Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, May 24, 2011

Dawa ya moto ni moto-13



Bosi aliingia ofisini akijua Maua yumo humo ndani, akiwa na hasira kuwa Maua ana mbinu za kutaka kumharibia ndoa yake na maisha yake, kwa kumpigia simu ambayo kama angeipokea mke wake angekuwa matatani. Akajiuliza akilini kwanini Maua afanye hivyo, akasema kwa sauti; `ngoja nisiandike kwa mate wakati wino upo, tutapambana humu ndani, atanitambua kuwa mimi ni nani. Kabla hajakizungusha kitasa, mara  mlango ukafunguluwa kwa kasi na jamaa mmoja akiwa kavaa miwani meusi akatokeza na kumgonga Bosi, ambaye kwa vile hakutarajia hilo akajikuta anapepesuka karibu adondoke.
‘Wewe vipi, mbona…’ kabla hajasema kitu jamaa yule akamshika mkono kwa kumzua asidondoke, na kusema `samahani mzee, nilikuwa sijui upo mlangoni, na nilikuwa na haraka kidogo….,’ akasema huku anaondoka.
 Bosi akajiuliza akilini mbona hakumbuki kumuona mfanyakazi kama huyu, na amefuata nini humu ofisini, na kwa vile kavaa mawani meusi hakuweza kabisa kumgundua kuwa ni nani, akataka kumuita amuulize, lakini akazarau akijua kuwa kama katokea humu ndani ofisini,  Maua atakuwa anamfahamu. ‘Nitamuulizia Maua …kuhusu huyu jamaa, asije akwa ndio mshirika mwenza wa kunihujumu…hawaniwezi kama ndio hivyo..’, akaingia ndani na kufunga mlango, huku akisikia sauti ya pikipiki ikiondoka huko nje.
 Alifulululiza moja kwa moja hadi ofisinii kwake akaweka briefcase yake mezani. Akakaa kweny kocho, akashika kichwa kufikiri, halafu akainuka kuiendea simu ya mezani, akiwa na nia ya kumpigia Maua aje ofisini kwake. Akawaza, kuwa Maua yupo ofisni kwake, sijui anafanya nini, akatizama mlango wake ambao ulikuwa umefungwa nusu, na alikuwa akiona mlango wa ofisi ya Maua, kwani ofisi ya Maua imetizamana na ofisi yake, akaona ni heri amuendee huko huko ofisini kwake, kuliko kipiga simu. Akainuka na kuelekea ofisini kwa Maua,…mara akasikia kama mtu kafungua mlango wa nje na kufungwa, akajiuliza ina maana yule jamaa karudi tena, au Maua katoka nje kumkimbia. Akaacha kufungua mlango wa Maua na kuelekea ofisi wanapokaa wafanyakazi wengi, akaangalia huku na kule, lakini hakuona kitu.
‘Nina uhakika kuna mtu kaingia…sasa kaenda wapi,…akazunguka huku na kule lakini hakuona kitu, akarudi pale alipotoka na kuuelekea mlango wa ofisi ya Maua na kuufungua…
Taratibu akafungua mlango wa ofisi ya Maua na kabla hajasema kitu alijikuta akibakia mdomo wazi, akaduwaa mlango, akasita kidogo huku akihakikisha kuwa kweli macho yake yanaona kweli, anachokiona, kwanza akashikwa na butwaa, akageuza kichwa kuangalia ofisi ya wafanyakazi wengi, halafu kwa haraka akaufungua ule mlango wa Maua kwa mapana, na kukimbilia ndani.
‘Maua vipi, wewe Maua una nini…’ Maua alikuwa kimya.  Maua alikuwa kalala sakafuni,na jinsi alivyo alionyesha kabisa yupo katika hali mbaya. Bosi akaanza kuingiwa na wasiwasi, alichofanya ni kushika shingoni mahala mapigo ya moyo yanaposikika…alitulia kidogo na kusikiliza mapigo ya moyo na kwa mbali akasikia mapigo hayo kwa mbali akugundua kuwa Maua kazima,…akainua mkono wake na kuweka vidole viwili sehemu inaposikika mapigo ya moyo, alihisi  mapigo ya moyo yalikuwa kwa mbali…,  
  Alipohakikisha kuwa Maua yupo hai akamkagua kuwa ana majeraha sehemu yoyote ya mwili, akakuta hana hata mchubuko mmoja,…na alipoangalia karibu na mkono wake kulikuwa na DVD, ya rangi, ambayo ilikuwa na picha…akajikuta moyo wake ukipasuka alipoziona zile picha …akashikwa na butwaa…akaikagua haraharaka, akahema na harakaharaka akaitumbukiza kwenye kikasha chake na kufutika ndani ya droo za meza ya Maua akahakiksiha imeifunga ile droo vyema,akaona huo sio muda wa kuitizama. Akamuendea Maua, na mawazo yake ya haraka akawa anamuwaza yule jamaa aliyetoka ndiye msababishi wa haya yote, ni nani huyu? Au walishindwa kuelewana, kukatokea mapigano, na huyo jamaa alipoona kaua akakimbia…au atakuwa nani yule?
