Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, May 17, 2011

Dawa ya moto ni moto-10



 Tuendelee na kisa chetu, rejea pale Maua alipodondoka kitanda ni na kuzirai, ilikuwaje pale....tuingie ndani ya kisa: Ingawaje sijui kuwa tupo pamoja au naenda kivyavyangu...
                                        
                                                                      ***************

Maneno ambaye kwa muda mwingi alikuwa kasimama pembeni mwa kitandani alishuhudia mkewe akiidondosha ile simu kitandani, na baaadaye akashangaa mkewe akibadilika na ghafla akadondoka pale kitandani. Ilikuwa ni bahati kuwa yupo juu ya kitanda. Maneno alipoona hivyo akamsogelea mkewe na kumshika mkono, akamuita ‘Maua , Maua, vipi tena, ndio hicho kichwa au nini kimezidi…Maua, Maua …’ alipoona kimya na mkono upo lepelepe akashikwa na mshangao, akakimbilia pale kitandani, na kumuinua Maua kichwa, akakuta mtu kalegea, …`Oh, ina maana mtu ananifia hivihivi…hapana, hapana…haiwezekani, Mungu wangu, Maua amka, …amka Maua…’ akajikuta akisema kwa sauti.
 Alipoona kimya, akajua sasa kumekucha, mtoto wa watu keshakata roho,….akashika kichwa, akatizama juu, akajiuliza kimoyomoyo, atasemaje kwa wazazi wake, mtu karudi akiwa na hali kama ile, ataulizwa mkeo alilala wapi…akamsogelea Maua akamshika shingoni sehemu inayoonyesha mapiga ya moyo, akaona kimya…mwili ukaanza kumlegea, jasho likaanza kumtoka. Akamwachia haraka kitandani, akasimama pembeni, akamwangalia tena Maua, akajikuta haamini, ina maana kweli sasa hana mke. Ina maana sasa anarudi kijiweni, ina maana, sasa…labda ataishia gerezani, mungu wangu.
‘Mungu wangu Sasa nifanyeje, akachukua simu na kutafuta simu ya dakitari anayemjua, akapiga ile namba , ikawa haipatikani, akasonya, akatafuta nyingine, simu ikasema inatumika. Akaiweka pembeni , akamsogelea Maua pale kitandani, akamuinua kichwa, na kukiweka mapajani kwake, huku akimpepea na kitabu huku akiomba kwa Mungu amsaidia, …., na huku machozi yanamtoka, alijikuta akisema kwa sauti kubwa.
‘Maua usiniache mpenzi, Maua usife ukaniacha kwenye njia panda, …nitaishije mimi bila wewe…nakuomba usife Maua, kwani kumetokea nini, mimi nitakuja kusema nini kwa wazee wako, kuwa nimeshindwa kuishi na wewe mpaka unakwenda huko, wanakufanyia sijui kitu gani….Oh, mungu wangu’ Akahisi kitu, akamwangalia Maua usoni, ajiuliza, nimehisi kma kidole kikitikisika, akamshika mkono, akashika …shingoni, akahisi mabadiliko akaona mkono ukitikisika, akamwangalia usoni, na mara macho yakaanza kucheza cheza.
‘Oh, thank God,…Ohh, Maua, …Maua, Maua…’ akaita tena na tena.
Maua akafumbua macho na kuangalia, halafu akatikisa kichwa , halafau akayafumba tena, …baadaye akayafumbua na kumwangalia mume wake, ambaye alikuwa kamshikilia na kumlaza mapajani. Akawa anashangaa, akauliza kwa sauti isiyotoka, `kuna nini…’
 Maneno akakiondoa kichwa cha mkewe mapajani akamweka vyema kitandani huku akishangaa, tukio zima, lilivyokuwa, kwani limeanzia pale mkewe alipomuomba simu, akapiga namba, halafu akadondosha simu nay eye akadondoka kitandani na hata kupoteza fahamu…! Alipokumbuka hiko harakaharaka akaichukua ile simu akijua kuna taarifa ya msiba, …akaitizama ile namba akaipiga, lakini simu ikasema uneyempigia hapatikani, akamweka mkewe vizuri na kumfanyia huduma ya kwanza hadi pale alipofumbua macho vizuri
‘Vipi Mkewe wangu kuna nini kimetokea…’ Maneno akauliza hata bila kongojea mkewe atulie vizuri.
‘Kuna nini kimetokea, kwani imekuwaje…?’ Maua akainuka na kujikuta akishangaa, halafu alipokumbuka kile alicjokisikia kwenye simu, akainuka kabisa kitandani, akamwangalia mumewe, ambaye alikuwa kashikilia simu yake, akamsogelea
‘Hiyo simu yako ..hebu nipe…kuna mtu kanishitua kweli kweli…’ akasema Maua kwa wasiwasi, alimtizama mume wake kwa wasiwasi, aliitizama ile namba akakuta imeshapigwa tena, ina maana mume wake keshampigia huyo mtu na huenda kayasikia yale aliyoyasikia wakati ule.
