Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, June 1, 2011

Dawa ya moto ni moto-17



Moto uliokuwa ukiwaka kwenye nyumba moja ulizusha gumzo kubwa, kwani watu wengi walikuwa wakiishuku hiyo nyumba kuwa ina mambo zaidi ya inavyoonekana, na wengine walisema huenda kuna mitambo ya kutengenezea video, ingawaje siku moja polisi walivamia lakini walipotoka hapo walisema hawakuon kitu. Kauli hii haikuaminiwa na wengi, wakijua jamaa anayemiliki nyumba hiyi ni tajiri sana ,lakini hakuna ambaye aliweza kuingia hapo tena na kuthibitisha kuwa kweli mitambo hiyo au mashine kama hiyo ipo au la.

Moto huo ulianza kidogo kidogo, na kwa vile hakukuwa na mtu aliyeruhusiwa kuingia humo, na ukuta uliozungushwa hapo ulikuwa mkubwa, moto huo uligundulika wakati umeshakuwa mkubwa. Mwanzo kulionekana moshi ukitanda hewani, watu wakzani ni mtu anachoma takataka, lakini kila saa ilivyokwenda ndivyo moshi ule ulivyokuwa mkubwa, na baadaye moto ukaonekana ukitanda hewani!
   Moto ulipozidi watu walishituka na kuanza kuhangaika, kwani ungeliweza kuvuka na kuvamia nyumba nyingine, na hapo ilionekana wazi kuwa nyumba nzima ilikuwa imetanda moto na kwa hali ilivyokuwa nyumba hiyo itakuwa imeshaanza kuteketea, …wenyewe walikuwa hawapo, na mara nyingi huwa wanatoka mapema na kurudi usiku, hata mlinzi siku hiyo hakuwepo. Baadhi ya wasamaria wema walipigia simu `fire’ kuomba  zima moto waje, lakini hata pale kikosi hicho kilipofika hakikuweza kuokoa lolote. Ungeingiaje kwenye nyumba hiyo, ilibidi wajaribu kutupa maji kwa mbali!
Baadaye wakati kumeshapoa,ilikuja pikipiki na kusimama karibu na geti, wakakutana na askari akawauliza wao ni nani, wakasema wao wanaishi humo ndani, akawaambia kumetokea moto, na inavyoonekana nyumba imeteketea kabisa, lakini ukuta na jinsi kulivyo hakuna aliyeweza kuingia ndani, ila moto umeshazimika, kwahiyo wafungue waangalia na ikibidi uchunguzi ufanyike nini chanzo cha moto. Yule mtu akafungua mlango wa geti na kuwaambia wale askari haina haja, alivyoona kila kitu kimeteketea, kama atawahitaji atawaita.
Basi wakaingia na pikipiki lao ndani, na baadaye wakatoka na kusimama pale mlangoni kwa muda, huku wakiongea.
‘Duh, balaa gani hili jamani, sasa tutamwambiaje bosi, maana hili halielezeki, na simu yake ndiyo hiyo haipatikani...’ akasema mmojawapo.
‘Hata mama nawaza bila kupata jibu, hebu tufunge hapa turudi mjibi, tutajua nini la kufanya hukohuko..’ akasema mwenzake
‘Lakini hii sio bure lazima kuna mtu kasababisha huu moto, na nitamgundua tu, ole wake…’ ilisikika sauti ya jamaa mmoja ambaye inaonekana kama anahusika zaidi humo ndani. Alikuwa akihangaika sana kuangalia huku na kule, aliwafuata polisi na kuongea nao, kuwa wao sio wahusika wakubwa, lakini mwenye jengo akifika ataonana nao, wale polisi wakaona wanapoteza muda wao wakaondoka!
‘Bosi hawezi kufanya lolote hapa, …akipata hii tarifa kutachimbika, lakini ina maana kila kitu kimeharibika hivihivi, hakuna jinsi nyingine ya kupata vitu vyetu, sasa itakuwaje ile tenda….’ Akasema mwenzake
‘Fuatilia ule mzigo, uupate haraka kwa hali yoyote ile, nasikia mteja wetu kalazwa hospitali, sasa wewe hakikisha unaingia ofisini na kukagua kil mahala, ukiupata ule mzigo tutaufanyia kazi, kumbuka wadau hata bosi asijue hili, sisi tuasema kila kitu tulikileta humo, na tulikuwa tukisubiri kukiweka vyema, sasa moto umeharibu kila kitu…na kama unavyoona mteja hajasema lolote, simu zote muhimu hazipatikani, hatuna jinsi, na tutatoa shinikizo gani kwake…, tutafanyaje…lazima hicho kilichopo kifanyie kazi, …’ akasema yule jamaa, akionekana kuchanganyikiwa!
‘Mimi nahisi moto huu unaweza ukahusiana na watu wa mteja wetu…nilikuwambia bosi umtumie na yule mwingine, sasa unaona hatuna akiba tena,…’ akasema mwenzake huku anapanda juu ya pikipiki
