Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, October 30, 2009

Nitajiajirije-sehemu ya pili(kuwahi sikupata)

Jua lilikuwa kali sana, na jasho lilinitoka kama mtu aliyemwagiwa maji, sikujali, nilichotamani nifike nyumbani mapema nipate maji ya kuoga. Nilikuwa nimekwenda Mombasa kuchungulia internet, kwenye internet café , kwani internet café ni adimu maeneo ya Gongolamboto, ukiipata, unaweza kuambia mtandao hakuna, au kama leo nimefika wanasema hakuna umeme, na ilikuwa siku ya mgawo wa umeme. Wanasema ule mgawo wetu usio rasmi upo palepale, wa baadhi ya maeneo kutokupata huduma hii ya umeme kwasababu `eti tramsfoma’ haina nguvu ya kuwasha maeneo yote ya Umeme utakao Kisarawe! Kwahiyo kunakuwa na `line tofautitofauti’ leo wanapata hawa kesho wengine, kwahiyo hata kama ni siku yenu ya mgawo, unaweza usipate umeme!

Wakati nipo njiani gari moja likanipita na halafu likasimama mbele yangu, hali niliyokuwa nayo sikupenda kabisa kuingia ndani ya gari la mtu, itakuwa kero ya haraufu ya jasho kwenye gari za watu, siunajua tena, lakini nilipomuona aliyekuwepo ndani ya gari hilo , sikujali ikabidi nipate lifti ya muda.

`We msomi vipi, unatembea kwa miguu toka Mombasa, hadi wapi?, kumbe unaishi huku?’ rafiki yangu alinikejeli. Sikupenda hilo neno `msomi’ na sikuelewa alikuwa na maana gani alipolitamka mara ya kwanza. Nikawa namshangaa nakumsalimia lakini akawa haijibu ile salamu yangu na badala yake akawa ananikoga kwa kejeli!

`Nyie wasomi mnanitia kichefuchefu, kwasababu nilitegemea saa hizi,(Akainua mkono kuingalia saa yake ya thamani kubwa) upo ndani ya gari la kifahari lenye AC, lakini kukuona unapiga TZ 11, nimegundua kuwa kweli, kuwahi sikupata. Ukiwa na elimu unakuwa umewahi, kama nyie mliosoma mpaka vyuo, sijui mnaviitaje vile! Lakini sisi wa `division zero ya elimu tunakuwa tumechelewa asu sio? Lakini nashangaa, sie tumefika `tukachukua’ tukawaacha nyie mnasubiri eti eehe, sheria, eeh, taratibu maalumu, eeeh, kufanykazi ofisini…now your late’ Rafiki yangu aliendelea kunikoga, na nilishindwa kumkatisha na kumuelimisha kwanini imekuwa hivyo, kwani sidhani kama angenielewa, nikabakia kutabasamu.

Rafiki yangu huyu ni mmoja ya waliofeli kidato cha nne wakati wetu, baada ya matokeo haya sikumuona tena, na sikutegemea kukutana naye maeneo kama haya. Kipindi hicho alikuwa mwembamba, ingawaje alituzidi umri , lakini tulikuwa na umbo kuliko yeye kwa muda ule, leo anaonekana tofauti, kibonge cha mtu, kitambi kwa sana na mvi za kitajiri zilishamtanda kichwani.

Njiani alikuwa akiongea yeye tu, akitamba na kuniambia kuwa ingawaje yeye alipata ziro ya elimu, lakini alikuwa na `Division one ya maisha’ Aliniambia kuwa maisha yake yalikuwa yakuhangaika katika biashara, kiasi kwamba uzoefu alioupata hata msomi wa namana gani hawezi kumfikia. Anajua siri za kuingiza mizigo toka nje ya nchi na jinsi gani anavyoweza kupambana na watu wa bandarini au uwanja wa ndege ambao aliwaita `vibaka wa mali ya walalahoi’