‘Umempigia huyu mtu simu…?’ akauliza Maua.
‘Mtu gani, …?’ Maneno akauliza kwa mshangao,
‘Naona hapa umepiga hii namba tena…? Akasema Maua huku akipiga ile namba, na sauti iliyotoka ilisema namba unayopiga haipatikani
`Lakini mke wangu hiyo ni namba yako, ina maana hiyo ni simu yako imepatikana, au sio, sasa ulipompigia huyu mwenye simu yako alisema nini,…kwanini akushitue kiasi hicho hata kupoteza fahamu, au bado ni tatizo la kichwa…au kuna taarifa nyingine mbaya alikuambia aliyeishika hiyo simu?’ akauliza Maneno.
‘Nilipoteza fahamu, nani, mimi…hapana, ….hata hivyo hakuna taarifa mbaya, zaidi ya hayo mambo ya kiofisi hakuna zaidi, lakini achana nayo, hukuongea naye kitu chochote, au umesikia nini?’ akauliza Maua.
‘Eti hukupoteza fahamu, Maua, naona labda malaria imekupanda kichwani, bora twende hospitali ukachunguzwe vyema, …halafu bado unaendelea kuuliza eti nimesikia nini…?,nimesikia sauti za ajabu ajabu tu…au ulitaka niseme nini!’ Maneno akasema kwa mzaha, huku akiogopa kusema zaidi kwani alikuwa hajui ajibuje hilo swali aliloulizwa.
‘Sauti gani za ajabu-ajabu Maneno unajua unanichanganya mara useme nilipoteza fahamu sasa wasema sauti za ajabu ajabu, zilikuwa zinasemaje hizo sauti…?, walikuwa wakiongea nini..? akauliza Maua kwa wasiwasi.
‘Wewe sasa unaumwa, achana na hilo, twende hospitali, jiandae twende…’ akasema Maua `kwanza kama kuna mtu kaiokota simu yako, nielekeze mimi nikapambane naya, wewe ukatibiwe na upate muda wa kupumzika…’ akasema Maneno.
‘Kichwa kimepona kiajabu kabisano, mimi sumwi malaria wala nini….ila hapa nilipo nina mawazo yanayozidi maumivu ya kichwa, naomba uniache kidogo..’ akasema Maua huku akishika kichwa, halafu akamwangalia mumewe na kuuliza tena kuwa kweli hukusikia lolote wakati alipoipiga hiyo namba. Maneno akamwangalia mkewe bila kusema lolote, alikuwa kichwani akijiuliza ni kwanini mke wake achanganyikiwa baada ya kupokea ile simu, na hata kupoteza fahamu, na sasa anazidi kudadisi kuhusu kilichoongewa kwenye simu,…’ akamtizama Maua usoni, na Maua akakwepesha macho na kutizama pembeni.
Wakakaa kimya kwa muda kila mtu akiwaza lake, lakini Maua akawa hatulii , mara aijaribu kuipiga ile simu, …lakini ilikuwa na ujumbe ule ule kuwa namba unayopiga haipatikani, jaribu tena baadaye.
Maneno alishindwa amsaidieje mkewe, kwani alionekana kuchanganyikwia sana, mara ashike simu, aipiga , mara ashichi hiki akiache , mara akae, ainuke, hata  ule usingizi au kichwa kilichokuwa kikimuuma, vimetoweka. Akataka kudaidisi zaidi lakini akaona ampe kwanza muda mkewe ajiweke sawa, huwa anamuelewa sana mkewe akisema `nipe nafasi kwanza’ ana maana gani, anahitaji muda wa kutafakari kwanza, halafu atakuambia anachotaka kukuambia.
 Maua akatoka pale kitandani na kukimbilia bafuni, huko alijimwagia maji haraka haraka huku akiwaza mengi, na alipofikia kuwaza yale yaliyotokea kule hotelini…alihisi mwili ukizizima kwa woga, akijiuliza kwanini alifikia kutenda tendo kama lile, ina maana ilikuwa ni pombe…mbona baada ya kunywa zile pombe hakumbuki nini kilitokea zaidi…nakwanini bosi wake alimng’ang’ania anywe pombe, hii haionyeshi kuwa kulikuwa na mango kama huo, ili alewe , afanye kile alichofanya na matokea yake yawe kama hayo.
`Lakini baada ya kunywa ile pombe ilikuwaje,…akajaribu kukumbuka, lakini haikuja akilini…akakumbuka tu pale alipoamuka na kujikuta yupo kitandani, …tena uchi, tana alijihisi kuwa kafanya tendo….`ooh, ina maana yote ilikuwa ni mbinu ya bosi, kunahandaa kwa pombe, ili niliwe, halafu anifanyie vile…, ibilisi mkubwa yule, yaani mapaka anileweshe…I will kill him…I swear, I will kill him…’ akajikuta akisema kwa sauti
