Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, January 7, 2011

Aisifuye mvua imemnyea-20


 Docta anarudi toka Ulaya baada ya muda, je nini matokeo ya maisha ya Ulaya, na wamekuja na zawadi gani, je nini kitatokea katika maisha yao hapa nchini , ndani ya nyumba yenye vituko. Tuendelee na sehemu inayofuata.
                                              ***************************
                                                  ********************
                                                       *************
  Huko nje Docta na Maua walikaa miaka mitatu. Na wakabahatika kupata mtoto mmoja wa kiume. Mkataba ule ukaisha na wao wakaona wasiingie mkataba mwingine kwanza , wakaona ni vyema warejee nyumbani, ili familia ijue kwao kabla ya kurudi tena, kwa mpangilio wao waliona warudi nyumbani wake mwaka, halafu warudi tena Ulaya. Maua alikuwa na ujauzito wa mimba ya pili, kwahiyo familia ilikuwa ikikuua, na matarajio yakawa mengi ndani ya familia.


Maua kipindi alichokuwa huko Ulaya alijibidisha sana na masomo na alikuwa katika hatua nzuri ya masomo ya unesi, na matarajio yake ni kusomea udakitari wa kawaida. Na hili alilifanya kwa bidii kubwa sana , na hata Docta aligundua kuwa Maua ana akili za ziada, ila mwanzoni hakupata nafasi hiyo na ingeipata labda angekuwa mbali zaidi, na aliahidi kumuendeleza zaidi na zaidi hadi afikia malengo mazuri.

Docta alikuwa keshafungua zahanati yake huku nyumbani na aliona ampe mkewe nafasi ya kuhudumia kama muhusika mkuu, kwani Docta alikuwa kaajiriwa katika hospitali kuu ya taifa na hapo kwenye zahanati yake alikuwa akifika kwa masaa maalumu. Alimwamini mkewe kuisimamia ile zahanati yake na aliwaajiri madakiari wengine kuweza kuiendeleza na wateja walikuwa wengi japo ilikuwa mpya.

Waliporudi hapa Dar walifikia moja kwa moja kwenye nyumba yao, nyumba yao iliwahi kupangwa na mtu mmoja, mtu huyu alipanga kwa mkataba wa miaka miwili, lakini alikaa mwaka mmoja akaondoka, yeye alisema ameondoka kuhamia kwenye nyumba yake. Na kwahiyo wakati Docta wanarudi na familia yake waliikuta nyumba haina mtu. Na mimba ya Maua ailishafikisha miezi sita na bado alikuwa na nguvu za kufika kazini na kurudi nyumbani kwa kazi nyingine .

‘Maua mbona huna raha, tangu turudi umekuwa mtu wa hasirahasira. Nakikuambia kuwa hili usifanya unafanya, unatakiwa kutulia nyumbani shughuli za jamii mara leo kule kesho huku zitakuumiza, hawo hawajali afya yako…’ akamwambia mke wake lakini mkewe akiinuka nakuondoka. Docta akashangaa mabadiliko ya tabia ile, lakini moyoni akasema haya ni mambo ya kawaida ya uja uzito.

Walikaa hapo na miezi tisa ikapita hakuna cha mtoto, miezi kumi, kumi na moja, kumi mbili…Docta akachanganyikwa, cha ajabu kila wakienda hospitalini halionekani tatizo na inaonyesha kuwa mambo bado. Wazazi wao wakashauri Maua ahamie kwao ili na wao wawe karibu naye. Siku alipohamia kesho yake akajifungua Mtoto mkubwa na ikawa furaha kwa familia hii, kwani sasa wana watoto wawili.

‘Mume wangu mimi naona kuna tatizo kwenye nyumba yetu…’ akasema Maua baaday ya kujifungua

‘Tatizo gani , Maua, usiwe na imani potofu, hebu nipe sababu kubwa sana ya kuamini maneno yako…

‘Mume wangu mimi naona kuna tatizo kwenye nyumba yetu…’ maneno haya yalijirudiarudia kichwani yakawa kama wimbo , kila siku ikawa ndio chanzo cha mfarakano ndani ya nyumba, huanzia kwenye tatizo jingine na mwisho huishia kusingizia nyumba kuwa ina tatizo. Docta akajiuliza ina maana kweli nyumba kama nyumba ikawa ni tatizo, akawa haelewi akilini. Alimwangalia mke wake akihangaika na mtoto ambaye tangu arudi toka kwa wazazi alipojifungulia amekuwa akilia usiku kucha, na hata mtoto mkubwa amekuwa akiumwaumwa, tofauti na walipokuwa Ulaya. Docta hilo alilichukulia kama mabadiliko ya hali ya hewa tu. Hakuwa na imani nyingine kama alivyokuwa akifikiria mkewe.

