Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Sunday, December 27, 2009

Iga lakini usiige Tembo...

Mbele yangu kulikuwa na mabinti wane, lakini walivyoonekana walikuwa katika makundi mawili. Kundi la kwanza la mabinti wawili walikuwa wamevalia ‘kimama’ nimetumia hilo neno kama nilivyowasikia katika maongezi yao, na kundi la pili walivalia ‘kimtindo’ wao walitumia neno la kiingereza `ki-fashion’


Mabinti hawa walikuwa na rika moja, na walibahatika kusoma shule moja, katika shule za msingi. Wawili waliovalia kimtindo walibahatika kwenda sekondari na sasa walikuwa kidato cha nne. Lakini hawa wengine wawili hawakubahatika kuendelea na masomo, kama nilivyowasikia ni kutokana na kipato cha wazee wao, kwani walikuwa tayari kuendelea kusoma lakini hali haikuwaruhusu.

Wale waliofaulu, waliwafahamu wenzao kuwa darasani walikuwa wakijitahidi lakini bahati haikuwa yao, ila wao pamoja na juhudi za wazee wao kuwapatia masomo ya ziada, lakini hata mazingira wanaoishi yaliwasaidia kufanya vizuri zaidi kwenye mitihani yao.

Hawa ambao wamevalia kimama, kwa vile walikuwa nyumbani au kutokana na shinikizo la wazee wao au wao wenyewe kupenda, waliolewa na mmoja alikuwa na watoto wawili na mwenzake alikuwa na mtoto mmoja, na wanaishi na waume zao hapa jijini.

Mimi ilibidi nipunguze mwendo ili nisikilize yale mazungumzo yao, ambayo mwanzoni yalikuwa kuwasikitikia wenzao kuwa walitakiwa wasome kama wao lakini hawakujaliwa, lakini baadaye yalikwenda kwenye kusutana, hasa kutokana na mavazi naminendo ya hawo waliojaliwa kusoma.

‘Nyie mnaonekana wazee, mama-mama, kwasababu ya mavazi yenu, mikanga, mishungi, hamuoni kuwa mnajizeesha’ wale wasomi waliwasuta wenzao

‘Sie kweli ni mi-mama, kwasababu tuna watoto, tuna waume na tunalinda heshima zetu, kwasababu hapa anaweza akatokea mkwe wangu, nitamuangaliaje usoni kama nimevaa kama nyie hivyo’ mmoja wa wale binti alisema

‘Hiyo ni unyanyasaji wa kijinsia, kwani yeye hajui kuwa huu ni wakati wa mitindo, ukiwa nyumbani vaa hizo khanga, tanda ushungi ili mkweo asikuone, lakini upo mitaani lazima ujimwage kisasa, ni lazima muende na wakati jaman, mtazeeka muda sio wenu, angalieni tupo rika moja, lakini akipita mtu hapa nyie mtapewa shikamoo, sie habari gani’ mmoja wa wale binti wasomi alisema.

‘Jamni sawa, endeleeni na usomi wenu, tuachieni na ushamba wetu, sie tumeolewa na moja ya adabu za kuolewa ni kujiheshimu, hatutaweza kuvaa kama mlivyovaa, hata kama mie ningekwenda kusoma hadi chuo kikuu, kwasababu elimu haifundishi mtu kukiuka maadili yake’ mmoja wa wale binti walioolewa alisema.

‘Maadili gani tumekiuka, hebu nielezeeni, zamani wazee wetu walivaa vipande vya nguo, matiti nje, au hamjasoma historia nini, sasa sisi tukivaa hivi tumekosea nini, hii ni kasumba ya kutonyanyasa wanawake, mngesoma mngegundua hili, lakini kwa vile mumewekwa ndani basi kila kitu kama mume anavyotaka, mimi ndio maana sipendelei kuolewa lakini kwa vile ni lazima sina jinsi, nataka niwe huru, nivae nitakavyo, nifanye nipendavyo..’ mmoja wa wale binti wasomi aliongea huku anachnaganya kiingereza na Kiswahili.

Mazungumzo haya yaliwavuta wengi ambao tulikuwa tunasubiri basi, mimi niliyafaidi zaidi kwasababu niliongozana nao hadi kituoni na tukabahatika kupanda basi moja hadi Kariakoo. Katika mazunguzo yao niliwaza sana kuhusu haya mabadiliko ambayo yanaitwa kwenda na wakati, na wakati wenyewe ni hali ile wanayofanyawenzetu hasa mataifa yaliyoendelea, hili ni dhahiri kwa wenye kutafakari.

Nilibahatika kusoma kwenye mtandao mmoja wakati wazee wakizungu wakihojiwa kuhusiana na maadili ya watoto wao, wazee hawa walikataa kabisa kuwa hayo wanayofanya watoto wao sio maadili yao, na kweli ukiangali enzi za kale kidogo za Waingereza, utaona mavazi yao yalivyo, mabinti walivaa magauni marefu, na mashati ya mikono mirefu!

Niliwaza sana yule binti msomi aliyetoa hoja kuwa enzi za mababu zetu walivaa vpande vya nguo nna kuacha matiti nje, na kudai kuwa kama ni kufuata maadili yetu basi tuvae kama walivyovaa mababu zetu. Hapa nilimuona kuwa elimu yake haijamsaidia kupambanua mambo, kwasababu elimu humsaidia mtu kuona uzuri na ubaya wa jambo, na kuliweka jambo hilo katika faida kuliko hasara. Hoja yake ilikuwa katika kutetea mavazi na taratibu wanazofuata kuwa ni za kisasa, ni za kwenda na wakati, akilinganisha na wenzetu wazungu wanavyovaa!

Mimi kwa ushauri wangu kama kwenda na wakati ni kuiga wazungu, sio mabaya, lakini tungeanzia kuiga katika maendelo zaidi, tubuni vitu vya maendeleo, viwanda , uzalishaji na baadaye tutajikuta tukiwa sawa na wao, ili hata tukivaa, tunaweza kujivuna kuwa sisi ni sawa na wao, sisi tunakwenda na wakati kama wao, lakini tufanyalo ni kuiga yale yanayobomoa zaidi kuliko kujenda, na hii ni kuiga tembo, matokeo yake tunayaona, ukimwi wanaokufa sana ni sie, njaa, umasikini na elimu yetu ni yakuiga na kukopi zaidi na matokeo yake kila kiti mpaka apatikane mfadhili toka nje. Tuige, sawa nakubali lakini tusiige tembo…

From miram3

1 comment :

Anonymous said...

Wewe sasa unawachokoza wenyewe, unafikiri msomi atajitanda kanga au ushungi, ataonekana wapi kuwa kasoma?