Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, April 8, 2011

Je imani yako ni sawa na matendo yako?‘Nimeshukuru kuja kuniona, hali yangu ndio kama mnavyoiona, nimetumia kila dawa lakini sioni dalili ya kupona…labda ndio safari imefika, mliojaliwa kuniona sasa, huenda msinione tena…na…’ ilikuwa sauti ya Mzee mmoja ninayemjua, nilienda kumjua hali kwani nilisikia kuwa anaumwa sana , alikuwa na shinikizo likafikia kiharusi, na sasa kupooza , mkono na mguu wake ,hauna nguvu. Ni mzee ambaye nilimpenda sana kwa hekima na maneno yake ya kiimani.
Niliposikia maneno yake ya mwisho nilishikwa na butwaa, sikuamini kuwa yanatoka mdomoni mwake, nikaona niulizie ili nipate uhakika.
‘Unasema unataka kupelekwa kupata kikombe  kwa babu Loliondo, lakini huna pesa, za kukufikisha huko, nakumbuka mambo kama hayo siku za nyuma ulikuwa ukituasa, kuwa mungu tumuweke mbele, na yakuwa kama umejitahidi kutafuta dawa na hujapona, mkabidhi mungu wako , kwani kuumwa ni kafara la mazambi au sio…?’ nikauliza.
‘Ndio hivyo, lakini likikufika imanii inaponyoka, na hata ukisikia kuwa kuna dawa ambayo ukiipata utaponyoka ki-imani utatamani uipate…Unasikia sana kijana wangu, imani ni kazi nzito sana,  kwa sisi binadamu, hasa sisi kizazi cha sasa, imani ilikuwepo enzi hizo za watu walioishi na mitume ..sio sasa, kwanza hali zetu ni duni, pili mitihani ni mingi , na tatu imani zetu nii haba, …’ akaendeela kuelezea sana, lakini bado nilikwazika na kutaka kujua kama yeye anajua hivyo mbona anashindwaa kuikabili ile hali.
‘Nikukumbushe kisa kimoja  kijana wangu, kisa cha jamaa wa imani. Jamaa huyu alikuwa mcha mungu sana, na imani yake ilikuwa inakwenda sawa na matendo yake. Yeye alikuwa hasengenyi na kama atafika mahala akiongea kwa muda anaziba mdomo wake kabisa kwani anajua kuwa mkikaa sana kuongea lazima itafikia mahala mtaanza kuteta na kusengenya. Yeye alikuwa akienda dukani akipimiwa mchale au sukari, anahakikisha anapata sawa na kutokana na mizani, kwahiyo kama umempimia katika kibaba ukaongezea, anaiondoa ile nyongeza, anasema hiyo sio halali yake.
Huyu jamaa alikuwa mcha mungu wa matendo, kwani alikuwa na daftari lake ambalo anaandika upande mmoja matendo mema na upande mwingine matando mabaya kama alikosea , kwani kuna macho yanatamani, kuna msikio yanasikia ambayo hayatakiwi kusikika, kuna miguu iinatupeleka kusikofaa, kuna mikono inashika yasiyofaa kushikika, kwahiyo sio kazi rahisi kujikinga na makosa yote kwa siku, yote hayo aliyaweka kumbukumbu, ikifika jioni anaangali mahesabu na kama makosa yamezidi matendo mema, kesho yake anafunga na kutubu, na kama alimkosea mtu anakwenda kumuomba msamaha, hadi ahakikishe amesamehewa.
 Huyu ndiye mtu aliyejaliwa kii-mani, kwanza alimcha mungu wake kisawasawa, akamwamini na kumtii, halafu akawa amesimamia kimatendo kuthibitisha imani yake. Ili kuhakikisha hili, siku moja akiwa kwenye kikao cha maongezi ya kidini, akaja jamaa mmoja akikimbia akawasalimia na kawa haraka akamwambia yule jamaa ambaye kwa muda huo alikuwa akifundisha wenzake maswala ya kidini.
‘Mwalimu nyumbani kwako kuna moto na nyumba yako imeungua …sidhani kama utakuta kitu..’ akasema yule mtu, na mwalimi akatabasamu na kusema `sio kweli…’ halafu akaendelea kufundisha, na wale waliokuwa wakifundishwa wakawa na wasiwasi, lakini walipoona mwalimu wao bado anaendelea kufundisha wakadhania labda huyo jamaa aliyefika alikuwa na utani na mwalimu wao.
Mara akaja mtu wa pili na habari kama hiyohiyo, akasema moto huo ni mkubwa sana, umeunguza nyumba zote ikiwemo ya mwalimu, lakini mwalimu yule akasema kauli yake ile, ile kuwa `sio kweli’
Hawajakaa sawa, akatokea jamaa mwingine, yeye alipofika pale anapofundisha mwalimu huyo, akasimama kwa muda , alikuwa akimwangalia yule mwalimu anavyofundisha , halafau naye akakaaa kusikiliza lile somoa, na ghafala akaomba kuongea kidogo.
