Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, May 19, 2011

Dawa ya moto ni moto-11



 Bosi alikuwa kachanganyikiwa, akitafuta mbinu za kumnyang’anya mkewe ile simu kabla haijaipiga ile namba iliyoita,…na wakati anawaza nini fanye mkewe alikuwa mwepesi alikuwa keshaipiga ile simu, na akawa kaiweka sikioni kwa muda, halafu akaitoa haraka sikioni na kuiangalia…akaiangalia ile namba halafu akaipiga tena, …wakati anasikiliza sikioni akawa anamwangalia mumewe machoni. Na hapo Bosi akaanza kuhisi woga, aliua kwa muda ule alikuwa akisikilza yle maneno.
‘Unajua watu kama nyie mnanitia nyongo na kutamani kufanya ubaya ubaya…unafikiri mtanishinda ujanja sio, nina uhakika hii ndio namba uliyopigiwa mara ya mwisho,na huyo hawara wako aitwaye Maua, na kwa historia inaonyesha ni mtu mnayewasiliana naye sana, …’ akaiweka ile simu mezani na kumwangalia Bosi
Bosi alishuru sana kusikia kuwa namba haikupatikana, ….na hili litampa muda wa kukutana na Maua kabla hajapiga tena, akatamani aichukue ile simu ampigie Maua ajue ni kwanini kampigia simu na kuweka maneno kama yale, huyu mwanamke kumbe ni mtu wa hatari, mmmh hanijui mimi, ngoja tu nitakutana naye…akakumbuka maneno ya mwisho kuwa kuna mzigo wake ambao asipouwahi utaishia mkononi mwa mkewe, na….`mzigo, mzigo gani huo, tena ..utaishia mikononi mwa mke wangu…ana maana gani huyu…ooh, balaaa’ akashika kichwa
‘Mke wangu ngoja niende nikaonane na huyo mfanyakazi mwenzangu, kwani nimekumbuka kuwa kulikuwa  na kazi nahitajiwa niichukue, kwa ajili ya watu wa TRA, nahisi ndio hiyo anayonihitajia ni kwa ajili ya watu wa TRA, …haya mambo ya kodi, tusipoyaweka sawa haraka iwezekanavyo, tutakuwa katika mshikemshike…siunajua tena mambo ya kodi, tulichelewesha tuka…aah, we acha tu’ akawa anaongea huku anavaa, mkewe alikuwa kimya hasemi kitu anamwangali tu.
Bosi akavaa nguo zake haraharaka huku anaongea , alipomaliza akachukua `briefcase’ yake akamwangalia mkewe kutaka kumuaga, mkewe akainuka taratibu pale alipokuwa amekaa, akasogea kwenye kabati la nguoa, akavua nguo zile alizokuwa kavaa, akachukua gauni lake kubwa refu akalivaa, ni gauni maalumu kwa safari za haraka haraka, akamwangalia mumewe, kama vile anamuonyesha kuwa kapendeza au la, halafu akamfuta…
Bosi  akabaki mdomo wazi akijua leo mkewe anataka kumuaga kwa mtindo gani, akasubiri hadi alipomkaribia, kama vile anataka kumbusu, taratibu akanyosha mkono wake ule ulioshika ile `briefcase’ na kuichukua, halafu akasogea pembeni, na kumwachia mume wake nafasi ya kupita; akamwambia  ‘haya twende,…’ akasema huku anaonyesha mkono wa kumuelekeza mume wake apite. Na kabla mume wake hajajua nini mkewe kapanga, akasikia maneno yaliyomvunja nguvu;
`Nahitaji tuongozane huko unakotaka kuchukua huo mzigo…namimiangalau niwajibike kwa hili, kwani watu wa TRA, nafahamiana nao sana…usiwe na shaka mume wangu, twende, hata ukitaka nimpigie jamaa yangu nitampigia atakuasaidia…twende, twende usichelewe…’ mumewe akabakia mdomo wazi, akamwangalia mkewe, halafu akasema
‘Sawa twende, kama umefikia hapo…una maana huniamini tena, twende…’ akamfuata mkewe nyuma.
‘Hili sio swala la kuaminiana hapa, hili ni swala la mke na mume…kila mtu analinda chake, mimisio mjinga kama unavyodhania…twende, usichelewe…’ akamsukuma mumewe waondoke.
