Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, January 3, 2011

Utangulizi wa kisa kifupi `mwenye kovu usidhani kapoa'


Karibuni tena baada ya mapumziko mafupi, natumai tutakuwa pamoja na niwaombe radhi kwa kuwa kimya kwa kipindi hiki cha sikukuu za mwaka mpya. Blog yenu inawapenda sana, na ipo nanyi wakati wote. Kwa kuwekana sawa tungependa kutoa utangulizi huu wa kisa kifupi cha mhanga wa kubakwa tulichotumiwa muda kidogo, karibuni sana. Na kisa chetu cha `aisifuye mvua' kinaendelea kama kawaida




Wanasema ukisema kwangu kunafuka moshi ujue kwa mwenzako kunawaka moto, na kwingine kunateketea kabisa. Baada ya kupokea kisa hiki, na kusikia matukio ya visa vingi kama hivyi nikaona nisiendelee kukishikilia hiki kisa, au kukiweka kapuni kama mtoaji alivyodai kuwa nimekiweka kisa chake kapuni.


Wakati mwingine unapokea kisa au kuhadithiwa kisa, ukajikuta unaogopa, hasa ukijua wahusika wapo na sio mbali wapo katika jiji hili na kisa kama hiki kilikuwa kama siri ya watu wachache, na ilifanywa hivi ili mama wa mtoto aliyebakwa asijue, na masikini mama huyu amefariki dunia kwa maradhi na hakuwahi kulijua hili.

Visa vya uabakaji vimekuwa vikitolewa mara kwa mara, na vinapotokea wengi wanakuwa hawaamini, na huishia kusema `hizo ni tamaa za wanaume…’. Lakini pake kisa kama hiki kinapotokea kwa mtu wake wa karibu ndipo anashituka na kusema `Jamani dunia hii imekwisha…tufanyee jamani…’mpaka tukio hilo litokee kwa mtu anayemjua ndipo unasadiki na ndivyo ilivyokea kwa kisa hiki kinachokuja hapa.

Nimeona nikitoe mapema, kabla hatujamalizia kisa chetu kinachoendelea cha `aisifuye mvua imemnyea, na kisa kile cha nani kama mama ambacho kinakuja karibuni’ na kama inawezekana tungelivitoa vyote sambamba, kama nafasi ingekuwepo, lakini sio rahisi kihivyo. Kisa hiki cha ushahidi wa ubakaji sio kirefu na sikutaka kukifanya kiwe kirefu kwani tumeshakutana na visa kama hivi kwenye visa vilivyotangulia,lakini kwa maombi ya mtu aliyekutwa na hili, na kwa matukio mengi yanayozidi kutokea tumeona tukitoe hewani.

Kisa hiki kina mafundisho kadhaa kama utakavyokiona mwenyewe, na usisome kama kujifurahisha tu, soma katikakati ya mistari utagundua nini kichochezi cha wimbi hili la ubakaji na huenda ukitaja sababu wengine watasema hapana, ni `tamaa za wanaume tu…’ hapana matukio kama haya yalikuwepo kabla lakini sasa utanadawazi unayaweka hadharani….nisawa ni tamaa, ni sawa ni kapanuka kwa utnadawazi nk, je hili linatosha, na nani wanaoumia sana? Je inatosha tu kufikiria hivyo, hakuna jema la kusaidia kuondoa hili linalofungamana na `utandawazi huu’?Na kwanini tusijaribu kuchukua tahadhari kwani najua sheria zipo, tunajua ubaya wa haya majambo na tunajifanya pia kuwa wacha mungu! Lakini bado yanatokea…changamoto kwetu wanajamii!

Kisa hiki nilipokisoma nikakumbuka siku moja nilipofika ufukweni nikakuta baba anaogoela na mabinti zake ambao wapo baleghe, vichupi na niliyoyaona pale, nikasema kweli `sasa tume-endelea, na uzungu umefika Bongo’ Ni kweli tamaa za kimwili zinatofautiana kati ya mtu na mtu, kuna ambao nafsi zao zinajua wazi kuwa huyu ni mtoto wangu hata iweje siwezi kuruhusu tamaa hizi kunitawala, kwani huyu ni binti yangu, huyu ni mwanangu, hata kama hujamzaa wewe , na huyu ana hekima na utambuzi na anaweza akakaa akaavyo na binti yake asijihisi lolote. Wapo hatukatai, lakini…

Lakini wapo wale marafiki wa ibilisi, huyu akiona paja, huyu akiona sehemu zinazostahili kufunikwa, huyu akihisi tu maumbile tofauti na yake keshaahthirika, na baya zaidi huyu ni mume au mke wa mtu. Hawa ni wagonjwa tupo nao, tunaishi nao, hatuwezi kuwatenga, na sio rahisi kuwajua. Lakini swali kubwa ni kwanini afikie kumtamani binti yake, au mtoto mdogo, au vyovyote iwavyo, kwanini afikie hadi kuathirika kwenye mabasi kwa kushikwa na mfadhaiko kwanini…hili swali tumeliuliza sana, na majibu ni ya mkato `ni tamaa tu za wanaume…’

Mimi katika kisa hiki nimejifunza kubwa kuwa mabinti zetu tuwe tunawapa tahadhari sana katika uvaaji wao, na sio jambo jema kuingia kwenye vyumba vya wanaume, au chumba cha wazazi hasa ikiwa ni binti na aliyepo humo ni baba, au hat wavulana kuingia kwenye chumba cha wazazi akiwemo humo ni mama, ingawaje visa vya wakina mama kufanya dhambi hizi ni vi chache ukilinganisha na akina baba , lakini tahdhari kabla ya hatari. Ulimwengu umerejea enzi za sodoma na gomara. Ulimwengu tunaousoma kwenye vitabu vitakatifu kuwa kulikuwa na kisa hiki na kile kibaya na kukatokea maangamizi umerejea kwa kasi kwenye kipindi chetu hiki, na ukichunguza sana, utaona ulimweng wetu huu umezidi….

Kuna mmoja kasema itafikia siku ya hukumu shetani atatukana kabisa kuwa yeye hakufikia hapo,hakutushawishi haya tuyafanya sasa hivi, hata yeye mwenyewe anashngaa, ina maana sisi wenyewe tumezidisha. Tahadharini kabla ya hatari. Karibuni kwenye kisa kifupi cha `Mwenye kovu usidhani kapoa’.

Ni mimi: emu-three
Enhanced by Zemanta

5 comments :

Anonymous said...

Mambo yameanza motomoto, mbona unachelewesha, twataka hicho kisa kwanza , hizi porojo baadaye...mmh, tumekumiss sana M3. WE LOVE YOU M3

mumyhery said...

hadithi njoo!!!

samira said...

love u m3 hope umefurahi na mapumziko vipi mkasa wa aisifuye mvua imemnyea inaendelea lini
happy new year

emuthree said...

I love u 2 Samira, hope u a doing fine! Karibu sana, kisa chetu kinaendelea, ila tukio hili lilinigusa sana nikaona niliweke hewani ili tupate mawazo ya watu, huenda katika kujadili lingeweza kupatiwa ufumbuzi.
Je fikiria kama ingekuwa wewe limekutokea ungechukua hatua gani?

samira said...

da yaani m3 nimeguswa sana nampa pole yalomfika katika ulimwengu huu hakuna imani
mungu akuzidishie imani nawewe m3ulotuandikia mkasa huu bila wewe tusingejuwa