikawaje, …’ akauliza dakitari. Na huyo mtu akasema `Usiku ukaisha na kesho yake nilikuwa mapumziko nyumbani kwangu na familia yangu. Mara nikasikia kuwa nina mgeni, nilikuwa nimelala, na jinsi ilivyokuwa usiku nilikuwa sitaki usumbufu, ilimradi mke wangu asijue nini kilitokea, nikawa najifanya nina usungizi mzito, wakati kiukweli usingizi ulikuwa haupatikani kabisa, nilikuwa na mawazo kwa dhambi ile….
‘Nimesema sitaki mgeni ..nimechoka, nikawa mkali kweli, lakini mke wangu akasema mgeni huyo ni nesi ninayefanya naye kazi anasema ana ujumbe muhimu, nikauliza nesi huyo anaitwa nani, akamtaja jina lake, niliposikia hilo jina niliamuka haraka kitandani, na bila kusema kitu, nikatoka na nilipomuona nilitamani nimumeze kwa hasira, nikajifanya hakuna kitu nikamkaribisha chumba cha maongezi, nikahakikisha kuwa mke wangu katoka nje , halafu nikaanza kuongea kwa hasira, kumuuliza kafuata nini nyumbani kwangu…’ akasema huyo jamaa.
‘Sasa hivi unakuja juu kwa hasira, nimefuata nini, mbona jana usiku hukuwa hivyo…au kwa vile umapata ulichokitaka, sasa …’ akaniambia yule nesi kwa sauti, iliyonifanya niweke kidole mdomono kumuonyesha kuwa anyamaze, lakini kabla hajaendelea akaanza kulia na kutoa, na baadaye akatoa bahasha, na ndani ya ile bahasha kulikuwa na kanda ya DVD , akanipa na kuniambia niiangalie eti mimi nimeamua kumharibia maisha yake kwa kumdhalilisha. Niliposikia hivyo nikahawa na wasiwasi na hisia zangu zikawa zimenipeleka mbali sana.
Nikaichukua ile kanda haraka na kuitizama, hakuwa na kitu juu, cha kuonyesha lolote baya, kwahiyo usingejua ndani kuna nini, nikachukua `laptop ‘ yangu, ambayo haikuwa mbali, nikaiweka ile kanda, na kabla haijaanza kuonyesha hicho kilichomo, yakapita maandishi ya kisema kanda hiyo haifai kuonyeshwa kwa watoto, na yaliyomo ni mambo ya siri kubwa, kwani yalichukuliwa kwa watu wawili walioamua kuivunja ndoa yao kimatendo, nan i tukio kweli tupu, kwa….’ Akakatisha hayo mazungumzo na kutulia kwa muda,mpaka dakitari akamuuliza ilikuwaje baadaye.
‘Baadaye, …sitaki hata kuhadithia nilichokiona mle ndani, ila baadaye ikapigwa simu na mtu nisiyemjua akidai kuwa anataka kuonana na mimi kuhusiana na hiyo DVD, kuwa inafanyiwa kazi kwani kuna sehmu yake ya pili ambayo ndio inaonyesha kila kitu kwa uwazi, nifike hospitalini kwenye chumba cha maongezi nitakutana na huyo jamaa. Niliitoa ile DVD haraka kwenye laptop yangu, nakuiharibu mbele ya yule binti kuhakikisha kuwa haifanyi kazi tena, na wakati nafanya hivyo akatokea mke wangu na kuniuliza kwanini naharibu hiyo DVD, nikasema ni kazi niliyompa huyu nesi kaifanya isivyotakiwa…basi baadaye nilienda kuonana na huyo jamaa, akanipa masharti kadha mojawapo ni kutii yale nitakayo agizwa, ili kanda hiyo isisambaye..’ akasema huyo mgeni.
‘Kwanini usiwaambie polisi…maana hiyo ni `pure blackmail…’ akasema dakitari.
‘Niwaambie polisi, aheri sikuwa na wazo hilo, kwani hujui nini kinanednelea , huwajui hawa watu, kila unalofikiri wao walishafikiria kabla kuwa utachukua hatua gani…na huko utakapokwenda utakutana na nani, na huyo utakayekutana naye ni mtu wao….sasa nini kitakachofuata, wanatoa nakala moja kwenye gazeti la udaku, kama `trailer’…’ akasema huyo mgeni.
‘Hicho ni kitisho tu, ndugu yangu, hawo ndivyo walivyo, kuna kikosi malumu cha kupamabana na hawa watu wanawajua mbinu zao, …lakini nisiseme mengi, ila ilikuwaje baaaye..’ akauliza yule dakitari.
‘Ilikuwaje baadaye, huwezi kuamini nilikuwa kama kaondoo, kila wasemalo nakubali, na mwishowe nikawa ndani ya kundi.
‘Kama ujuavyo mke wangu nampenda sana, tumetoka naye mbali, tumahangaika kimaisha mpaka tukafanikiwa, na familia yao imechangia kiasi kikubwa sana kufanikisha haya, sasa aonyeshwe huo uchafu nilioufanya na yule nesi, nikajikuta nakubali kama walivyoniambia, …na nakumbia baadaye sikujutia kujiunga na hilo kundi, kwani pesa zipo nje nje,na kila ninachokitaka nakipata, sasa nataka nini katika dunia hii…’ akasikika yule jamaa akitamba na kukohoa kinamna ya madaha.
‘Bwana acha nife na umasikini wangu, kama nyie mnauona ni umasikini, lakini mimi najiona nipo vyema kabisa, sina shida …natala hela za nini zaidi, hii dispensary inanisaidia napata mshahara wa kunisaidia, …sioni kwanini niingie kwenye tamaa.
‘Mimi nimekutonya hilo kama rafiki yangu, sina zaidi la kukuambia, ila wao najua watakualika kwa njia waijuayo wao, ila nakushauri usije ukalogwa ukasema naenda polisi, hasa kwa haya niliyokuambia kwani wao wameshalijua hilo mapema, nina uhakika utakayekutana naye ni mtu wao, na yupi ni yupi huwezi kuwajua….’ Huyu jamaa akasema.
