Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, October 23, 2009

Haki kwa wote

Tatizo la umeme lilinifanya nifikiri mara mbili wakati naelekea internet cafe. Imenibidi nipangilie muda wa kwenda kutegemeana na mgao wa umeme. Leo nimefika kwenye cafe nikakuta hakuna umeme, nimewauliza wanasema ulikuwepo ila umekatika ghafla. Kukatika huku sio mgawo kwani ilikuwa ndio siku ya umeme kuwaka kwenye maeneo yetu.
`Mbona muda wa kuzima umeme hawaliangalii hili, kuwa kuna muda wakati wa kuwaka umeme, unazima kwa sababau maalumu, kuzima kama ni masaa kumi, utazima masaa yote, lakini kuwaka kama ni masaa kumi, kuna kuzimika kwa dharura, huu mgawo hauna haki' jamaa mmoja akawa analalamika
 Ni kweli haki ni ngumu kupatikana. Wenye sheria wanatunga ili haki iwepo, lakini kuna muda haki inakuwa na makengeza. Na mara nyingi haki kwa mnyonge ni nadra. Chukulia mfano kama mtakwenda polisi wewe mlalahoi na tajiri, atakayesiklizwa vizuri ni tajiri, kwasababau yeye haki kwake ina uzito kuliko kwako. Hata umeme, kukatikakatika haiwezi ikawa sawa kwa sehemu zote, zipo ambazo hata kama ni zamu zao utakatwa kwa bahati mbaya.
 Nilirejea nyumbani nikiwa shingo upande, na nilipofika nyumbani nikakuta mtoto wangu karudishwa shule eti kwasababu hajamalizia ada. Ilibidi nifunge safari hadi shuleni, kuwaomba angalau wanivumilie kipindi hiki cha mtihani wa kimaisha, lakini wakagoma, wakasema kama ningekuwa bado nipo kazini wangenifikiria, lakini kwasababu bado nipo nyumbani bila kazi itabidi wanipe siku mbili za kulipa. Haki hapa imemwangalia yule aliye na ajira kwasababu anakitu cha kuegemea, wewe uliyemtaani huna haki.
 Haki haki, haki, haki kwa wote ipo wapi?

From miram3

4 comments :

Anonymous said...

Haki kwa wote!! haki hiyo utaipata wapi wewe, labda mbinguni

Kinsa said...

kaka nasoma hii blog yako kwa kweli inanipa darasa kubwa sana la maisha mzee..Duuh!!!anyways kaka we kaza buti ugumu upo kila sehem..zidisha juhudi na uombe, mungu atakusaidia...Vipi ukiazisah vibiashara vidogo vidogo...Pia unaonekana ni muandishi mzuri...jaribu pia kupeleka makala sehem mbalimbali na hata kuandika kitabu cah hadithi na upeleke kwa publishers...unaweza ukafanikiwa sana tuuuu..Ajira zinatufanya tuwe wajinga sana wakati mwingine!!!!!

Anonymous said...

Haki haipatikani hasa hapa Tanzania

Anonymous said...

Wewe ni Cuf nini?