Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeSaturday, January 8, 2011

Aisifuye mvua imemnyea-21

Maua alimwangalia mume wake kwa mshangao, akaangalia nje kama kuna watu , lakini ilikuwa bado mapema sana, hakukuwa na dalili yoyote ya watu, akageuka kumtizama mume wake ambaye alikuwa kachukua taulo anakimbilia bafuni. Akaamua amfuate hukohuko, na kumuuliza,


`hivi imekuwaje. Hebu niambie…’ akasema mke wangu akiwa kashika mdomo.

‘Mke wangu huyu mtu anayenifanya hivi anafikiri mimi niataogopa, hanitishi hata anifanyie vitimbwi gani mimi najua kama nikufa nitakufa kwa siku yangu, na hivi vitwimbwi vyao najua ni mazingaumbwe tu, watafanya watachoka, lakini mimi siogopi…’ docta akasema nakuingia bafuni na kujifungia huko. Alipofika bafuni kufungulia maji anakuta kinachotoka ni damu….’ Akaishika ile damu, akainusa, akapiga chafya sana, halafu akasogea na kuchukua chomo kilichowekea sabauni akachukua yale maji kidogo kwenye kile chombo akasema nitaenda kuyapima nihakikishe kuwa ni damu kweli au ni viini macho vyao.

‘Sasa nitaogaje, akajiuliza…’ wazo likamjia akamuita mkewe aje, na mkewe alikuja haraka akijua kuna tatizo limetokea, akamwambia unayaonaje haya maji. Mkewe akashangaa kusikia swali la namna hiyo, akayachota maji mkononi na kuyaangalia, akasema `mbona maji ya kawaida tu, mbona sioni kitu cha tofauti,Docta naye akayaangalia tena yeye mwenyewe akayaona yamerudia hali ya kawaida, akamwambia mkewe `tafadhali naomba unisubiri nioge. Akaoga haraka halafu akaongozana na mkewe hadi chumbani akawa anajifuta mwilini na lile taulo, na kila akijifuta anakuta taulo limejaa damu, akamwangalia mkewe ambaye likuwa akimwangali kwa mshangao.

‘Hebu niambie nini kinaendelea, maana sikuelewei, ‘ akauliza mke wake

‘Huoni chochote kwenye hili taulo’, akamuuliza tena mkewe, mkewe akaliangalia lile taulo na kusema mbona halina kitu ni safi kabisa, akaongezea kusema, `taulo hilo nimelifua jana safi kabisa, sio chafu…’ kwani mkewe alihisi kuwa mumewe analalamika kuwa taulo ni chafu.

‘Basi mke wangu nitakusimulia nikirudii kazini, usihofu, naona vinavyotokea hapa ni viini macho kutaka kunivuruga akili na macho yangu, sijatishika bado, wajaribu mengine, huyu anayetaka kutuchezea, naaendelee tu, lakini sitarudi nyuma…’ akaondoka zake.

Mkewe alibaki ameduwaa, mume wake alitoka wapi usiku na tena uchi, ina maana labda kaambiwa na hawa waganga wa kuondoa haya mashetani afanya hivyo, au kuna dawa zilitakiwa kutengenezwa mtu akiwa uchi. Haiwezekani, mume wake hawezi kamwe kufanya hivyo, sasa ni kitu gani kimetokea, au mume wake ana mambo ya chini kwa chini, na kwanini akamwita bafuni, kaoni nini cha ajabu…hapana lazima kuna kitu kinaendelea hapa, lazima awasiliane ni kiongozi wangu wa dini, huenda akagundua jambo lilojificha ambalo akiliwahi linaweza likatatutulia haya matatizo…,

‘lakini kwanini tuendelee kung’ang’ania kuishi kwenye nyumba yenye shida naman hii, nyumba haina amani, tangu turudi toka Ulaya ni matatizo, hata mtoto kachelewa kuzaliwa na inawezekana ni sababu ya hii nyumba…hapana, lazima nimshawish huyu mume tuuze hii nyumba tutafute nyingine. Wanaume wabishi jamani…’ akajikuta kuongea mwenyewe kama kachanganyikiwa.

