Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeMonday, January 18, 2010

Mdudu kala mafaili yangu

 Ndugu wapendwa, flash yangu ambayo huwa naweka kumbukumbu zangu imeingiwa na wadudu kiasi kwamba kila kilihokuwepo kimeenda na maji. Nikajaribu kuandika mambo mengine n, lakini cha jabu nilipofika kwenye internet cafe yakawa hayafunguki. Nimetahayari sana, kwani nilikuwa na matukio mengi sana, lakini muda wa kuyaandika upya kwenye intenet cafe inakuwa haitioshi, ni gharama kubwa kwangu ukizingatia bado nipo kijiweni. Naombeni msikate tamaa, nitafanya kila bidi niwaletee vituko nilivyokutana navyo. Kuna ndoto ya ajabu, watu wanakatwa makoromeo, nami nipo kwenye foleni hiyo. Kuna vituko vya jamaa aliyetakiwa aoe kwao akakataa, kila akioa anakutana na maajabu. Yapo mengi lakini nifanyeje ili niyaweke hadharani?
From miram3

1 comment :

Anonymous said...

Siunajua tena dunia yetu hii ya tatu