Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, May 27, 2011

Dawa ya moto ni moto-15Inspecta Tuzo alikuwa akiwa kwenye ofisi yake ambayo alikabidhiwa aliporudi toka masomoni, alichukua moja ya faili lililokuwa mbele yake na kutabasamu, akikimbuka miaka miwili nyuma alivyokuwa akinyanyasika, kila alipofanya kazi yake lijikuta akiishia patupu, anamkamta mtuhumiwa siku ya pili anaachiwa eti kwasababu ni mtoto wa mkubwa na hakuna ushahidi. Akaahidi kuwa atafanya bidii hadi afikie cheo ambacho atakuwa na maamuzi ya watuhumiwa. Na kweli akapata bahati ya kusoma na na alipohitimu akapewa cheo alichokuwa akikiota.
Aliliinua lile faili tena na kuliangalia juu, limeandikwa nini, lilikuwa faili aliloliacha miaka miwili iliyopita la kazi maalumu, kazi ambayo alihangaikia mwishowe akaishia kuwakamata watu na baadaye wakaachiwa eti hakuna ushahidi, …leo karudi lazima atafute huo ushahidi kwani watu wale wale bado wapo nab ado wanaendelea na uhalifu wao, aliapiza kuwa hatamaliza mwaka, atakuwa kawaweka ndani na kama atashindwa tena mwaka huu inabidi hilo faili lifungwe, na kwake itamshushia hadhi kwani alishawahi kugombana na mkuu wake kwa kutoa kilichoitwa shutuma kwa watu hawo ambao wanaitwa wakubwa! Alijaribu kipindi cha n Yuma kukusanya ushahidi kuwa huenda wanahusika na genge liloluzuka likiwa na malengo ya kuwachafulia baadhi ya watu majina yao kwa kuwadhalilisha kwenye magazeti na mitandao, na pia kuuza kanda zilizopigwa marufuku!
 Aliwahi kuwafuatilia baadhi ya watu aliowashuku lakini ushahidi alioutoa ukapotezwa kiaina, na tangu siku hiyo akawa hawaamini tena wakubwa zake. Sasa karudi na kupewa rungu, na moa ya kazi yake ni kulisafisha jina la kituop chao, na hapo akapewa kazi maalumu ya kupambana na genge haramu lililozuka ambalo limefikia hatua kutishia amani…anatakiwa kutafuta ushahid wa kulimazliza hilo genge, nani yupo nyuma ya hilo genge na linapata wapi ufadhili. Yeye mwenyewe anajua kweli genge hilo lipo, na alishawahi kuliingilia na kugundua uhusika wa genge hilo na uuzaji wa madawa ya kulevya, lakini hakuwahi kupata ushahidi ambao ungeweza kuwasimamisha mahakamani, na alioupata ukapotezwa!
‘Haya mambo ya kisheria bwana, mtu unamshika moja kwa moja …lakini eti hakuna ushahidi wa kisheria…ninaahidi sasa wakati umefika, tutapambana ama zangu, ama zao, lazima mhusika nitamweka mkononi mwa sheria, hata kama wanajifanya kuwa wanawanasheria wa kuwalinda, …ukweli utadhihiri mahakamani!
 Ili kufanikisha lengo lake akawatafuta vijana wake aliowaamini, katika kazi hii, vijana waaminifu, akawapa shule na jinsi gani ya kuweza kuwanasa wahusika amabaop ni wajanja na wana uzoefu wa kazi zao.
‘Angalieni sana, wahusika hawa inawezekana wakawa ni watoto wa wakubwa, au wakubwa wenyewe na wanalindwa sana, cha muhimu ni kuhakikisha tunakusanya ushahidi ambao hautaweza kukwepeka, hivi sasa kuna kundi limeanzishwa na wahusika ni wale wale, kundi hili limezua biashara ya kanda za ngono, kanda za kuwazalilisha watu…cha muhimu ni kugundua hiyo mitambo yao ya kutengeneza hizo kanda ipo wapi. Humo humo wanauza madawa ya kulevya, wana silaha kali, majambazi wa hali ya juu, ambao wameweza hata kuibia benki. Mtandao wao ni mkubwa una mikono ya watu mashuhuri….sasa msifanye pupa, kitu cha muhimu ni kuwafutailia bila hata wao kujua.
‘Wewe Dimo, ni mtaalamu wa mitandao, na simu, tumekupeleka kufanyakazi kwenye kampuni hiyo ya simu, ili iwe rahisi kwako kuweza kuwanasa hawa watu, kwani wamekuwa wakitumia njia ya mawasiliano kufaniskisha malengo yao, wanabadili namba nk, lakini kwa utaalamu wako utaweza kuwagundua hata kwa sauati…kazi kwako, fanya kazi yako vyema, nina fununu kuwa kuna jambo linatendwa na limeshaathiri watu, na …nina uhakika ni kundi lile lile lilozua balaa la mitandao ya kashifa, ni kundi lile lile lilokuwa likiuza madawa ya kulevya, ni kundi lile lile lilokuwa likitumia simu kuwatapeli watu…wanajibadili kama kinyonga…’
 `Kazi kwasasa, haihitaji presha kubwa, pole pole kwanza, twahitaji uangalifu wa hali ya juu, kwani kundi hili lipo kama Mafia, wakikugundua kuwa unawafuatilia, watatumia mbinu kukuondoa dunia, bila kubakiza ushahidi wa wao kukamatwa, hawachelewi kumuondoa mtu duniani. Kuweni waangalifu sana…’ akamaliza maelezo yake na kuwapa kazi hiyo vijana wake…
 Inspekta Tuzo akaangalia saa yake na ya ukutani, akawaza hivi kijana wake aliyekuwa akimfuatilia mtu wa pikipikii mbona hajampa taarifa yoyote, akainua simu na kumpigia
