Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, March 19, 2010

Kufa hatufi lakini cha moto tutakiona

`Balaa gani hili jamani, sasa nitapata wapi hela za kurudisha mkopo wa watu' alisikika jamaa akilalamika kwa fundi wa vitu vya umeme. Fundi alikuwa akikagua friji lake huku akiwa anamsikiliza mteja wake, lakini alijua kabisa hicho kifaa mteja wake hawezi kukinunua.
'Kwani ilikuwaje?' jamaa mmoja akadadisi
'We acha tu, huu mgawo wa umeme utatuacha wazawa masikini. Unajua sijui ilikuwaje, kwani wakati umeme uliporudi saa nne ile, siunajua wanakata umeme hadi saa nne za usiku, basi waliporudisha kumbe familia yangu ilikuwa haikuzima hili friji, basi umeme ulivyokuja ukaja mwingi, au sijui ilikuwaje, tulichohisi ni harufu ya kuungua kitu. Na kwasababu hatukuwa na wasiwasi tukawa tunaendelea na shughuli zetu. Ngoja nichungulie maji ya baridi ndani ya friji, nikakuta maji yanamwagika nje. Friji likawa halifanyi kazi. Kwa fundi ananitajia kuwa kuna kifaa kimeungua na gharama yake inazidi hata bei niliyonunulia hili friji. Friji hili nilinunua likiwa kuukuu kazini kwa mkopo....' Aliendeleaa kuelezea kisa chake ambacho kilizua tatizo juu ya tatizo jingine.
'Nikiwa nahangaika kutafuta fundi mara nikasikia kelele toka nyumbani, ikabidi nirudi mbio, nafika nakuta moshi umetanda ndani, kumbe pale palipokuwa pamewekwa mshumaa, umedondoka, na kulalia kabati, siunajua mshumaa una kitu kama mafuta, badi ukaanza kuliunguza kabati la nguo. Na humo ndani kulikuwa na nguo za biashara za mama watoto. Nguo hizo alizipata kwa mkopo wa kikundi. Hutaamini nguo zote zimeteketea na moto...' Aliinama chini kwa majonzi.
'Sasa mama ananilaumu mimi , kuwa nimemuanzishia mkosi, kwani kwenye kulinunua hili friji, nilimkopa hela zake toka kwenye mkopo wake huo aliochukua wa nguo, anadai nisingemkopa balaa hilo lisingetokea. Sasa nifanyeje, ananidai, nadaiwa kazini na sina hela za kulitengeneza hili friji, na bado mgawo wa umeme unatuandama.
 Yule fundi akacheka, akasema ama kweli `kufa hatufi lakini cha moto tutakiona' aliposema maneno haya akajipweteka chini. Nilimwangalia kwa makini, na alipoona namkodolea macho akanionyesha juu kwenye umeme.
'Umeme umeenda kwao, wameshakata tena...'
'Kweli lakuvunda halina ubani' nikajisemea na kuondoka, kwani nami nilileta pasi yangu anitengenezee, sasa atafanyaje kazi na hakuna umeme.
From miram3

No comments :