Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, February 4, 2011

`hali zote'...mambo kufa, kufaana!



Joto kali sana leo, nimewasha kiyoyozi cha gari lakini haisaidii kitu..’ huyu alikuwa bosi wangu akilalamika huku anaangalia kiyoyozi cha ofisi kuwa kinafanya kazi kweli, kipo kinafanya kazi lakini kutokana na joto lilivyo hapa Dar kilionekana kama hakipo. Nikakumbuka kuwa wenzetu huko Ulaya wanalaalmika na baridi, na sio baridi ile ya hapa kwetu , bali ni baridi ya barafu. Je hali kama hiyo ingetokea hapa kwetu ingekuwaje, maana umeme wa mgawo, labda magogo msituni yangeisha kwa kuchomwa mkaa


Ni kweli hapa Dar, sasa hivi kuna joto kali, na inachangiwa zaidi na ukosefuu wa miti, utashangaa ukipita sehemu za barabarani unakuta miti imekatwa, na huoni dalili ya miti mingine iliyopandwa ili ukikatwa mmoja unachipua mwingine, je kwa hali kama hii joto litakwisha kweli, Dar inageuka kuwa jangwa, na mijumba inahumuka kama uyoga. Hatukatai hayo ni manendeleo , lakini je tutaishia kuwa na viyoyozi mpaka mabarabarani. Na heri tunaodoea viyoyozi vya ofisini, ingawaje kiafya inatuathiri, kwani unatoka kwenye kiyoyozi ofisini unaingia kwenye tanuri la moto nyumbani kwako!

Niliwahi kutoa wazo kuwa ingekuwa jambo la muhimu serikali ikapitisha sheria kuwa kila kaya, kila nyumba lazima ipande miti angalau miwili kwa nyumba, kama hii ingepitishwa ungeona mabadiliko makubwa sana hapa Dar, lakini kama ujuavyo, huenda kitu kama hiki kinasubiri mfadhili, huenda mipango hii ipo, au inatakiwa iwe kama mradi Fulani…lakini joto lililopo hivi sasa lingetosha kutupa shule.

Hulka ya binadamu tulivyo ni kusahau, kipindi hiki cha joto, maswala ya watu kujenga bondeni ayansahaulika, watu wanajenga, watu wanauziwa maneo ambayo ni mapitio ya maji, na kwasababu mtu hujui na una shida ya eneo la kujenga unanunua , mvua zikianza ndio tunaanza kushituka, oooh, waliojenga mabondeni muondoke, ooh…kwasababu hatutaki kujifunza kutokana na mabdiliko ya hali ya hewa. Kipindi cha joto kitupe fundisho la kukabiliana na joto, kwa kuhakikisha kuwa mvua zikianza tunapanda miti kwa wingi, ili hata joto likiana tuna vivuli vya kujifichia.

‘Duuh, umeme umakatika, balaa gani hili…’bosi akainuka haraka toka kwenye kiti chake na kukimbilia nje akiwa na leso ya kufutia jasho, na bahati nzuri kuna miti imependwa hapoo karibu na ofisini, akawa anapata upepo wa asili, huku anajipepea na mkono wake, akisubiri jenerata liwashwe. Sisi watu wa hali zote tukawa tunamshangaa anavyopata taabu, hakuzoea hali kama hiyo masikini wa mungu! Mimi nikawaza kichwani, huyu kazoea kiyoyozi, toka nyumbani, garini hadi ofisini, lakini hebu rudi nyumba kwetu ambapo maisha yetu ni `hali zote’, kuna watoto wadogo ambao ukiwaangalia sasa hivi utawaonea Huruma, mwili umejaa vipele vya joto…hawa wataishije, au ndio wakomae ili wawe `hali zote’ kama wazazi wao? Labda ndio maana umeme unakatika kama mataa ya barabarani, ili tuzoee hali zote, na aheri ingekuwa kama mataa ya barabarani ungeshukuru, kwani hayo yanawaka kwa muda maalumu, lakini umeme wetu unakatika mchana kutwa!

Jamaa yangu anasema kuna siku kapata hasara ya nyama, alinunua kwa ajili ya shughuli yake, akaweka kwenye jokofu, umeme ukawa haupo siku nzima, alipoichukua kesho yake, haitamaniki…ikawa hasara! Je tunajifunza nini na tatizo la umeme kipindi hiki cha shida, ili tujiandae kwa baaadaye, je ina maana hatuna utaalamu(wataalamu) wa kugundua njia mbadala, badala ya kutegemea `mvua’. Kwani hayo maji hayawezi kuvutwa na bomba toka sehemu nyingine, ili kujaza kina cha hilo `bwawa’ nimewaza sana kuhusu hili, lakini nikajisema huenda kwa vile mimi sio mtaalamu wa mambo hayo, basi najifikiria nianavyo tu…lakini mimi nina imana kuwa wataalamu wapo na wakiwezeshwa wataweza kupambana na hili tatizo, …lakini watawezeshwaje, wakati bajeti haitioshi…haitoshi kwa vitu kama hivyo, inatosha kwa magari ya wakubwa…Au? Nawaza tu mtoto wa `hali zote’

Kusahau ni hulka yetu wanadamu, maana kama tusingelikuwa tukisahau huenda hata akina mama wasingependa kujifungua tena. Lakini kuna mambo ambayo sio ya kusahau, kwa mfano sasa hivi mwavuli unaonekana ni takataka, nimekuta mwavuli mzuri tu upo jalalani, nikauliza hivi huu mbona bado unafaa kutumika…jibu ni kuwa wanini na joto lote hili. Tumesahau kuwa pindi siku zijazo, mvua zitaanza kunyesha, je tumejiandaaje na kukabiliana na mvua, au ki mawazo yetu ni kuwa, tusubiri siku ikifika itakutana na mambo yake, kwani hawo watengeneza mwavuli watapata wapi pesa, …maana mmmh,.. kufa ni, kufaana, …

Ni wazo tu la ijumaa,

Ni mimi: emu-three

8 comments :

Yasinta Ngonyani said...

