Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeSaturday, April 2, 2011

Wazo la Jumamosi-usisahau asili yako` Mjukuu wangu nakuambia kitu kimoja, kila mwanadamu ana ubinafsi, hii ni hulka yetu, kila mmoja anataka kupata, kila mmoja anataka kupendwa, kusifiwa nakadhalika, hakuna anayependa kuitwa mbaya, hajui, ..au hakuna anayependa kukosa, na kila mmoja anajiona yeye ni bora…na kwa hili watu wanatawanyika huku na kule kutafuta zaidi na zaidi, lakini …asili ni muhimu sana…usisahau asili yako.’ Hayo ni baadhi ya maneno yahekima ya  babu yangu enzi za uhai wake.
Jumamosi ya leo nimefika ofisini, nikiwa na mengi , mojawapo ni kuendeleza kile kisa chetu cha nani kama mama, lakini kabla sijaanza kuandika nikajiwa na wazo,…nikamkumbuka babu yangu huko alipo, niliwaza sana, nilikiwaza kizazi chatu toka aondoke, hadi kikafikia hapa nilipo. Ni safari ndefu kwani yeye alikua akatafuta masiha yake, akaoa akazaa watoto wake na watoto wake wakazaa tukaja sisi, na sisi tumezaa na hata wengine watoto wao wamezaa, na waliozaliwa pengine wamezaa…! kabla sijaendelea naomba nitafute kichwa cha habari cha hiki ninachotaka kuandika, oooh naona niite tu `wazo la Jumamosi’.
Nilijaribu kukaa na kuorodhesha kitu kama mtririko wa familia yetu toka babu, hadi wajukuu hadi watukuu, nikajikuta na orodha ndefu ajabu, nikajiuliza hivi wote hawa tunajuana kweli, nikaamua nijiridhishe moyo wangu kwa kuangalia yale majina ya wanandugu nakujiuliza huyu ni nani, anafananaje, nikashindwa kugundua wote, kwasababu familia zimatawanyika kila mmoja akitafuta riziki yake.
 Wengi wetu tunakutana kipindi cha shida, na mara chache kipindi cha raha kama vile harusi, …na hapo ndipo tunaanza kuulizana hivi wewe ni nani, …basi inakuwa raha ya aina yake, hata inafikia hatua mnasahau kuwa mlikuwa katika jambo fulani na huenda lilikuwa ni la shida kama vile  msiba.
Nikajiuliza, hivi kwanini …hasa huku Afrika hatuna utaratibu wa kuweka kumbukumbu za vizazi, …ndio kuna kumbukumbu zile za vyeti vya kuazaliwa na vifo, lakini haviingi kiundani na kuandika kizazi hadi kizazi, hili linakuwa jukumu la wanafamilia husika, na baya zaidi wanafamilia hawana muda nalo, `kwani litakusaidia nini katika kutafuta mkate wako wa kila siku’ wengi wanatasema hivyo kama wanavyosema `demokrasia au kupiga kura kutanisaidia nini…unaweza ukashangaa kuwa maneo haya yanaweza yakasemwa  hata na muhitimu wa chuo kikuu!
Niliwaza kisa kimoja cha wanandugu walio-oana , walikutana kimjini mjini, wakapendana,…siunaua tena, mtu anajiependa sana mwenyewe, sasa itokee bahati unampata mwenzako wa jinsia tofauti anafanana na wewe, ni wazi kuwa utampenda…hawa jamaa binti na mvulana wakapendana, na kwa vile siku hizi ni lazima uonje mboga kwanza ili ijulikane kuwa imeiva, au imekolea chumvi, vijana hawa wakavunja amri ya ngapi vile…sijui, lakini mwisho wa siku binti akapata uja-uzito. Basi ile onja-onja ikafikia mahala pake, vijana wakaona ni vyema tufunge ndoa kabisa.
Safari ikapangwa kwenda kwa wazazi, na ukumbuke hawa vijana walikutana hapa mjini, aheri ya kijana mwanaume alikuwa anakujua kijijini kwao, lakini bintii alizaliwa Dar, Mwananyamala hospital, akakulia Dar, hadi kufikia hatua hiyo ya kukutana na kijana mrembo. Wazazi wao walikuwa watu wa mishe mishe, leo Kenya kesho Ulaya, na vijana halikadhalika, kwahiyo hawakuwa na muda wa kuwapeleka watoto wao kijijini. Na bahati ilivyo, wazazi wakafungua kampuni yao Kenya, lakini binti yao huyu kwa vile alikuwa anasoma hapo chuo kikuu ikabidi awe anabakia Dar-es-salam.
‘Baba mimi nimepata mchumba, na anataka kunipeleka kijijini kwa wazazi wake, akanitambulishe, na kama ikiwezekana tufunge ndoa..’ binti akampigia baba na mama yake simu.
‘Sawa mwaneti lakini unamjua vyema huyo mvulana..’ akauliza mama kwenye simu
‘Namjua vyema sana na ….na bahai nzuri nina ujauzito wake..’ akasema binti.
‘Wow, nice, kumbe tunataraji mjukuu, sasa uwe mwangalifu….najua umekuwa sasa, na una tamaa ya maisha, lakini umaharakisha sana, sio mbaya, kama imetokea hatuna jinsi…tunacho-omba, elewaneni halafu tutakuja tupange harusi…unasema huyu mvulana anafanya kazi wapi…?’ akauliza na mengi n, mengineyo, mwisho wa siku mambo yakawekwa safi.
