Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, March 16, 2010

ajali haina kinga?

`Yallah, tunakufa, oooh, Mungu wangu...' Kelele za vilio wengi wao wakiwa akina mama zilisikika pale gari lilipotaka kutumbukia kwenye mtaro. Wengine walishaanza kufungua madirisha wakitaka kuruka, na sijui wangeangukia wapi, kweni kwa upande ule wa mataro kulikuwa na maji machafu, na ukirukia dirishani utaangukia kwenye hayo maji au ujigonge kwenye ukuta wa huo mtaro na maanake kuumia, na kw upande wa pili ni barabarani magari yalishaanza kuondoka kwa kasi!
 Muda mfupi uliopita watu walikuwa wakimshangilia huyo dereva kuwa anaweza kazi, kwani foleni ilikuw ndefu, lakini aliweza kutoka nje ya barabara na kutafuta upenyo wa kupita mpaka tukafika mbele kidogo ya wengine. Wakati mwingi katika kupenyapenya gari lilikuwa likiyumba na watu walikuwa wakibadilika kutoka kwenye kujishangilia na kupiga kelele za uwoga.
 Foleni za magari zimekuwa zikiongezeka siku hadi siku na sijui lini tutaweza kuondokana na tatizo hili, na matokeo yake ndio hayo kuwa magari mengi yamekuwa yakipata ajali kwa kutaka kupenyapenya nje ya barabara na kutumbukia kwenye mitaro, na hata kugongana kwa ajili ya kutaka kuwahi mbele au kukatisha mbele. Niliwahi kutoa maoni kwenye makala isemayo `shida ya usafiri na foleni Dar'
 Chakushangaza ni hiyo hali ya watu kushangilia pale dereva anapoonyesha ufundi wake wakupenya au kwenda kasi ili kuwahi kabla ya wengine. Na tushukuru safari iwe salama, kwani ikiwa kinyume chake wengi wataishia kumlaumu dereva kuwa alikuwa akiendesha kasi nk. Tunasahau kuwa wakati mwingine sie abiria tunakuwa chachu ya kumshabikia dereva kuwa aendeshe kasi ili watu wawahi na wengine husifia gari fulani kuwa linajua kukwepa foleni.
 Tukumbuke kuwa ajali haina kinga, lakini je unaweza kwenda kusimama barabarani wakati magari yanapita kwa kuwa ajali haina kinga? haiwezekani utaonekana una mapungufu fulani. Hata hii hali ya kwenda mwendo kasi au kupenyepenye kwenye maeneo yenye hatari haina tofauti na huyo anayesimama katikati ya barabara wakati magari yanapita, ni kujitakia ajali, na sio ajali ya bahati mabaya. Tuweni macho na tuwe wachunga tunapokuwa ndani ya magari. Tukiona dereva anakosea tumuonye na sie tusiwe wakwanza kushabikia mwendo kasi kwani wakuumia na sie na wakati mwingi dereva anaokoka kwani yeye huiona ajali ikija, je wewe uliyebanwa kwenye kiti utaokoka vipi, nyie mliojazana kwenye basi kama magunia mtajiokoaje?

From miram3

1 comment :

Anonymous said...

Wewe eti ukae barabarani, kwasababu ajali haina kinga, hapo umejitakia. Ni kweli madereva wengi wanachangia vifo, kwasababu wao ndio wanaojua sheria za kazi zao hawatakiwi kuwasikiliza abiria