Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, October 9, 2009

Na pia tuchangie matatizo

Cherekochereko zimeisha, bwana kamapata bibi na bibi kamapata bwana, watu tukaagana na siku nyingine ikaanza. Nikiwa natafakari halihalisi na kujipapasa mfukoni kuangalia salio nikakumbuka kuwa miongoni mwa tuliowaalika sikumuona, si mwingine ila mmoja wa marafiki zangu wa karibu bwana Sitasahau. Niliona Kwa vile sina majukumu yoyote kwa muda ule nifike nyumbani kwake nikamuone, kwani nilipata fununu kuwa anaumwa.
Nilifika kwake na kumkuta kweli akiwa kitandani na nilivyomjua hali, nilishangaa kumuona mwenzangu akigubikwa na machozi, nikahisi huenda ni kutokana na madhila ya ugonjwa. Nilijaribu kumliwaza na kumwambia yote hayo ni mapenzi ya Rabana, ajipe moyo atapona tu.
`Rafiki yangu, machozi haya sio sababu ya huu ugonjwa, kama ingelikuwa ndio sababu ningeshakaukiwa na hayo machozi kama yangelikuwa yanakauka. Kinachoniliza ni kujiona nimetengwa na jamii. Jamii ileile ambayo wakati hali yangu ni nzuri ilikuwa haiishi kupiga hodi si usiku au mchana. Leo nataabika , huku nikitaraji chochote kutoka kwa wale marafiki zangu, lakini imepita miezi, na hutaamini, ni wiki sasa, sijamuona mtu wala ndugu, na wewe ndio pekee nimekuona leo…’ machozi yalimzidi kumtoka kiasi kwamba hata mimi niliona machozi yakinilengalenga.
Baada ya mazungumzo marefu niligundua kitu kimoja kuwa marafiki wengi hupendana kipindi cha raha, na kipindi hiki kama unazo utapewa sifa za kila namna, na wageni hawataisha kufika nyumbani kwako. Lakini pale utakapoonekana huna tena, au ni mtu wa kusaidiwa marafiki watakuwa mbali nawewe. Hii ni kawaida yetu binadamu.
Rafiki yangu huyu, anaumwa, na matatizo yake yalihitaji, licha ya matibabu mazuri vilevile alihitaji ushauri nasaha, kwani walivyosema wataalamu tatizo hilo kuondoka kwake alihitajika afanyiwe upasuaji, na upasuaji huo ungemgharaimu kiasi cha shilingi laki nane za mwanzo. Jamaa yangu huyu, hela hizo kwasasa hana, kwasababu kipindi kingi alikuwa anahangaika huku na huko kwa matibabu ya mkewe ambaye naye alikuwa anaumwa maradhi mengine tu, ikiwa ni miuongoni mwa mitihani iliyomkuta, na kumfanya atumie hela nyingi na kwa mapenzi ya Mungu mkewe akafariki dunia.
Nikakumbuka kua juzi, juzi tu tulikuwa tukisherehekea harusi, harusi ambayo mikakati yake, vikao na mengineyo vilitugharimu muda, na pesa, ili kufanikisha jambo hilo la heri Ni jambo la heri kwani kiimani tumeambiwa ndoa ni nusu ya dini, na kama umekuwa mmoja wa kulifanikisha hili huoni kuwa ni miungoni mwa waliopata heri kubwa. Lakini sasa kwanini pia hatuweki vikao vya shida, vikao vya kusaidiana, vika vya kumsaidia yule aliyekwama kimatibabu, au vikao vya kuwasomesha wale waliokwama katika ada, au vikao vya kuwezeshana kujiajiri ambapo heri zake ni kubwa zaidi!
Katika maisha yetu, vikao vinavyotiliwa mkazo ni vikao vya harusi na msiba. Harusi hata kama mtu hana atajikwamua atafute ili amchangie jirani, ndugu au rafiki yake. Halikadhalika vikao vya msiba, kila mtu akiambiwa atakimbilia kutoa ile akiba yake ya mwisho ili mazishi yafanikiwe, na huenda huyu anayekwenda kuzikwa aliomba hela ya matibabu akakosa, lakini leo anaenda kuzikwa watu wanatoa michango mara mbili ya ile hela aliyohitaji kwenye matibabu. Ina maana tunafurahia kufa kwake kuliko uhai wake?
Sijui na sielewi...!
Kama umejaliwa kupitia blogi hii hebu tupeane ushauri kwanini inakuwa hivi!


From miram3

1 comment :

Anonymous said...

Kwasababu ya kupenda mnuso, starehe na ni sehemu ya kujionyesha, lakini kumsaidia mtu hailipi papo kwa papo. Tuanzeni kujenga tabia hiyoi huenda tukapata baraka za mungu