‘Hizi ni imani mara nyingi huja na kupita, lakini…mmmh, nakumbuka huko nilipokuwa nikisoma mwanzoni kuna majumba yametelekezwa kwa imani hizihizi…mmmh, lakini wote ni binadamu, mkiamini inaitikia katika imani zenu, mimi siamini hayo, na nitaaminije wakati sioni mantiki yake…ok! ‘ Aliwaza na kuwazua bila jibu.

Siku hiyo alikuwa kachoka sana, akakimbilia kulala mapema, hata mke wake alipokuja chumbani alishangaa kumuona mume wake kalala mapema sio kawaida yake, akamuuliza unaumwa yeye akasema hapana nimechoka tu nimeona nilalae mapema, sina tatizo. Basi ilipofika saa nne za usiku , kile kivumbi cha mapaka kikaanza kazi yake juu ya bati, mara mlio kama wa bundi ukawa unasikia kwenye mti uliopo hapo nje. Docta akaona atoke nje na tochi yake yenye mwanga mkali.

Alipotoka nje akayakua hayo mapaka yamesimama karibu na mueleeko wa dirisha wanapolala. Cha ajabu licha ya kumuona na ile taa yenye mwanga mkali hayakushituka, yalikuwa yanamwangalia tu. Docta akayatizama, halafu akatoa simu yake yenye kamera ya video akayachukua picha na kuyaona yalivyomokodolea macho hata bila kuogopa.

‘Hawa wadudu wa ajabu kweli, hawaogopi, ni marafiki wa binadamu hawa, lakini hawajui kuwa wanatusumbua, eti watu wanasema ni wanga, paka awe mwanga, hivi wenzangu wanafikiria nini akilini mwao, paka, mnyama…hebu niwasogelee nione watakimbia…akawasogelea lakini walisimama vile vile.

Aliyatizama moja baada ya jingine kwa kutumia kamera ya video, halafu akachukua kitu kama baruti, inayotoa mlio na cheche za moto akirusha katikati ya yale mapaka, ule mlipuko na moto, uliwashitua wale mapaka yakaruka huku na kule kukimbia, Docta akacheka na kusema kumbe na nyie waoga, akaingia ndani na kupitiwa na usingizi.

‘Ilikuwa kama njozi, ambayo hunitokea mara kwa mara nikajikuta naamuka kitandani nakutoka nje palepale yalipokuwa yamesimama yale mapaka, na nikayakuta yamerudi na kusimama pale pale, na ilionekana paka mmoja kaumia, yaliponiona mengine yakawa kama yanaondoka, lakini mengine yalismama pale pale. Mara nikajisiskia kitu kama kizunguzungu, na giza likatanda usoni, na nikajikuta kama napaishwa na mara na nikadondoshwa sehemu yenye majani, na akili ilivyonirudia nikjikuta sehemu ambayo nakumbuka niliwahi kufika kabla, nilitizama huku na kule na kumbe ni makaburini. ..’ alisema Docta

‘Nakumbuka niliwahi kuchukuliwa hivihivi kinjozi, na Safari ya mwanzo nilipofika hapa nakumbuka sikuweza kabisa kujigeuza, na ilikuwa kama hisia, lakini safari hii nilijiona katika hali ya kweli, hali ambayo niliweza kujigeuza na hata kuinuka na kukaa, lakini…sikuona watu.Nikajaribu kuangalia huku na kule, lakini kulikuwa na ukimya wa ajabu. Lakini kabla sijaamua lolote mara nikasikia upepo ukivuma na ulipotulia nikasikia sauti za watu ambazo sikuwaweza kuona uelekeo wa zinapotokea!.

‘Tumfanye nini huyu mtu…’ , sauti moja akasema

‘Tumuue tunywe damu yake, nyingine ikasema’ na kelele za mingurumo na vicheko visivyoeleweka vikasikika.

‘Hapana, nimewaambia huyu ni mtu wangu, niachieni mimi, yeye mwenyewe kama ana kiburi atajimaliza kwa mikono yake mwenyewe, nilimwambia auze ile nyumba, atafute sehemu nyingine, hajasikia, hajui nini kitamwandama, yeye na familia yake hawatapata raha kwenye hiyo nyumba, kama anavyoteseka mwana wa familia hii naye ataishia hukohuko, mwanetu katusaliti nini adhabu yake…sasa mwacheni huyu, mwacheni….!’ Sauti ya kicheko ikasikia, na kukawa kimya.

