Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeThursday, January 6, 2011

Aisifuye mvua imemnyea-19

Docta akakuna kichwa na akilini akawaza mengi, …hivi kweli upo uwezekano huo, kama uwezekana huo upo kwanini nisimuoe yule binti mrembo, …haiwekani, na…kweli … mmmh, anavutia…lakini hapana kama rafiki yangu alifikia kuchemsha kwa huyo binti, sembuse mimi, …je mimi nisiyependa uhasma, nataka mtu aliyetulia kama Maua. Hapana yule sio aina yangu, aina yangi ni Maua …


Akamtizama Maua kwa makini halafu akasema haya yafutayo;

‘Maua, sitanii, wewe ndiwe c haguo langu naomba ulipokee hili kwa moyo mkunjufu, kama kweli unanipenda kama ninavyodhania, naomba unikubalie hili ombi langu, na ujue kuwa sitanii. Maua nakupenda sana, sizungumzi kiutani, naamanisha hivyo, nakuomba ukubali uwe mke wangu , na ukikubali hili nitakuwa na nafasi ya kukuelezea matarajio yangu, lakini naomba sana uwe huru moyoni mwako...!’ Docta akasema na kumshika Maua mkono wake na Maua akataka kukataa kukamatwa ule mkono, lakini hisia na mwili ukakataa na kujikuta anahisi kama kashikwa na umeme.

Maua akatabasamu na akajikuta unashika mkono wa Docta kwa nguvu halafu akauachia na kuinua mikono yake juu Mbinguni na kusema kwa nguvu.

`Ahsante Mungu wangu, hatimaye umesikia dua yangu, mimi kiumbe dhaifu, mimi nilijona sina mbele wala nyuma, hatimaye…’ akaanza kulia na akageuka kumwangalia Docta huku machozi yakiwa yamefunika mboni za macho yake na kusema kwa sauti

‘Nipo tayari kama kweli usemayo yanatoka moyoni mwako basi mimi nipo tayari kwa saa yoyote kuwa mke wako, hata mimi nakupenda Docta wangu, kama umaridhika na mimi na….basi nipo tayari hata sasa hivi tufunge ndoa, na sijui nitashukuru vipi kama unayosema ni kweli…Oh , Mungu wangu naomba iwe kweli…’ akageuka kuwaangalia wazazi wao ambao walikuwa wanawaangalia kwa furaha kubwa sana.

‘Maua wewe ni msichana mrembo, una tabia nzuri, na wewe ni chaguo langu, hata wazazi wamekubali hili, ila kuna mambo yametokea ya haraka na hili la ndoa limakuja harakaharaka, sikutaka nikuharakishe hivi, lakini nahisi yote ni matakwa ya muumba. Inabidi tufunge ndoa haraka, na ujiandae kwa safari ya kwenda Ulaya, na huko utasoma kama kawaida, nataka usome kama malengo yangu yalivyokuwa,

‘Je upo tayari kwa hili, ndoa ya haraka na safari ya haraka, natumaii upo tayari kwani sidhani kuwa una ndugu wa kukuzuia , , naomba sana unikubalie ombi langu ukiwa huru na usichukulie kuwa nimekulazimisha kwa njia yoyote ile, uwe huru moyoni mwako. Docta akatoa pete aliyokuwa kaiweka kwenye koti lake na kumuonyesha Maua, akasema,

‘Kama upo tayari, na unapenda kuwa mchumba wangu na hatimaye mke wangu, pete hii iwe shahidi wa tukio hili, ni pete niliyoinunua siku nyingi, na nilikuwa nasita kukukabidhi, lakini leo imetimia muda wake, je upo tayari nikuvike kidoleni mwako…’

Maua akaiangalia ile pete, akamwangalia Docta na kuhisi mwili ukisisimuka, akajisemea moyoni, mbona mambo haya yanakwenda haraka kupita matarajio, hapati hata muda wa kufuria moja, yanakuja mengine bora zaidi, akainua kidole chake na kumkabidhi Docta amvike hiyo pete. Docta akawaangalia wazee wao ambao nawo waliona Docta akiharakakissha mambo , lakini wakajua kuwa inabidi iwe hivyo, kwani safari ipo karibuni na muda ni mdogo na mabo ya kufanya yapo mengi

Docta akakishika kidole cha Maua na kukibusu kabla hajakivika pete, na baadaye akakivika pete, ambayo utafikiri alipima kidole chake kabla hajainunua. Maua bado alikuwa kashikwa na bumbuazi . Akakinyosha kidole chake huku anatabasamu , akiwa anamwangalia Docta kwa jicho la kutoamini halafu akajikuta machozi yakimtoka tena, hakujua kwanini, ni kwa ajili ya furaha au ni kwa kutoamini!