Haraka haraka, akataka kupiga simu kuwaambia getini wamzuie huyo mtu, lakini kwa muda kama ule huyo jamaa alijua kama kaondoka na pikipiki sio rahisi kumpata tena. Akageuka kuangalia pale simu inapokaa, akakuta haipo, akatizama kule na kule akaiona simu imedondoka chini ya meza..
Akaona akiendelea kuitafuta itampotezea muda akachukua simu yake ya mkononi akapiga namba ya getini na kuwauliza walinzi huyo mtu aliyetoka na pikipiki wanamjua na ameshakwenda mbali. Akaambiwa keshaondoka, na atakuwa kaenda mbali kwasababu kaondoka na pikipiki, wao walinzi walijitetea kuwa walijiua labda Maua anamfahamu, kwani waliingia pamoja.
`Kwani kuna tatizo bosi…’Akauliza mlinzi
‘Hapana, kama kuna tatizo nitakupigia, lakini kama huyo jamaa atarudi niarifu mapema..msimruhusu akaondoka…’akasema Bosi. Na mlinzi alikuwa anataka kusema kitu, lakini Bosi akakata simu kabla hajasikia nini mlinzi alikuwa akisema, aliona hana muda wa kumsikiliza tena, anatakiwa kuona hali ya Maua kama ni lazima amkimbize hospitalini.
Akamsogelea Maua na kujaribu kumuinua na kumweka vizuri, akaona hiyo haifai, akambeba kishida hadi ofisini kwake ambapo angeweza kumlaza kwenye kochi kubwa. Akambeba kwa shida hadi ofisini kwake, akamlaza vizuri na kumlegeza vifungo vya shati, halafu akatafakari, amfanyeje ili azinduke, akaona kuna njia mbili, kutumia mikono kwa kumbinya kifuani au kutumia mdomo. Akahema akamsogelea Maua na akaona atumie mdomo.
 Mke wa bosi alipita pale getini wakati  mume wake keshaingia ndani na alifanya hivyo baada ya kuwaona wale walinzi wakiongea kwa ndani wakati geti wameliacha wazi. Alipanga kuwa wakimuuliza atajua nini cha kuwaibu, lakini alishangaa hawakumuuliza lolote wakati anaingia ndani, wao walikuwa wakibishana mambo yao. Akasogea kuelekea ndani na alipoliona gari jingine limo mle ndani mbali ya gari la mke wake akajua hilo linawezekana kuwa ni gari la Maua. Akawa na hamu sana ya kukutana na huyo mwanamke anayemzuzua mume wake, yeye alimuita Malaya wa mume wake.
 Akilini mwake alijenga hisia kuwa atawakuta katika hali ambayo itadhihirisha hisia zake, kuwa kweli ni wasaliti wa ndoa zao..akawapa muda, halafu akamua kuingia ndani. Alishangaa walizi wale hawakuwa na habari naye, na huenda hawakumuona, akajiuliza akilini, walinzi hawa wanalinda nini sasa. Akakumbuka ile pikipiki iliyotoka kwa mwendo kasi karibu imgonge wakati anapita pale getini, …akasonya, ‘ole wake ningemjua ni nani, kazi ingeota mbawa…’ akasema kwa sauti…Akasogea hadi mlango wa ofisi akazuga kidogo kupoteza muda halafu taratibu akafungua malango na kuingia ndani, akaufungwa kwa taratibu.
 Kwanza alikimbilia chooni, akajiweka sawa, na kusubiri kidogo, akasikia sauti ya mtu akija kuelekea chooni au alikuwa akitembea humo ofisni. Mke wa bosi hakutaka kabisa ajulikane yumo humo ndani, kwahiyo alijikausha na kukaa kimya akiomba huyo mtu asije akafungua mlango wa chooni, na kugundua kuwa kuna mtu ndani. Baadaye alisikia sauti ya huyo mti ikiondoka,…`hizo sio sauti ya nyayo za mume wangu…atakuwa ni yeye…’ akasema moyoni. Akasubiri kama nusu saa, akahakikisha kuwa kama ni wapenzi watakuwa wamshajisahau … akafungua mlango wa chooni na kutembea kuelekea ofisi ya mume wake.

