Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, March 2, 2010

Mama wa kambo-4

                                                   Na kisa cha msamaria mwema


Nje mjumbe akakutana na mume wa mtu, na katika kuongea ili kupoteza lengo akasema, `unajua rafiki yetu katenda usamaria wema, kumhifadhi mtu aliyeomba hifadhi kwake usiku wa manane, sasa tunataka kujua ni nani, sijui mwenzangu hamjambo huko kwako?’ akamuuliza yule mume-wa mtu, ambaye alikuwa akijaribu kufungua mlango aingie ndani, lakini mjumbe alikuwa kasimama katikati yake.

Mjumbe alimkumbuka vyema jamaa huyu alipomwangalia vyema, kuna kesi moja ililetwa kwake, akiwa kapigana na mwenzake kwa mapanga, kama ingelipelekwa polisi angelikuwa bado yupo kifungoni. Walitumia busara na kuwasuluhisha,na baadaye wakakubaliana jamaa huyu angaramie matibabu. Huyu jamaa ni lile kabila lenye hasira, kwao kupigana, kutoana ngeu ni jambo la kawaida. Hapa mjumbe akaguna na kusema moyoni `hapa ilihitajika busara ya hali ya juu’.

Mjumbe wakati anajaribu kumweka huyu jamaa sawa, akakumbuka alipoongea na mjomba wake asubuhi. Mjomba wake huyu alimpigia simu kumuuliza hali kwani walipoachana jana alikuwa hajisikii vyema kiafya. Alimwambia hajambo kidogo, ila kaamushwa asubuhi sana kwasababu kuna tatizo limetokea katika eneo lakena anahitajika kulitatua.

‘Tatizo gani tena mjomba, huo ujumbe utakumaliza kabla muda sio wako’ Akasema mjomba mtu ambaye ni asikari polisi, katika kitengo cha uasikari kanzu. Alimpenda sana mjomba wake huyu kama baba yake mzazi, na mara kwa mara walitembeleana . Na kwa jana walipoachana katika maongezi yao, mjomba mtu alimshauri mzee wake huyu kuwa muangalifu katika maamuzi ya kesi zinazoamuliwa kienyeji. Alimshauri kuwa unaweza ukatenda jambo kwa nia njema, kiudugu, kama litaisha inakuwa ahueni, lakini jambo hilo likienda kombo ujue sheria itakuandama.

‘hiyo usijali, tuna uzoefu na mambo haya, hayo ya huko shuleni kwako utayatumia muda ukifika, bado sie tuna ujima wetu…’ akasema mjomba mtu huku akiinuka kuondoka, na kulalamika maumivu ya kiuno na mgongo. Mjomba mtu akamshauri mzee wake huyu wapiti hospitali lakini ombi halikukubaliwa.

Mjomba-Askari alitafakari maelezo aliyopewa na mzee wake, akahisi kuna tatizo, sijui ni kwasababu ya kazi zake au ni kwasababu ya kumonea huruma mjomba wake, lakini alihisi kuna haja ya kujua zaidi, ili amsaidie mjomba wake na mambo mengine ya kisheria. Alijua wajumbe wengi huchaguliwa kwa sababu ya uzoefu wa kijamii,. Lakini sheria zinaweza zikapuuzwa kwasababu za ujirani na matokeo yake yakawa mabaya baadaye.

‘Sawa mjomba nimesikia hayo maelezo lakini, angalia na afya yako kwanza, kazi zipo, haziishi na hakuna atakayekujali kama hukujijali mwenyewe’ alimshauri mjomba wake kwenye simu ya asubuhi.

‘Ndio hivyo sawa mjomba, lakini sijambo usitie wasiwasi, lazima wengine tujitolee, ni kama nyie polisi mlivyo, likitokea jambo hata kama ni usiku hata kama hujiskii vizuri inabidi uwajibike tu, kazi zetu ni wito, mjomba wangu’ akasema mjumbe.

‘Sasa mjomba kama ni tatizo kubwa useme mapema, ili niwapigie wenzangu ofisini, wawahi na gari, nahisi inaweza ikawa tatizo kubwa!’ akauliza mjomba mtu

‘Sidhani kama ni tatizo kubwa..’ Ngoja nifike kwanza huko, kama ni tatizo kubwa tutakufahamisha. Hizi ni moja za kazi zetu, zikifika kwenu ujue tumeshindwa kuzitatua.

‘Ndio Mjomba, lakini bado nina wasiwasi, naomba uwe mwangalifu, lolote linaweza likawa, kama vipi ngoja polisi waje kwanza, sie ndio kazi zetu hizo, siunajua kama mtu kafa, utasumbuliwa sana, lakini kama tukifika wenyewe tutaangalia nini kilitokea na ushahidi hautavurugwa..’

‘Aaah, usifike huko mjomba, ngoja tuyamalize kimitaani,hajafa mtu bwana, unajua tena wakifika polisi yatakuwa makubwa, kumbe kilikuwa kitu kidogo, nyie mtakifanya kikubwa…unajua walivyonielezea, alikuwa mzima, hana jeraha, la kufa…hapana, kama kuna zaidi tutawasiliana’. Ikawa mwisho wa mazungumzo yao, na hapo akajuta kwanini hakumwambia aje ili wasaidiane, kama kuna kubwa liwe mkononi mwa polisi!

Alimgeukia Yule jamaa, akamvuta pembeni, ili wajaribu kuongea na kupoteza muda

‘Kwangu mjumbe sijambo, ila nimeshangaa kuniita asubuhisubuhi, nimefika kwako, ajabu nikakuta haupo, siunajua tena ukiitwa kwa mjumbe, unajiuliza mengi, nimetenda kosa gani..’akasema akiwa na wasiwasi

‘Kwani unahisi umetenda kosa?’ mjumbe akamuuliza

‘Aaah, kosa, aaah, sijatenda kosa..kosa gani mjumbe, mambo mengine ni kawaida tu, mume na mke kukorofishana ni jambo la kawaida, sijui labda…’ akataka kuuliza kitu halafu akasita

‘Hujui labda nini..ongea tu usijali..’ na kabla hajasikia kauli ya huyu jamaa, wakasikia sauti zikiita toka ndani, kuwa mjumbe anaitwa mlango umefunguka.

Haya wapendwa mlango umefunguka, huyo mgeni yupoje, yupo hai au kafa? Tuonane baadayeFrom miram3

No comments :