‘Sasa nini lengo lao, ni nini wanachokitaka…’ akauliza dakitari.
‘Wanachokitaka ni kuhakikisha kuwa dunia hii inakuwa mikononi mwao, dunia iwe huru kama wanavyodai, wanaitumia neno `free mind’…yaani binadamu awe huru, awe na utashi wa kufanya alitakalo, bila uwoga au kizuizi fulani, ukijiskia kutembe uchi, tembea, …na vitu kama hivyo…uwe huru…na maisha yako upendavyo na uwezevyo, kwa mfano madawa ya kuelvya yawe kama sigara, watu..watumie wapendavyo…unajua kuna biashara zikiruhusiwa pesa itakuwa nje nje, kwa mfano ya madawa ya kulevya na bangi, mfano kuna biashara ya chini kwa chini ya mapicha ya uchi haya yanawaingizia mapesa kibao, mfano, makasino, mfano…umalaya, watu wajiuze na bishara kama hiyo iwe biashara kama biashara nyingine..sasa ukiangalia kuna vizuizi vikubwa viwili, dini ikiwa inaongoza, na pili katiba za nchi…hivi wanavipiga vita sana.
‘Hawafanikiwi kwa hilo..nakuhakikishia hizo ni ndoto za mchana…’ akasema dakitari.
‘Sawa, labda usemavyo ni kweli,hata mimi nilisema na kuwaza hivyo kabla, niliwaza hivyo lakini siku zilivyokwenda na kulisoma hilo kundi, na kuona wanayofanya, nahisi tuendapo tutaingia wenyewe mmoja baada ya mwingine, kwani wanachokifanya, hawana haraka nacho, wao walivyoanza kwanza kabisa ni kubadili tabia za wa kuwapata watu na kuwasomesha, unafadhiliwa halafu unatakiwa ulipe fadhila, unapewa misaada unatakiwa ulipe fadhila…utumwa wa aina yake …. Angalia vijana wetu wanavyobadilika kirahisi, mateja..ulevi kupindukia..na mienendo yao, nikuulize kitu, wewe ulijua kuwa nchi kama za Waarabu kungetokea haya mabadiliko kama yanayotokea sasa hivi, …hebu fikiria hawa watu wanashida gani ukilinganisha na sisi, …kwanini sisi tusiwe  wa kwanza kufanya hivyo wafanyavyo wao…sisi ni masikini, tuna shida, lakini imeanzia kwa wenzetu ambao tunaona wana afadhali…’ akanyamaza kidogo halafu akasema
`Wao wameanza huko,  na walioanzisha sio kundi kubwa kama unavyodhania, walioanzisha hilo vuguvugu, ni huenda ni hawo waliotengenezwa, ni hawo wanaotaka mabadiliko ya haraka, lakini mwisho wa siku sio kwa manufaa ya wengi….lakini kwasababu ya maisha yalivyo, uroho wa madaraka na kwasababu wengine walishachoka na maisha ya watawala, wanateseka wananyimwa haki zao, uhuru wa maisha wayatakayo, wanajiona hawana raha ndani ya nchi yao, ni raisi kwao kujiunga  kirahisi, lakini hawajui nini kitafuata baadaye…hawajui kabisaaa..masikini ya mungu…’ akasikika huyo mtu akiongea kwa sauti ya huruma.
‘Sasa wewe kama unajua hivyo kwanini umejiunga na kundi hilo…?’ akauliza Docta, lakini yule mtu hakumjibu, akaendelea kuongea na kusema;
‘Hili kundi, wana mikakati yao ya kuua utamaduni wa imani za dini, wanajua huko kwa Waarabu ndipo kwenye kiini cha `imani za dini’ hizo, ambazo kubadili tabia na tamaduni zao zinahitaji ujanja, na akili , sio papara au miguvu kama zamani……hizo imani zinatakiwa kuvunjwa nguvu kidogokidogo…kwa kudhoofisha tamaduni zao, ….’ Akanyamaza kidogo
‘Sasa huku kwetu kuna nini mpaka waweke kambi, ? ni swali hata mimi nilikuwa nikijiuliza, lakini nikuambie kiukweli, huku kwetu kuna utajiri  wa hali ya juu…huwezi amini…lakini hawana haraka sana na sisi kwani bado tunapambana na maadui watatu wakubwa, ujinga umasikini na maradhi, haya yanatutosha kutumaliza, kwahiyo hawana shida sana na sisi, ni kiasi cha kusema nenda kushoto, tunakwenda, nenda kulia tunakwenda…hakuna shida kabisa…
‘Nikuambie ukweli ndugu yangu, hizi mbinu wanalizotumia kwa mtu kama mimi ni kwa watu wachache ambao lazima waingizwe kwenye kundi hili haraka ili kufanikisha lengo lao…watu watabadilika, maisha yatabadilishwa…kwani watakaojaa madarakani ni nani kama sio wao…’ akasikia yule mtu akivuta kiti, na kusema, `hawa hapa kwetu wanajiita `watashi huri’ au `freeman, …’ ni tawi dogo tu la kundi kubwa ambalo linajulikana kama `freemason’
‘Unasema nini, …’ akasikika dakitari akiuliza kwa mshangao.
‘Hiyo ndiyo habari yenyewe….’  Na baadaye kukawa kimya, na Inspecta akasoge pembeni na kujibanza kwenye chumba kingine, hakuweza kusikia yaliyoendelea baadaye, lakini haikuchukua muda mlango ukafunguliwa na yule jamaa akatoka na mtu dakitari. Na inspecta alipomuona sura ya yule mtu alishituka  alitamani kumtokea na kumzaba kibao…hakuamini…hakuamini, na kusema neno moja tu `msaliti mkubwa wewe…. ama kweli sasa dunia imekwisha’.

