Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeWednesday, December 22, 2010

Aisifuye mvua imemnyea-15

‘Una maana gani kusema hivyo Docta..’ akauliza kwa makini na kuishikilia simu vyema masikioni, na akili sasa ikawa imetulia kusikiliza kinachoongelewa kwenye simu, kabla hajapata jibu, mlango wa nje ukagongwa, na hiyo sauti ilimshitua hadi akadondosha simu, …akasikia tena mlango ukigongwa, akaikota simu haraka, huku anasikia Docta, akisema `halloh, halloh…’ lakini aliogopa kumjibu, akairudishia sehemu yake na kukimbilia kufungua mlango!


                 *******Je iliendeleaje, karibu tuwe tuendelee na sehemu nyingine ya kisa hiki********

                                                                **********

Ilikuwa asubuhi sana dakitari wa Sinza akawa na kimuhe muhe cha kusikia kauli ya Maua, alidamka isivyo kawaida akajiandaa kwenda kazini, lakini akaona apitie nyumbani kwa akina Maua kwani anajua kila alifairi wanaamuka kufuatilia maziwa. Aliharakisha na kuondoka, na kweli alipofika karibu na geti la mlango wa nyumba ile akakuta unafunguliwa na Maua atatokeza na chombo cha kubebea maziwa. Aliendesha gari lake hadi karibu yake.

‘Maua ingia nikusogeze, nimepitia njia hii leo’ akasema huku anachungulia dirishani

Maua alishangaa, na hakubisha akaingia ndani ya gari, na wakati linaondoka akawa anashindwa nini atamjibu huyu mtu, kweli anataka kuolewa , lakini kuna shule, na pia alihitaji muda wa kuongea na Docta wake. Akasema hawezi kuitupa bahati ya kusoma, lakini pi akuolewa ni muhimu. Sasa nimjibuje huyu mtu…mbona bahati zinakuja kwa mitihani ya namna hii, akawaza na kumuomba Mungu amsaidie asikose hizo bahati!

‘Vipi Maua natumai umefikiria ombi langu kwa makini, na mimi nataka kama ikiwezekana tufunge ndoa haraka iwezekanavyo, au anasemaje…’ akamgeukia kumwangalia.

‘Haraka hivyo, haiwezekani, kwanza hujanijua vyema, licha ya mimi kuonana nawe mara chache sana, pia nahitaji muda wa kutafakari hilo ombi …’ akasema na kutizama nje.

‘Mimi nimeshakujua vya kutosha, sina shaka na hilo, shaka ni wewe tu kukubali, na siku hizi kupata mume wa kukuoa ni …lakinii sawa, nitakupitia mchana mara moja tutaongea zaidi, nina nafasi mchana, usijali mimi sina nia mbaya kwako, wewe uwe na amani kabisa, …’ akasema huku anasimamisha gari, kwani eneo wanapochukulia maziwa lilikuwa sio mbali sana. Maua akashuka na kumshukuru Docta wa Sinza akaondoa gari kuwahi kazini.

Ilikuwa saa mbili Docta wangu hajaonekana , ikawa kila mtu anajiuliza huyu Docta vipi, jana mwenyewe kaahidi kuwa atafika asubuhi sana , lakini kimya kuna nini. Maua akawaza na kuwa na wasiwasi huenda kuna jambo limetokea, akatamani kuwaambia wazazi wampigie simu Docta wake, lakini akaogopa kuwa ataambiwa ana kimuhemuhe. Lakini mbona Docta wangu hajapiga simu kuwaarifu kuwa kuna tatizo!

‘Kama ana zarura ana simu yetu mbona hajatupigia, hawa watu sio wakuaminika sana. Unasikia Maua, hatuna nia mbaya na wewe, hapa ni kwako, kama asipokuja wewe utaendelea kukaa hapa tu, na huenda ukapata mume mzuri wa kukuoa, …’ akasema baba mwenye nyumba.

Maua alitamani kuwaambia kuwa keshapata mtu ambaye kaahidi kumuoa, hilo halina shaka, lakini akanyamaza kimya,akijua hayo yana muda wake, sio leo… huku akiwaza nini kimempata Docta wake. Akasema moyoni, huenda alikuwa anadanganywa tu , na Docta wa Sinza akija ni bora amkubalie ajue moja kuwa anajiandaa kuolewa. Akaanza kurudisha vitu vyake ndani, akijua safari ya kwenda kwa Docta wangu haipo tena!

Docta wangu aliamuka asubuhi kama kawaida, na wakatii anajiandaa kuondoak ikapigwa simu toka hospitalini kuwa kuna dharura anatakiwa haraka hospitalini, Simu kama ile haina mjadala, akachukua kile kinachochukulia na kuondoka haraka hadi hospitalini, na huko akakuta mgonjwa hali yake mbaya anatakiwa upasuaji wa haraka. Ikabidi aianze kazi hiyo mara moja akisaidiana na wenzake, na mpaka wanamaliza imeshaingia saa tatu.