 Basi vijana hawa wakachukuana hadi kijijini kwao, sitaki kutaja wapi, ili nisichokoze watu. Wakafika wakakaribishwa vyema na wenyeji wao ambao ni wazazi wa mvulana. Na kilichowaleta kikawekwa bayana, na wazazi wa mvulana wakawa hawana kipingamizi, kwani binti ni mrembo, ana adabu, msomi, anatoka familia ya kitajiri …ila familia aliyoitaja ikamgusa baba mtu, akauliza mara mbili tatu,lakini hakuelewa, kwani jina la familia linavyotajwa, linatajwa kwa lafudhi ya kiingereza, kwahiyo yeye aliona sio kama alivyofikiria, ila kila akimwangalia yule bintii anakumbuka  kitu…ikawa ni hisa tu.
‘Mke wangu unajua nimemkumbuka sana ndugu yetu aliyeondoka  hapa nyumbani siku nyingi sana, alitoroka hapa nyumbani akaenda mjini na huko akajishughulisha na kusoma hadi akafika Ulaya, sijui siku hizi yupo wapi…nimemuwaza sana hadi kumuota…’ akasema mume mwenyeji wa vijana maharusi wararajiwa.
‘Kwanini umemuwaza sana hivyo…’ akauliza mkewe.
‘Hata mimi sijui.
Siku zikaenda na tarehe ya harusi ikapangwa, na ikapendekezwa kuwa harusi ikishafungwa Dar, basi kwa vile wanafamilia hawataweza kusafiri hadi huko, fungate na kila kitu kifanyikie kijijini, …ikakubalika kwani binti alipenda sana mandhari ya kijijini. Ikafanyika hivyo, na ujue kuwa mimba ile bado ilikuwa changa na hata wanandoa hawa hawakuifichua kwa wazazi wa mvulana.
Baada ya harusi vijana wakafunga safari ya kwenda kijijini, na bahati nzuri wazazi wakasema ni vyema wawasindikize vijana wao ili wakaone huko binti alipokupenda kufanyia fungate badala ya majiji ya raha kama Dar , Zanzibar au Nairobi au hata ulaya kama wangelipenda hivyo, kwani wazazi pesa ipo…
Safari ikaiva wakaongozana wanafamilia hawo, na kila hatua baba wa binti akawa anashikwa na butwaa, ni siku nyingi sana alitoka kwao hata ile kumbukumbu ilishamtoka, alitoroka akiwa darasa la pili hadi kafikia hatua ya kuwa na mtoto ambaye anataraji kuwa mjukuu hajakanyaga kwao au kuwasilian na nduguu zao…
‘Huku tunakokwenda ni kwetu…mimi asili yangu ni huku, ni bahati sana kuwa binti yetu amefanya nirudi maeneo ya kwetu. …’ akasema baba wa binti. Na wakaingia kijijini, na kukaribishwa na wenyeji. Kwa muda huo waliokuwepo ni akina mama wakipika pika, akina baba wapo mashambani wakivuna na mengineyo.
Jioni ikafika, wazee wakarudi na kuwakuta wenyeji. Familia hii ya mvulana ilijaliwa, kwani jamaa aliwekeza, kwahiyo kijijini alikuwa mmoja wa walio-nacho na alijenga mbali kidogo na familia yao ya asili.
‘Karibuni sana wageni, maana hii ni Baraka, na watoto wali[posema fungate litafanyikia huku nilifurahi sana…sasa kabla ya yote ni bora kutambulishana, au sio…’
zoezi likaanza, na aliyeanza ni mama wa binti kwani `wanawake kwanza’ akajielezea hadi mwisho, wakafuata wengine na mwisho akafuata baba mtu.
‘Mimi ni mzaliwa wa hukuhuku, lakini kijiji cha….cha sikumbuki jina vizuri, ila wazazi wangu wanaitwa…mafalume, na wanajulikana sana huko kijijini kwetu, nakumbuka niliondoka nikiwa darasa la pili…na sikumbuki tena ….’ Kabla hajamaliza alishituka baba mwenyeji akidondoka pale kwenye kiti…ikawa mshike mshike…hadi alipopata fahamu ni usiku wa manane, ikalazimu walale hadi asubuhi ili kesho apelekwe hospitalini.
Kulipopambazuka, jamaa aliamuka mwenyewe mapema, akaomba mgeni wake wa kiume aitwe, na kumbe alishamuita baba na mama yake mzazi ambao siku ya jana hawakuwepo, …baba mzazi alipofika na kukutana na mgeni…alipomtizama mgeni aliyefika akashituka na …lakini akaficha kilicho moyoni, mama mtu naye akashikwa na kitu moyoni, siunajua tena damu ni nzito kuliko maji.
‘Mke wangu unamuonaje huyu mgeni wetu mwanaume…’ akuliza kwa kunong’ona
‘Hata mimi nawaza hilohilo…nakumbuka mbali sana, lakini ni kufanana tu, mimi sizani kuwa ndio hivyo. ..’ akasema mkewe. Basi yule mwenyeji akaambiwa ajitambulishe tena, akajikuta anamtaja baba ambaye ndiye aliyekuwepo mbele yake …lakini masikini alishamsahau…

