Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, June 10, 2011

Dawa ya moto ni moto-20 Bosi aliinua kichwa chake ambacho kilishaondolewa lile bandeji kama mhogo alilokuwa kavikwa kichwani, na kujiona kama mtu aliyevuliwa mzigo mzito , akatikisa kichwa chake kuhakikisha kuwa ni kizima, hakuamini kuwa bado yupo hai, alimwangalia yule nesi aliyekuwa akimfanyia hiyo kazi na docta, docta baadaye aliondoka muda mfupi baadae na kumwacha yule nesi akimalizia kazi nyingine, za kumsafishha na kuhakikisha kuwa mgonjwa yupo katika hali nzuri, na pia kumpa dawa alizoandikiwa.
 Bosi akili yake ilikuwa imegibikwa na mambo mengi, alipozindukana tu alisikika akiita Maua, maua mbona umenifanyia hivyo…madocta walimuuliza Maua ni nani, hakuweza kuwapa jibu. Baadaye mke wake alikuja , na kusalimiana naye, na aliambiwa kuwa mke wake kila siku alikuwa karibu yake. Akamwangalia mke wake kwa macho ya huruma, akijua kuwa yote ambayo kajitolea katika maisha yake, bado yeye amekuwa sio mume mwema, akasema moyoni, siku nikifanikiwa kuwapata hawa watu waliotaka kunimaliza na kuona kila kitu kimetulia nitamsimulia mke wangu yote yaliyonisibu kama njia ya kusafisha ndoa yake.
‘Mke wangu samahani sana kwa haya yote, nimekuingiza katika maizo yasiyokuhusu…’ alimwambia mke wake.
‘Mume wangu cha muhimu sasa ni kuangalia afya yako, mengine hayana umuhimu kwa sasa, kwani hakuna aliyeona kile nilichokiona, hata kama ungelikuwa wewe ungelichukua hatua niliyoichukua, ni hasira na …ni fundisho kwa wanaume wasiojali ndoa zao, ndoa sio kitu cha kuchezewa…!’
Alikumbuka jinsi alivyojitetea kuwa sio kweli kama alivyodhania, alikuwa akijaribu kumzindua Maua kwa njia ya mdomo kwa mdomo ili kumfanya mgonjwa mapigo ya moyo yafanye kazi…, hapo hapo mke wake alidakia kwa kusema, kwanini alichagua njia hiyo asitumie njia ya kifuani kwa kumkandamiza mgonjwa kwa mikono miwili ili mapigo ya moyo yafanye kazi yake, akaamua kutumia mdomo, kwa vile aliona ni kawaida kwake, ….
Bosi kila alichojitahidi kujielezea alijikuta akiandamwa na sababu ambazo zinamtia hatiani…na kama asingekuja docta na kuingilia kati angejikuta katika hali mbaya. Docta alikuja na kumkanya mke wa Bosi kuwa mgonjwa hajapona,hatakiwi kupewa shinikizo la kufikiri sana, ataumia kichwa, ambacho kinahitaji mapumziko ya muda kidogo, hapo ndipo kukawa kimya …
Bosi akainuka pale kitandani na kumwangalia nesi akiwa katika pilikapilika zake, akakohoa kama kumshitua vile na kusema;
‘Nesi ule ujumbe wangu uliufanyia kazi, maana huyo jamaa ni muhimu sana kwangu…’ akauliza Bosi,
‘Upi tena wewe, hebu pumzika kwanza, unasema ujume ule wa kupiga simu kwa huyo jamaa au sio? Akasema nesi na kugeuka kumtizama Bosi akiwa kaka kitandani. Bosi alikuwa kaamua kumwagiza Mume wa Maua afike hapo hospitalini, baada ya kuulizia kuhusu Maua na kuambiwa Maua kalazwa hapo hospitalini pia, akiwa kama kachanganyikiwa hajui lolote, yupo kama zezeta, akaona lazima afanya juhudi ule mkanda aliouona ofisni kwa Maua unakuwa katika usalama, na alifikiria sana, ni nani anaweza kuuficha ule mkanda, kwasababu ukiangukia mkononi mwa maadui utaleta kashifa, na pia akiupata mke wake, itakuwa ndoa imekwisha na anaweza kuishia kifungoni kama sio kutupwa mitaani kwa kashifa nzito.
Aliwaza, sana nani ambaya anaweza kumwamini, amuagize ukaufiche ule mkanda, aliouona ofisni kwa Maua hakuweza kumwamini mtu, aliona mume wa Maua anafaa, kuuchukua na hata ikiwezekana auharibu, lakini hakupenda uharibiwe, alitaka kuuona una nini, na kwanini Maua akaamua kuandaa mkanda kama ule ambao ungeliweza kuangamiza ndoa yake…akawaza wafanyakazi wote anaofanya nao nani wa kumwamini , hakumpata wa kumwamini, karibu wafanyakazi wote nii wajanjawajanja hawaaminiki. Mwishowe, akaona ni bora zaidi kwa mume wa Maua kumpa kazi hiyo.