 Alipofika akaona mlango wa ofisi inayotazamana na ya mume wake ambayo anaijua kuwa ni ya huyo Maua ipo wazi , hakutaka kuitizama vyema hiyo ofisi ya Maua, mawazo yake yalikuwa kwenda moja kwa moja kwenye ofisi ya mume wake, na kwa vile huyo Maua hayupo ofisni kwake basi atakuwa ofisini kwa mume wake. Leo nitawafuma moja kwa moja, akatizama huku na kule kama atapata silaha ya kuwaadhibu, lakini hakuona kitu cha maana. Akasogea kwenye ule mlango ambao ulikuwa haukufungwa vyema,ina maana wanajiamini kiasi hicho hata mlango hausimikwi…sawa, tutaona, taratibu akausukuma, ili kupata ushahidi…taratibu, na bahati nzuri mlango hautois sauti…taratibu akausukuma.
Mke wa bosi alijikuta akishikwa na butwaa, shinikizo la damu likaongezeka, akasisimuka na mwili, akaanza kutetemeka, na kama sio ujasiri alio nao angedondoka chini hata kuzimia, alichofanya ni kuchukua simu yake yenye kamera na video akaanza kuchukua lile tukio, hakuamini kuwa mume wake kweli ndivyo alivyo, ina maana ile kauli yake aliyomtamkia muda mfupi uliopita ilikuwa ya uwongo, ‘eti anampenda…’ alishalainika na kauli ile, na kuanza kumwamini mume wake, lakini alichikiona wakati ule kilimtoa imani kabisa na kumchukia mume wake kama nini sijui.
Kitu kilichomshangaza ni hali ya yule mwanamke, mbona kalala, halafu katulia kimya, na mikono imelegea pembeni..mume wake ndiye anashusha mdomo na kukutunisha na wa huyo mwanamke….akajiuliza mke wa bosi, akasema moyoni, keshalegezwa na mahaba yao haramu, ngoja niwaonyeshe kuwa mimi ni mwanamke wa shoka, ngoja nikatafute silaha, nitahakikisha anatoka maiti humo ndani, akakimbilia stoo, ambapo alijua kabisa kuna panga, au nyundo na kweli akapata chuma cha haja, akarudi kule mbiombio, na kuusukuma mlango kwa nguvu, hakujali tena, alichofanya ni kuinua kile chuma kikatua kwenye kichwa cha mumewe…..
Oh, naona leo niishie hapa, tuonane sehemu ijayo


Ni mimi: emu-three

4 comments :

samira said...

jamani kashauwa ona sasa hasira za mkizi
m3 mambo yanazidi kunoga haya nasubiri nione itakuwaje
tupo pamoja mtu wangu

Nancy M said...

Duh!!

Faith S Hilary said...

Kha!! Sasa na mihasira yake kafanya kitu hata hajui ni nini yeye akili zake zilivyomtuma ndio hivyo hivyo...mmmh...mke wa bosi kiboko jamani I hope asimdhuru Maua maana kama ndio mumewe keshammaliza..

Anonymous said...

M3 tupo pamoja usicheleweshe muendelezo wake kisa kinazidi kuwa kitamu ona sasa hasira hasara haya tunasubiri tuone itakuwaje