Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeMonday, March 22, 2010

Kaoa au kaolewa

`Jamani nyie wanaume hebu msaidieni mwenzenu' Ilikuwa kilio cha wanawake waliokuwa wamejikusanya nje ya nyumba ya jirani. Mimi nikaingiwa na hamu ya kujua huyo mwanaume mwenzetu ana tatizo gani mpaka hawa akina mama wamuonee huruma. Nikasogea kwenye ile nyumba, nakuchungulia ndani kwa kupitia mlango wa geti. ndani kule nilimuona jamaa ambaye kwa kweli tunafamiana juu kwa juu, lakini sijui undani wake zaidi. Pale alikuwa kachuchumaa akiosha vyombo na pembeni yake kuna lundo la nguo nafikiri ni kwa ajili ya kufua.
'Tumsaidie kwa vipi kwani tunaona hana matatizo ya kiafya na pale alivyovua shati inaonyesha katoka kunywa chai nzito' mmoja wa akina baba alieyekuwepo pale akasema huku akitaka kuondoka.
'Subiri wee baba, tukutonye, huyu jamaa, mnavyomuona ndio hivyo kila siku, akiamuka kufanya kazi zote ambazo mke wake angezifanya, lakini hilo sio baya...' akawa anaelezea mwanamke mmoja aliyeanzisha huu mjadala.
'Jamani hivi nyie wanawake mnataka nini, kila siku mnalalamika maredioni , kuwa wanaume wanawaonea, leo hii mwanaume kaamua kumsaidia mke wake mnaanza visa vingine...' akasema yula baba akionyesha kukerwa.
'Lakini mbona hamtaki kusikiliza ukweli , sio kama unavyozania wewe. Jamaa huyu kaoa kwao kijijini akamleta mkewe hapa Dar, kufika tu, kazi ikaota mbawa, akashindwa kujihudumia, sasa mkewe akaomba wakaishi hapa kwa dada yake. Ina maana huyu jamaa na mkewe wanaishi kwa shemeji yao. Hilo sio baya maisha ni kusaidiana, lakini huyu jamaa ananyanyaswa, na mkewe wakishirikiana na dada wa mkewe.
 'Inavyoonyesha huyu jamaa hana usemi tena, kwani yeye sasa ndiye mfanyakazi wa ndani na amekuwa kama zezeta fulani, unaona lile lundo la nguo huenda hata nguo za ndani zipo mle, afue, akaoshe vyombo, akafangie ndani, apike, hawo wanawake wawili wamekaa ndani wanaangalia televisheni...' akaendelea yule mama kuelezea visa vingi anavyofanyiwa yule jamaa.
 Mimi niliwaza mengi, nilijaribu kuangalia gharama za chumba, kama angelipia alitakiwa alipie kwa chumba elifu ishirini na tano, chakula kwa mwezi kwa mapungufu  kwa watu wawili ni shilingi 150,000/- na mengineyo. Sasa nafikiri kama hizo huduma za chakula, chumba na mengineyo wanapewa na shemeji yao, kufanya kazi hizo sio mbaya! Lakini...
 'Jamani mapenzi ni kitu kinachotafsiriwa na wanaopendana, hamjui kwanini jamaa anafanya hivyo, licha ya mapenzi si ndio analipia hizo huduma anazopata. Cha kumsaidia ni kumtafutia kazi nyingine na sio kumteta kuwa kawa mume bwege' akasema jamaa mwingine.
'Nyie wanaume mna kazi kwelikweli kuelewa, huyu mwenzenu mtamuita nani, kaoa au kaolewa?' akasema mama mmoja.
'Kaolewa na shemeji yao' akasema mwanamke mwingine.
'Sawa yote kwenu hayana heri. Hamjui mwenzenu ana mipango gani hapo, maisha ya hapa mjini ni akili kichwani mwako. Fikirieni yenu, huenda yenu yanawashinda lakini mnazoea kuchunguza ya wenzenu' akasema yule mzee huku anaondoka zake. Nami nikaona nijiondoe pale kwani sidhani kuna cha kusaidia. Eti tutamsaidiaje mtu kama huyu?
From miram3

No comments :