Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, February 3, 2010

Ndoto ya ajabu

Kisu kikali kirefu kilikuwa kikipanda juu na kupita kwenye koromeo la mtu nisiyemuona kwa sura, ingawaje ilioneka kama ninamfahamu vile, makali ya kile kisu yalimeremeta na kumfunika sura Yule mtu, na hata kumfunika sura mchinjaji na kila nilivyojaribu kuinua kichwa au kugeuza ili niwaone vizuri sikuweza. Nilijaribu kuinua mikono ili niyapanguse macho yangu kuondoa ukungu wa mwangwi wa ule mwanga wa yale makali ya kile kisu bila mafanikio kwasababu mikono na hata miguu ilikuwa imefungwa na minyororo ya chuma.


Nilihisi kuwa karibu na wenzangu ambao nao walikuwa katika hali kama yangu. Kwa mpangilio ule tulikuwa tukipangwa makundi ya watu kadhaa, wakiisha yanaletwa mengine, na kundi lililopo sasa lilikuwa kundi langu. Niliwaza jinsi ya kujinasua, lakini kila nilivyowaza nilijikuta nikikabiliwa na vikwazo, na ili kwenda kuchomoa moja ya mnyororoniliyofungwa nayo ilibidi niwavuke wenzangu waliopangwa karibu nami, na hawakubali uwavuke kwasababu ukiwavuka zamu yao itakuwa karibu na hata nikiwavuka kwa mbele kulionekana vitu kama ukuta wenye seng’enge zilizotegeshwa umeme, na kuwekwa vibao vyenye maneno fulani.

Seng’enge ya ukuta wa kwanza iliandikwa ngawila, nilihisi kuwa pale palihitajika pesa, ili upite, na si pesa ndogo, na hata kama ni ndogo inategemea uwezo wako wa kuzipata, sijui ilihitajika kiasi gani lakini niliona sifuri nyingi tu. Nikagwaya nakujiuliza ina maana wote waliokuwa wahanga wa lile bisu hawakuwa na hizo pesa. Labda kikwazo cha ukuta wa pili

12 comments :

Anonymous said...

Hii inatisha kama ingekuwa mimi, ningeacha kabisa kulala

Anonymous said...

Good

Anonymous said...

Ilikuwa ya kutisha sana

Unknown said...

Haha

Jay Melia said...

Fupi mno

Unknown said...

Je inaishia hapo

Unknown said...

Ukweli

Anonymous said...

Whoever wrote this insha he/her has a talent

Anonymous said...

Waa is that really true hongera Kwa ko

Anonymous said...

Good

Anonymous said...

Good πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ’―πŸ‡ΈπŸ‡΄πŸ™πŸ‘πŸ€πŸ‡¨πŸ‡¦πŸ‡ΈπŸ‡΄✍️πŸ‡¬πŸ‡§πŸ†πŸ₯‡πŸ₯‡πŸŽ§πŸŽŸ️

Anonymous said...

Anonymous i am happy πŸ˜ƒ thank you πŸ™ for your service sir