  Wakati hayo yakiendelea Maua alikuwa keshafika kwenye ile hoteli aliyolala jana yake, hakupenda kabisa kufika eneo hilo tena, kwani lilimkumbusha machungu ambayo huenda hatayasahau, na huenda yanampeleka pabaya…ni kweli alivutika na bosi, akatamani awe rafiki yake, lakini sio kihivyo, na wala sio kwa haraka hivyo, na kwa mtindo huo…
‘Hii lazima Bosi alipanga, ili kunikomoa, ili …ole wake, ole wake, nasema atanijua kuwa na mimi ni mtoto wa mjini…’ akajikuta akiapiza huku anaendesha gari kwa kasi, na alipokumbuka kuwa yupo barabarani  na watu wa usalama wa barabarani wanaweza kumsimamisha na kumpotezea muda  akapunguza mwendo na kwenda mwendo wa kawaida. Alipofika kwenye ile Hoteli, alisimamisha gari lake sehemu yanapowekwa magari,  akavaa miwani ya jua ili kuficha sura yake na akatoka haraka haraka kwenye gari, hakumbuki kufunga mlango vizuri, lakini alipofika mbele, akatoa `remote’ na kuiminya, gari likatoa mlio, na hapo akawa hana wasiwasi na gari lake na kuingia ndani ya ile hoteli.
Hakuwa na wazo la kuangalia pembeni kwani wakati anaingia ndani ya ile hoteli, pikipiki moja ilikuja na kusimama pembeni kabisa ya gari lake, na muendeshai akashuka akawa kama anakagua gari la aMaua, halafu akaangalia mlangoni mwa ile hoteli, kipindi ambacho Maua alikuwa anaishia ndani, na huyu mtu bila kupoteza muda akaeleeka kwenye ule mlango wa hoteli naye akaingia ndani. Pikipiki kama ile ilikuwa imesimamishwa mbali kidogo na maegesho, na muendeshaji wake alikuwa kasimama mbali kidogo akiangalia mlango wa ile hoteli.
  Maua Alipokanyaga lile busati la hotelini mle ndani, akili ikamkumbusha taswira za jana…ikamfanya kichwa kiume, akajikuta anasikia kama kutapika, kizunguzungu kikamjaa machoni, akapepesuka karibu akadondoke, na bahati nzuri, alikuwa karibu na mhudumu wa mle ndani akamshika kabla hajadondoka…
‘Upo safi binti, naona kama unaumwa, nikusaidie nini…pole sna, au kinywaji cha jana…’ akasema yule mhudumu, na Maua akshituka, ina maana hawa watu wanamkumbuka…oooh, akatamani arudi alikotoka, lakini akasema moyoni, maji nimeshayafulia nguo, sina budi kuyaoga. Akamwambia yule mhudumu ahsante , hana tatizo kama hilo, nilijikwaa tu, akasema na kujiweka sawa na kuelekea mapokezi.
 Maua alikasohea hadi sehemu ya maulizo akawaambia kuwa kapokea ujumbe wa simu kuwa kuna mzigo wake hapo hotelini je anawezaje kuupata na nani alimpigia simu.
‘Hapa kuna kitengo cha mizigo, watu huleta mizigo yao, na huwapigia watu wao wanaotaka mizigo hiyo iwafikie, na wengine wanatuachia maagizo tuwapigie wenyewe, …sogea dirisha lile pale utaambiwa jinsi ya kuupata mzigo wako…na maeelzo zaidi’ akasema muhudumu wa pale maulizo.
 Maua akasogea hadi pale alipoelekezwa akajitambuslisha, na akaambiwa aonyeshe kitambulsho au pasi ya kusafiria, halafu akaambia aandike jina na sahihi yake,…baadaye akapewa bahasha , iliyoandikwa jina lake, akaichukua na kabla hajaondoka akakumbuka kitu.
‘Jana nilikuwepo hapa, na…nilisahau simu yangu..sijui kuna mtu kajitambulisha kuokota kitu kama hicho?’ akauliza Maua.
