Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeWednesday, March 17, 2010

Kufa kufaana

`Malaria haikubaliki.. huu sasa ni wimbo wa kibiashara zaidi, mwanangu tangu juzi anaweweseka na homa juu, na najua kesho au keshokutwa atafuata mwingine' alikuwa akilalamika jamaa mmoja tuliyekutana naye hospitali ya serikali. Nilijaribu kufikiri ana maana gani kusema huo usemi umegeuka kuwa msemo wa kibiashara zaidi, nikataka kumuuliza lakini kabla sijafungua mdomo wangu akadakia jamaa mwingine ambaye pia alikuwa amemshika mwanae mkono;
`Tatizo la nchii kila kukitangazwa ugonjwa fulani kuwa ni janga, au kitu chochote kuwa hicho sasa ni janga la kitaifa, basi ishakuwa biashara. Angalia haya malaria, nimesikia kuwa kuna neti zimetolewa kama msaada, hivi kati yenu kuna hata mmoja amewahi kuzipata hizo neti..' akatugeukia kusikia kauli zetu. Wote pale tulibaki kimya, kwani hata mimi nilisikia kuna neti zilitolewa kama msaada, lakini kwa uoni wangu hizo neti zisingetosha kuwagaia wananchi wote huenda zimepelekwa mahospitalini au kwenye sehemu za serikalini..
'Hizo zimeshageuka mradi...' akasema mwingine
'Haiwezekani, unawafahamu Marekani kweli wewe, huwa wanafuatilia sana mambo yao, kama zingetumiwa vibaya ungeshasikia mtu kawajibishwa. Nafikiri kuna utaratibu serikali umeweka kuhakikisha kuwa zinawafikia walengwa, na henda hizo za hati punguzo zikawa miongoni wa hizo' akasema mama mmoja aliyavalia suti, na wengi wakamgeukia wakihisi ni mtu wa serikali.
 Mimi nikawa nimetekwa na mawazo kisai kwamba sikuweza kuyafuatilia haya maongezi. Nilikuw nikijaribu kufikiri njia ya kupambana na hili tatizo la malaria. Hoja ya kibiashara iliyotolewa na huyu jamaa ingekuwa na mantiki kama angesema hili tatizo tunaliangalia katika matibabu zaidi kuliko kinga. Nasema hivi kwasababu wanaliotoa huo usemi wa malaria haikubaliki walikuwa wakitangaza vifaa au dawa zao, lakini kitu muhimu sio dawa, ni kinga.
 Kwa fikira zangu hawa wafadhili wangelenga zaidi katika kupambana na mazalia ya mbu, wakatoa chanjo, wakatoa dawa za kunyunyuzia kwenye maeneo panapolundikana maji machafu na huu ukawa uataratibu wa kila balozi. Hawa wajumbe wa nyumba kumi wapewe hizo dawa wahakikishe maeneo yao yanadhibitiwa ili kuondoa kabisa mazalia ya mbu. Lakini ukifanya hivyo biashara ya dawa iataenda wapi? je viwanda vya neti na dawa za malaria sizitafungwa. Ndio maana huo usemi ukatolewa ili kuwavutia wanunuzi wa dawa, wanunuzi wa neti.
 Kinga ni  bora kuliko tiba huo ndio ungefaa kuwa usemi wetu wananchi. Huenda ingelifaa sisi wenyewe kuanza huo mchakato, kuwa maeneo yetu yasiwe na malundikano ya maji machafu, takataka na yale yanayosaidia kuzaliana kwa mbu. Na wajumbe wetu wawe wakali kuhakikisha kuwa maeneo yao hakuna vitu kama hivyo. Katika mikutano yao wajadili jinsi ya kupata dawa za kuwaua hawa wadudu, nahisi hii ingesaidia kuliko kuagiza madawa ambayo kila leo yanaishiwa nguvu. Lakini tujiuilze, ina maana hili kweli halijulikani? linajulikana lakini kufa-kufaana. Wewe uumwe malaria ili wenzako wapate mishahara!
 Hayo ndio ya leo sijui nyie mwasemaje?
From miram3

1 comment :

Anonymous said...

Malaria, malaria haikubalikiiii...kawimbo katamu, lakini mmmmh, ngoja nisiseme