Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, March 15, 2011

Utangulizi-Dawa ya moto ni moto(blackmail)


Katika pita pita yangu nimekuatana na kisa ambacho nimeona kwa wapenda tamithilia na visa vya makosa ya jinai wanweza kukipenda. Mimi mwenyewe nilipokisikia kisa hiki sikuamini kuwa nchi kama Tanzania kunaweza kufanyika jambo kama hili. Kwasababu `kashifa’ hapa kweti ni kitu cha kawaida, na hazimgusi mtu kihasa, na kumfikisha kufanya jambo baya kama la kimauaji. Mtu anafumaniwa anaona kwake ni sifa, kwa kujikosha! Na vitu kama hivyo
Wakati natafakari hili, nikakumbuka kuwa bado tuna kisa cha Nani kama mama, ambacho nimekuwa nikisita kukiendeleza kwa sababu mbali mbali, ikiwemo ...ambazi zipo nje ya uwezo wangu. Lakini hata hivyo nilitaraji kuwa hicho kidogo ninachotoa siku moja moja kingekuwa na wachangiaji kadhaa. Nikagundua huenda ukiandika kisa kirefu sana kinachosha wapenzi na ukizingatia wengi hawapendi kusoma vitabu..., sasa nifanyaje! Nitajitahidi nikamilize kinamna, kwani maji ukishayafulia, huna budi kuyaoga!

Sasa nilipokutana na kisa hiki nikaona labda nibadilishe muelekeo niandike mfumo wa tamithilya. Hii nafikiri, itawafurahisha sana wapenzi wa blog hii, na hasa, wale wanaopenda visa vya mfumo wa tamithilya, …ni kisa kilitokea , kikafichwafichwa, na wadodosaji wakakinyaka, nami bila ajizi nikaamua kukifanyia kazi, na nilipokiingilia kiundani nikakuta kumbe haya mambo hata bongo yapo, …

`Kashifa ni mbaya sana, na mara nyingi ikimtokea mtu wa hali ya juu inakosesha usingizi na hata kuleta magonjwa ya shinikizo la damu. Hebu wewe fikiria una kazi yako nzuri, na una familia yako yenye stara, na usigependa jina lako na kazi yako iharibike. Anatokea mtu hohehahe, kwa lugha ya sasa tunamuita `mlalahoi’ anatishia kuonyesha uchafu wako uliotokea, ambao ukisambaa, kazi basi, heshima hakuna..na huenda ukafirisika kabisaa, utafanyeaje?

Kwa wenzetu wazungu, kadhia ya kashifa ambayo imegundulika na mtu , na matu huyo akataka kuitoa, lakini akasema ili nisiitoe basi tukubaliane kuwa sitaitoa na ushahidi nilio nao nitakupa kwa marejesho ya thamani fulani wanaita `blackmail’

Nikapitia mtandao wa wikipedia nikapata ufafanuzi huu, kuwa `Blackmail is the act of threatening to reveal substantially true information about a person to the public, a family member, or associates unless a demand is met. This information is usually of an embarrassing, socially damaging, and/or incriminating nature. As the information is substantially true, the act of revealing the information may not be criminal in its own right nor amount to a civil law defamation; it is the making of demands in exchange for withholding the information that is often considered a crime.’

Nilipotosheka na ufafanuzi huu, nikaanza kukusanya `ushahidi’ wa kisa hiki na nimeanza sehemu ya kwanza, ipo tayari kuweka hewani. Lakini je mtakuwa tayari kupokea taimithilya ambayo nahisi inaweza ikawa ndefu? Nimeuliza tu kutaka maoni, lakini inabidi nikitoe hiki kisa, ili kinisaidie mwenyewe katika harakati za kukusanya visa ambavyo vinaweza kunisaidia kutunga vitabu. Ni kisa cha kusisimua kwa kweli, tukisome kwa makini.

Nawashukuru sana wale wote ambao hawaachi kunitembelea hata katika hali ngumu, na hii imenipa faraja, kuwa labda na mimi naweza nikatunga kitu kikagusa nyoyo za watu. Najua kuna wengine hawataki iwe hivyo, wanataka iwe vile, lakini kwa visa kama hivi nataraji vinaweza kusaidia hata watoto, kwa mfano nimekuwa nikipendelea kutoa kisa na kuweka methali., au misemo ya kiswahili. Ukikisoma kisa vyema utagundua nini maana ya methali hiyo au msemo huo, hii itamsaidia mwanalugha, mwanafunzi au yoyote anayependa lugha ya Kiswahili kwa marejeo na ufafanuzi. Lakini hata hivyo nia yangu ni kutoa visa katika halisia yake.

Basi nawaombeni muwe tayari na kisa kipya cha `Dawa ya moto ni moto’ Huu ni msemo ambao mhusika mkuu aliutumia katika mkasa uliompata. Naombe tuwe pamoja
mimi: emu-three
Enhanced by Zemanta

14 comments :

samira said...

ni kweli usemayo samahani kuuliza vipi ile nani kama mama
tupo pamoja m3

Malkiory Matiya said...