‘Inawezekana iwe au isiwe, tutafanya uchunguzi, lakini,vyovyote iwavyo wadau wasijue lolote…achana na hilo, hapa sio mahala pa kuongea lolote twende zetu’ wakasema na kuondoka lile eneo. Na wakati huo huo jamaa mmoja aliyekuwa nyuma yao akapiga simu na kuongea na mtu mwingine.
‘Taarifa muhimu, inasadikiwa athari bado ipo alfa-2, waundaji wapo mbioni kuitibua na hata kuikuza athari, ulinzi na ufuatiliaji ni muhimu….vyanzo vya athari vimeteketea ‘ akakata simu.
                                     *********
Maneno akafika maeneo ya hospitalini akiwa na haraka kujua nini kaitiwa, ingawaje alikuwa na nia ya kufika hapo kumuona mke wake, lakini huo muito alioitiwa ulimtia wasiwasi. Tangu mwanzo, nia yake kubwa ni kumuona mke wake. Hakujua maendeleo yake, ingawaje kule kituo cha polisi walimhakikishia kuwa mke wake hajambo, kachanganyikiwa tu kidogo…kwanini kachanganyikiwa, …akajiuliza bila kupata jibu.
Akiwa kafika hapo hospitalini akawa anawaza jinsi gani alivyoachiwa kwa dhamana, kwa kosa ambalo mpaka sasa hajalijua. Wanasema wamemshika kwa ajili ya uchunguzi, mbona yeye peke yake, …Alishukuru alipokuja yule jamaa ambaye alijitambusha kuwa anafanya kazi kwa mkwe wake, yeye ndiye alifanya taratibu zote hadi kuachiwa kwa dhamana. Na kwahiyo aliona ni vyema kwenda kuonana na mkwe wake kumshukuru …lakini alichelea sana je akifika kwa mkwe wake atamwambia ilikuwaje…akasita kwanza , lakini hata hivyo alijua lazima atakutana na mkwe wake, la muhimu ni kuonana na Maua kwanza kabla hajaonana na mkwe wake.
Aliporuhusiwa kuondoka kule mahabusu, alitamani apitie hospitalini moja kwa moja, lakini jinsi alivyokuwa kachafuka, akaona afike nyumbani kwanza ajimwagie maji. Na kwa vile pikipiki lake lilikuwa limehifadhiwa hapo hapo kituoni akaliomba na kukabidhiwa, alipoliwasha akalikuta linafanya kazi, akashukuru na kuodoka nalo. Akafika kwake na kukagua nyumba nzima, akakuta hakuna kilichopotea au kuibiwa, ila kumepekuliwa kila kona. Harakaharaka akajimwagia maji huku akiwa anajiangalia kwenye kiyoo, hakuamini kabisa kuwa ni yeye. Midevu ilikuwa imejaa kidevuni, na hata uso wake ulikunjamana kama mzee.
‘Yote haya sababu ya mawazo, nawaza kama nina familia kubwa, …nina kila kitu, lakini nina dhiki ya kukosa raha, sijui kwanini, …’ akajisema mwenyewe!
Alitamani anyoe yale madevu, na kujiweka katika hali yake ya kawaida,…lakini vifaa vya kujinyolea havikuonekana pale alipozoea kuviweka. Alishangaa jinsi nyumba ilivyo, alijua kabisa kuna mtu kapanguapangua, maana jinsi alivyokuwa kapanga vitu vyake, alikuta sivyo kabisa, sasa inakuwaje mpaka wachukue mashine yake ya kujinyolea…akashangaa sana. Kwa hali aliyo nayo aliona ni bora atoke apitie dukani akanunue mashine, hakupenda kabisa kunyolewa saluni.
Mawazo hayo yalimfanya afike hospitalini bila kujua,… na alipofika hapo hospitalini, akiwa na midevu yake ambayo alisindwa kuinyoa, kwani aliponunua ile mashine ya kujinyolea, na karudi nyumbani, lilitokea jambo lililomkatisha kufanya kazi hiyo! W
Wakati anajiandaa kunyoa alisikia simu yake ikiita, mwanzoni aliidharau, lakini ilivyoendelea kuita, akaweka ile mashine chini, na kuiendea simu yake, ambayo ilikuwa kwenye shati alilokuwa kalivaa alipofika hapo, akaipokea ile simu, bila kuangalia nani aliyepiga. Sauti kwenye simu ilijitambulisha kuwa ni mfanyakazi wa hospitali, na anaarifiwa kuwa kuna mgonjwa anamuhitaji haraka,…
‘Mgonjwa, mgonjwa gani huyo…?’ akauliza
‘Kwani wewe huna mgonjwa unayemfahamu aliyelazwa hapa hospitalini, wewe fika utamjua ni nani,…kasema ni muhimu sana’ simu ikakatika.
Maneno akachukua taulo na kujifuta ile sabuni aliyokuwa kapaka kidevuni tayari kwa kujinyoa, alikuwa hajaanza kupitisha mashine, alichofanya ni kuchukua kitana kidgo na kuziweka safi zile ndevu , halafu akavaa moja ya nguo zake haraka akatoka nje na kuhakikisha amefunga vyema nyumba!. Akilini alijua kabisa ni mke wake, akalirukia pikipiki lake ambalo amelizoea sana! Hakujua nyuma yake kuna pikipiki kama nayo inaelekea hukohuko.