Alipotoka chumba cha upasuaji akawa anasubiria mgonjwa kuzinduka, akakumbuka miadi yake na Maua, akakumbuka kuwa alitakiwa ampeleke chuoni! nMhhh kazi hizi bwana, ukiwa ndani ya kazi hizi mawazo ya kitu kingine hupotea kabisa, wewe na kazi yako, wewe na maisha ya mgonjwa…ndio siri kubwa ya mafanikio ya kazi zozote, weka akili yako kwenye hilo jambo, utalifanya kwa ukamilifu…akatabasamu kwa fikira hizo…lakini sasa akina Maua na familia yao watalielewa hili, watajuaje wakati hakuwafahamisha, akachukua simu kutafuta namba ya anapoishi Maua, akagundua kuwa alibadili `line’ jana akitafuta namba zake za zamani, na hakukumbuka kuirudishia ile `line’ yake mpya, na `line’ ya zamani haina namba za anapoishi Maua au namba ya Rozi. Akagwaya afanyeaje,

Alitafuta namba ya chuo anachotakiwa kumpeleka Maua kwenye kitabu cha simu akaipata, akawapigia na kuwaarifu kuwa ameshindwa kufika leo na mwanafunzi wao mtarajiwa kwasababu ya dharura iliyompata, na wao wakamwambia nafasi yake bado ipo ila asikose kesho yake. Akashukuru kuwa hilo kalitatua, sasa atawasilianaje na akina Maua. Na wakati anawaza hili akaitwa ndani kuwa mgonjwa kazindukana.

Alifika kumhudumia huyo mgonjwa na mpaka anamaliza saa nne imeshagonga, na mpaka anakabidhiana na mwenzake na maswala mengine ya kikazii saa tano imeshaingia. Akapanga mambo yake mengine harakaharaka na kuomba mungu lisitokee jingine la zarura, na baadaye akamuomba msaidizi wake aendelee na yaliyobakia akaingia ndani ya gari wazzo lake ni kufika Sinza, akaeleze nini kilichotokea.

Docta wa Sinza naye alimalizia kazii zake harakaharaka na akawa na nia ya kuwahi kumchukua Maua wakapate chakula cha machana na waongee kidogo ili kumuweka sawa, na safari hii alitafuta zawadi nzuri ambazo alijua Maua atazipenda sana. Akasema lazima atumie mbinu zake kuhakikisha Maua anamkubalia, lazima…akacheka. Akawaomba wazazi anaoishi nao, kiheshima, mara nyingi anawaomba wote wawili Rozi na Maua, lakini Rozi alikuwa shuleni, nah ii ikawa bahati kwake!

Ilikuwa saa Sita na Maua keshakata tamaa na alikuwa kawaambia wazazi wake kuwa Docta wa Sinza kamuomba wakale chakula cha mchana wote. Na wazazi wale wamemzoea huyo mtu, na sio mara ya kwanza kutoa ombi kama hilo, wakamkubalia. Kwahiyo akavalia nguo zake vizuri na kujikwatua, akijua anakwenda kukutana na mtu ambaye kaaahidii kuwa atakuwa mume wake. Alishaamua kichwani kuwa Docta wake hana umuhimu na yeye, kama kamweka siku nzima anamsubiria je wakioana siitakuwa hivyo kila siku. Akaichukua ile zawadii aliyopewa na Docta wa Sinza na kuiweka kifuani, akasema huyu ndiye anayejua kupenda, …mara akasikia honi ya gari nje, akajua mara moja kuwa ni Docta wa Sinza kaja.

Akajiwekaa vizuri na kujiangalia kwenye kiyooo kabla hajatoka nje. Na huko nje akasikia kama watu wanongea na kukaribishwa ndani, akajua docta wa Sinza kaingia, na wakitoka wote kupata chakula cha mchana atampa jibu safi kuwa kakubali haina shaka, …

 Haya haya kumekucha, madocta marafiki wakubwa wote wapo `in love..' kwa Maua itakuwaje, tuendeleel kuwepo!

Ni mimi: emu-three

5 comments :

Candy1 said...

Nasubiri ngumi kati ya Docta na Docta....hahahhaha!!! Maua naye ana-jump into conclusions aaah! kwanini asisubiri? Hajui kazi zao ni "DOCTOR"...Maua I am disappointed in you lol!

Pamela said...

doctors na usomi wao wakitupiana ngumi itashusha hadhi yao candy1! Ni kawaida wanawake huwa tunajump to conclusion kwa kosa dogo tu la mwanaume!! Tuwemo nataka kujua walivyokubaliana mmoja aumie mwingine apate jamani maumivu ya mapendo mabaya pole sana doc wa cnza cjui ulikubalije yaishe m3 kesho post mapema ukate kiu ya wafuatiliaji....

Koero Mkundi said...

Candy najua itakuwa ni kasheshe walahi

Anonymous said...

DU! sasa kazi kwao Drs.Heb 2subiri utamu huo. Yaan umekatisha penyewe kabisa, mmmmmh!!!!!!!

BN

SIMON KITURURU said...

Tupo na twaendelea kuwepo Mkuu!