‘Mhh, nenda dirisha lile pale , ndilo linaloshughulika na mambo hayo’ akaelekezwa . Maua akasogelea ile sehemu aliyoelekezwa na kumkuta askari na mtu mwingine, akawauliza swali kama lile alilouliza kule mwanzoni. Yule mtu anayeshughulika na maswala hayo akachukua daftari akatafuta, akatikisa kichwa na kusema `Hapana,…hamna simu iliyopatikana jana, unaweza kukumbuka uliisahau wapi maana hapa hakuna tabia ya wizi, kama ulisahahu ndani itapatikana tu…’ akasema mhudumu huyo.
‘Siwezi kukumbuka ni wapi ila, kuna mtu kanipigia simu , na huyohuyo ndiye aliyeniambia nije nichukue mzigo wangu…’ akasema Maua.
‘Tatizo ni kuwa hapa tunapokea mizigo mingi sana, hata kamera yetu ya uaslama inayoonyesha watu wanaoingia inakuwa vigumu kumnasa mtu halisi aliyeleta mzigo upi , labda mzigo huo uwe na alama maalumu ya kutofautisha au uwe unamjua huyo mtu …’ akasema yule mhudumu.
 Maua akaona anapoteza muda, akaona kwanza akaone ni kitu gani alichopewa na kitu hicho kimetoka kwanani huenda kukawa na malekezo ya kuipata simu yake. Akatoka nje ya ile hoteli na kuingia ndani ya gari lake. Aliona sehemu muhimu ya kuufungua huo mzigo wake ni ofisini kwao, kwahiyo moja kwa moja akaelekea ofisini kwao, hakujua kuwa nyuma yeka kulikuwa na pikipiki ikimfuta.
 Maneno alishangaa, kuona mtu akiendesha pikipiki, na pikipiki ile ilikwa sawa kabisa kama yake na mwanzoni hakumgundua hadi pale alipokuja na kusimamisha pikipiki karibu na gari la mke wake. Yeye hakushuka mara moja kwenye ile pikipiki, alitizama huku na kule, halafu akatoka kwenye ile pikipiki na kukagua gari la mke wake halafu akaelekea kwenye mlango wa ile hotelini.
Baadaye sana mkewe alipotoka nje ya ile hoteli yule mwendesha pikipiki naye akawa nyuma yake, utafikiri ni mlinzi wake. Na alikuwa kavaa vitu masikioni, kuonyesha kuwa alikuwa akiwasilina na watu, kama walinzi wa karibu wa watu wakubwa wanavyofanya.
`Ina maana mke wangu ana bodyguard siku hizi hata mimi sijui..’ akajiuliza Maneno.
Maneno akawa na shauku sana ya kumwangalia yule mtu, kwani mkewe alipotoka tu mtu huyo akawa anamfuta kwa nyuma, na jinsi anavyomfuata ni kama vile watu wanajuana. Akaingiwa na wasiwasi kuwa huenda sio mlinzi kama anavyozania,  au ndio huyo aliyempigia simu, …labda wanajuana…, mbona hana wasiwasi kabisa, lakini hata hivyo mbona mkewe alipotoka hawakuonekana kuongea hata neno moja. Yule mtu alisogelea pikipiki yake na alisubiri mpaka  mke wa jamaa alipoondoka ndipo akamfuta kwa nyuma na pikipiki yake.   Maneno alipoona vile akataka kumpigia simu mkewe kumuonya kuhusina na huyo mtu, lakini akaona ni mapema kufanya kitu kama hicho.
Maneno naye bila kupoteza muda akawafuata kwa nyuma, lakini alijaribu kuwa mbali sana na gari la mkewe na yule muendesha pikipiki, akawa pia anahakikisha kuwa haachwi mbali sana.  Kichwani aliwaza mengi, alikumbuka visa vya ujambazi , matapeli ambao wanaweza wakapiga simu kuwa una mzigo, kumbe ni kukuhadaa ili mwisho wa siku wakupate kirahisi…hata kutekwa nyara…oh mke wangu, aepushiwe na balaa hilo!
‘Kwanini mke wangu hakunisikiliza…tatizo hawa wanawake waliosoma, wanajiamini kupita kiasi…ok lakini ingekuwa vyema tukaongozana, mimi ni mume wake.., maana hii saa …’ akakatisha mawazo, pale mkewe alipoendesha kwa kasi na kupitiliza njia ya kuingia kwao, akajiuliza huyu sasa anakwenda wapi.