‘Mwalimu samahani, nimekuja na nilikuwa nikitafuta mwanya wa kukuelezea taarifa ya moto, ambao umetokea maeneo ya kwenu, nyumba zote zimeteketea, hutaamini, kama kulikuwa na yumba , watu karibu wote wapo hapo, lakini wewe sikukuona, wakati nyumba yako ipo maeneo ya hapo. Lakini mwalimu cha ajabu nyumba zote zimeungua ila ya kwako tu, imesalimika, nikajaiuliza sana wewe una kinga gani….’ Akasema yule mtu
‘Hiyo ni kweli, nyumba yangu haijaungua,…’ akasema mwalimu.
‘’Kwanini mwalimu kwanza umakataa kauli za watu wa mwanzo kuwa sio kweli nyumba yako haijaungua, lakini kauli hii ya mwisho umeikubali kwanini, na ulijuaje kuwa haijaungua?’ wakauliza wanafunzi.
‘Kwasababu naamini maneno ya imani niliyofundishwa, kuwa ukiomba kwa imani na kumuamini mungu kuwa yeye ndiye mlinzi, basi huna wasiwasi, najua kabisa atanilinda, na alichosema hakiwezi kuwa uwongo…mimi kila siku asubuhi nikiamuka namuomba mungu wangu na namkabidhi mali yangu yote katika ulinzi wake na naamini kwa dhati kuwa yeye ndiye mlinzi, hakuna mwingina anayeweza, hata kama nitaweka mlinzi mwenye bunduki, hawezi kunilindia kama mwenyezimungu. …, nakumbuka kabisa asubuhi nilimuomba mungu hivyo, …ndio maana sikukubali kabisa maneno ya watu wa awali,…kwasababu maneno ya munguu hayawezi kuwa ya uwongo.’ Akatulia halafu akamgeukia yule jamaa aliyeleta hiyo taarifa akamuuliza ` hebu tukuulize ilikuwaje huko?’ akasema mwalimu.
‘Moto ulianza  nyumba ya jirani, karibu na nyumba yako, ukateketeza nyumba zote za jirani, , na nyumba ile ilyoanza kuungua ilikuwa na sim-tank kubwa, likadondoka na yale maji yalimwagikia kwenye eneo lako, kukawa na bwawa la maji kwahiyo moto ukawa haukufika kwako, lakini nyumba zote za jirani ikiwemo hiyo yenye sim-tank hazipo tena, ni magofu matupu…
‘Sasa kijana wangu kuna nani mwenye imani kama hiyo hivi sasa?’ akauliza mgonjwa wetu tuliyekuja kumuona , akiwa kitandani , hajiwezi.
‘Hatujui, tulizania labda wewe unaweza ukawa, miongoni mwa wachache..’ nikamwambia, akatabasamu na kucheka, akasema, …`imani ya kufundisha, ni nyepesi sana, lakini imani ya kutenda ni ngumu kuliko unavyofikiria, …lakini sio kweli kuwa ni ngumu kihivyo, kwamba hatuwezi kuitekelezea, ila nyoyo zetu ni zaifu…kwasababu huenda tunasema mungu …lakini kiundani sana hatuna uhakika na mungu…,hebu kumbuka siku ile ya mabomu, ni nani alisimama akasema ngoja nimuombe mungu wangu kwanza anipe ulinzi wake, akasali kwanza…nasikia kuna ambao walikuwa kweye ibada walikatisha wakatimua mbio, kweli si kweli? …’ akasema na kuhema.
 Nikukumbushe yule kiongozi wa dini aliyekimbia makaburini, pale mtu katika jeneza alipotikisika, …alitikisika tu kwasababu hakuwekwa vizuri, basi watu wote akiwemo mkuu wa dini walikimbia, hebu jiulize kwanini walikimbia, hata kiongozi wa dini akatimua mbio…ina maana kweli watu hawapendi mtu huyo arudi tena duniani?, mbona walikuwa wakimlilia sana,…? sasa kazindukana, kafufuka, au kama ilivyokuwa siku ile,…watu wanakimbia, wanamkimbia mtu waliyekuwa wakimlilia...hebu jiulize kwanini?...imani zetu ni haba, imani zetu haziendani na matendo yetu….
 Hilii ni wazo tu la Ijumaa ya leo 


Ni mimi: emu-three

3 comments :

Malkiory Matiya said...

"Imani bila matendo" au "Matendo bila imani" kipi kimtangulie mwenzake hapa!

emu-three said...

Mkuu Malkiory mimi naona `imani inatangualia kwanza, baadaye vitendo!
Mfano niulize kidogo, unaweza kula kwanza ndio uhisi njaa, au unahisi njaa kwanza ndio ule...hisia inakuvuta kutenda, au sio, ...TUJADILIANE HILI WAKUU!

Yasinta Ngonyani said...

Hakika sijui tusema siku hisi IMANI zimekwisha au ndo ule mwisho wa dunia...imani