Hahahahaha, Emu-three awali ya yote naomba ukanushe kuwa wewe si " dada Miriam"

Kuhusu wazo lako la kuandika kitabu kwa kufanya makusanyo wa simulizi zako ni jambo la maana sana. Juu ya watu kutochangia napenda nikutoe hofu, kubaliana na mimi usomaji na kuchangia ni mambo mawili tofauti, hivyo wewe endelea kufanya vitu vyako. Lengo ni kutoa elimu, hivyo mtu anaweza kusoma na pengine akakosa muda wa kuchangia mawazo,hilo lisikukatishe tamaa.

roger moore said...

Habari yako ndugu yangu emu-three mimi ni mpenzi sana wa blogyako maana mpaka nimeweka ktk simu yangu upande wa Bookmark kwani hata nikiwa kazini break nakuwa nasoma visa vyako.
Tuwache hayo mimi nilikuuwa nakuuliza kama unaweza najua unaweza kutokana na visa vyako hivi,kama mtu akakuomba umuandikie SCRIPT ya story ya movie yake au film documentary,ni hayp tu ndugu yangu.
mdau wako...Roger from UK.

Anonymous said...

Tatizo lako huwa humalizi story naona hata hii utaikata njiani. Ingawa una visa vizuri watu huwa wanapenda mtiririko ili kuleta ladha katika story sasa ikiwa kabla story moja haijesha umeleta nyingine watu tunaloose interest ndio maana hatucomment.

Kabla hujaleta hiki kisa malizia kila kisa cha mama na mtoto, mbona ni kisa kizuri sana! Hata kama una mpango wa kuandika kitabu baadae basi summarize ili utakapokuja kuandika kitabu ndio kiwe na maelezo marefu, lakini cha msingi wewe malizia kile kisa kisha watu tutasoma hiyo hadithi hizo siku za usoni otherwise nachelea kuwa wengi wetu tutaogopa kusoma hadithi au visa ambavyo tunajua hatutauona mwisho wake!

emu-three said...

Mkuu Malkiory hata mimi nimecheka sana, ila ukiwa mwandishi...nahisi kuwa wewe majina yote ni ya kwako, jinsia zote ni za kwako, kila kitu ni cha kwako,ni vyema ukubali yote.Ndivyo nilivyo mimi.
Wengine wananiita `mdada', mkaka, Miriam,...nani vile, kwangu safi kabisa, kwasababu ndio sifa ya mwandishi, .....
Mimi nafurahi kuitwa vyovyote vile mkuu!
Nashukuru sana mkuu kwa ushauri wako, umenipa moyo saana, kwani nilishakata tamaa nakuona huenda ninachoandika hakikidhi haja maridhawa. Ni kweli wengi wanasoma, na nshukuru nimeona watu wametumiana kwenye mitandao na mwisho wa siku nikatumiwa na mimi, kwani aliyetuma hakuandika imetoka wapi. Hii imenipa faraja kuwa kumbe kuna mawakala wazuri wa kusambara `ujumbe ' ili angalau kile kidogo mtu alichojaliwa kutoa kinawasaidia watu!
Shukurani mkuu na shukurani wapenzi wote wa blog hii.

Candy1 said...

Kama hakitomalizika hapa, basi endelea "kupigania" nafasi na muda pia wa kutoa hicho kisa kwenye kitabu...lakini hata hivyo, niko tayari na kisa cha Blackmail...tuone itakuwaje...

emu-three said...

Samira, Nani kama mama ipo inendelea, nilitingwa kiasi na kuna vitu nilikuwa naulizia kwa jamaa aliyenisimulia hiki kisa chenyewe, ...usiwe na wasi wasi kinaendelea, na kama wapenzi walivyosema wapo tayari hatua kwa hatua, basi nitakiendeleza kama kilivyotakiwa kiwe.
Kisa kimeingia hatua ya pili. Ukumbuke hatua iliyopita msimuliaji alikuwa mama anamsimulia mwanae, sasa kulitokea kitu, ...ikabidi simulizi hilo likatike, mtaona kwenye kisa,

emu-three said...

Kuhusu kuwa naweza kutengeneza 'script kwa ajili ya movie'(kutoka kwa Roger) .Mimi sioni ugumu wa kutengeneza kitu kama hicho, kwani movie ni kama hivyo visa.
Wewe nipe kisa unachotaka, au hiyo movie iweje, ya tukio gani, au kama unataka mimi nikubunie kisa, naweza...na hii labda tufanye nje ya pazia,(kwa kupitia e-mail) au kama unataka kiwe hewani kwangu haina mbaya.
Nashukuru sana kuwa umpenzi mzuri wa blog hii na umefikia hatua ya kuniamini kuwa naweza. Karibu sana!

emu-three said...