Kimiya kile kilimifanya nizinduke kiakili, na mara nikajiona nipo katika hali ya kawaida, lakini nipo porini, nipo …oh nipo makaubirini. Docta akaendeela kuongea. Nilishituka nakugundua kuwa sasa sio ndoto, ila ni kweli tupu. Nikaangaza macho huku na kule, lakini sikuona kitu zaidi ya wadudu wa usiku, mipaka na mandege ya ajabu ya kiruka huku na kule. Nikaangalia pale nilipokuwa nimelala, ni kwenye majani, nilipojiangalia mwenyewe, nikashngaa, nilikuwa uchi , uchi kabisa, bila nguo. Mungu wangu nitafanyaje, sina simu kama ningempigia mke wangu au jamaa yangu aniletee nguo, ..

Nikafikiri haraka, nikijua muda ule bado ni alifajiri, watu hawajaamuka, nikakurupuka mbio kama mwizi, nikaelelekea eneo la nyumba yangu, ilikuwa sio mbali sana na kwangu, nilipofika nikatizama mlindi nikamkuta bado kalala, nikaingia taratibu hadi mlango wa kuingilia ndani nikakuta upo wazi nikafungua na kuingia ndani. Nikatembea taratibu kuelekea chumbani kwangu.

‘Baba nanihii unatoka wapi saizi ukiwa uchi namna hiyo, usiniambie na wewe……

*******Jamani naona kwa leo tuishie hapa, nilidhani nitakikimbiza hiki kisa leo tufikie karibu na mwisho lakini mambo bado mazito. Je Docta kageuka mwanga…mkewe anashangaa, mume yupo uchi kama alivyozaliwa, kuna nini? Na je Docta atachukua hatua gani ? Tuendelee kuwemo, na nawaomba msichoke

Ni mimi: emu-three

9 comments :

Anonymous said...

Nani achokee wewe kuna mtu anachoka kulmba asali...mmh, lakini hii mpya, mtu anarudi uchi...hii kweli ipo?? lakini wanga sio mchezo, hama docta, watakufanya vibaya!

elisa said...

haya sasa..mi nasubiri mwisho wake tu

emuthree said...

Msijali wanasema ukiyafulia maji nguo utayaoga tu...msikonde wala kupungua uzito mwisho wa kisa hiki wakaribia soon!

Pamela said...

dr wangu aache ubishi ahame tuu maisha gani ya mashaka hayo

Anonymous said...

Sasa Dr kapatikana na ubishi wake.
Jamani jamani, mapepo haya, nikweli nyumba nyingi utakuta mke na mme vurugu kila siku mme mkali kupita kiasi au mke mkali kwa mme kupta kiasi, mpata unajiuliza kulikoni?

Huenda hiyo nyumba utakuta ni mawakala wa shetani (labda mmoja wapo anaenda kwa shongoma, au wote) lazima nyumba iwe na vurugu.

Au kama hiyo nyumba ya Dr. aliyonunua kumbe ina mapepo.

jaman wadau, M3 anatupa somo nzuri sana ktk maisha yetu haya. Hili ni fumbo lenye fundisho kubwa.

Tuwe makini na hivi vitu, ktk jamii hii tunaoyoishi vipo.

Tunatakiwa tusali sana kwa imani. MUNGU pekee ndio MKOMBOZI wetu.

Ubishi nao sio mzuri, mfupa uliomshinda fisi je wewe binadamu utaoweza?

BN

Faith S Hilary said...

Pamela na Anonymous yaani you couldn't be any more right. Docta mbishi huyuuuu!!! hahahaha! yeye chochote kile haamini, anaona sasa!!! shauri yake, asije akazushiwa kawa kama Tiger Woods hehehehe!...mi nipo

Albert Kissima said...

Dockta mwenye pamoja na maswahibu yoooote hachoki, mimi ntachokaje! Hapa till being understood!

Simon Kitururu said...

Mkuu nakusoma usione kimya ukafikiri .........!:-(

EDNA said...

Jamani Dr ubishi sio mzuri,ila haya mambo omba uyasikie tu kwa mwenzio yakikukuta ni balaa....Mmmmmh Mungu na atuepushe.