 Maua aliacha kuoga akaenda kujitizam kwenye kiyoo, akaona jinsi sura ilivyobadilika kwa muda mfupi, alijiona mzee, akakunja uso na kurudi kuoga, akajipaka sabuni kwa wingi na kujimwagi maji, na kila alivyowaza, ndivyo alivyozidi kujipaka sabuni ….‘Haki ya mungu, hili litafika mbali, sikubali kuzalilishwa, halafu ndio akaamua kunirekodi ili anizalilishe, tutapambana naye, ngoja nikamuone sasa hivi, najua yeye ndiye kanipigia simu akijifanya mtu mwingine…lakini mbona kasema kuna mzigo wangu ambao nikichelewa utamfikia mume wangu na baba yangu…ni mzigo gani huo…mmmh,’ akafunga maji kwenye bomba, akachukua taulo, hakutaka hata kuifuta akasema `Tutapambana huko huko,…’ akasema huku akiwaza yale maneno yalivyosema `mzigo upo hotelin…’,  akajiuliza kwanini uwe hotelini..? akajikuta akijiuliza maswali mengi  huku akitoka kule bafuni.
 Akatoka bafuni na kuelekea chumbani ambapo alimkuta mumewe akiwa kasimama akichungulia nje kwa kupitia dirishani, na simu ipo pale pale alipoiacha kitandani, na Maneno aliposikia akiingia akageuka haraka na kumwangalia mkewe, akashangaa kumuona akiwa na mapovu masikioni, na sio kawaida yake. Maua ni matanashati na anajua kujiweka sawa, sasa hili linaashiria kuna tatizo kubwa… akamwangalia mkewe na kumuonea huruma! Alimshangaa pale alipomuona anavaa nguo zake za kazini tena kwa haraka haraka, na kuchukua begi lake…Maneno akakaa kimya tu.
Maua alipovaa nguo zake za kazini akageuka kuondoka, akakumbuka kitu, akamgeukia mumewe.
‘Samahani sana mume wangu huyo aliyeokota simu huenda akawa ni bosi wangu wa kazini, na anataka kunichezea shere, au kweli kuna matatizo ya mahesabu ya jana, na alivyosema ni kuwa watu wa TRA, wamegudua kuwa tumekwepa kodi nyingi sana na wanaweza kutufunga,…hilo sio jambo dogo niliyosikia inaonekaana hakuna mema, ….ngoja nikamuone bosi, kwani kumbe jana alichukua simu yangu, na …’ akawa keshafika mlangoni huku akiongea.
‘Lakini wewe Mua siunaumwa, ulipofika hapa ulidai kichwa kinauma sana, hebu jifikirie wewe kwanza na afya yako, huyo bosi mweleze kuwa hali yako sio shwari na kama ni kazi za kuchukua au kumpelekea huyo bosi wako niagize mimi nitaenda kuzisimamia.. na hawo watu wa TRA, watawafunga hivi hivi tu…mbona haiingii akilini’ akasema Maneno huku anasogea mlangoni.
‘Hapana mume wangu sipendi kabisa kukutumbukiza katika matatizo kama hayo, hutaweza kujua nini kimetokea ni maswala ya kimahesabu yanahitaji mtu aliyeyasomea, wewe tulio hapa, nitakujulisha nini kimetokea…’ akasema Maua huku kashikilia mlango. Maneno akawa hana jinsi akashusha mikono na kujipiga kwenye mapaja akionyesha kushindwa la kufanya, akageuka na kumtizama mkewe, ambaye alikuwa akiishia nje.
 Maua akafunga mlango na kumuacha mume wake ndani akiwa kaduwaa, alipofika nje akakumbuka kitu akarudi ndani haraka , na kumkuta mume wake akijaribu kuipiga ile namba, lakini ilikuwa haipatikani! Maua akamtizama Maneno na kumwambia asiipige tena hiyo namba kwani atamharibia mambo yake ya kiofisi… akasema Maua huku akirudi tena nje, alipofunga mlango akakumbuka kuwa kasahau kile kilichomrudisha, alisahau ile tabia yake ya kumbusu mumewe kabla hajaondoka. Alipogundua hili akarudi tena ndani kwa haraka na kumkuta Maneno bado kasimama akiwa kaduwaana hajui afanye nini…akamsogelea na kumshika , halafu akambusu kwa haraka na kusema `bye, take care honey..’
 ‘Take care honey…?’ Maneno akayarudia yale maneno kwa mzaha, pale mlango ulipofungwa, akatizama dirishani, lakini hakuridhika akawaza, akasema, hapana huyu ni mke wangu na nawajibika naye, kwanza anaumwa, pili kapata simu ya kumchangaya kichwa, itakuwa sio vyema nikakaa humu ndani kama gogo, lazima nikasaidia lile ninaloweza kusaidia….. Alipowaza hivyo, akajitizama kwenye kiyoo, akaona haina haja kubadili nguo, akafunga milango na kuhakikisha kuwa kile kitu kipo makini, na kwa haraka akatoka nje, na alipofika nje akakuta mkewe keshaondoka. Hakupoteza muda akafuta pikipiki yake na kuidandia huyo akaingia barabarani. Aliendesha kwa muda muda akijua huko ndipo alipoelekea mkewe.
                      