‘Je sasa nifanyeje, maana nikijifanya mjanja naweza kujiingiza kwenye mkenge, na nikiwa kimya mke wangu anaweza kuzurika,,,,;’ akaishika simu yake, kutaka kumpigia mkewe…akakumbuka kuwa mke wake hana simu…akatikisa kichwa,na kujikuta katika njia panda kimawazo. Kilichomshangaza zaidi ni kuona pale mke wake badala ya kuingia kwenye barabara ya kurudi nyumbani kwao, yeye kapitiliza na hajui anakoelekea ni wapi, hata hivyo akaendelea kumfuata kwa nyuma na kwa mtindo ule ule wa kuhakikisha anakuwa mbali na wao.
 Huku kwa Bosi na mkewe wakaingia ndani ya gari, na bosi akaliwasha gari lake, kichwani akiwaza afanyaje, akiwa kasha ndani ya gari akaona aghairi na mpango wake wa awali,  badala ya kwenda hotelini alipoagizwa aelekee ofisini na kuvunga hili na lile, na anavyomjua mke wake alivyoo ataamua kurudi nyumbani. Mkewe hapendi mambo ya kusubiri subiri. Akaendesha gari wakiwa kimya, mke wake anaangalia nje, yeye na usukani wake.
‘Mimi nilifikiria huo mzigo unaufuata hotelini, mbona tunaelekea kazini kwenu?’ akauliza mke mtu.
‘ Hotelini, kwanini hotelini, mmmh mimi nimekuambia ni mambo ya TRA, …ndio kazi nzima tuliihamishia hotelini, ili kupata nafasin na utulivu, lakini huo mzigo nataraji utakuwa ofisini , kwani huyo mfanyakazi mwenzangu ndiye aliye nao…tatizo ndio hilo simu yake haipatikani tena…’ akasema Bosi.
‘Jaribu kumpigia tena na tena,…’ akasema mke wake kwa mzaha.
‘Tatizo lako mke wangu huniamini, sijui unanionaje mimi…hii ndio kazi yangu, unajua jinsi gani baba yako alivyoniamini na kazi hii, nikivurunda unafikiri yule mzee atanielewa kweli..’ akasema Bosi.
‘Hilo najua , lakini tatizo lako unapenda sana kazi na dawa…hilo, litakupeleka pabaya, unajua pabaya…haya we, wewe cheza na hii familia, ikifikia muda wa ubaya , hutaamini kuwa ni mimi , muda huo sitojali kabisa kuwa wewe ni mume wangu…hilo nakumabia ukweli…’ akasema mke wake kwa hasira.
 Bosi aliposikia maneno haya akajuta kwanini aliingiwa na vishawishi vile, ni kweli anampenda Maua, lakini Maua ni mke wa mtu, halafu…tukio zima lilivyotokea mbona limeenda kinyume na alivyotarajia, kwanini imetokea vile, au kuna watu wamepanga iwe hivyo…haiwezekani, ni nani ambaye angeamua kufanya jambo kama hilo, `mbona sina watu walio-onyesha ishara kama hiyo…hapana, huyu ni Maua anajifanya mtoto wa mjini…ngoja nitakutana naye…’ akajisemea kwa sauti ya chini kwa chini , na kujisahau kuwa yupo kwenye barabara na kuikuta akiendesha kwa kasi isivyo kawaida, kumbe pembeni walikuwepo watu wa usalama, wakaliona hili.
Mara nyuma wakasikia king’ora cha polisi.
‘Hivi wewe una akili kweli,  huoni umewashitua traffic, sasa unaniingiza katika ujinga wako…’ akasema mke wake, wakati yule traffic keshawafikia akanyosha mkono wa kulisimamisha hilo gari, Wakasogea pembeni na kusimama.
‘Wewe dereva upo kwenye mashindano ya magari, au unajifanya barabara ni ya kwako peke yako, unajua sheria za ualama barabarani, hebu kwanza nipe leseni yako…’ akasema traffic, na wakati huo mke wa bosi akatafuta namba kwenye simu yake na kwa haraka akaipiga namba hiyo.
‘Kaka tumekutwa na kisanga, …barabarani, na hapa tupo na traffic, naomba msaada wako…ndio naelewa hilo, ni huyu mume wangu, sijui anawaza nini…nini eti nini…hapana, ok, sawa tutaongea hilo baadaye ila limalize hili kwanza…hayo tutaongea baadaye…
 Je nini ina maana gani, je haya mafuatano yataishia wapi, naomba nimalizie hapa kwa muda maana nina tui la ofisni, Tuwe pamoja!

