Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, December 14, 2010

`Nani kama mama' inakuja upya


 Kutokana na maombi ya wapenzi wengi wa blog hii, tumeonelea tukirudishe kile kisa cha `NANI KAMA MAMA’ Kwa undani zaidi na kwa ubora wake. Nakumbuka tulikikatisha kwasabau kadhaa, na moja ni kuwa ilikuwa sijapata sehemu ya kujishikiza, na nikawa nakileta moja kwa moja kutoka kwenye intenet café, kwa ufupi na bila sikuwa naweza kukipitia kwa marekebisho ya hapa na pale!


Aidha, nimegundua kuwa sasa nina wapenzi ambao wanaopendelea kusoma hivi visa, na hawachoki kusoma visa hivi kwa urefu! Na kwahiyo basi ili kukitoa kisa hiki kwa urefu na ubora wake, nikagundua kuwa ndani ya kisa hiki kuna tatizo moja ambalo ni ugonjwai! Ni ugonjwa unaojulikana kitaalamu kama `amnesia’

Amnesia ni ugonjwa unaotokana na kukatika kwa kumbukumbu zako za nyuma kwa ghafla, na kusahau kabisa kuwa wewe ni nani na umetoka wapi, na unachoweza kukumbuka ni hapo ulipo, yaani kama vile unazaliwa upya. Inaweza ikatokea kwasababu mbali mbali,ikiwemo kupata mshituko, kugongwa kichwa, au kutatizwa na janga Fulani, kama vile mtu kazama maji kwa muda mrefu na matatizo mengine mengi.

Kisa hiki `nani kama mama’ kitaangaza hili pamoja na mazila wanayopata akina mama, sio tu kutokana na mfumo dume, bali pia, hata kutokana na ubinfasi wa nafsi na roho mbaya miongoni mwa akina mama wenyewe! Hutaamini haya lakini yapo na akina mama wenyewe wataliunga mkono hili!

Je mama yako mzazi anaweza akasahau machungu ya uzazi ageuka kuwa adui yako? Ni jambo lisilokuja akilini, na wenye roho pupa hukingiwa na mitihani hii na mwisho wa siku hujuta, lakini kwa wale wenye kutafakari wakijua kuwa kila jambo hutokea ili iwe sababu, na sababu hiyo huleta fundisho kwetu! Hujenga moyo wa subira, na kumuomba mola, na mwisho wa siku faraja huja kwao. Subira katika maisha ni kitu muhimu sana, ukizingatia kuwa dunia hii imejaa mitego ya kimaisha ya hapa na pale, kuna kupanda na kushuka, kuna raha na mchungu, yote ni kwa ajili yetu sisi binadamu!

Kisa hiki ni mfululizo wa hisia zenye kutoa machozi, lakini ni fundisho katika jamii zetu, Tumeona huko kanda za juu watu hudiriki kuwaua wazee kwasababu za imani haba, swali la kujiuliza akilini ni je hawa wanaoitwa wachawi kwanini wawe ni wazee tu, na utasikia sifa au dalili za watu hawa ni mabadiliko ya kimaumbile, mfano macho kugeuka rangi, nk,. Hili ukichunguza sana utaona hutokana na adui ujinga, na rafiki yake `umasikini’ kama tungelisoma kuwa mtu anavyokuwa kutoka ujana kwenda uzee, maumbile nayo hubadilika, ikiwemo macho. Na akili nazo hubadilika na utawakuta wazee wengine hufanya mambo yasiyo ya kawaida, ni kutokana na kuchoka kwa akili.maisha magumu , na kutokujaliwa kwa wazee wetu hawa! Hakuna utaratibu bora wa kuwaenzi hawa wazee, zaidi ya jamaa zake, na jamaa zake ndio hawo wanawageuka na kuwaita wachawi…jamani ndio malipo ya wazee hawa?

Kuna methali ya kipare inasema `kidere usimseke isagho, ambu yavyo na mtondo washoghola(Jani linalochipukia la mgomba lisimcheke jani la mgomba lililokauka, kwani ni kesho na keshokutwa nawe utakauka )! Ni swala la muda tu!

Natumai sitakuwa nimewachosha kwa kukirudia kisa hicho upya , na kukiendeleza, na natumai tutakuwa pamoja. Karibuni sana! Tuombeane uzima na majaliwa ya sehemu ya kuijishikiza!

JE MPO TAYARI AU MWATAKA VISA VIPYA?

Ni mimi: emu-three

11 comments :

EDNA said...

Lete lete mambo

Anonymous said...

Kuna mtu anakaribishwa chakula akatae, na chakula yenyewe ni ile moyo inapenda...tuletee huo uhondo M3, MENGINE MOLA ATAKULIPA

SIMON KITURURU said...

Lete utamu Mkuu!

Malkiory Matiya said...

Natamani vile ungefanya collection ya visa hivyo na kuviweka ndani ya kitabu na kukisambaza kwenye maktaba ili iwafikie wasomaji wengi.

Candy1 said...

kwa sisi ambao hatukuona ilivyoanza basi kopi na pesti au weka link tuanze mwanzo ili inogeeee, mi nipo tayari M3 - Bring it on! hehe

elisa said...

M3 tunashukuru sana kwa msaada wako ..! Ndio unatusaidia , hivi visa vinatufundisha mengi yanatokea kwenye maisha yetu ya kila siku, ; ila mimi nilikua na ombi kwa nini tusimalizie kwanza ile ya ''aisifuye mvua imemnyea '' ili tusiache tena viporo ?
Na mimi nakumbuka kuna kisa tena ambacho hukukimaliza,ngoja nikumbuke..

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

Em3, unauliza ndevu kwa osama?leta mambo banaaa!

Anonymous said...

Please, hurry up!

Jane said...

Nashukru sana kwa kuleta tena hiki kisa, kuanzia mwanzo. Na ninashukru kwa kuwa unapitia comment za watu na kujua wanataka nini. Mungu akupe uzima na afya njema na akujalie hapo pasiwe pa kujishikiza tu bali pawe pako pa kudumu. Ikiwa ni pamoja na ungezeko lako la mshahara wote tuseme AMEN. Kweli watu wangekuwa wanajua thamani ya hawa wazee kusingekuwapo na mauaji ya vikongwe kama ilivyo sasa, huwa natamani babangu angekuwepo na kushuhudia mafanikio yangu ambayo yameshababishwa na yeye. Mmmmmh! ngoja niishie hapa maana naongea utafikiri naleta kisa kingine. tupe mambo M3.

Anonymous said...

Hiyo methali kuna ya kiwswahili chake? Hebu unaitamkaje ...mmmh mambo ya lugha bwana, lakini tafsiri yake imekaa vyema, ukiwa kijana usifikiri utadumu kijana, lzima siku utaitwa baba, na hatimaye babu, kwahiyo maandalizi mazuri yaanzie ujanani, adamu busara na hekima ukizeeka...ndio lazima tuzeeke!

Yasinta Ngonyani said...

Mmm! mpaka utuulize? we leta si unajua chochote kiletwacho mezani kinaliwa.....