Ni mimi: emu-three
Enhanced by Zemanta

5 comments :

samira said...

m3 makubwa naona docta wa pili kundi lake ndo walomfanyia mauwa unyama ule wa dvd
swali hawa watu wanataka nini
cant wait

Yasinta Ngonyani said...

inatisha kiduchu,,inasisimua na siwezi kusubiri.Kweli hapa duniani kuna mambo "kweli dunia imekwisha"

emu-three said...

Wapendwa wangu, nilitaka leo kuendelea na sehemu nyingine, lakini tatizo la mtandao na umeme, limekuwa kikwazo. Sehemu inayofuata ipo tayari, na swala la kuipitia kidogo na kuiweka hewani.
Nilitaraji kuwa sehemu hii ingekuwa na maswali mengi ya `kulikoni' lakini nimeona wengi wameielewa. Kuna mamb o nilikuwa nayafuatilia ili kujua ni `kwanini', ...kwahiyo tuwe pamoja ili tuweze kufaidikia na kisa hiki. Natumai hamjakichoka, kwani ndio mambo yankwenda kule penyewe kutokana na kichwa cha habari.
Ni kweli Samira utashangaa zaidi kuhusiana na hawa madakitari..., na dada Yasinta, mabo yanakuja , kuogopesha, kusisimua na kila kitu utakipata. Nawashukuru kwa kuniunga mkono kivitendo.
TUPO PAMOJA

Anonymous said...

Ndugu yangu wee haya mambo unayosimulia kama hadithi ni kweli kabisa hakuna moja la uwongo humo. Ukiangalia kinadada wanavyotembea uchi na wanavyocheza kuashiria ngono kila mahali mpaka kwenye muziki wa taarabu, na hiyo ngono inavyofanywa wazi wazi kwenye mahall ya muziki tumemzidi hata huyo shetani. Labda niseme ni Illuminate ndio wahusika na si freemasons maana uanachama wa freemason uko wazi lakini huwezi kujua hao wa Illuminate na alama zao za vidole kama pembe. Na wanaoingia huko lazima wawe matajiri wa kutupwa ghafla tu.

Jamani nilitumiw picha kwenye email ya msichana kwenye hall hajulikani kama anavaa au anavua hiyo nguo; nimeona aibu kuiforwad kwa wanaume, maana nusu ya mgongo iko wazi, imeziba kiunoni lakini sehemu ya juu ya matako iko wazi kabisa yaani chupi imeshushwa chini ya matako, sijawahi kuona hicho kivazi hata kwa wazungu pamoja na kukaa kwao miaka, literary the girl was naked mtu akitaka ngono kiasi anainama basi kazi kwisha. Mwingine picha yake ilitolewa kwenye gazeti moja la udaku yeye anadai usiku havai nguo ya ndani kabisa kisa inamtia uzito, eeh mungu tunusuru waja wako maana gharika ikija haichagui kuwa wewe ulikuwa msafi au vipi inatusomba wote kweli dunia imekwisha tusubiri kiama.

Faith S Hilary said...

hehehe "freemason"...doh doh doh!!! kwa kweli unasoma huku unaogopa kama alivyosema dada Yasinta hapo juu...pia poleni na matatizo ya umeme M3...sijui yataisha lini...japo kwa muda basi :/...bado nipo!