Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeWednesday, October 7, 2009

Elimu bora bora ni ipi

Katika pitia-pitia yangu kutafuta nafasi za kazi ndani ya magaezeti kila nafasi niliyoiona haikukosa kipengele kama zingatio kinachosema:

`Muombaji awe anajua kuongea na kuandika Kiswahili na Kiingereza kwa fasaha’
Moyoni mwangu nikajisemea kuwa hiyo `kiswahili’ hapo imewekwa kama geresha, nahisi mtoa tangazo angelipenda aseme `muombaji ajue kuongea na kuandika kiingereza kwa fasaha’ kwasababu gani, hawa wageni wanaoajiriwa kwa wingi nchini kwetu wanajua Kiswahili?
Singependa kuongelea sana maswala ya lugha kwani mjadala wake ni pevu, nia yangu nikuongelea swali nililowahi kutoa nasaha zangu kwenye mtandao wa `haki elimu’ swali hilo liliuliza `Elimu bora ni ipi?’

Kujibu swali hili mdomoni ni rahisi, lakini kivitendo ni swali gumu na linalohitaji upambanuzi yakinifu unaombatana na uzoefu katika jamii zetu, kwasababu nianvyo mimi elimu ni njia ya kujifunza hali halisi ya maisha yapi mazuri na yapi mabaya na jinsi ya kuweza kupambana na mzingira yanayomzunguka kwa uelevu na kwa urahisi zaidi. Huenda tafsiri hii isiweze kukidhi haja maridhawa, kwasababu kama nilivyosema awali, kuelezea kwa mdomo ni rahisi kuliko vitendo halisia. Lakini elimu kama elimu ni muhimu na hazina pekee kwa wanadamu, swali ni je elimu hii ipatikanaje, na itambuliweje!

Elimu ya Tanzania imetokea mbali, na upatikanaji wake umekuwa wa kutegemea sana siasa ya nchi kuliko utaalamu wake. Mtanisaidia hapa kama nitakosea. Elimu enzi za sera ya Ujamaa na kujitegemea uliangalia sana ujumla wa jamii, kuwa kila mtu anatakiwa asome `kila kitu’ ili kimsaidie katika kuijenga jamii, yaani wewe uwe na utashi wa sayansi au usiwe nao ulitakiwa uisome sayansi na masomo mengine, nafikiri sababu kubwa ni kuwa hata kama huna utashi na hiyo sayansi, lakini katika maisha yako bado utatakiwa ukutane na mambo yanayohusina na somo hilo.

Sera za nchi zenye siasa ya `Kibepari’ ni za ushindani zaidi, na kila mtu anatakiwa ashindane kivyakevyake, kama utaona mbio zako ni za kisayansi zaidi basi unatakiwa upitie huko, ili upate faida kubwa kwenye kile ulicho na ujuzi nacho, halikadhalika katika masomo mengine. Hii ni elimu ya kimasomo, elimu inayopatikana darasani. Je hakuna elimu nyingine nje ya darasa?

Mababu zetu wa Pwani walisoma sana Kiarabu, hata barua zao utazikuta zikiandikwa kwa herufi za Kiarabu, hawa baadae waliambiwa hawajasoma, kwasababu hawajui kuandika herufi za Kilatini, je Wachina na Kichina chao, Wajerumani na Kijerumni chao! Huku tusiende kwani utakuwa mjadala mwingine.

Kuna elimu ya kimazingira, elimu uliyoikuta kwenye jamii, elimu hii haitaki kwenda darasani, kwani ipo maeneo unapoishi, ipo kwenye maisha unayoishi na ipo ili uonekane mwanajamii. Tabia, na tamaduni mbalimbali ni moja ya vitu vinavyoonekana ndani ya elimu hii. Elimu hii mara nyingi haipewi kipaumbele na inawezekana kwa wengine wasiitambue kama elimu, ingawaje kwa wenzetu , hata sisi kwa miongo hii ya karibuni elimu hii imeanzishiwa mashule, kwasababu kubwa kuwa elimu ni kwenda darasani. Nani atajua umesoma kama huna cheti, hujui Kiingereza!

Sasa swali likazuka elimu bora ni ipi na je ni lazima ili uelimke uende darasani, au elimu ni kujua Kiingereza vizuri, au ni kwenda shule na kusoma madarasa yote, au ni kusoma ili kujua Nyanja Fulani, au ni kusoma ili uweze kuyawezesha maisha?

Swali hili nilipomuuliza msomi mmoja alisema elimu bora ni yote unayofikiria wewe, kwa mfano ili upevuke kielimu lazima uijue lugha, na hasa Kiingereza, akasema Kiswahili sio muhimu kwasababu tunakijua na tunaishi nacho! Ukishaijua lugha vizuri itakufanya uyasome masomo yote bila wasiwasi, na baada ya kusoma utaweza kuyamudu maisha yako, kwasababu kazi zinazotangazwa utakuta chini wameanisha `ujue kuongea na kuandika Kiingereza fasaha’ kwahiyo kama hujui Kiingereza hupati kazi hata kama ile kazi inayotangazwa unaijua vilivyo. Hii ndio elimu ya msomi wetu.
Kutokana na majibu haya nikajiuliza maswali mengi, kama elimu ni lazima ujue lugha hasa ya Kiingereza, basi Wachina, au Wajerumani watakuwa na elimu duni ukilinganisha na Waingereza!
Hebu jamani tujadiliane hili, elimu bora ni ipi?

From miram3

1 comment :

Anonymous said...

Hii ingejadiliwa vizuri na wataalamu lakini inavyoonekana wachangiaji wengi wanapenda blog za picha na habari.Ipo siku waiagundua hii blog, nakuhakkishia utapanda chati. Usichoke, kwani unavyoandika havichujuki, vinaweza vikasomwa hata baada ya miaka kenda na bado vinaenda na wakati. Keep it up