Alipofika pale hospitalini, kabla hajaiweka pikipiki yake vyema, mara ikaingia pikipiki kama yak wake na kupitiliza hadi sehemu ya mbale, na mwendeshaji akateremka kwenye pikipiki yake na kuchukua mkoba aliokuwa kauweka kiti cha nyuma. Aliingia mlango wa jengo la hospitali. Maneno akawaza, mbona ile pikipiki inafanana na ya kwake ambayo aliona siku za nyuma, akaingiwa na shaka na kujiuliza huyu mtu ni nani, akaanza kumfuatilia kwa nyuma.
 Maneno akamfuatilia kwa nyuma na alihakikisha hamtoki machoni, na kusahau kuwa aliitwa kumuona mgonjwa aliyemuhitaji, na alitakiwa kupitia mapokezi ili aulizie huyo mgonjwa ni nani, lakini mawazo yake yalikuwa kwa huyo mtu,ambaye naye hakupitia mapokezi, alipita moja kwa moja kuelekea wodi za wagonjwa waliolazwa…..Alikuwa na uhakika kabisa sio yule jamaa aliyemuona ile siku, ni tofauti kabisa!
Alimuona yule mtu akiingia moja ya wodi, naye akajitahidi mpaka akaingia mle ndani, …yule mtu akaingia chumba kimojawapo, Maneno akasubiri, kwenye kile chumba mara akatoka dakitari akiwa kavaa mavazi ya kidakitari. Maneno akasubiri kumuona yule mtu aliyeingia,na hapa aliingiwa na shaka, kama yule kaingia humo halafu katoka dakitari , basi huyo jamaa ni dakitari pia, lakini akashituka kidogo na kukumbuka kitu. Akamfuatilia yule mtu na kugundua kavaa viatu vyekundu, oooh, ndiyo yule jamaa, kabadili na kuvaa mavazi ya kidakitari, simuachi huyu mapama nione mwisho wake, akasema huku anafuatilia nyuma.
Maneno akamfuatilia kwa nyuma, yule jamaa ambaye sasa ni dakitari mwenye viatu vyekundu akaingia chumba cha wagonjwa wa uangalizi wa karibu, lakini sio mahututi, ila wanahitaji kuchunguzwa kwa makini, au kulindwa, na hapo Maneno akakumbuka kuwa mke wake inasemekana kachanganyikiwa, kwahiyo huenda yupo kwenye wodi hiyo, na huko ndio jamaa huyu anaelekea…akajiuliza akilini sasa afanyeje, alikuwa akiwaza hili huku anamfuatilia huyo jamaa ambaye alionekana kama dakitari, hana wasiwasi.
Maneno naye akaingia na kumuona yule jamaa akifungua chumba kimojawapo mle ndani, maana ile wodi ina vyumba ndani kwa ndani, nafikiri ni kwa aili ya kuweza kuwahudumia wagonjwa wao kwa makini na uangalizi. Hapo Maneno akashindwa ataingiaje mle, akawaza  sana, baadaye akaamua kuingia  hivyohivyo na kusimama mlangoni wa kile chumba akasikiliza kwa ndani. Alisikia mtu akiongea, lakini hakusikia kujibiwa. Akausukuma mlango taratibu, na alipopata upenyo, akachungulia kwa ndani, akamuona yule jamaa akiwa kasimama, pembeni mwa kitanda, na alionekana kama anatoa  kitu mfukoni, kilikuwa chupa na sindani.
`Huyu anaweza akawa dakitari kweli, lakini kwanini hivyo vifaa viwekwe mfukoni, ninavyojua vifaa kama hivyo huwekwa kwenye kibeseni …’ akawa anawaza, na wakati anawaza akasikia sauti iliyomshitua
‘Unasikia wewe dada, unajifanya bubu sio, …hii dawa hapa dawa, ni kikupiga hii dawa kwa sindano, ikiingia mwilini tu, kwanza utasikia maumivu makali halafu mwili `utaparalize’ itafanya mwili wako upooze kabisa, na hutaweza kutembea milele, utakuwa mfu aliye hai…ninachokuomba ni kuniambia ule mkanda tuliokutumia upo wapi, hilo tu…pesa umeikwamisha mpaka sasa, hilo halina maana kwa sasa ila ile DVD, ipo wapi…?” akasema yule mtu akimsogelea yule mwanamke aliyelala pale kitandani.
Mahali aliposimama Maneno hakuuweza kuona nani kalala pale kitandani, lakini Maneno akahisi huenda ni mkewe, na hayo maneno aliyosikia yakamtia kiwewe, kwanza DVD YA ya nini, ina muhimu gani kiasi hicho, halafu….akasema lazima amuwahi yule mtu kabla hajafanya lolote, akasogea karibu na mlango na kuusukuma pole pole, na wakati huo yule jamaa alikuwa akimalizia kuiweka ile dawa kwenye sindano, halafu akaiweka hewani kuiweka sawa na sehemu ya dawa ikamwagika kutoka kwenye ile sindani kama wafanyavyo madakitari. Maneno akasogea karibu na mlango na kuusukuma polepole na mara akasikia sauti kwa nyuma……