 Hebu fikiria mwenyewe ilikuwaje baada ya kadhia hiyo…siwezi kumalizia hili kwasababu sio kisa cha kuendelea , ila nimekichomeka ndani ya wazo la jumamosi, na najua sio mara moja au mbili tatizo kama hili kutokea, na utagundua kuwa ni ile kasoro ya kutokujenga tabia ya kuwasiliana au kuweka kumbukumbu za vizazi…mwisho wasiku mtaulizana, `nani alaumiwe’ maisha ndivyo yalivyo, watu lazima watawanyike wahangaike kutafauta mkate wa kila siku…lakini kwanini tunasahau kule tulipotoka, na kama ni hivyo, kwanini tusiwe na tabia ya kuweka kumbukumbu , au kuwasimulia watoto wetu asili zetu hata kama kuwapeleka huko kijijini imeshindikana, lakini wasimulieni watoto wenu, wajue asili yao…wekeni kumbukumbu vyema. Mimi nimelianza hili kwa moyo mmoja, je wewe?

NB: Ukitaka kuweka rekodi ya familia yako, unaweza ukaingia hapa: http://www.genopro.com/setup/

Ni mimi: emu-three

7 comments :

SIMON KITURURU said...

Usisahau asili yako!

Hapa Mkuu umemaliza YOTE tokea kwenye kichwa cha habari ukiniuliza mimi!

EDNA said...

Duuh nimekuvulia kofia...ni vizuri kulifanyia kazi swala hili.Asante Emu 3

Mwanasosholojia said...

Mawazo mwanana yenye kuupiga msasa ubongo, umefanikiwa kunifanya nione vitu vingi vingine ambavyo sikuvifiria awali, asante sana Emu-three!

emu-three said...

Nimefurahi wakuu, kama ujumbe ni muruwa...basi tuanzishe Geno...au kuna blog imewahi kuanzishwa ya mambo haya, ili tujimwage na kumbukumbu zetu...ilikuwa ni wazo tu!

Yasinta Ngonyani said...

Hakika leo umesema kweli kwani hii ipo sana na wengi sana wanasahau kwao na wapo wale wanaojifanya kusahau kwao kwa makusudi au pia hawataki kwao. Ni ushauri mzuri sana huu kuandika wapi unatoka, wewe ni nani nk...ili baadae na wajukuu nao wataweza kujua na kwa mtindo huo hawataweza kuoana ndugu kwa ndugu ambayo ni mwiko kabisa---Ahsante sana kwa hili binafsi nilifanyia kazi .....jumamosi njema.

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

M3, hii si mara ya kwanza...ninaijua familia moja ambayo wameoana mtu na mpwawe. Fikiria kitandani wanaitanaje...Mume, Mjomba, mpwa?....mie sjui

Kimbembe kinakuja...
1..pale wadada na wakaka wa mwanamke wanapokuja kumtembelea.....wengine wanawita mke wa mjomba wengine Dada..na kwa wale wanaomwita dada wanashindwa kumuita mjomba wao shemeji :-(

2. Pale kaka na dada wa mume wanapokuja wanashindwa kusalimiana...wamitwe shemeji ama mpwa.

Thanks God kuwa ni wasukuma na ile salaam ya heshima hutawala ya 'engolo, eng'washi, eminza' inafunika hayo.

Ila wamezaa watoto bright kweli ng'wanawane manake wengine wanadai ati mkizaa ndugu kwa ndugu utapata watoto taahira...lol!

Mcharia said...

Hata mimi nusura yanikute.