‘Bosi kuna kitu nilikuwa nakifuatilia kabla sijakupigia, kwani ile sehemu alpha-2, kumetokea jambo, na huenda mpanda pikipiki akawa kaacha athari, kwani aliondoka muda kabla athari hiyo haijaenea, nina wasiwasi huenda hiyo athari bado imo kwenye hiyo nukta…
‘Ipo athari ya damu, au ya kiakili tu…’ akauliza Tuzo.
‘Ipo ya damu, na huenda ikavuka mpaka…nipe dakika kumi tutawasiliana’, simu ikakatwa.
‘Ipo athari ya damu…?’ akayarudia yale maneno, halafu akashika kichwa, `Ndio yale yale niliyowambia wakubwa zangu miaka miwili iliyopita, kuwa haya maswala yatavuka mpaka, na huenda yakazua mauaji…sasa ndio hilo, …’ akakuna kichwa na mara akakumbuka kitu, akainua simu na kupiga namba. Simu ile iliita mpaka ikakatika, akaguna , hii sio kawaida akapiga tena, ikawa vile vile. Akachukua kofia yake na kutoka nje, na alipokuwa analiendea pikipiki lake akasikia simu ikiita.
‘Vipi kuna lolote kubwa..?’ akauliza
‘Ndio tena kubwa lao, sasa hivi kuna watu watatu wametolewa pointo alpha-2, uhakika wa kifo bado, ila mmoja wao yupo katika hali mbaya. Wapo wanawake wawili na mwanaume mmoja, na nahisi ni athari inafanya vitu vyake.
‘Umesema wanawake wawili…unaweza kuniapa sifa zao, au unawafahamu vyema ni akina nani’ akauliza Tuzo.
Akasikiliza kwa makini toka kwa mmoja wa kijana wake, na aliposikia sifa ya mwanamke mmojawapo, akatikisa kichwa na kulirukia pikipiki lake na kuingia barabarani.
                                  ********
 Maneno hakujua kabisa kwanini akamatwe na kuwekwa chini ya ulinzi, aliwauliza askari waliomkamata kuwa yeye ana kosa gani, na kwanini akamatwe, askari wakamwambia ni sehemu ya kazi zao, lazima awekwe chini ya ulinzi kwasababu yeye alikuwa kwenye tukio na wengine wote wapo kwenye hali mbaya, wameumizwa, na hawawezi kuelezea chochote, inawezekana yeye ndiye kawazuru hawo watu, kwahiyo kiutaratibu atazuiwa kituoni kwa kuhojiwa kama hana kosa ataachiwa.
‘Kama sina kosa nitaachiwa…nimeshateseka huko gerezani baadaye mnaniachia ..haki gani hiyo, mimi nimewaambia kama isingekuwa mimi, mke wangu angekuwa mfu,…yule mwanamke ndiye muuaji mwekewni ndani…’ akasema Maneno.
‘Huyo mwanamke yupo chini ya ulinzi, yupo hospitali, hatuwezi kumakamata wakati hali yake sio nzuri…’ akasema polisi.
‘Najua kabisa huyo inawezekana ni mtoto wa bosi, mtajifanya anaumwa ili asiwekwe ndani, sisi walalahoi ndio wa kuteseka, naomba sana  mumuangalie mke wangu anaumwa…na naomba nijue hali yake…’ akalalamika Maneno.
‘Usijali utajua hali yake muda ukifika…’akaambiwa, na kufungiwa kwenye chumba cha kituo hicho, alikuwa peke yake siku hiyo!
                                            **********
Inspekta Tuzo aliendesha pikipiki lake hadi hospitali aliyoelekezwa, na alipofika hapo akaongea na askari wa zamu ambaye alikuwa akiwalinda majeruhi waliolazwa humo. Na akaelekezwa kule alipolazwa mwanake mmojawapo ambaye alitaka aonane naye, akaingia ndani na kumkuta huyo mgonjwa akiwa kalala. Taratibu akakisogelea kile kitanda na kumwanagalia yule mwanamke!
Yule mwanamke ghafla akashituka ba kufunua macho, na alipomuona Tuzo akainuka haraka na kusema `kaka aheri umekuja, maana hawa askari wananihoji utafikiri nimeua, labda kafa, lakini akifa ni kosa lake, sitajutia kabisa, ila nimewaambia siongei chochote mpaka wakili wetu afike.
‘Kwani uliona nini cha kukufanya uchukua hatua hiyo…huoni kuwa umajitakia tatizo ambalo litakusumbua na hata ku…ok, hebu niambia ilikuwaje,..’akauliza Tuzo. Na akasikiliza yale maelezo hadi mwisho, …akafikiri kidogo halafu akainuka na kusimama, akasema, `no bora uonane na wakili wetu, kama litatokea baya, basi ajue nini la kufanya, hata hivyo, umejeruhi, na kueruhi huko ni kosa,…ngoja nimpigie wakili wa familia aje muonane naye, mimi sitakiwi kuhusika….unanielewa lakini..’ akasema Tuzo, na kuondoka.
Tuzo alikiendea chumba kingine akasogea kitanda alicholazwa mwanamke ambaye naye alifikishwa akiwa kazirai na haijulikani ni kwa tatizo gani, kwani yeye hakupatikana na jeraha lolote. Tuzo akasogelea kile kitanda na kumwangalia yule mwanadada kwa karibu,alikuwa kakaa pembeni mwa kitanda akiwa kainama huku ameshika kichwa…Tuzo akamsogelea, na kabla hajafika karibu yake ,yule mwanamke akainua kichwa na kumwangalia Tuzo. Tuzo kimoyomoyo akasema huyu mwanamke kajliwa uzuri, ni nani huyu..?