Mara akasikia mtoto analia kwa sauti ya ajabu, akakimbilia ndani kuangalia, akamkuta mtoto ana joto kali sana, akatumia ujuzi wake wa matibabui kuishusha ile homa, lakini wapi, mtoto analia anachemka joto lipo juu, …akaona ampigie simu mwenzake, na bila kupoteza muda mwenzake akaja wakaona wamkimbize hospitali kwenye vipimo zaidi. Walipofika wakashangaa, mtoto hali yake safi kama kawaida anacheka,wakaangaliana machoni na kushindwa kuelewa nini kimemshusha homa yule mtoto. Wakarudi nyumbani.

Ilipofika usiku yule mtoto mkubwa akaanza kupiga makelele, kuwa mara kaona paka, mara kaona hiki, akawa kama mtu amepagawa, ikawa kuhangaika usiku kucha, na baada ya muda mipaka ikajaa juu ya bati inatembea utafikiri watu, kwani paka kama alivyo hana sauti akitembea juu ya bati, lakini sauti liyokuwa ikisikika hapo ni zaidi ya paka. Docta hasira zikampanda akachukua baruti zake akatoka nje na kuzifyatua juu ya bati. Ile mipaka ikakimbia na kukatulia kidogo, lakini mtoto akawa kama kachanganyikiwa ikawa hivyo hadi asubuhi, walipoamuka wakaona wamkimbize hospitali, na ajabu walipofika hospitalini mtoto alikuwa hana tatizo tena…

‘Hii sasa kali, nahisi hawa watu wanataka kushika pabaya,..’ akasema docta na akaona labda ampigie yule mtaalamau aliyemsaidia kusafisha hiyo nyumba na wadudu wabaya, lakini ikawa simu yake haipatikani. Akamuuliza mkewe anashauri nini, mkewe akamwambia waiuze ile nyumba watafute sehemu nyingine, kwani hakuna amani ..’

‘Hilo haliniingii akilini, kwasababu gani, kwani nyumba hii tumemdhulumu mtu, tumeiba, tumeipata kwa haki zote,kama kuna mtu kaona tumemdhulumu, kwanini haji hadharani tukaongea, kwanini iwe viini macho tu. Hilo bado sijaliafiki mke wangu, tukiogopa mambo kama haya, elimu yetu ya udakitari itakuwa haina maana kabisa…’ akakatishwa na sauti ya mngurumo mkubwa uliotetemesha nyumba, na sauti kama za panya zikilia kwa mfululizo, na hali hii ikawafaya watoto wapige makelele ya kilio.

‘Sikiliza mke wangu, mimi naona wewe uende ukakae kule kwa baba na mama kwa muda mimi nataka nipambene na hawa watu peke yangu, naona mkiwa humu mtanitia woga, haya ni mazingaumbwe na naona nyie mshaanza kuogopa.

`Sawa , mimi kwa usalama wa watoto tutaondoka, na sijui kama mimi nitarudi tena kwenye nyumba hii, hapana hali kama hii maana yeka nini..’ akasema mkewe akiondoka kutayarishwa nguo na vitu kwa ajili ya kuondoka kesho yake.