Wazo la ijumaa hii si mbaya hata kidogo. Binadamu kwa kweli ni viumbe vya ajabu sana. Na pia haturidhiki na kitu/kila tulichonacho. Nachotaka kusema hapa ni kwamba wengine wanalalamika joto na wengine wanalalamika baridi na wengine mvua hakuna katikati. Na hilo la kukukata miti na bila kupanda tena kwa kweli ni mbaya mno, tukizingatia pia miti inatusaidia kupata pumzi sasa kama tunakata yote napata hisia baada ya muda tutashindwa kupumua na hvi jiji linavyozidi kupanuka.
Umeme hata mie naamini kuna wataalamu tena wengi tu wanaoweza kufanikisha kupata umeme wa maji na nadhani ingekuwa safi sana. Ila kwa sasa inaonekana ni muhimu gari la mkubwa na mtoto wa mkuwa kusoma shule nzuri....Kuna wakati naona aibu kwa kweli..mmm kaaazi kwelikweli ila tutafika tu!!!

malkiory said...

Poleni sana kwa joto. Ndiyo hali halisi ndugu matabaka sasa Tanzania ni kitu cha kawaida. Kama ulivyosema, kuna watu hawana habari na joto unalolizungumzia kwani air condition ni kuanzia nyumbani hadi ofisini. Isitoshe hata nyumba zao hazikosi kuwa swimming pool.

Isingekuwa kifo cha Sokoine, leo hii matabaka haya yasingekuwepo Tanzania. Mafisadi wa enzi hizo walimtoa roho kwa kuhofia kufilisiwa.

Simon Kitururu said...

Kwa BINADAMU kuna mambo ambayo sio ya kusahau! Na hili la joto lilitakiwa liwe fundisho kwetu kama la kuishi kwenye BARAFU lilivyofanya wenzetu wagundue vitu kibao kwa kuwa ilibidi.


Umeniwazisha sana MKUU!

Faith S Hilary said...

Kama ulivyosema nyinyi mnalalamika na joto, sisi huku tunaganda kabisa na baridi na poleni kwamba huo umeme pia unazidisha machungu. Natumai kwamba hayo matatizo ya umeme kutakuwa na suluhisho maana vitu vitakuwa haviendelei kabisa, tabu tupu

Rachel Siwa said...

mmmmhhhhh kazi kweli kweli,pole wangu maana nimekusoma vyema lakini nimekosa jibu!!!kweli Bongo tambalale ok ndiyo nyumbani!!

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Sitaki kuonekana kwamba nawasifia wazungu kiholela lakini jambo moja ambalo limewasaidia sana kuweza kuendesha mipango yao kwa ufasaha ni kupanga mipango yao kabla. Ukiangalia kwenye mikakati yao, tayari wanajua watakachokifanya baada ya miaka mitano ijayo. Yaweza kuwa ni kwenda kupanda mlima Kilimanjaro au kupumzika tu katika visiwa vya Zanzibar. Hata serikali zao zinajibidisha sana kufanya vivyo hivyo. Hakuna mambo ya kukurupuka na kuanza kuagiza mitambo mibovu ya kufua umeme wa dharura na upuuzi mwingine kama huu. Wanajaribu kutafuta masuluhisho ya kudumu kwa matatizo yao.

Suala la umeme tangu uhuru hadi leo hakuna kinachofanyika bali ni kubabaishana tu. Mpaka lini? Bado hatujawa siriazi na jinsi tunavyoendesha mambo yetu; na kama ambavyo nimekuwa nikisema mara nyingi, matatizo yetu mengi ni ya kujitakia tu! Cha kusikitisha ni kwamba wanaoumia zaidi ni walalahoi!

emuthree said...

Kweli mliyonena majirani zangu, nawashukuru kuwa tupo PAMOJA' na jukumu la ncho yetu ni sisi sote, hata ukiwa nje, kwenu ni kwenu.
Na nawashukuruni sana, kuwa hata kama upo wapi bado mna `uchungu' na nchi yenu, na nyie sauti zenu zinasikika kwa mbali zaidi, zaidi ya sisi tuliopo humu, tukila vumbi..
Kweli bongo ni tambarare..lenye vumbi..na hatujui humo ndani ya vumbi kuna nini...lakini wapo hawalioni hilo vumbi, na ukiongea unaweza ukazibwa mdomo na kuambiwa `mchochezi'...unawasumbua wakubwa wanakula vyao
Ni hayo wenzangu!

EDNA said...

Duuuh,Bongo noma ila ndio kwetu hatuna jinsi.