                     Je kuna nini kitatokea; tuzidi kuwepo sehemu inayofuatia; tukumbuke kisa hiki kimegubikwa na usaliti, na `u-blackmail' nisaidieni kiswahili safi cha `blackmail'


Ni mimi: emu-three

9 comments :

Pamela said...

ucwe na wasiwasi M3 tuko pamoja tunapita kimya kimya... kwa kweli hii story inapandisha mapigo ya moyo na kutaka kujua kila hatua itakayofuata

Nancy M said...

Tuko pamoja na tutaendelea kuwa pamoja... maana hiki kisa ni babkubwa

samira said...

m3 tupo pamoja mambo maziri nimependa sana cant wait

Rachel Siwa said...

Kaka Moto wako si wavifuu nakuaminia!!!!kazi nzuri pamoja kaka.

Faith S Hilary said...

M3 ndugu yangu sasa nimerudi tena "officially" hehe never miss hata iwe Alhamisi. Nimesoma toka pale nilipoiacha mpaka sasa na naona mambo yanazidi kupamba moto kwa kweli. Nipo kama kawa niendelee kujua ya Maneno, Maua, Bosi na mkewe..bila kumsahau baba yake Maua...kazi ipo hapo!

EDNA said...

Mmmmh kaka unatisha sana wewe,maana mtu unasoma mpaka mwili unasisimuka.

chib said...

Najua ... Candy karudi, muhimu kupata hadithi za kusisimua na kusahau ushabiki wa....
Mkuu Emu3, udumu sana

emu-three said...

Nashukuru wakuu, wajumbe, wapendwa kuwa tupo pamoja maana ukiandika halafu watu wakapita kimya kimya, utashindwa kujua umekwenda vyema au vipi?
Nawaombeni angalau hata salamu, sio mbaya!
Tuwepo kwenye sehemu inayofuata, mambo ya mfuatano...itakuwaje soma sehemu ya 11, ujionee!

Yasinta Ngonyani said...

kweli pombe si maji...Maneno sijui atafanikiwa ...

neno blackmail ni saliti:- kumtisha mtu kwamba atafichua siri/maovu yake ili akupe fedha/upendeleo.

Na kubaliana na Edna ni kweli unasoma mpaka mwili unasisimka kazi nzuri sana ila mimi bado nakushauri kuhusu kitabu....