Ni mimi: emu-three

6 comments :

samira said...

sasa kazi kwelikweli mauwa una mtihani dada

Faith S Hilary said...

Mmmh Maneno jamani si angeendelea kumtafuta mkewe tu naona kawa mdadisi sana! Mi nipo kama kawa

emuthree said...

Tuendelee kuwa pamoja, nasikitika leo kuwa nimeshindwa kuendeleza sehemu inayofuata, tatizo lile lile la umeme, na majukumu mazito ya ofisini, lakini msijali,nikipata nafasi kidogo nitaweka vitu, kama kawa, msicheze mbali kwani sasa sehemu inayokuja ni bab kubwa, kwani ndio pale kiini cha hiki kisa kinaingia!
Kuna mpelelezi anafanya vitu vyake kwa kazi, yupo mzee mkwe wa bosi, naye ana kikosi chake cha upelelezi, yupo baba yake Maua, naye anacho...kwanini viwepo vyote hivyo, kuna nini kizito kinatafutwa. Pia wahalafu wanacho cha kwao,na wao wamegawanyika sehemu mbili...tuwepo tuone, naomba tukumbushane nikisahau kipengele mahala!
TUWE PAMOJA

Anonymous said...

Mmmmh!!! mie moyo unanienda mbio kwa woga. Maneno nae si apige simu polisi? kwavile, ndio stori hiyo lazima iwe na changamoto. Maneno udadisi wake utamponza.
Lete vitu boss wangu, mambo mazuri. Tupo pamoja.

BN

samira said...

m3 leo umenipa headline ya maana sana ni kweli wewe hodari hivi kinatafutwa nini pande zote za family na watu binafsi wanataka nini kuna siri gani zaidi
tupo pamoja
thanks m3

Simon Kitururu said...

Mmmh!