Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Monday, January 11, 2010

maiti hana rafiki

  Jana nilikuwa mazikoni, na wakati tumemaliza kumzika jirani yetu aliyefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu hivi.Kiiongozi wa dini alitoa mawaiza kidogo, ambayo yaliwagusa wengi tuliokuwepo. Alisema wafiwa wanashukuru sana kwa wema wenu wa kuja kumsitiri ndugu yetu huyu. Wafiwa wamesema hawana cha kuwalipa kwa wema wenu huu, na muendelee na moyo huo. Wamesema hawana matanga, kwahiyo mnaruhusiwa kurejea makwenu na kama kutakuwa na cha ziada watawaarifu.
 Lakini wamewaomba wandugu wa karibu warudi nyumbani kulipo na msiba ili waweze kutathimini yote. Lakini najua ndivyo ilivyo, ndugu wa karibu wataitisha kikao chao na cha kwanza kuulizana ni je ndugu yetu huyu alikwa na nini? Na huenda ile nyumba ya marehemu imeshatafutiwa dalali, na kila mmoja ameshapanga nini cha kurithi. Lakini je tujiulize ni ubinadamu gani tulioufanya hapa. Mwenzetu alikuwa na jumba kubwa, lakini leo hii tunakuja kumfukia hapa kwenye kachumba kadogo ka futi sita kwa tatu. Je hakuna hata mmoja ambaye ana mapenzi ya zati na marehemu akabakia naye hapa angalau kwa siku moja? Alituangalia akisubiri jibu , na kimya kilitanda.
 Ni nani angebakia hapo, hebu tujiulize. Hapa nilikumbuka kisa kimoja, wakati watu wanaomboleza, wengi walikuwa wakilia na kujibamiza chini, na chumbani wakuu wa dini walikuwa wakimuandaa maiti. Sijui ilikuwaje maiti akasogezwa vizuri ili awekwe kwenye jeneza. Mke wa marehemu akaomba aingie chumbani anachotayarishwa maiti angalau amuombee maiti dua ya mwisho, wakati huo alishavikwa sanda na ilibakia awekwe kwenye jeneza. Basi akaruhusiwa.
 Kumbe yule maiti katika kumfunga mkono ulikuwa kidogo umeinuka juu. Yule mama akawa analia anaomba anamshikashika eneo la kichwa yule marehemu. Mara ule mkono uliokuwa umewekwa vibaya ukajinyosha, na ile hali ikamfanya maiti atikisike kidogo. Pale alikuwepo kiongoziwa dini na wasaidizi wake. Wote waliona ule mtikitisiko, na kilichotokea hapo hutaamini, mlango ulionekana mdogo.
 Swali likaulizwa je hawa watu walikimbia nini? Jibu ni rahisi ingawaje tunajifanya vinginevyo. Maiti hana rafiki. Ukishaitwa maiti wewe sio rafiki wa mtu, ingawaje watu wanatoa mapesa mengi ili kusaidia mazishi na nk, lakini moyoni kuna mengi ambayo kama yangewekwa wazi tungesadikisha kuwa kweli ukifa umeondoka na kitu kimoja tu ulichokifanya katika maisha yako, nacho ni matendo yako mema.
From miram3

No comments :