‘Nimekubali Docta wangu na chozi langu hili linalotoka ni ishara ya kutoakuamini hivyo, ni kitu ambacho kila siku nilkuwa nikikiwaza kuwa itokee kama hivi, nakupenda sana Docta wangu na naahidi nitakuwa mke mwema kwako …’akavaa ile pete vizuri, huku anaiangalia kidoleni, ni pete ya gharama sana, akawaza na baadaye akawageukia wazazi ambao bado walikuwa kimya, akahisi huenda hawakukubalian kwa hili kwani anakumbuka kuna siku aliwakuta wakiongelea swala la kumtafutia mtoto wa mchumba na wakawa wanapinga yeye kuolewa na mtoto wao, na huenda bado wa msimamo wao huo. Akasema moyo , kama hawapo razi basin a yeye hatakuwa radhi , ni bora ndoa tu isiwepo, akainua uso kuwaangalia kwa mashaka..

Aligutuka kusikia vigelegele vikitoka kwa mama , na baba naye akajiunga na wote wakamsogela Maua na kumpa mkono wa pongezi. Maua alimrukia mama na kumkumbatia , na baba akamshika mwanae mkono na kumwambia kuwa , azima yao imepata Baraka zao zote, na mipango mingine ianze mara moja kwani hakuna muda wa kupoteza.

Hutaamini yaliyotokea baadaye kwani mipango ya harusi ilianza kesho yake, Na Maua aliomba aende katika kituo chake alicholelewa kwani hapo ndipo alipopaona kama nyumbani kwake. Alipofika kituo alicholelewa na alimkuta mkuu wa kituo akiwa na wageni, lakini alipata muda wa kuongea naye na alipomuelezea hilo, yule mlezi hakuamini, na baadaye akamwahidi kuwa yeye atamwandalia kama mzazi wake, kwahiyo aende huko anapoishi akaage rasmi na kuja kukaa pale kwa muda, mpaka ndoa itakapopita. Yuile Mlezi wake au mwalimu wake , alikuwa na ugeni toka nje, walikuwja wafadhili wa kituo kile, na akaona aunganishe mambo yote pamoja, shughuli ya kuwakirimu wageni wake na harusi hiyo. Akakutana na watu wake wa karibu na wafadhili wake ambao walikubalina kuhakikisha harusi hiyo inakuwa ya aina yake.

‘Huyu ni mtoto wetu tumemulea wenyewe, basi tumuonyeshe kuwa tunamjali, ..’ wakasema wafadhili.

Na hayo yakiendelea hapo, Docta alikuwa akihangaika na vibali vya kusafiria alikuwa hajui kuwa wazazi wake walikuwa wakialika watu na kutayarisha harusi ambayo wao walishakuwa na mpangilio nayo siku nyingi na walitaka mtoto wao imkute kama mshangao. Na ndugu zake Docta walikuwa wapambe wakubwa wakuhangaika huku na kule kuhakikisha kuwa harusi hiyo inafanikiwa licha ya kuandalwia kwa muda mfupi.

Siku ya harusi ikafika Docta alikuwa katoka kwenda kukamilisha mambo ya safari, na alijua akirudi anatoka na wazazi wake na watu wachache kwenda kwenye nyumba ya ibada kufunga ndoa, hakujua kabisa kuwa kuna maandalizi makubwa yamefanywa na wazazi wake. Asubuhi ya siku hiyo, aliamuka kwenda kuchukua tiketi ya kusafiria aliporudi nyumbani alikuta watu wengi, hakuamini hilo, je ugeni huu ni waharusi yake, mbona hakumbuki kuwaalika. Hakutaka iwe shughuli kubwa sasa , lakini watu waliojaa mle kama ni kwa ajili ya harusi basi sio shughuli ndogo tena. Kwanini wazazi wameamua hivyo, hawajui watamkwamisha na gharama za kuwalisha hawa watu…

‘Watu walikuja kumlaki na kumpa mkono wa pongezi, mara huyu kaja mara huyu anampa pongezi , na alipofika ndani ikawa muda umekwenda, na akashangaa kumkura rafiki yake wa Sinza keshafika, alimwambia aje, lakini hakuwa na uhakika way eye kufika, na akahisi labda bado ana kinyongo naye.