Ilipofika usiku kulikuwa kimya kwa muda, lakini baadaye Docta akajisikia vibaya sana, kitu kama homa,moyo kwenda mbio, akameza vidonge vya kutuliza maumivu. Ilichukua muda ile hali na baaadaye akashikwa na usingizi, ndani ya usingizi ikamtokea ile hali ya mwanzo,i ambayo hupenda kumtokea mara kwa mara, ile hali ya utotoni ya kuteswa na mama wa kambo, akawa anaamrishwa kama mtumwa, fanya hiki na huyo mtu anayemuamrisha ana umbo la kutisha, na kashika kiboko chenye moto, ukigoma unachapwa. Mara akaamrishwa aichukue kamba aitundike juu ya nguzo za paa, kuna sehemu iliyokuwa wazi akalazimishwa kupanda juu na kuifunga ile kamba na baadaye akaamrishwa kutengeneza kitanzi, na akaambiwa alete kiti, na kuamrishwa kupanda juu ya kiti karibu na ile kamba inayoninginia ikiwa na kitanzi, akaambiwa ajivike shingoni.

‘Haya huu ndio mwisho wa mateso yako, unakumbuka mateso yako ya tangu utotoni, unaona matatizo yanayokuandama ndani ya nyumba hii, nab ado yape mengine, dawa ni hicho kitanzi, kitanzi kitamaliza yote hayo, wewe unachotakiwa kufanya ni kukisukuma hicho kiti, kamba itafanye kazi yake…’ sauti ya kutisha ikamwamrisha

‘Haya sukuma kiti au nikuchape na hiki kiboko cha moto…’

‘Pale nilikuwa nikitetemeka kwa uwoga, kwani vile viboko sio mchezo, akikuchapa maumivu yake ni makali, lakini, kuna sautii nyingine ambayo hunijia kunipa matumaini hii naitambua kama sauti ya mama yangu mzazi, iliniomba sana nisifanye wanavyotaka hawa watu. Lakini ajabu sauti hiyo ilikuwa ikififia na kushindwa na sautii hii kali inayoniamrisha kuwa nisogeze kiti nimalizane na matatizo ya dunia.

Kwa mbali nikasikia sauti nyingine, hii nikaikumbuka kuwa ni sauti ya mke wangu, na hii ilikuwa ikija kwa kasi na hata baaadaye ikanidindua ndani ya ile hali kama ndoto…

‘Hapo rafiki yangu niligwaya, ina maana kweli nilitakiwa nijiue bila mwenyewe kupenda, na hili tendo likanifanya nianze kuwa na wasiwasi kwa mara ya kwanza. Na kutokana na ile hali mke wangu akasema hawezi kuondoka na kuniacha mwenyewe, kwani naweza kujimaliza mwenyewe, kwani yeye alishaamini kuwa nina dhamira ya kufanya hivyo, labda kutokana na mateso na matatizo yanayonitokea, nilijaribi kumshawishi aniamini lakini akawa hakubali.

‘Nimegundua kuwa unataka kujiua uniachie haya matatizo, una lakoo jambo, tangu jana, mara urudi uchi, mara unaona damu na sasa hii ni kubwa kuliko kutaka kujiua, hapana, hapa haachwi mtu, wewe na mimi mguu kwa mguu hadi kwa wazazi wetu. Huko tutajua moja…

‘Sasa rafiki yangu hayo ni baadhi ya mdhila ya hiyo nyumba. Nyumba niliyoigharamia sana, ni nyumba niliyoipenda kupita kiasi, lakini…..Inanifanya nichukue hatua ambayo sikuitegemea kabisa, na hatua ambayo nimeichukua ni kwa usalama wa familia yangu, sifanyi hivi eti kwa kuogopa hayo mashetani, kamwe siyaogopi, na bado sijakata tamaa, lazima nifanye jambo, lazima nijue nini kimejificha ndani ya mauzauza ya hii nyumba, nikigundua najua nitakuwa nimefanya jambo moja kubwa sana, lakini nahisi kuna kitu …..’ akakuna kichwa na kuangalia ndani ya laptop yake

‘Nahisi kuna vitu vimepandikizwa ndani ya nyumba ile, na ni aina ya mazingaumbwe, au sijui tuiiteje, hayo yananijia akilini hivyo, kwasababi yamenikuta mengi kuhusiana nah ii nyumba, na cha ajabu tukiondoka mle mambo huwa shwari kabisa. Mhh, ama kweli aisufuye mvua imemnyea….’ Alipofika hapo rafiki yangu akafunga komputa yake ndogo na kujiandaa kuondoka.

