Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, December 17, 2009

Busara haina gharama

`Jamani, jamani, huyu jamaa vipi…’ Oooh, nguo yangu jamani…’


kilikuwa kilio cha sie wapiti njia, huku tukijaribu kujifuta maji yaliyoturukia, kwani yalikuwa machafu, na huenda nguo zetu zikabaki na madoa-madoa. Siunajua tena jiji letu hili, mvua ikinyesha kidogo mabwawa ya maji machafu kila mahala.

‘Lakini huyu dreva ina maana hakutuoana aache barabara yote hii atufuate huku’ mwingine alidakia, akiwa na tai yake na shati lake jeupe ambalo sasa lilionekana la rangi ya madoa madoa ya matope. Kwakweli kama alikuwa na safari ya ukweni au ofisini, itabidi abadilishe ratiba, vinginevyo ataonekana kiroja.

Wakati tunalalamika na kujifutafuta mwenye gari lile alikuwa akituchungulia dirishani kwa hamasa, huku akijaribu kupambana na madimbwi mengine, lakini alipofika mbele kidogo gari lake likazimika. Fikiria mwenyewe hali iliyomkuta mle ndani, akijua kabisa wananchi watembea kwa miguu aliowapita na kuwachafua walikuwa wakitembea kuelekea usawa wa pale gari lake lilipozimikia.

Tukiwa tunaongea na kujifanya hatujali kwa yaliyotokea tulimkaribia yule dereva na gari lake. Kwa muda ule alishatoka nje na kujaribu kuangalia jinsi gani ya kulitoa gari lake pale llilipokwama. Kwa jinsi ilivyo alihitaji msaada wa kusukumwa, alitugeukia na kutikisa kichwa.

‘Jamani samahanini sana, simnajua tena barabara zetu hizi zilivyo, nilikuwa nikikwepa makorongo na bahati mbaya nikawalowesha, samahanini sana…’ aliongea maneno mengi yakujitetea, lakini hakuna aliyemjali kwa wakati ule, kila mmoja alikuwa akiangalia asije akaloweshwa tena na magari mengine yaliyokuwa yakipita.

‘Jamani naombeni msaada wenu, mnisukume kidogo, samahanini sana kwa kuwalowesha, ni bahati mbaya..’ yule dereva aliendelea kuongea na kujitetea. Sisi kama binadamu tukaona hakuna jinsi, tukamsaidia kusukuma gari na kwa aibu akatuuliza wapi tunakwenda ili atushushe mbele, lakini hakuna aliyemjibu , kila mmoja akaendelea na safari yake.

Kisa hiki kilinikumbusha siku moja nilipomtembelea dada yangu maeneo ya Mabibo, ilikuwa sijafika siku nyingi kidogo, na hutaamini jiji hili kwa maeneo yaliyojengwa kiholela hubadilika kila siku, leo kumejngwa hivi, kesho ule mtaa uliokuwa ukiujua utaukuta umepotea na badili yake kumepita ukuta wa nyumba.

Siku hiyo nilikuwa na haraka kidogo nikaona nichepuke mitaa ya kati na kati ili nifike haraka. Kimtaa hicho kilikuwa kidogo na mbele nikapita kwenye mbele ya baraza ya nyumba, mbele yake kulikuwa na watu wanacheza karata. Kwa vile nilikuwa na haraka, sikupenda kuwasumbua kwa salamu, nikawapita mbio. Nilipofika mbele nikakuta kile kimtaa kimefungwa kwa ukuta wa nyumba. Ikabidi nirudi, na pembeni kulikuwa na vichochoro viwili, nikawa nababaika nipitie wapi ili nitokezee mtaa wa pili.

Niliwasogelea wale jamaa waliokuwa wakicheza karata nikawasalimia, nakishangaa wamekaa kimya, nikarejea ile salamu lakini hakuna aliyenijibu. Nikaona niulizie tu kuwa ni upi mtaa unatokeza barabara mtaa wa pili, jamaa wamabaki kimya. Nikageuza njia na kurejea nilikotoka, huku nyuma nilisikia kicheko, na mmoja akasema hii ndio gharama ya kukosa busara, kapita hajatusalimia halafu anarudi kutuuliza njia…

Busura haina gharama yoyote zaidi ya kuangalia utaratibu wa kijamii ulivyo, kama ni sehemu ya salamu toa salamu , kama ni sehemu ya kutafadhalisha toa `tafadhali’ kama wenzetu wazungu walivyo hata akitaka kupokea simu atakuomba tafadhali. Huu ndio ubinadamu, huu ndio utu, nah ii ndio hekima ya kuishi ya watu.

Hutaamini hata kwenya mahospitali utakuata mtu kwa vile anajuana na dakitari anawakuta watu wapo kwenye foleni, yeye badala ya kuwaomba radhi anawapita na kuingia kwa dakitari. Hata m,aofisini, bosi anaingia ofisini anawakuta wafanyakazi wake wanachapa kazi, badala hata ya kuwaambia `Hayi’ anawapita kama maboga. Hii sio busara, tupendane na tuheshimianeni kwa kuwa waungwana, kwani busara haikugharimu kitu zaidi ya kutamka maneno machache tu, na huenda hayo maneno machache yakawa hayakupungizii kitu.

From miram3

1 comment :

Anonymous said...

Pia busara haina tajiri wala masikini.