Yule ni rahisi kumdanganya kuwa ule mkanda ni wa kikazi, ile picha pale juu imewekwa kama kivutio katika maswala ya kibiashara, na hairuhusiwi kuchezwa kwenye DVD, mpaka iwekwe vyema kwahiyo asije akajarubu kuicheza kwenye DVD, kwani itaharibika mpaka iwekwe, akiicheza itafutika…akawaza mbinu hiyo akaona itakubalika kwa mtu kama yule…alimjua vyema kuwa na tangu alipomjua alikuwa kamdharau sana kuwa anaweza ni mume wa ndio, ndio tu…lakini je akiamua kuungalia, si ndio atakuwa kachangia kuvunja ndoa ya mwenzake…hapana, yule jamaa anavyomjua akimwambia kitu atafuata kama alivyoagizwa, ni kama atamua hivyo ni heri yeye auone, na hata ndoa yo ikivunjika lakini ana uhakika siri haitaenda mbali, kuliko ifike kwa mke wake!
‘Nesi naomba umpigie tena yule jamaa simu kuna kitu kikubwa nataka  kumwagiza ofisini…’ akasema Bosi. Yule nesi akamwangalia Bosi na kumuuliza kwanini hakumwagiza mke wake wakati muda wote alikuwepo humo naye. Bosi akamjibu mambo mengine hayamhusu mke wake ni siri kati yake na huyo jamaa, na anaomba kabisa asimwambie mkewe wake kuhusu hilo jambo.
‘Naomba sana nesi hili halimhusu mke wangu, ni dili zangu za kibiashara na huyo jamaa…’ akamsisistizia
‘Wanaume bwana wote akili zenu na mawazo yenu ni sawa, huyo jamaa nina uhakika yupo njiani, au keshafika ila hajagundua wapi anatakiwa aingie wapi, nitakwenda kutangaza kwenye kipaza sauti, kuwa kama kafika aje huko wodini….’ Akasema yule nesi
              ************
 Maneno alikuwa kafungwa mikono na miguu na kuwekwa chumba cha wagonjwa wa upungufu wa akili, alijaribu kujitetea, lakini wale askari waliishia kumcheka, na kumdhihaki kuwa kichaa chake kinaonekana kinapona karibuni, lakini ngoja wanamsubiri docta aja kumwangalia kama kweli anayosema ni sawa au ndioo kichaa kinazidi kumchanganya.
‘Mimi sio kichaa nawaomba munielewe hivyo…jamani jamani mumefanya makosa makubwa, na kama mke wangu atadhurika, nitahakikisha nawachukulia hatu kubwa sana…’ akasema
‘Hahaha, wewe una mke , mke gani atakubali kuolewa na kichaa..hahahah’ wakasema wale walinzi
 Mara wakasikia kipaza sauti kikitangaza, kuwa `kama Maneno keshafika anatakiwa kufika wodi no 12 harak iwezekanavyo’
 Maneno aliposikia hivyo akajaribu kuinuka na kusema `mnasikia hili tangazo, ndio mimi Maneno naitwa huko wodini haraka iwezekanavyo, naomba mnifungulie jamani….’ akasema na wale walinzi wakamwangalia kama mwanzo na kuangua kicheko.
‘Eti wewe ndio maneno, na kweli wewe ni mtu wa maneno, lakini tatizo una upungufu wa akili, subiri docta akutibu kwanza…’ wakasema kwa kumzihaki. Na Maneno akazidi kuwasisitizia kuwa yeye sio kichaa, yule docta kamsingizia ilia pate kutoroka!
Tangazo lile lilirudiwa mara kwa mara, lakini Maneno hakupata nafasi hiyo, kwani hawo walinzi hawakumwamini kuwa anaitwa Maneno, na hata kama angekuwa anaitwa Maneno , wao wameambiwa na docta kuwa huyo ni kichaa anatakiwa kuwekwa chini ya ulinzi mpaka taarifa nyingine itakapokuja. Maneno akawaza  afanye mbinu gani za kuwafanya hawa watu wamkubali kuwa ndiyo yeye Maneno, akaona wao kama walinzi hawatamsaidia kitu ni bora aharakishe docta aje, yeye anaweza kumsaidia. Akaanza kuleta vurugu kuruka huku na kule, na kujibamiza chini.
‘Simnataka mimi niwe kichaa, sasa nakuwa kichaa kweli kweli…muiteni docta wenu au najimaliza mwenyewe…’ akasema huku anajirusha na kujibamiza ukutani.
‘Wewe kichaa utaumia, shauri lako…’akasema yule askari mmojawapo akionyesha wasiwasi, na askari mwingine akamshauri kuwa ni bora wakamuite docta aje haraka, ili amdunge sindani za vichaa, na hii mbinu ya Maneno ikafanya kazi, kwani wa wale walinzi akaondoka kwenda kumuita docta, walikuwa kila mmoja anataka aende yeye…lakini hatimaye mmoja akatoka mbio akisema anakwenda kumuita docta.

