Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeWednesday, September 2, 2009

WAKATI UKUTA


Muda ni kitu muhimu sana katika maisha yetu, mara nyingi tunajali muda pale tuanapokuwa ni miadi fulani, lakini mara chache sana tunaangalia muda katika maisha yetu, jinsi gani umri unavyokwenda, jinsi gani tunavyopoteza muda kwa kitu ambacho hakitatusaidia, jinsi gani tunavyopoteza muda kwa kukaa kijiweni, jinsi gani tunavyopoteza muda kwa maongezi ambayo hayatusaidii zaidi ya kutetana, utani na kujadili mambo
yasijenga au kuleta maendeleo.
Wakati leo tarhe 2-09-2009, nafikiria kuhusu muda, akili zangu zikanipeleka kwa jamaa mmoja ambaye aliamua kuutumia muda wake kwa
njia ya kutafuta elimu. Jamaa huyo alipomaliza shule kidato cha sita aliajiriwa na kampuni moja binafsi,
humo alikuta anakwazwa na lugha hasa ya Kiingereza, akaona aache kazi kidogo akaisomee lugha, na kwa vile alikuwa
namwamko akaiwezea hiyo lugha vyema, akaomba kazi akapata, kwani siunajua tena nchi yetu, kusoma nikukijua kizungu
Kampuni alioajiriwa ikawa pamoja na lugha inampandisha muda daraja na fani yale alivyoisomea, kwahiyo mara kwa mara
akawa anakwazana na meneja utawala, na meneja huyo aliishia chuo kikuu.Jamaa akaona huyu ili nimuweze na mimi
niende kusoma chuo kikuu, akaomba kusoma akapata nafasi na kweli akamaliza na kurejea ofisini,na akapata nafasi nzuri
katika kuwajibika akajikuta kila akitafuta pesa anakwazwa na meneja wa fedha, akaona kumbe umeneja fedha ni mzuri
akaenda akasoma CPA,alipomaliza akaomba kazi sehemu nyingine kama Chief Accountant, akapata kirahisi,
pesa ikawa kwenye milki yake,lakini kila akitaka malipo lazima ikaizinishwe na meneja fedha, ana B.A, ana CPA, ooh,
ngoja nikasomee MBA, akasome na akafaulu, akatafuta kazi sehemu nyingine na bahati nzuri akapata ubwana fedha.
Jamaa akajikuta pia kwa vyovyote hawezi kuuzinisha kitu bila pia director wa kampuni kupitisha mkono wake, na
hii ilimkwaza,akasema kwanini nisiusomee huu udirector, akachukua uprofessor, mmmh, sasa akaona ameshinda,
Katika mihangaiko yote hii ujue kuna swala la muda,umri ukawa juu, na muda mwingi aliutumia kwenye masomo
na kazi alikuwa hana muda wakuangalia maswala mengine ya kijamii, hutaamini hata kuoa ilikuwa bado, umri sasa
ni miaka 47. Akafikiri mke mzuri ni yupi, akafanya uchunguzi na baadaye akaona atafute mke msomi, alihangaika lakini
hakupata yule ambake ataivana naye. Akasikia mitaani kuwa mke mzuri ni wa kutoka kijijini. Huyu utamlea mwenyewe,na
nii rahisi kukutii.
Na kweli kwa elimu yake, kipato na wadhifa akampata binti mzuri wa darasa la saba. Jamaa hakujali maneno kuwa binti
huyu ni sawa na binti yake kama angeoa mapema. Kazi ikaanza hapo. Yeye alikuwa anautaratibu wake nyumbani,kila kitu
mahali pake,maisha yake ndani yalipangwa kama ofisi,sasa kila kitu hakiendi kama alivyotaka,wakati mwingine anakuta
sufuria la ugali ndani ya fridge. Aliongea mpaka akaishiwa, siunajua tena utofauti wa kufikiri ulivyo hapo.
Pamoja na mengine ya ndani, na baada ya kupata watoto wawili, mambo yakawa shaghalabaghala, ikabidi jamaa aanzekulewa
ili akirejea nyumbani asihamanike. Ulevi ukawa ndio dawa,mara matatizo ya shinikizo lamoyo ukaanza,mara kisukari.
Jamaa akawa hajielewi, 'hivi na elimu yangu yote hii maisha mbona hayaniendei vyema, nimekosea wapi'.
Hili ni swala muhimu wakati tunaangalia muda. Huyu jamaa kajiuliza hivi kwasababu licha ya mapungufu yale lakini
elimu inamsaidia kutafakari na kujiuliza, na hii kujiuliza ni upevu wa elimu. Na hili pia ni changamoto kwetu kuwa
elimu si shule pekee,elimu si lugha kujua tu lugha, elimu ni jinsi ya kupambanua mazingira yetu,tuishije, tuupange
vipi mambo yetu ili tuendane na muda tukiangalia pia na swala muhimu la umri, kwani wakati ni ukuta.

From miram3.com

No comments :