Kwanini nakatisha visa...labda niseme ukweli kuwa wakati naanzisha blog hii nilikuwa na dhamira ya kuifanya `Diary'...blog ya kumbukumbu, na nia iwe na visa vidogovidogo vyenye mafunzo.
Na hita hivyo hivi visa unavyosoma hapa ni matukio ambayo nimekutana nayo, au jamaa yangu yamempata, anaponisimulia mimi natengeneza kwa njia ya stori(kisa)
Kama ni dairy, basi kila siku nakutana na matukio, na matukio mengine hayastahili kucheleweshwa, yatakuwa hayana maana. Na matukio yalivyo, mengine ni kisa tosha kabisa.
Samhanini sana kwa kufanya hivyo, ila nahisi kama nitakuwa sitoi kisa kwa muda muafaka, nikija kukitoa baadaye naweza nikakosa hata `ushahidi'.
Ila wazo lako ni zuri na nashukuru sana kuwa wewe umekuwa `muwazi kwangu' napenda namna hiyo.
Naomebini sana, kila mtu akiona nafanya kinyume, animabie ili nami nijue jinsi ya kujirekebisha. Mimi ni `all for all'...
Nashukuru tena sana mpenzi wangu wa blog hii, usikate tamaa kwa vile nakatisha katisha...na kama kuna kisa nimekikatisha hakijakamilika nikumbushe nitakimalizia!

SIMON KITURURU said...

Mkuu naungana na wasemao usimaindi sana Comment kutokuwepo! Wengi tupo na tunafuatilia ingawa wakati mwingine hatukomenti sana kutokana na mambo tu mengine!


Na mimi ni miongoni mwa ambao mara nyingi hua twaanzaga kisa kutokea sehemu ya kwanza na kukifuatilia mpaka mwisho.

John Maembe. said...

Habari Em-3.
Mimi nimefikiria nimeona kuwa wazo langu kuhusu hii blog ni kwamba kwa kuwa visa na matukio mengine ni ya papo kwa hapo ni bora uendelee kufanya kama zamani yaani upo katikati ya kisa flani lakini unatupasha juu ya kisa fulani ambacho kinaendana na wakati tulikuwepo kama juzi ulivyotupa cha "Sema, Useme, Usiseme, Itakuwa_!" hii inaonyesha dhahiri kabisa kuwa ni jinsi gani unatujali wadau wako bila kusahau kutuachia ahadi ya kwamba utakimalizi kisa ambacho ulikiacha. Kwani vingine hadi kuvimalizia vinahitaji wahusika kukupa mrejesho ambazo ni sababu ya wewe kuwa nje ya uwezo wako.

Kuhusu hiyo Blackmail, mimi ni mmoja kati ya wadau ambao wamekubali kukianzishwa kwa hiko kisa (Tamthiliya) 7b mi ni mpenzi wa kusoma soma vitu vingi sitachoka hata kama itachukua mda mrefu kiasi gani, nakuhakikishia 2takuwa pamoja na nawaomba wadau wengine tujumuike pamoja.

Nakuunga mkono kuhusu swala la Uandishi na sifa nzuri ya uandishi ndio km uliyoielezea hapo awali kaza buti Mkuu tutafika tu, japokuwa kuna changamoto nyingi kwani nimeshakuwa na mawasiliano na waandishi wengi ambao nilikuwa mteja kwao kwa kutofanikisha kutoa sehemu ya pili ya kitabu au kukimalizia na walikuwa wakisema "Tunawapenda na kuwashukuru wateja wetu ambao mpo mstari wa mbele katika kusoma vitabu japo si Tanzanians wengi hawapendi kusoma vitabu, lakini kaka kinachotushinda sisi kuendelea au namna gani ni gharama za uchapishwaji wa kitabu pamoja na kulipia kiingie sokoni(Kudhibitishwa). Ndio sababu tunashindwa kuendelea" Hayo ndo yaliyobeba ujumbe wa waandishi wengi niliokwisha ongea nao. So, Mkuu usikate tamaa we fanya vitu vyako hata km utakutana nazo km hizi lakini "Jana tofauti na Leo"

Ahsante Sana na Kila la Kheri.

emu-three said...

Mkuu Kitururu, TUPO PAMOJA, wewe ni nugu yangu, na nahisi tunatokea kumoja, ...Nashukuru kwa nasaha zako:
Mpenzi wa blog hii Maembe, umenihamasisha sana, na kweli jana sio kama leo. Nakuomba ujisaili kama `mpenzi wa blog(followers) kwani wewe ni mmoja wa wapenzi wanaosoma na kuchangia kwa kiasi kikubwa. KARIBU SANA,
Na wengineo hasa wale wanaosoma na kufkisha ujumbe kwa wengine, nao nawashukuru sana.
NITAJITAHIDI KADRI NIWEZAVYO KUWAPA KILE ROHO INAPENDA,...
TUWE PAMOJA!

Yasinta Ngonyani said...

MMM! wala usiwe na wasiwasi we andika weka wasomaji tupo ingawa kuna wakati huwa nakabiriwa na mengi lakini usidhani kuwa sikusomi hapana hakuna hata moja mada uloandika sijasoma. KWA HIYO WEKA WEKA TUPO PAMOJA DAIMA.

emu-three said...

Dada Yasinta na wewe tena, wewe ni zaidi ya jirani wa kuombana chumvi..Niseme wewe ni ndugu yangu, TUPO PAMOJA, NSHUKURU SANA KUWA ALWAYS TUPO PAMOJA!