‘Hali yako dada, mimi ni askari mpelelezi, nilikuwa nataka kukuhoji kidogo kama hutojali. ..’ akasema na kuja kukaa karibu na kitanda, akasubiri kusikia lolote kwa yule mwanamke lakini yule mwanamke alikuwa kimya akimwangalia tu. Akauliza tena na tena, lakini hakupata jibu, wala hakuweza kusikia sauti yoyote kutoka kwa yule mwanamke! Mwanzoni Tuzo alidhania huenda yule mwanamke anafanya hivyo kama alivyofanya yule mwanamke wa mwanzo kuwa ataongea pale wakili wake atakapokuwepo, lakini baadaye alipokuja dakitari akagundua ni tatizo.
‘Huyo mwanamke kapata mshituko mkubwa ambao umemuathiri, na tangu aletwe hapa hajaweza kuongea hata neno moja…ni atahri za mshituko, sasa bado tunajaribu kumchunguza zaidi kuwa ni kwanini na kwanini athari hiyo imfanye ashindwe hata kuongea..’ akasema dakitari.
‘Sio kwamba anafanya makusudi?...’ akauliza Tuzo, na kabla docta hajamwambia kitu akaongezea kuuliza `Hana ndugu au jamaa..?’ akauliza tenaTuzo.
‘Tangu alatwe hapa hajatokea jamaa yake yeyote, na tulizani labda ni kwasababu ya usalama, huenda askari wamewazua, lakini nilipowauliza askari wamesema hajatokea jamaa yake hata mmoja, huenda hawajajua, na kwakuwa haongei tunashindwa kuwasilina na jamaa zake.
‘Na nimesikia kuwa kuna mwanaume ambaye naye kaletwa hapa, yupo wapi na hali yake ikoje?; akauliza Tuzo.
‘Huyo hali yake sio nzuri, yupo `ICU’ huwezi kumuona, ana jeraha kubwa kichwani, bado anafanyiwa uchunguzi, haijaulikana kama kuna athari ndani ya kichwa au la…kwa ujumla hali yake ni mbaya….

Ni mimi: emu-three

4 comments :

samira said...

mambo jamani sasa itakuwaje na kaka ndo mpelelezi kwa upande wa pili nahisi baba wa mauwa ameingia mitini kwa sababu zake , may be not
m3 thanks u mambo mazuri

SIMON KITURURU said...

Ee Bwana !Ngojea tusubirie tuone itakuwaje!

Candy1 said...

mmmh...kwa kweli balaa!!! bibie hataki kusikiliza mashtaka japo kaharibu na bado hajui kwamba ame "overreact"...tuone Maua na Bosi watakuwaje....nipo kama kawa

Teuvo Vehkalahti said...

Greetings from Finland. Thus, through a blog is a great get to know other countries and their people, nature and culture. Come take a look Teuvo images and blog to tell all your friends that your country flag will stand up to my collection of flag higher. Sincerely, Teuvo Vehkalahti Finland