Ni mimi: emu-three

4 comments :

samira said...

jamani watu kwakujiingiza kwenye matatizo haya sasa ashajiharibia bosi
na inaonekana ni familia ya hatari haya mi nasubiri kwahamu nijuwe itakuwaje
thanks m3 kwa kuwa nasi unajitahidi dada au sijuwi kaka unisamehe sielewi

emuthree said...

Nashukuru sana Samira, kwani leo nilikuwa nasubiri sana kusikia wapenzi wangu watasemaje, kabla sijaanza kuchanganya mambo, maana hatua zinzokuja ni za kuchanganya changanya...
Usijali Samira, wewe unaweza kuita upendavyo, dada, kaka, vyovyote uonavyo inafaa. Ila wengi wananiita 'kaka emu-three'...!

TUPO PAMOJA DAIMA!

Anonymous said...

Una utajiri wa kutosha ndugu yangu kazi iliyobaki ni kuufanyia kazi. Ukimaliza hiki kisa kikusanye sehemu zote uziweke kwenye kitabu ama sivyo wajanja watatajirika mgongoni mwako, si unajua Bongo hakuna sheria kali kuhusu wizi wa kukopi kazi za watu (pligiarism)? Cha msingi kiweke kwenye manuscript na uanze kupanga kitabu sasa. Utakuja kunambia matokeo yake wala usione kuwa ni kazi ngumu.

Hujui tu kuwa uko very talented in creative writing ungekuwa nchi za wengine wewe ni tajiri wa kutupwa kazi yako ni kukaa kwenye nyumba yako ya pwani au shamba(cottage) unaandika vitabu kimoja baada ya kingine, ukimaliza unaitwa kwenye signing of your book! Maybe you will be there one day, dont you ever ghive up writing. Anza kidogo kidogo hata elfu 3 kwa kitabu baadae watu wakishazoea kazi zako utauza mpaka bei ambayo utashangaa. Nakumbuka zamani nilikuwa napenda vitabu vya Willy Gamba vya Elvis Musiba na vitabu vingi tu vya kina Kezilahabi (Rosa Mistika) Naamini sasa tumepata mwandishi wa style ile ya kina Willy Gamba na kina Kezilahabi sio hadithi tunazozisoma simeigwa kutoka hadithi za kizungu. Mshukuru mungu sana kwa kipaji chako!

Subira

Yasinta Ngonyani said...

Hapa patamu sana na pia pabaya sana. maana hapa wote Bosi na Maua wapo hatarini...ngoja niendelee ili nijue nini kinaendelea