Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, September 4, 2009

WAZEE NI KISIMA CHA HEKIMA

Nikiwa nakatisha mitaa nilimkuta mzee mmoja akiwa amekaa upenuni mwa nyumba, alikuwa amechoka na alionekana kukata tamaa, kwa kukosa huduma au kwa misongo ya kimaisha ambayo hana uwezo wakupambana nayo tena. Niliwaza sana nakujiuliza kuwa leo ni yeye na kesho ni mimi au wewe, kwani uzee haukwepeki, hauna dawa na wala siugonjwa ambao una tiba, ukija umekuja.

Kwa hili niliwaza sana na nilipofika ofisini nilijaribu kuangalia akiba yangu ya uzeeni ya zaidi ya miaka kumi, nilikuta jumla yake haiwezi hata kuweka genge la biashara. Nilijiuliza hivi hela zinazokatwa kwa wafanyakazi wote nchini haziwezi zikajenga huduma maalumu kwa wazee hawa, na je serikali zetu hizi zinawajali wazee kwa namna ya kutoa huduma muhimu kwao!. Na je wazee wana umuhimu gani tena katika jamii zetu hizi hasa hili taifa la amani la Tanzania, au ndio ukizeeka ndio basi tena, `mwacheni huyo ni mzee'

Wazee ni hazina ya hekima, inahitajika kuenziwa na kutunzwa, kwani kila siku hekima hii hupungua kutokana na ama kwa kupungua kwa umri au kutokana na mipangilio mibovu iliyopo kwenye jamii. Ndio maana majanga, vita na kupungua kwa `riziki' kunaongezeka katika jamii nyingi.

Nchi za wenzetu kwa kuliona hili walianzisha sehemu maalumu za kuwatunza wazee wetu, aidha wazee hawa wakifikia umri wa kustaafu wanakuwa na kiinua mgongo ambacho kitawafanya wasitaabike katika maisha yao ya uzeeni. Kiinua mgongo hiki kwa nchi za Kiafrika ni kidogo sana,kwani mpaka mtu anafikia kustaafu, ile thamani ya ile hela haiendani kabisa na maisha halisi. Na baya zaidi waajiri wengi wanawalipa wafanyakazi wao mishahara ya tonge mdomoni(hand-to-mouth). Mishahara hii huwezi hata kuweka akiba, utawekaje akiba wakati hata hiyo bajeti ya kukufanya ule kwa mpangilio haitoshi!

Nashangaa kabisa hata wabunge wa nchi zetu hawalizungumzii hili, watalizungumziaje wakati wao wakistaafu wanakiinua mgongo. Wewe na mwenzangu na mimi una `kivunja mgongo'. Ni vyema wakajua kuwa hiyo neema mpaji ni mtoa ridhiki, huwezi jua kesho na keshokutwa. Ni vyema kukawa na malengo ambayo sio tu yataisadia jamii hii, lakini pia utaratibu huo utaisaida nchi ineemeke kwa kupata baraka kutoka kwa wazee wetu hawa.

Taratibu kama matibabu, usafiri na huduma nyingine za kijamii zingeangalia pia umri,kuwa mtu akifikia miaka ya uzee ambapo mtu huyu hawezi tena kuwajibika basi pia huduma hizo zitolewe bure kwa watu kama hawa, ukichukuliwa wengine waliajiriwa na kutumikia nchi yao,na kukatwa kodi kwa miaka nenda rudi, sasa kazeeka, anatupwa kama kamasi. Na ukiangalia kitakwimu wanaobahatika kufikia umri wakuitwa `wazee'ni wachache sana, kwahiyo gharama za kuwahudumia sio kubwa .
Hili ni ombi langu kwa wahusika, na nafikiri kwa wale wanaojali wataliona hili na kuniunga mkono kwani kuna usemi wa Kipare unaosema `Jani changa la mgomba lisimcheke jana kavu kwani kesho na kesho kutwa utaishia hukohuko'

From miram3.com

2 comments :

Anonymous said...

Nani kama wazee, tusipowaheshimu wao tutapata laana, kuwasaidia nii moja ya heshima kubwa
Mbona kimya, busara zako twazihitaji miram3

emuthree said...

Ni kweli Any. 1:25, kuwaheshemu kwa mdomo tu haitoshi inahitajika huduma na kuwaenzi kwa vitendo.
Nilikuwa sipo hewani kwa muda, nilifiwa na nimesharejea nahitaji sana ushirikiano wenu.