Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Sunday, December 27, 2009

Mwaka Mpya!

`Mlio wa mawe yakirushwa juu ya bati viliniamusha ndani ya ndoto tamu, ndoto ya safari za kimaisha, unapata , unakosa. Na kwa vile nilikuwa nimechoka sana nilijivutavuta kuamuka nikijipa moyo kuwa huenda ikawa mmoja alikuwaa akiua panya na bahati mbaya akagonga bati, lakini makelele vurugu, nyimbo na mawe kuendelea kugonga juu ya bati vilifanya usingizi upotee kabisa na kunifanya nichungulie dirishani. Hamadi! nilikoswakoswa na jiwe lililogonga nondo ya dirisha na kama isingekuwa ile nondo ningekuwa sina jicho. Kwa tukio lile ilinifanya niruke kitandani na kutafuta mahali nilipoliweka rungu langu ili nikapambane na hizo vurugu.


Nilipofika nje nilikuta umati wa watu, wakiwemo wapangaji wenzangu wakiwa nao katika mkumbo wa kushangilia, lakini miongoni mwao walikuwemo wenye majeraha yanayovuja damu, kiasi kwamba nilishindwa kujua ni sherehe za aina gani zimetokea zinazoambatana na kuumizana. Waliomizana walikuwa wamelewa chakari na katika kulewa huko kukatokea ugomvi ambao uliopelekana kuumizana, lakini swali likanijia akilini, kwanini hali hiyo itokee sehemu zote, kwani nilidhani ni sherehe iliyokuwemo ndani ya nyumba nilikopanga, lakini cha ajabu makelele yalikuwa yameenea kila kona, vurugu , vifijo mawe kurushwa ovyo, mipira ya magri kuchomwa moto!

Bahati nzuri nikasikia mmoja akiseme `happy newa year’, nikaangalia saa yangu nakuona ni saa sita na dakika kadhaa, nilkaduwaa kweli ni mwaka mpya, nakujiuiliza nini hasa tafsiri ya maeneo haya `happy new year’ au mimi kiingereza changu ni cha chini ya miti!. Niliwaangalia wenzangu kuhakikisha kuwa wote wamelewa au ndio hiyo kusherehekea mwaka mpya. Niliwaona wengine ni wazima kabisa, ndipo nikakumbuka hadithi za ujahilia ambapo watu walikuwa wakisherehekea mwaka mpya kwa mitindo huu hadi kuuana, kutoa makafara na vitu kama hivyo.

Nilijiuliza maswali mengi ambayo nilikosa majibu, kuwa kusherehekea mwaka mpya kwa mtindo huu kuna maanisha nini? Nikitu gani tumekishinda au tumemshinda nani? Kwasababu mweza wa yote ni Muumba, ndiye ilibidi tumshukuru, kwasababu chochote na musda wowote anaweza kubadili kibao, furaha ikabadilika na kuwa majonzi. Au tunajiona majabali mbele yake kuwa hakuweza kuzitoa roho zetu kwa ubabe wetu? Hilo tunajidanganya.

Wapo wenzetu wapo mahospitalini hawajiwezi , hawajapenda hili, wapo wameshatangulia mbele ya haki hawakupenda hili, yote mwenye uwezo nayo ni muumba, kwahiyo kuupata mwaka mpya zi ujabali, au uhodari wetu. Tunatakiwa tumshukuru yule mwenye mamlaka aliyetuwezesha hili, na sio tumkufuru.

Kulipopambazuka tulisikia vituko vingi vilivyotokea mitaani, watu waliibiwa, watu waliumizana na baya zaidi wapo waliopoteza maisha kwa kusakamia pombe za ushindani. Mashindano hayo yalitayarishwa ili kuuaga mwaka, na mshindi ni yule atakayeweza kunywa pombe nyingi zaidi. Na mshindi kweli alipatikana lakini ushindi wake na zawadi yake ikawa ni umauti.

Mimi kwa ushauri wangu, kumaiza mwaka ni kazi kubwa , kwani tumekumbana na majanga mengi, tumekutana na mitihani mingi ya kimaisha na kwahiyo tunahitajika kukaa chini na kutafakari wapi tumekosea , tumefaidika nini na nini malengo yetu ya baadaye. Na hili haliwezi kuja kwa kulewa, kupiga makelele na kuwabughuzi wagonjwa ambao wanahitaji utulivu.

Ni vyema tukajenga utaratibu mzuri wa watu kukutana kwenye nyumba za ibada, watu wakamshukuru muumba, watu wakapeana nasaha za kiimani kuliko kumweka shetani mbele. Kuna mmoja alisema ukiuanza mwaka kwa balaa utaishia kupata mabalaa mwaka mzima, sasa hayo matendo tunayofanya sikujitafutia mabalaa. Kwanini kuliko kulewa na kufanya masherehe ya kufuru, pesa hizo tusiwapelekee wasiojiweza, wajane, watoto mayatima na wagonjwa tukapata thawabu, na Baraka Tubadilike na twende na wakati, kuliko kurejea enzi za ujahilia.

From miram3

1 comment :

Anonymous said...

Huo ni ulimbukeni tu wa watu wachache ambao kila jema hutaka kulitia tope, kilalaheri uzidi kutupa maneno ya hekima