Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, March 2, 2010

Maoni yangu

‘Kama nikupatikana mwaka huu nimepatikana kweli’ alisema jamaa mmoja ambaye nilimkuta akiwa anajaribu kuifuta alama kubwa ya X iliyochorwa kwenye nyumba yake. Alama hii iliashiria kuwa jengo hilo na mengine mengi yaliyochorwa hivyo yanatakiwa kuvunjwa kwasababu yamejengwa maeneo yasiyoruhusiwa. Majengo haya yalikuwa karibu na barabara, na barabara hii ilitakiwa kuongezwa upana. Sasa chakujiuliza ni kuwa hawa wanaotakiwa kubomolewa gharama zao watarejeshewa?


‘Mimi na wenzangu tulijaribu kulalamika lakini imeshindikana kwasababu, wanavyosema waliokuwepo awali ambao ndio waliotuuzia walishalipwa, na kweli walituonyesha kumbukumbu za malipo hayo. Lakujiuliza ni kuwa tangu tunaanza kujenga walituona, hawakutuambia, tumekaa muda mrefu hakuna cha taarifa au onyo kuwa eneo hilo mlilojenga halistahili…’ alisema jamaa huku akiendelea kuifuta ile alama sijui ili iweje, kwani kwa maelezo yake lazima majengo hayo yavunjwe.

Ni kweli wakati mwingine inabidi kujiuliza, hizi serikali za mitaa, au hawa wajumbe wetu , kwanini wasiwe na ramani za maeneo yao na ikibidi kuyazungukia mara kwa mara ili kuona kuwa maeneo ambayo hayaruhusiwi kujengwa , hayajengwi? Labda wana kazi nyingi za kiofisi, na watu ndio wanaotakiwa kuhakikisha kuwa maeneo walionunua yanastahili kujengwa au la. Lakini tukumbuke kuwa wananchi walivyo, wengi uelewaji wa sheria ni mdogo. Na isitoshe watu wnadai kunakuwa na ukiritimba wa kupewa ramani za maeneo, ingawaje sasa hivi nijuavyo mimi hali imeboreshwa, na unaweza ukaifuatilia ramani hiyo serikali za mitaa, kama utakumbuka makala ya nitajiajirije sehemu ya kwanza.

Kwa maoni yangu, hawa wajumbe, na watu wa serikali za mitaa, wawe macho sana na maeneo, na kuhakikisha mara kwa mara wanatembelea maeneo yao, nafikiri hii ni moja ya kazi zao. Na pia serikali za mitaa kwa kupitia wajumbe wake wahakikishe wanawaelewesha wananchi wao umuhimu wa kutojenga maeneo yasiyoruhusiwa na ni vyema kukawa na alama zilizo wazi kuwa eneo hili haliruhusiwi kujengwa au kufanyiwa biashara. Hii itasaidia kuwaokoa wananchi na umasikini. Kwasababu kama mtu kachukua vijisenti vyake vyote na kuvizamisha kwenye ujenzi au biashara na mwisho wa siku anabomolewa au biashara yake inachukuliwa nini matokeo yake kama sio umasikini.

Sheria zipo, lakini utekelezaji hasa kwa wanachi unakuwa mgumu, wengine wanazielewa , lakini wapo wengine hawazielewi kabisa, na ukimuuliza kuhusu eneo atakuambia, eneo nimenunue kwa pesa yangu bado serikali inawekee masharti, mara kodi, mara hiki, …sasa mtu kama huyu anatakiwa kuelimishwa ili ajue nini umuhimu wa sheria kama hizo. Pia wasimamizi wa sheria hizi wasibakie maofisini na kusubiri utekelezaji wake , wawe wanawatembelea wanachi kwa kutoa semina , mikutano ya mara kwa mara, mabango ya maonyo vyote hivyo vitasaidia.

Ni vyema tukaelewa kuwa mwananchi wakati mwingine ni kama mtoto mdogo, usipomuonya , na hata kumpiga vibogo hatakuelewa, na huenda akapuuza. Sheria ngapi tumezisikia, lakini hazitekelezwi, nakumbuka kuliko na utaratibu kuwa watu wasivute sigara ovyo, kwenye msongamano wa watu, lakini hutaamini watu wanavuta sigara ovyo, au maswala ya takataka, au mabasi hasa daladala kujaa kupita kiasi, au maswala ya takatak kutupwa ovyo, kwenye mifereji ya maji machafu na kadhalika. Sasa kungekuwa na wafuatiliaji na adhabu zikatolewa ingesaidia kuziweka hizo sheria hai. Hayo ndio maoni yangu

From miram3

1 comment :

Anonymous said...

Everyone loves what you guys are usually up too.
This sort of clever work and reporting! Keep up the fantastic works guys I've incorporated you guys to blogroll.


Feel free to visit my blog - mypcbackup home