Nilimwangalia rafiki yangu yule ambaye alionekana kukonda kwa mawazo na hakuwa na raha kabisa, nikafikiri sana nimshauri nini.

‘Hivi uliwahi kukutana na yule mzee uliyeonana naye kwa mara kwanza, unakumbuka ulivyoanza kunielezea ulisema kuna mzee jirani, ulimuona karibu na hiyo nyumba, akasema anaijua hiyo nyumba vizuri, nafikiri anajua mengi kuhusina na hiyo nyumba na huenda ikaleta msaada fulani, lakini kwa ushauri mzuri uza hiyo nyumba, mengine yafuatiliea kama unapenda, hii ni kwausalama wa familia yako. Utulivu wa familia yako utakuwezesha kufanya mambo yako mengine ya maendeleo, pia hata wewe ukirudi nyumbani unahitaji utulivu wa akili na mwili pia, sasa unaishi sehemu ambayo huvipatai hivyo , nini maana yake...uza tafuta nyumba nyingine...' nikamshauri hivyo

‘Umeniambia jambo la maana ngoja nikamuone huyo mzee huenda kweli ndiye anayechezesha mazingaumbwe yake, nikigundua kuwa ni yeye nitamchukulia hatua na….

Rafiki yangu alitoka haraka na kuingia ndani ya gari lake, ‘…nitakuarifu nini kimetokea pindi nikionana …naye’

Akaondoka na hapo ikawa mwishoo wa mkasa huo kwa siku ile, mengine yalitokea baadaye nikawa nayapata kwa vipande vipande, na nategemea kuleta hitimisho ambali litakamilisha kisa chetu hiki .

Ahsanteni, na nashukuruni kwa uvumilivu na najua bado yapo maswali mengi kichwani mwenu, kama ilivyokuwa kwangu kabla sijapata `hitimisho’. Tuwe pamoja kwenye hitimisho, ambalo linaweza kukufanya ugundue kitu kuhusiana na majengo yanayotelekezwa na watu au viwanja…

Ni mimi: emu-three

6 comments :

Anonymous said...

m3 nakushukuru sana na nimepata funzo kwenye dunia yetu hii na mambo yapo m3 sijuwi itakuwaje maana mimi karibu nataka kuhamia kwenye nyumba ya mume wangu ambayo kanunuwa ilikuwa ya urithi
mmmhh naona bora nifanye duwa kwanza

Candy1 said...

Dah, I can't believe mwisho wa kisa hiki unakuja...yaani yaani I was enjoying this and I am sure mwisho wake pia utakua mzuri bila kusahau kisa kitakachokuja baadae...nipozzzz M3 ;-)

Anonymous said...

Kweli bado kuna maswali mengi yanahitaji majibu, kama utamalizia hapa utakuwa hujatutendea haki, eeeh, kwa mfano Docta atahama au hahami, ? nk

emu-three said...

Naona kabla hatujahitimisha nisikie maoni na maswali, ili hitimisho liweze kuyajibu na kutekeleza maoni yanahusiana na hiki kisa.
Karibuni sana!

elisa said...

mmh mimi nataka kujua hitimisho lake na alifanyeje kama alihama au kuna kitu alifanya ikasaidia kuondoa hayo madudu ???..!! duniani kuna mambo jamani..dah !

Anonymous said...

Twasubiri hiyo sehemu inayokuja, wengine tunaomba isiishe kwani utamu wake hauelezeki, lakini lazima kuna mwisho wake, twaomba usiwe wa kukatisha...lete safiii, hata kama inabidi uendeleze sio noma, ...au sio
Shukurani sana kwa kujitolea muda wako na kutuletea visa kama hivi, hatuna cha kukulipa, bali shukurani tu