Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, January 11, 2010

ndugu tegemezi

 Leo nimeona nimtembelee jamaa yangu ambaye tuliwahi kuwa naye huko Mzumbe, na kumpa hongera kwa kuhamia kwenye nyumba yake mpya. Alihamia kama mwaka uliopita, lakini sikuwahi kuhudhuria sherehe yake ya kuhamia, kwahiyp leo nikaona niione nyumba yake na kujua nini siri ya maendeleo yake.
‘Jamaa yangu (alitumia neno –‘mate’), hali imeniwia ngumu ajabu, sikutegemea kama hali ingekuwa hivi. Tangu nihamie kwenye nyumba yangu, nimekuwa mtu wa kuhangaika zaidi ya nilivyokuwa kwenye nyumba ya kupanga. Majukumu yameongezeka, hali imeniwia ngumu kiasi kwamba nafikia kukufuru kuwa aheri nisingekuwa na nyuma hii…’ aliinua mikono juu na kuomba msamaha kwa Mungu amsamehe kwa kauli yake hiyo.
‘Mimi unanishangaza, wenzako tunafurahi kwasababu ukiwa kwako, ni siri yako, kama umekosa au umepata ni wewe na familia yako, sasa iweje wewe iwe kinyume?’ Nilimuuliza.
‘Ni sawa, lakini sio mimi, kwasababu kwa shida natakiwa kila siku nilishe familia ya watu kumi.Watu kumi, kuondoa watoto wangu watatu , mimi na mke wangu. Fikiria mshahara ninaopata, inabidi kila siku niishie kukopa’ Aliinama chini akitafakari halafu akaita ndani niletewe kinywaji, lakini mimi nikamshukuru kuwa sikai sana.
 ‘Usikatae kinywaji kwasababu nimeongelea hili, kwasababu nahisi jamii nyingi za kiafrika tunatatizo hili, ila wakati mwingine unamueleza rafiki yako, huenda akakupa mawazo’ alisema wakati ananisindikiza.
 Niligeuka kuiangali anyumba yake, ni nyumba nzuri ya kifamilia, yenye vyumba vitatu, chumba kikubwa cha kulala , vyoo viwili, jiko , chumba cha chakula na sehemu kubwa ya chumba cha maongezi. Niliipnda jinsi ilivyo, ingawaje rafiki yangu alijuta kuwa nayo, lakini nilimpa heko kwa kazi nzuri aliyoifanya.
 Aliniambia kuwa inabidi watoto wake walale kwa shida kwani kitanda kimoja inabidi walale watoto wane, ambao wengine ni wa jamaa zake waliokuja kuishi naye na vyumba vingine vyote vimejaa wadogo zake na jamaa wa ndugu zake. Wote hawa walikuja Dar, ili wapate msaada wa kielimu au kazi au kupata msaada wa maisha kwasababu kijijini hali hailipi.
 Haya ndiyo maisha yetu tulio wengi. Labda wenzetu waliojaliwa, ambao familia yake ni yeye , mkewe na watoto wake, lakini sie ambao hata kusoma kwetu tumefadhiliwa ama na baba wadogo, wajomba au kaka, tumepitia maisha haya. Ni majukumu ambayo huwezi kuyakwepa au kuyakataa, kwani ukikataa, utaulizwa wewe umesahau wapi ulikotoka.
 Lakini hali ya miaka ya nyuma ilikuwa na baraka,sio kama sasa. Wazee wetu pato lao liliweza kuwatosheleza, na kuishi na familia zaidi nay a kwake. Hata ukiangali mishahara yao ilikuwa sio mikubwa lakini waliweza kuwachukua jamaa, zao kwa kuwaomba na sio sasa jamaa hawo wanakuja wenyewe hata bila kuitwa. Baraka za wema zao ziliongezeka na utashangaa maisha yao yalikuwa bora, kuliko sasa.
 Maisha ya sasa hivi mtu akiwa ni kipato kizuri, atataka kuwasomesha watoto wake kwenye shule za gharama, lakini enzi hjizo shule zilikuwa za serikali na kulikuwa hakuana ada. Siku hizi mtu atahitaji mfanyakazi wa ndani, wengine wanahitaji hata mlinzi, mhudumu wa shamba wakati enzi hizo, kazi kama hizo wangefanya jamaa zako, wadogo zako au watoto wa jirani zako ambao umewachukua muishi nao. Maisha yamebadilika na gharama zake zinakuwa kubwa kupita kiasi, hadi wale wenye uwezo wanaishia kulalamika kuwa maisha ni magumu kwao!
 Kutokana na mashinikizo ya kimaisha, kipato hakitoshelezi, ndugu tegemezi kuwa wengi, na ajira kutokuwa na uhakika, utakuta wengi wanaishia kupatwa na magonjwa ya moyo, shinikizo la damu , kisukari , vidonda vya tumbo na magonjwa kama hayo ambayo zamani yalikuwa ni nadra. Inabidi mtu afikiri zaidi ya kufikiri, apige bajeti ambayo haikamiliki, ajibane hata kula na bado ataishia kulaumiwa. Watamlaumu jamaa na ndugu zake ambao walitegemea msaada toka kwakwe kwasababu anakipatao kizuri , nyumba nzuri, na anawasomesha watoto wake shule nzuri lakini hataki kuwasaidia jamaa zake wengine kama alivyosaidiwa yeye. Haya ndiyo maisha yetu ya kutegemeana, huwezi kuyakwepa kirahisi kwasababu hata wewe uliwahi kuwa tegemezi.
From miram3
From miram3

1 comment :

Anonymous said...

Lakini wengiune wanajiakia mtu hana uwezo anawakaribisha jamaa zake kibao, ili kujionyesha kuwa anazo, siku anachacha anaanza kupiga moyowe.
Hata hivyo sio jambo jema kuwafaukuza ndugu zako, ila uangalie uwezoi wako