    
Huku kwa docta aliyeumizwa akawa kazindukana baada ya kupata matibabu, na alipoinuka cha kwanza ni kuuliza kuwa yule docta wa bandia kaenda wapi, wenzake wakabakia kumshangaa na kumuuliza ni yupi docta wa bandia , ikabidi awaelezee, jinsi ilivyokuwa. Na msako ukaanza, na pia aliomba kama kuna sindano imepatikana kule ndani, au dawa yoyote ikafanyiwe uchunguzi haraka iwezekanavyo.
Hivyo vitu vikafanyiwa kazi kwa haraka na bahati nzuri, sindano ikapatikana chini ya kitanda alichokuwa kalala Maua, ilipofanyiwa uchunguzi, iligunduka ni mchanganyiko wa madawa ya kulevya na madawa mengine, ambayo akidungwa mtu, unakuwa kama zezeta na na unaweza ukaamrishwa kufanya lolote  bila ya utashi wako au kujijua.
‘Yule docta mtaalamu wa Maua akashangaa dawa kama hiyo imetengenezwa wapi, nan i hatari kwa maisha ya mtu. Akawaza sana, lakini hakuwa na kumbukumbu yoyote kuwahi kuiona dawa kama ile kabla. Akatoa ombi kuwa vitu vile na vipimo hivyo vihifadhiwe kwa makini , kwani vitahitajika baadaye kwa uchunguzi na ushahidi vikihitaika. Akatoa taarifa kuwa Maua ahamishwe pale anapolala na kupelekwa sehemu nyingine ya usalama, ambapo atakuwa na ulinzi mkali uwekwe. Baadaye akakumbuka kitu na kuuliza;
‘Yule jamaa mnayesema ni kichaa yupo wapi…? akauliza
‘Yule kichaa…ooh, unajua huyo jamaa, tulijua kabisa ni kichaa, na ndiye aliyesababisha fujo za kuwaumiza , na yule wa uongo akawaambia walinzi wamkamate na kumweka chini ya ulizi kwani ni hatari, akaamrisha huyo jamaa apelekwe wodi ya vichaa kwani kachanganyikiwa, …’ akasema docta mmoja.
‘Ohh, nendeni mkamlete na ni vyema tukaliweka hili swala katika uchunguzi wa polisi, huenda wakatusaidia , vinginevyo tutaishia pabaya, kama hawa watu wameweza kuingia humu na kujifanya madocta, hamuoni tupo katika lawama kubwa…’ akasema yule docta. Huku akilini akiwaza jinsi ya kumpata Inspecta, kwani ndiye askarii anayemuamini sana kwa kazi hizi. Akawaambia wenzake atalifanyia kazi hilo swala mwenyewe la kuwaona polisi.
‘Alichukua simu yake na kumpigia Inspecta lakini alikuwa hapatikani, akapiga kituo cha usalama, ndipo akaakmbiwa Inspecta kapotea , haonekanii , lakini uchunguz bado unaendelea.
‘Kapotea mna maana gani , mkuu wenu apotee hivihivi, mbona mnatia aibu…’ akasema docta, na huko wakamjibu kuwa asiwe na wasiwasi wao wanajua nini wanachokifanya, wapo katika uchunguzi kama ana maagizo ayaseme kwani wapo watendaji wengine.
‘Watendaji wengine, kama hilo swala kubwa hivyo mumeshindwa kulishughulikia hili nikiwaambia mtanisaidiaje, naomba sana kama mkimpata mwambie Docta wake anamuhitaji hataka sana….’ Akasema na kukata simu.
 Aliangalia wenzake na kuuliza vipi huyo jamaa wanayesema ni kichaa keshaletwa, alipoambiwa bado , akatoka mwenyewe haraharaka kumfuata. Huku kichwani akisema lazima ampate huyo aliyemfanyia hivyo, kwani yeye amewahi kupitia uasikari, kazi hiyo anaweza akaifanya mwenyewe... Alipofika kule kwenye wodi ya vichaa aliwakuta wale walinzi wakibishana, kuwa nani aende kumfungua yule jamaa, kwani alionekana sasa nii hatari kwao.