`Nchi hii, wengi wanashindwa kujiajiri kwasababu ya vikwazo vingi, chakwanza, ni tatizo la umeme, hakuna kero kubwa kama ya umeme, lakini kwa vile sie tulishawahi na kuchukua nilibahatika kununua generator kubwa, sina shida ya hilo sasa, lakini lipo tatizo la pili la usafiri, foleni na barabara mbovu, nina gari lakini halinisaidii, siwahi kwenye miadi yangu, sijui ninunue ndege. Na tatizo la tatu rafiki yangu ambalo linakwamisha wengi ni utaratibu wa kodi zisizomjali mzawa. Ukiingiza kitu nchini, utalipia kodi ambayo itakufanya ushindwe kupata faida, na ili upate faida ina maana ujuane na wahusika, usiwe na mkono mfupi, siunajua bongo yetu hii. Lakini pia lipo tatizo la wajanja wanaochomoa baadhi ya bidhaa zetu, hutaamini kuna kipindi waliniibia laptop zangu tano ambazo nilizileta kwa ajili ya biashara zangu…’ aliendela kunielezea.

`Kwanza kabisa ili ujiajiri unatakiwa uwe na mtaji wa kutosha, ukianza na biashara ndogo ujue utapambana na askari wajiji, utapambana na serikali za mitaa, utapambana na vikwazo ambavyo ukiviendekeza, utakata tamaa. Unatakiwa uwe mjanja navyo, achana na taratibu, achana na kusubiri, wahi na chukua. Ukizoea hilo, unaingia awamu ya pili, wapi pakufanyia biashara, usilemae na eneo moja, usilemae na biashara aina moja, ruka kama mwewe anayetafuta kifaranga…’ Akaangalia saa yake halafu akaongeza mwendo wa gari.

`Lakini nyie wasomi mwataka utaratibu mnafika badala ya kuchukua msubiri, muweke bajeti, mfuate sheria, sijui ndio taratibu, sie wajanja tunafika tunachukua, ikifikia zamu yako ya unayesubiri utaratibu wenu, hakuna kitu, umechelewa, matokeo yake ndio hayo, mara redundancy, mara…pole sana rafiki yangu’.

Nikawa nimefika mwisho wa safari yangu, na kupanga kukutana naye siku nyingine. Nilimuaga huku nikitafakari sana maneno yake. Je kwa mtaji huu tutaweza kujiari kweli, soma nitajiajirije sehemu ya tatu. Na usisahau kupitia na kusoma nitajiajirije sehemu ya kwanza.

From miram3

8 comments :

Anonymous said...

Polndugu yangu, usikate tamaa,

Anonymous said...

It's enormous that you are getting thoughts from this article as well as from our discussion made at this time.
Also see my web page: air conditioner cost

Anonymous said...

I loved as much as you will receive carried out right here.

The sketch is attractive, your authored subject matter stylish.
nonetheless, you command get got an impatience over that you
wish be delivering the following. unwell unquestionably come more formerly
again since exactly the same nearly a lot often inside
case you shield this increase.

Also visit my web site: pregnant

Anonymous said...

It's a shame you don't have a donate button!
I'd certainly donate to this superb blog! I suppose for now i'll
settle for book-marking and adding your RSS feed to
my Google account. I look forward to fresh updates and will
talk about this site with my Facebook group.
Talk soon!

My web site :: Travel and Leisure

Anonymous said...

Great beat ! I would like to apprentice while you amend your website, how can i subscribe for a blog site?

The account aided me a applicable deal. I have been tiny bit
acquainted of this your broadcast offered shiny transparent idea

Feel free to surf to my webpage :: calories burned walking

Anonymous said...

This actually answered my downside, thanks!



Here is my weblog porno francais

Anonymous said...

We stumbled over here coming from a different web address and thought I
may as well check things out. I like what I see so now i am following you.

Look forward to looking at your web page again.


Also visit my web page - System Care Antivirus malware

Anonymous said...

Hey there! I know this is kinda off topic but I was wondering which
blog platform are you using for this site? I'm getting tired of Wordpress because I've had issues with
hackers and I'm looking at options for another platform.
I would be fantastic if you could point me in the direction of
a good platform.

My webpage - roblox cheats