Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, January 7, 2010

'Usilete Uswahili wako...'

 Mr Miram3, unaitwa ofisini kwa meneja utawala’ Ilikuwa sauti ya mama wa masijala ambaye alikuwa pia katibu muhtasi wa meneja utawala. Nilisikia mwili ukiisha nguvu na hisia zangu zikanipeleka moja kwa moja kuwa na mimi ilikuwa zamu yangu ya lupokea barua ya kupunguzwa kazi. Ilikuwa kipindi cha mapito kwa kampuni na imetokea mara nyingi kwa muda kama huu, kunakuwa na zoezi la kupunguzwa baadhi ya wafanyakazi kwa kisingizio cha kubana matumizi, cha ajabu baada ya siku kadhaa wanaajiriwa wafanyakazi wengine!


Niliinuka kwenye kiti changu na kuelekea iliko hiyo ofisi, na wafanyakazi wenzangu waliniangalia kwa macho ya huruma wakijua kuwa mwanzao naye ni siku yake. Hali kama hii ni ngumu na usisikie mpaka ufikie mazingira ya hizi ofisi za watu binafsi. Ofisi hizi , nyingine hazijali hata ile mikataba halali iliyowekwa na vyama vya wafanyakazi, leo wakiamua hivi kesho huna kazi, nenda uendapo. Nakumbuka kesi yetu ya kupnguzwa wafanyakazi isivyo halali bado inapigwa kalenda na bahati mbaya mwenyekiti wetu keshatangulia mbele za haki!

Nilipofika kwenye hiyo ofisi niliambiwa nisubiri kwasababu bwana mkubwa, meneja utawala anaongea na simu.Hali kama ile ya kusubiri ilizidi kuniumiza, nikifikia hatima baada ya kupata hiyo barua, nilifikiria jinsi ya kupata kazi nyingine na wakati huo nilitakiwa kulipia kodi ya nyumba ya mwaka, vinginevyo nihame. Je nikipata hivyo vijisenti unavyopewa kama posho ya kujikimu baada ya kupunguzwa kazi nilipie kodi ya nyumba au nitafute mradi gani wa kunifanya niendelee kuishi hujku natafuta kazi nyingine.

‘Mr, ingia ndani unasubiriwa’ aliniambia yule dada katibu muhtasi wa bosi. Niliingia na kumkuta meneja utawala akiwa ameshikilia faili, nilihisi ni faili langu. Hakujali sana kunisalimia, alikuwa akiendelea kuangalia kilichomo mbele yake, na baadaye kama mtu aliyegutuka alinikaribisha na kuniambia nikae kwenye kiti.

‘Unajua wewe ni muhasinu na tunakuamin sana, na hatutegemei mtu kama wewe unaweza ukafanya kitu cha ajabu kama hiki…’ Alianza kuelezea, nikaona ohoo, ina maana sio barua ya kupunguzwa kazi tena ni barua ya kufukuzwa kazi. Nilijaribu kufikia kosa gani ambalo ninaweza nikawa nimelifanya bila ya mimi mwenyewe kugundua bila mafanikio. Nikaona nisubiri hilo bomu litakapolipuka.

Mara yule meneja utawala akachomoa karatasi ya madai ya malipo, alipoichomoa nikagutuka kwasababu mimi ni mmoja wa anayehusika kuziratibu kumbukumbu za kiuhasibu za malipo, kwahiyo ina maana kuna kosa limetokea katika kazi zangu. Nikajaribu kuinuka ili niione ile nyaraka vizuri.

‘Unakumbuka taratibu zetu za madai, unapotibiwa unatakiwa ulete nyaraka ya dakitari na stakabadhi ya malipo iliyoainishwa anuani ya hiyo hospitali au duka ul;iponunulia dawa, sasa wewe unatuletea stakabadhi ya mitaani, ambayo unaweza wewe mwenyewe ukaitengeneza, hii ni kutokuwa makini na nikosa kawa mhasibu kama wewe’

Hapo nilipumua na kujua kumbe ni stakabadhi ya malipo niliyoipeleka kudai marejesho ya hela niliyotumia. Nilijua kuwa italeta shida ndi maana niliandika barua ya maelezo, ya kuwa hospitali niliyokwenda hawana aina nyingine ya stakabadhi zaidi ya hiyo na walinipa namba yao ya simu kuwa kama ofisini hawataikubali wawasiliane nao na wao watawaeleza kwanini bado wanatumia stakabadhi kama

rom miram3

1 comment :

Anonymous said...

Hata mimi hiyo siipendi kwanini tusipende lugha yetu, huo ni utumwa wa dhahiri.