‘Yupo wapi huyo mnayesema ni kichaa,…’ akauliza docta.
‘Yupo huku Docta, ungekuja na sindano kabisa maana hakamatiki, kapandisha ile ya hali ya juu, anaweza kukudhuru…’ akasema yule mlinzi huku akimfuatilia nyuma yule docta na kuwa kama anajificha nyuma ya huyo docta. Yule docta hakumsikiliza kabisa yule mlinzi akaelekea huko alipoelekezwa, kuwa ndipo alipo huyo jamaa, akashangaa chumba alichowekwa, ilikuwa tofautii na awapowekwa wengine…
‘Kwanini mumemuweka huku huyu jamaa, kwani ni mhalifu..?’ akauliza Docta.
‘Ni bora angekuwa mhalifu, hebu angalia alivyojifanya, anaruka juu anadondokea kichwa, yupo kama kima….oooh, docta tutauliwa hapa…’ akasema yule mlinzi, na aliishia kushangaa pale yule docta alipokwenda na kumuinua kichwa yule jamaa, kwani alijiinamia chini na alikuwa hawatazami.
‘Mimi sio kichaa, nyie walinzi…..’ akasema na lipoangalia na kukutana na macho ya docta akatabasamu na kusema; `Afadhali umekuja docta…hawa watu hawana akili, wamemuachia yule muuaji wanataka wananisingizia ukichaa…hawa hawafai kabisa kuwa walinzi…’ akasema huku akisubiri docta akimfungua kamba.
‘Docta unafanya nini, atakuumiza huyo jamaa, hebu sikia anavyoongea..’ akasema yule mlinzi.
‘Huyu sio kichaa, kichaa ni yule docta mwenye viatu vyekundu, mumemuachia, na sasa hosptali ipo hatarini, mtawajiba kwa hilo mpaka mumpate…mnasikia, nataka yule jamaa apatikane haraka. ..’ Akasema yule docta na kumshika Maneno mkono wakiondoka naye na kuwaacha walinzi mdomo wazi..
‘Docta nimeitwa wodi namba 12, ni muda mrefu sana wananiita, kuna jambo la muhimu sana…’ akasema Maneno.
‘Kwani wewe ndio unaitwa Maneno?’ akaluliza Docta.
‘Ndio mimi ni mume wa Maua…?’ akasema Maneno.
‘Kumbe ndio wewe, tumekuwa tukikutafuta tangu huyo Maua aletwe hapa, kwasababu kuwepo kwako ingesaidia sana kupona kwake, lakini tumegundua kuwa tatizo lake linatokna na madawa, na tulitaka kukuulizia maswali machache kuhusiana na hayo madawa!
‘Madawa, madawa gani hayo, mke wangu katika kitu akachokichukia ni madawa, akiumwa dawa nafanya kumshika kwa nguvu…’ akasema Maneno.Ni mimi: emu-three

6 comments :

samira said...

mambo mambo m3 hivi ni upinzani mkubwa na kwa nini yote hayo nasubiriiii

Goodman Manyanya Phiri said...

mmmh...mmmh..

...Lakini vyatu vyekundu na alievivaa bado wametoweka tu hospitalini hapahapa! Au yuko mitaani tayari na niyeye aliyemtorosha hata inspecta? Jambazi lina akili, aisee!

Swahili na Waswahili said...

Kweli dawa ya moto ni moto!pamoja ndugu!

SIMON KITURURU said...

SI utani dawa ya moto hiii!

Candy1 said...

Afadhali mambo kidoooogo yanaenda sawa na Maneno maana mmh...kwikwi kidogo ilitawala..bado hiyo DVD...na inspekta kapelekwa wapi...mi nipo kama kawa

Yasinta Ngonyani said...

Hakika dawa ya moto ni moto ...tupo tunafuatilia ndugu yangu...