Docta wa Sinza akamkaribia na kumshika mkono, akasalimiana naye kwa bashasha na kumpa pongezi nyingi na huku anamtania kuwa kaamua kufanya hivyo ili asije akazidiwa kete. Lakini Docta akamuelezea nini kimetokea na yakuwa yote ni Baraka za mungu, na wala sio kwa ajili ya ushindani. Wakacheka na kuingia ndani kujiandaa vyema. Waliulizana ni nanai atakuwa rafiki mwenza wa Maua, wakshindwa kuua hilo, wakasema kukisia kuwa huenda akawa Rozi.

Saa ikafika wakaelekea sehmu iliyotayarishwa ya kufunga ndoa, na kila hatua Docta alikuwa akishikwa na butwaa, hakujua hayo yote yameandalwia lini, na akawashukuru sana wazazi wake kwa hayo waliyomfanyia. Ndoa ikafungwa na kweli Maua alikuwa kamchukua Rozi kama rafiki mwenza wake. Na baada ya harusi wakaeleeka kwenye ukumbi ulioandaliwa na hapo walikuta wageni mashuhuri waliofika, wazungu wafadhili wa kituo cha kulelea watoto mayatima, pia walifika viongozi wa serikali. Docta aalijikuta akishikwa na mshangao mkubwa.

Wakati harusi ikiendelea rafiki yake alikuwa akimhadithia nini kimetokea kati yake na mpenzi wake. Docta wa Sinza alisema mwisho wake alikuja kukubali kuwa amchumbie yule msichana wake na wapo mbioni kufunga harusi , anasema anampenda yule msichana lakini ana makuu sana, anataka mambo ya urembo na mambo hayo ni gharama sana kwake, lakini wamekubaliana kuwa wataoana na mambo hayo yatakuwa yakijitegemea yenyewe, kuwa atakuwa na shughulli zake mwenyewe za urembo, na ayeye kama dakitari na kila mmoja atakuwa na mamlaka yake , asiingiliwe.

‘Hamuoni kuwa ndoa yenu itakuwa na matatizo kama mtawekeana mipaka ya namna hiyo’ akauliza Docta wangu.

‘Aaah, mimi najali, ilimradi tumekubaliana hayo, kwasababu unajua mimi nimetokea kwenye familia ya kiamsikini kabisa, na hawa ndio walioniwezesha, na …sio kwamba simpendi yule binti, nampenda lakini, familia zetu ni tofauti sana, na ndio maana nilimpenda Maua, kwani tusingetofautiana kimaisha. Lakini sasa hivi najua nini ninachokifanya, wanafikiri kuwa wataniburuza kwasababu ya utajiri wao, hilo halipo, nina malengo yangu muhimu. Ila nitajitahidi ndoa isivunjike, hilo naliahidi moyoni…’ Akasema Docta wa Sinza. Huku wanaingia ukumbini na kulakiwa na vifijo vya kiharusi,

Harusi ya Docta wangu ilifana sana, na ilikuwa kati ya harusi zilizoacha gumzo la aina yake, kwani wengi hawakuamini Docta kama yule kuja kumuioa yule binti. Na wasicha wengi waliokuwa wakimmezea Docta mate waliishia kubeza kuwa Docta hajui kuchagua, lakini ikawa, `walisema hataolewa mbona kaolewa’

Ndoa ikafungwa na Docta wakakamilisha taratibu za kusafiri, na baadaye ndiyo ikawa hii safari ya kwenda nje.

******* Je nini kitaendeela baada ya hapo

Ni mimi: emu-three

5 comments :

elisa said...

Mmmh haya asante basi M3..yaani kila nikimaliza kusoma natamani sana kujua kitakachoendelea

Anonymous said...

Kweli M3 unanikuna pale ninapowashwa, sijui nikuambie nini unielewe, lakini najua umenielewa, sina cha kukupa zaidi ya Ahsante sana. TWASUBIRI MUENDELEZO YAKHE, USICHELEWESHE SAANAH

John Mwaipopo said...

makala zimeenda shule

Anonymous said...

Mmmmmmmmmmh! M3 hii nimeipenda sana hii, leo. Hapa ndio ule usemi unadhihilisha kuwa PENZI halichagui. Umri, utajiri au maskini.

Thx M3. BIG UP

BN

Candy1 said...

kwahiyo mwisho bado sio? maana kama hapa ingekuwa mwisho basi ningeporomosha maswali kibao kwasababu kisa hiki kimekuwa kirefu na almost mtu unaanza kusahau yale ya mwanzo ila mimi sijasahau M3...kwahiyo hehe, usiache hata kitu kidogo...safari ya ulayaaaaa....mi nipo as usual! x